
mjanja sana maana pale angekuwa ni sawa amebadili chupa ila mvinyo ni
ule ule..!!! vipi na hapa kwenye ardhi ya madafu usajili gani
umetikisa? wa Okwi au..! Mwashiuya je…! lakini mbali na usajili wa
Azam, Simba na Yanga, kuna sajili zingine nyingi na nzuri ambazo
hazizungumzwi kabisa, anyway tuachane na hayo japokuwa leo sijakugusia
siasa japo kwa mbali..! ila fahamu ya kwamba Obama yupo Kenya na
ametoka “White house” ambapo “amemzingua” yule M-nigeria kumpa silaha
kuwaumiza “Boko haram”, ndo ujue ugaidi kwanini hauishi duniani…
Liverpool imesajili mshambuliaji mzuri na mkubwa ambaye alikuwa
anacheza timu ndogo na ya kawaida, sina haja ya kuzungumzia kiufundi
maana hapa akina Shaffih Dauda wamesha pazungumzia sana, ila leo
naomba umfahamu japo kwa uchache Christian Benteke, mshambuliaji
ambaye amefunga magoli 49 katika mechi 100 ila hazungumzwi sana,
lakini angekuwa Raheem au Walcott kafanya hivo ungeskia “Sky sport” au
“ESPN” wanamuandika kwenye vyombo vyao “World Class Striker” ila
tuyaache hayo leo nimekuwekea vitu vichache ambavyo pengine huvijui
kutoka kwa Christian..
Usajili wa Christian Benteke kutoka Villa park kwenda Anfield ndio
biashara ghali ya usajili kuwahi kufanywa na Aston villa tangu timu
hiyo ianzishwe mwaka 1874.
Christian Benteke mwenye umri wa miaka 24, alizaliwa Zaire {D R C}
katika jiji la Kinshasa, alihamia Belgium yeye na familia yake kwa
lengo la kuukwe utawala wa Mobutu.
Tofauti kabisa na wachezaji wengine, Christian Benteke anaamini
Thierry Henry ndo mchezaji wake bora mpaka sasa na anatamani siku moja
akanyage Mafanikio aliyoyapita Thierry Henry.
Katika usajili uliofanywa na Aston villa majira ya kiangazi mwaka
2012, Benteke alikuwa mchezaji wa nane kusajiwa pale Villa park nyuma
ya Karim El Ahmadi (£2m), Brett Holman (free), Matthew
Lowton (£3m), Ron Vlaar (£3.2m), Joe Bennett
(£2.75m), Jordan Bowery (£500,000) na Ashley
Westwood (£2m).
Anapenda sana basketball na mara kibao katika “interview” zake
amesikika akisema yeye ni shabiki wa kutupwa wa Cleveland Cavaliers na
ametokea kuipenda timu hiyo Kwasababu ya LeBron James.
Mnamo tar 15 September 2012, Benteke alifunga goli lake la Kwanza pale
EPL dhidi ya Swansea city akitokea “sub” baada ya hapo alikaa dakika
343 bila kufunga, ila baadae alikuja kuwa “mtamu” zaidi ya “mcharo”
katika ufungaji.
Benteke kama ni mshambuliaji, lakini pia anae mdogo wake anaecheza
kwenye klabu ya Zulte Waregem inayoshiriki ligi ya Belgium ambaye nae
anacheza nafasi ya ushambuliaji.
Baada ya kutua Villa park kwa kitita cha £7m, alitamka maneno machache
sana, “hatimaye nimetimiza ndoto zangu”
Tchaoooo