Friday, July 24, 2015

MAY D: SIKULIPA GHARAMA ZA STUDIO NILIPOFANYA KOLABO NA P-SQUARE

Mwimbaji maarufu wa Nigeria, May D.
MWIMBAJI maarufu wa Nigeria, aliyeshiriki na waimbaji P-Square katika wimbo wa ‘Chop my Money’ amekiri kwamba hakutegemea kufanya kazi na wanamuziki hao maarufu pia wa Nigeria na kwamba anashukuru kwamba hakulipa gharama zozote za studio wakati wa kurekodi wimbo huo.
P-Square.
Akihojiwa na shirika la Inspire Dot All kwenye kituo cha televisheni cha TVC kilichodhaminiwa na mtandao wa Nigeriafilms.com, alisema: “Wakati nafanya kazi na P-Square nilibahatika kwani sikulipa gharama zozote za studio.”
Aliongeza kwamba baada ya kurekodi na nyota hao, aliondoka na kwenda kurekodi na kampuni nyingine vibao vyake.