Habari mpya kama sio njema ni kuwa Wema Sepetu na Kajala Masanja wamemaliza tofauti zao zilizotokana na ‘beef’ lao lilichukua week kibao sasa. Kwa mujibu wa taarifa mpya mitandaoni ni kuwa mastaa hao wawili ambao waliwahi kuwa mashosti wakubwa walimaliza ‘beef’ lao katika sherehe ya kibao kata cha mwandishi wa magazeti ya Globalpublishers anayeitwa Imelda Mtema.
Katika tukio hilo mastaa kibao walihudhuria akiwemo Aunty Ezekiel ambaye kwasasa amekuwa karibu zaidi na Wema Sepetu. Nae Wema Sepetu kupitia Instagram ame-share picha hiyo hapo juu akiwa na kina Kajala na kuandika “nawapenda sana hawa hapa..jana hiyo kwa kibaokata cha Imelda Mtema”