Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts

Sunday, June 19, 2016

Jionee Mawaziri wa Sudan Kusini Wanavyovyaa

Kulia ni Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji huko Sudan Kusini bwana MABIOR GARANG (aliyevaa viatu vyeupe).

Katikati ni Waziri wa Ulinzi aliyevaa kandambili na utepe mwekundu begani,

Kushoto ni Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, aliyeshika kirungu nje ya ukumbi wa Bunge mjini Juba Sudan Kusini.

Monday, June 13, 2016

Aishi siku 555 bila moyo wake, akitumia moyo feki kwenye begi

Kwa wapita njia , kijana huyo mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa Michigan, alionekana ni mtu mzima akifurahia kuwapeleka watoto wake watatu katika park, akiwa na mdogo wake Dominique.
Kitu ambacho hakikuwa cha kawaida ni begi lake la kijivu alilolibeba mgongoni muda wote, ndilo lililokuwa likimuweka hai. Ndani ya begi hilo kulikuwa na mashine (power source) ya kusaidia kusukuma damu kwenye moyo huo feki kifuani kwake.
Moyo halisi wa Larkin ulitolewa kutoka mwilini mwake November 2014, na kuwekewa kifaa ambacho kilimuzesha kukaa nyumbani badala ya hospitali, wakati akisubiri kuwekewa moyo halisi wa binadamu.
Na hatimaye mwezi Mei mwaka huu, Larkin anaendelea vema baada ya kuwekewa moyo halisi wa binadamu katika kituo cha mishipa na moyo cha Frankel, katika chuo kiku cha Michigan, na kutarajiwa kurudi nyumbani kwake mapema ya wiki ijayo.
“Watu wengi wangeogopa kwenda muda mrefu na moyo feki, lakini nataka kuwaambia unatakiwa kwenda na woga, sikutaka kukubali upasuaji, ilinichukua wiki mbili kukubali, kwa sababu inasaidia, naenda nyumbani haraka baada ya upandikizaji, kwa sababu imenisaidia kuwa mwenye afya hata kabla ya upandikizaji”, alisema Larkin.
Kwa mujibu wa mtandao wa upandikizaji viungo (U.S. Organ Procurement and Transplantation Network), takwimu zinaonyesha kuna takriban wagonjwa 4,000 duniani, wanaosubiri kupandikizwa moyo wa binadamu.
Kijana huyo kutoka nchini Marekani alitoa wito kwa watu kujitolea viungo mbali mbali, ili kuweza kuokoa maisha ya watu wengine.
Imetafsiriwa kutoka CNN.
Mashine iliyokuwa ikimsaidia kusukuma moyo feki
Larkin akicheza mpira wa kikapu akiwa na begi lenye mashine inayomsaidia kusukuma moyo feki mgongoni mwake.

Rais Obama Atoa Amri kwa Bendera za Marekani Kupepea Nusu Mlingoti

Rais wa Marekani, Barack Obama ametoa amri kwa bendera za Marekani kupepea nusu mlingoti kwa heshima ya kuwakumbuka waathirika waliouwawa katika shambulizi baya la watu wengi kuliko yote katika historia ya Marekani.

Mtu mmoja mwenye silaha aliua watu wapatao 50 na kujeruhi 53 wengine ndani ya klabu ya usiku ambayo hutumiwa zaidi na mashoga huko Orlando Florida Jumapili alfajiri.

Obama alitangaza kuwa kicho ni kitendo cha kigaidi na kusema FBI wanaongoza uchunguzi. Amesema juhudi zote zinafanyika kujua nini kilimchochea muuaji huyo kufanya hivyo au kama alikuwa na ushirikiano wowote na makundi ya kigaidi.

Rais aliyekuwa amesikitishwa sana alilihutubia taifa lililopigwa na butwaa kutokea White House akisema ni rahisi kwa mtu kupata silaha kuwapiga watu mashuleni, makanisani, kwenye majumba ya sinema na klabu za usiku. 

Mwanasheria mkuu Loretta Lynch na waziri wa usalama wa ndani Jeh Johnson wote waliahirisha safari zao kwenda Beijing kwa mazungumzo juu ya usalama wa mitandao na maafisa wa China.

Thursday, May 5, 2016

Urusi Sasa Kujikita Tanzania, Yapanga Kujenga Mtambo wa Nyuklia Tanzania

Makampuni makubwa ya Viwanda na uzalishaji ya Kirusi ya "Russian Helicopters", "United Aircraft Corporation (UAC)" na "United Wagon Company (UWC)" yako tayari kuwekeza kwenye miradi ya viwanda nchini Tanzania.

Waziri wa viwanda wa Urusi amesema Urusi iko tayari kujenga nuclear reactor nchini Tanzania kwa ajili ya tafiti na kwa ajili ya mambo ya afya.

Huu ni mpango wa Urusi kufufua uhusiano wake na nchi za Afrika kwa upya tangu miaka ya 90 kwa kupitia mshirika wake wa zamani, Tanzania.

Sunday, May 1, 2016

Jipya kuhusu kifo cha Pamba Wemba, tazama huyu jamaa kwenye video anavyoihamisha kipaza sauti kinacho hisiwa kilikuwa na sumu.


Taarifa  ambazo zinazidi kuenea kwenye vyombo vya habari Congo na mitandao ya kijamii hata hapa Tanzania ni msiba wa Papa Wemba lakini sasa mjadala umehamia kwenye namna kifo chake

Kipande cha video kinachomuonesha jamaa akichukua mic halafu akairudisha kwenye stage na baada ya Pamba Wemba Kuanguka inadaiwa jamaa yuleyule badala ya kumsaidia alikimbilia mic ili isijulikane. Taarifa zinazoenea ni kwamba mic ile ilikuwa imewekewa sumu.

Hapa Mwanamuziki wa Congo anayeishi Tanzania, Papii Catalogue ameitafsiri video hiyo kwa lugha ya kiswahili, unaweza kuitazama……

PICHA 11 za Jengo la ghorofa 6 lililoporomoka na kuua watu 15 huko Nairobi Usiku wa Jana


Nairobi Nchini Kenya mvua zinazoendelea kunyesha wiki hii zimesababisha vifo ambapo mpaka sasa imeripotiwa watu 15 kufariki na kati ya hao 7 wamefariki baada ya jengo la ghorofa sita kuporomoka usiku wa April 29 2016 eneo la Huruma na zaidi ya watu 120 wameokolewa











Sunday, April 10, 2016

Mtu Aliyeambukiza Ukimwi Watu 200 Afungwa Miaka 25 Jela....


Daktari aliyewaambukiza wagonjwa 200 virusi vya ukimwi nchini Cambodia amehukumiwa jela.Daktari huyo bandia alipatikana na hatia ya kuwaambukiza takriban watu 200 virusi vya ugonjwa wa Ukimwi amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela kwa makosa yake.

Baadhi ya wahasiriwa wa makosa hayo wamekwisha fariki dunia, Yem Chrin alikuwa akitumia sindano zilizokuwa zimekwisha tumika kuwatibu wenyeji wa kijiji cha Roka bila ya kujua alickuwa akisambaza Virusi vya Ukimwi.Awali Chrin alikuwa ameshtakiwa kwa mauaji lakini upande wa mashtaka ukabadilisha shtaka na kuwa kuua bila ya kukusudia.

Kesi hiyo imefichua uhaba wa madaktari na ugumu ulioko kwa raia kupata huduma za afya katika maeneo mengi ya vijijini nchini Cambodia.

Utafiti umebaini kuwa zahanati nyingi katika maeneo ya vijijini huendeshwa na madakatari bandia ambao hawajahitimu kuwatibu wagonjwa.

Daraja La Kuunganisha Bara Afrika Na Asia Kujengwa

Rais Sisi na mfalme Salma wa Saudia
Mfalme wa saudia ametangaza kwamba daraja linalounganisha taifa hilo na Misri litajengwa juu ya bahari ya shamu.
Mfalme Salman alisema katika taarifa kwamba daraja hilo litaimarisha biashara kati ya mataifa hayo mawili.
Alitoa tanagazo hilo wakati wa siku ya pili ya ziara yake katika mji mkuu wa Cairo.Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi alisema kuwa daraja hilo litatajwa baada ya mfalme huyo wa saudia.
Rais Sisi ni mshirika wa karibu wa serikali ya Saudia.
''Tulikubaliana na ndugu yangu rais Abdul-Fattah al-Sisi tujenge daraja linalounganisha mataifa yetu mawili'',alisema mfalme huyo.
''Hii ni hatua ya kihistoria ya kuunganisha mabara ya Africa na Asia na itaimarisha biashara kati ya mabara haya mawili'',aliongezea.

Huyu Ndo Mwanafunzi Wa Kiume Anayepata ''Hedhi''

George na Amber May Ellis
George Fellowes ni mwanafunzi wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 22 na anaamni kwamba hata yeye hupatwa na ''hedhi ya kiume''.
Anasema kuwa ni rafiki wa karibu wa Amber May Ellis jirani yake na hivyobasi hupata uchungu wa hedhi kila mwezi rafikiye anapopata hedhi.
Uchungu huo anasema huwa mkali hadi kulazimika kuchukua likizo ya kuwa mgonjwa.Akizungumza na Newsbeat,George anaelezea:Nadhani ni swala la kifikra kwa sababu sisi ni marafiki wa karibu sana na tuna hisia sawa.
Katika kipindi cha miaka mitatu iliopita anasema kuwa amekuwa akipata uchungu wa hedhi na ishara hizo ni sawa na zile za wanawake.
Ninapata uchungu chini ya tumbo langu pamoja na katika kinena.Huwa nahisi vibaya na kuwa na hasira na marafiki wangu wengi.Pia huwa na hisia zenye mhemuko.
''Huwa sipendi kulia wakati huo lakini huwa na hasira nyingi.Kuna kitu kimoja kisichomuathiri George hatahivyo.
Sidhani kwamba wanaume wanaweza kupata hedhi bila kutokwa na damu'',anasema.
''Wakati unapokuwa rafiki wa karibu na mtu nadhani homoni zenu hufanana''.
Image captionGeorge na Amber May Ellis
George anaelezea kwamba wakati alipoanza kupata uchungu miaka mitatu iliopita alitaka ushauri wa daktari wake.
Lakini hakukuwa na maelezo hivyobasi alipewa dawa za kumaliza maumivu ya kinena.

Korea Kaskazini Yaujaribu Mtambo Wake Wa Makombora

Kim Jong-un
Korea Kaskazini imesema kuwa imefanikiwa kufanya majaribio ya mtambo wake mpya, ambao unaweza kurusha makombora kutoka bara moja hadi jiingine, katika juhudi za kuimarisha uwezo wake wa kufanya mashambulio dhidi ya Marekani.
Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vinasema kuwa zoezi hilo liliongozwa na kiongozi wa taifa hilo Kim Jong-un.
Jaribio hilo ni katika harakati za hivi karibuni za utawala wa Pyongyang wa kuunda zana za nuklia tangu ilipofanya jaribio lake la nne la makombora ya nuklia January mwaka huu.
Hatua hiyo iliiushurutisha Umoja wa Mataifa kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo vipya.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imetoa wito kwa utawala wa Pyongyang kujiepusha na vitendo vyake vya uchochezi.

Friday, April 8, 2016

Mbwa Anunuliwa Miwani, Viatu Na Headphone

scooby
MBWA mwenye umri wa miaka saba anayeitwa Scooby ni miongoni mwa mbwa 35 maarufu wanaotumiwa na Jeshi la Ulinzi la Uingereza amenunuliwa vifaa malum vya kumkinga hasa awapo kazini.
Private Megan Cropper, 20, with Scooby the Military Working Dog, who is equipped with his own PPE, to keep him safe in the harsh environment of the Jordanian desert. The British Army is currently staging its biggest overseas military training exercise in more than 15 years. See SWNS story SWMUTTS; One of the British Army's oldest working dogs has donned goggles and boots for the largest military exercise in a DECADE - as it trains to support our troops on the front line. Seven-year-old Scooby the springer spaniel is one of 35 hero working dogs currently taking part in Exercise Shamal Storm, the biggest military training exercise in a decade. The clever canine, who has been working for five years, completed a tour of Afghanistan in 2012 as a search dog, who is trained to sniff out explosives in vehicles and luggage. Alongside 1,600 soldiers and 314 vehicles, Scooby has gathered with his handler, Private Megan Cropper, in Jordan for a three-month training exercise. It is to test whether the Armed Forces could successfully mobilise in the event of a full-scale operation.
Scoobyamenunuliwa miwani maalum ambayo itamsaidia kuzia vumbi kuingia machoni, viatu maalum kuzui miba na vitu vingine vinavoweza kumletea madhara awapo kazini pamoja  headphone maalum kwa ajiri ya kunasa sauti mbalimbali zikiwemo za wahalifu na waongozaji wake.
Private Megan Cropper, 20, with Scooby the Military Working Dog, who is equipped with his own PPE, to keep him safe in the harsh environment of the Jordanian desert. The British Army is currently staging its biggest overseas military training exercise in more than 15 years. See SWNS story SWMUTTS; One of the British Army's oldest working dogs has donned goggles and boots for the largest military exercise in a DECADE - as it trains to support our troops on the front line. Seven-year-old Scooby the springer spaniel is one of 35 hero working dogs currently taking part in Exercise Shamal Storm, the biggest military training exercise in a decade. The clever canine, who has been working for five years, completed a tour of Afghanistan in 2012 as a search dog, who is trained to sniff out explosives in vehicles and luggage. Alongside 1,600 soldiers and 314 vehicles, Scooby has gathered with his handler, Private Megan Cropper, in Jordan for a three-month training exercise. It is to test whether the Armed Forces could successfully mobilise in the event of a full-scale operation.
Scooby ni miongoni mwa mbwa wakongwe kwenye kambi ya Jeshi ya Jeshi kikosi maalum cha mbwa (105 Military Working Dog Squadron). Amefanya kazi kwa miaka mitano tangu 2012 kwenye mapigano ya Afghanistan. Kazi yake kubwa ni ukaguzi wa mizigo, vyombo vya moto na kunusa ili kutambua kama kwenye kuna madawa ya kulevya.
Private Megan Cropper, 20, with Scooby the Military Working Dog, who is equipped with his own PPE, to keep him safe in the harsh environment of the Jordanian desert. The British Army is currently staging its biggest overseas military training exercise in more than 15 years. See SWNS story SWMUTTS; One of the British Army's oldest working dogs has donned goggles and boots for the largest military exercise in a DECADE - as it trains to support our troops on the front line. Seven-year-old Scooby the springer spaniel is one of 35 hero working dogs currently taking part in Exercise Shamal Storm, the biggest military training exercise in a decade. The clever canine, who has been working for five years, completed a tour of Afghanistan in 2012 as a search dog, who is trained to sniff out explosives in vehicles and luggage. Alongside 1,600 soldiers and 314 vehicles, Scooby has gathered with his handler, Private Megan Cropper, in Jordan for a three-month training exercise. It is to test whether the Armed Forces could successfully mobilise in the event of a full-scale operation.
Vifaa hivyo vitamsaidia wakati wa mafunzo maalum ya miezi mitatu nchini humo. “Mbwa huyo hang’ati hovyo. Amefundishwa vizuri na amezoea mazingira hasa ya kazi.” Alisema Steve Hood ambaye ni mkufunzi wa mbwa huyo.

Nyani Apandikizwa Moyo Wa Nguruwe

160406115349_k_h_fungscience_photo_library_512x288_khfungsciencephotolibrary_nocreditMoyo wa Nguruwe.
Maryland, Marekani
WANASAYANSI kutoka Taasisi ya Kitaifa ya Moyo, Mapafu na Damu huko Maryland nchiniMarekani wanasema kuwa wamefanikiwa kuweka moyo wa nguruwe katika nyani kwa zaidi ya miaka miwili.
Matokeo yake yanaweza kupiga hatua katika tiba ya upandikizaji wa viungo vya wanyama katika binaadamu huku kukiwa kuna upungufu wa binadamu wanaotoa viungo vyao.
mbegu-bora-kabisa-ya-land-race-ukifanya-mchezo-jamaa-kitunzwa-vizuri-anaweza-kufikisha-hata-kilo-250Nguruwe.
Upandikazi wa viumbe tofauti husababisha mmenyuko wa kinga na kusababisha kukataliwa kwa kiungo hicho na mwili unaofanyiwa upasuaji huo.
Lakini wanasayansi kutoka Marekani na Ujerumani walitumia muundo wa jeni pamoja na dawa zinazopunguza kinga. Kazi yao imeelezea katika jarida la mawasiliano ya kiasilia.
1Nyani.
Ni muhimu kwa sababu inaleta uwezekano wa kutumia viungo hivyo kwa binaadamu, kulingana na mwandishi mwenza Muhammad Mohiuddin kutoka Maryland, alikiambia chombo cha habari cha AFP.
Upandikizaji wa kutumia viumbe tofauti unaweza kuokoa maisha ya wengi kila mwaka ambayo hupotezwa kutokana na ukosefu wa viungo vya binaadamu kwa upandikizaji.
CHANZO NA BBC SWAHILI

Wednesday, April 6, 2016

Mila Za Kufukua Maiti, Kuziosha Na Kuzivisha Nguo Mpya Indonesia

1
Mkazi wa Toraja, Sulawesi Kusini, nchini Indonesia akiwavisha nguo ndugu zake waliokufa siku za nyuma.
UNAWEZA usiamini! Huko Toraja, Sulawesi Kusini, nchini Indonesia, wakazi wa huko wana mila ambayo kuna wakati wanawafukua ndugu zao waliokufa – wakiwemo watoto wadogo – wakawaosha, wakawafanyia kila usafi na kuwavisha nguo mpya za kuvutia.
2
Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo ambao husema wafu hao huendelea kuishi katika mioyo na akili zao, wanadai marehemu hao huendelea kutembea maeneo mbalimbali duniani wakiwa kama misukule au mizimu.
8
Wakati wa utaratibu huo ambao unajulikana kama Ma’nene, maiti hao hubebwa kutoka sehemu walizofia au kuzikwa na baada ya kufanyiwa mchakato huo wa kijadi, hutembezwa maeneo mbalimbali ya Jimbo la Sulawesi wakiwa katika mstari mmoja.
7
Baada ya utamaduni huo, maiti hao hurejeshwa katika majeneza ambayo hukarabatiwa ikiwa yameharibika wakati wa kuwatoa maiti au majeneza mapya hununuliwa kwa ajili ya kuwahifadhi tena.
5
Utaratibu huo wa Ma’nene ambao humaanisha ‘Sherehe ya Kuwasafisha Maiti’, hufanywa na watu wa Toraja kwa imani ya kuzirudisha roho za wafu katika vijiji vyao.
4
Hivyo, iwapo mtu alifariki akiwa safarini, familia huwajibika kwenda mahali alikofia na kumsindikiza kurejea nyumbani kwa kumtembeza hadi kijijini.
3
Katika siku za nyuma, watu wa eneo hilo walikuwa wanaogopa kusafiri mbali, wakiogopa kwamba pindi wakifia huko wasingeweza kurejea vijijini kwao.
6

Tuesday, April 5, 2016

Mahakama ya ICC yafuta kesi dhidi ya makamu wa rais wa Kenya William Ruto na Mwandishi wa Habari


Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) iliyoko The Hague nchini Uholanzi imefuta kesi dhidi ya Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto na mwandishi wa habari Joshua Arap Sang waliokuwa wakituhumiwa kuhusika katika vurugu na mauaji ya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Majaji wa ICC wameeleza kuwa wameamua kuiondoa kesi hiyo baada ya kuwepo kwa mkanganyiko katika ushahidi uliofikishwa mahakamani. 

Baadhi ya mashahidi walianza kubadili ushahidi wao huku wengine wakijiondoa kwa madai kuwa walishinikizwa au kushawishiwa kutoa ushahidi huo.

Katika uamuzi wao, majaji hao wameeleza kuwa kuondolewa kwa kesi hiyo hakuwazuii wawili hao kushtakiwa tena kwenye mahakama hiyo au mahakama nyingine ya kimataifa na kitaifa.

Uamuzi huo wa ICC umepokelewa kwa hisia tofauti nchini humo. Wapo walioufurahia na kueleza kuwa kesi hiyo ilijaa mihemko ya kisiasa zaidi na kwamba kwa kuachiwa huru Ruto atakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuendelea kuwatumikia wananchi wake kwa umakini zaidi. 

Lakini wapo wanaolalamikia uamuzi huo wakiwaangazia hasa wahanga wa machafuko hayo yaliyopelekea mauaji ya zaidi ya watu 1000 na kuwakosesha makazi maelfu ya raia.

Waathirika wa tukio hilo wanaonekana kuwa katika hali ya sintofahamu zaidi kwani uamuzi wa mahakama hiyo haukufikia hatua ya kuweza kubainisha iwapo Ruto na Sang walikuwa na hatia.

Nyota Wa Filamu Za Ngono Marekani Afariki

ry544
Amber Rayne enzi za uhai wake. 
ALIYEKUWA nyota wa filamu za ngono, Amber Rayne amefariki dunia nyumbani kwake mjini Los Angeles nchini Marekani maofisa wamethibitisha.
Marafiki na waliokuwa wafanyakazi wenzake walituma ujumbe katika mtandao wa Twitter wakimuenzi mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 31 ambaye alifariki akiwa usingizi wikendi iliopita.
amber_rayne
Amber Rayne.
Amber Rayne ambaye jina lake rasmi ni Meghan Wren alikuwa nyota wa filamu za ngono kwa muongo mmoja kabla ya kujiuzulu mwaka 2015.
Mkaguzi wa matibabu katika Kaunti ya Los Angeles ameiambia Newsbeat kwamba hakuna sababu rasmi ya kifo chake iliyothibitishwa. Hata hivyo wamesema kuwa familia yake imearifiwa.

Besigye Atiwa Kizuizini tena azuiwa kuingia Kampala

 Besigye amekuwa akizuiliwa na polisi nyumbani kwake

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye amezuiwa na maafisa wa polisi kuingia mji mkuu wa nchi hiyo Kampala.

Polisi wamemzuia alipokuwa katika makutano ya barabara za Mulago na Wandegeya karibu sana kuingia mji huo.

Wafuasi wake walikuwa wamekusanyika na polisi wametumwa kwa wingi eneo hilo.
Mwandishi wa BBC aliyeko Kampala Patience Atuhaire anasema polisi wamezuia watu kufuata gari la kiongozi huyo.

Gari ya Bw Besigye limebururwa na gari la polisi na kuelekezwa kituo cha polisi cha barabara ya Kira.

Maafisa wa polisi walikuwa wamesema Bw Besigye alikuwa na ruhusa kuingia mjini na kuhudhuria mkutano wa maombi katika makao makuu ya chama chake cha FDC kwa sharti kuwa asitatize shughuli mjini.

Bw Besigye amekuwa akizuiliwa nyumbani kwake Kisangati, viungani mwa mji wa Kampala, tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini humo Februari.

Mkuu wa polisi Kalekezi Kayihura aliagiza maafisa wa polisi waondoke nyumbani kwa Bw Besigye Ijumaa iliyopita.

Ndege Zagongana Na Kuwaka Moto, Jakarta – Indonesia

airplane (2)Ndege ya kubeba abiria ya Shirika la Batik Air
Jakarta – Indonesia
UWANJA wa ndege wa mji wa Jakarta nchini Indonesia umefungwa kwa muda baada ya ndege mbili kugongana.
Ndege ya kubeba abiria ya Shirika la Batik Air ambayo ni Air Boeing 737-800, yenye namba za usajili PK-LBS na namba ya safari 7703 kutoka Jakarta Halim Perdanakusuma kwenda Ujung Padang (Indonesia) ikiwa na abiria 49 na stafu 7 wakati ikipaa, ubawa wake uligonga sehemu ya nyuma ya ndege ya Shirika la TransNusa yenye namba za usajili PK-TNJ iliyokuwa ikibururwa kwenye njia ya kutumiwa na ndege kupaa au kutua.
batik_b738_pk-lbs_jakarta_160404_2
Ndege ya kubeba abiria ya Shirika la Batik Air iliyopata ajali.
Ubawa wa ndege hiyo iliyokuwa ikipaa uliwaka moto.
Maafisa wanasema hakuna aliyejeruhiwa wakati wa ajali hiyo iliyotokea Jumatatu usiku.
Abiria wote waliondolewa salama hakuna majeruhi wala vifo vilivyoripotiwa kutrokea kutokana na ajali hiyo.
Kisa hicho kilitokea katika uwanja wa ndege wa Halim Perdanakusuma mjini Jakarta ambao sana hutumiwa kwa safari za ndege za ndani ya nchi.
transnusa_at42_pk-tnj_jakarta_160404_1
Ndege ya Shirika la TransNusa iliyopata ajali.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, ndege hiyo ya Batik Air ilikuwa na watu 49, abiria pamoja na marubani.
Msemaji wa kampuni ya Lion Air Group, inayomiliki Batik Air ameambia mashirika ya habari ya kimataifa kwamba rubani amekatiza safari baada ya ajali hiyo na abiria wako salama.
Maafisa wa wizara ya uchukuzi ya Indonesia wamesema ndege hizo ziliharibiwa wakati wa kisa hicho. Video iliyopakiwa mtandaoni inaonesha miali ya moto ikitoka kwenye ubawa wa ndege ya Batik Air.
Indonesia ina historia mbaya ya usalama wa ndege licha ya kuendelea kufana na uchukuzi wa ndege hasa ndege za kubeba abiria za bei nafuu.
transnusa_at42_pk-tnj_jakarta_160404_map
Ramani kuonesha eneo la tukio ambapo ndege hizo zimegongana.
Mwaka 2013, ndege ya Lion Air ilipita njia ya uwanja wa ndege wa Denpasar, Bali na kutumbukia baharini. Watu 22 walijeruhiwa.
Mwaka uo huo, ndege nyingine ya Lion Air iliteleza ikitua kisiwa cha Sulawesi na kugonga ng’ombe.
Mwaka 2014, ndege ya kampuni ya AirAsia nchini Indonesia iliyokuwa safarini kutoka Surabaya hadi Singapore ilianguka baharini na kuua watu wote 162 waliokuwa ndani.