Showing posts with label TECHNOLOGY. Show all posts
Showing posts with label TECHNOLOGY. Show all posts

Sunday, June 19, 2016

Baada ya TCRA Kuzima Simu Feki, Wafanyabiashara Wamepata Soko Jipya la Simu Hizo


Moja ya habari iliyoripotiwa ni hii kutoka gazeti la Mwananchi, yenye kichwa cha habari ‘simu bandia zapata soko Msumbiji, Congo’.

Gazeti hilo limeripoti kuwa Siku mbili baada ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzima simu feki, wafanyabiashara wa simu hizo wamepata soko jipya katika nchi za Msumbiji na Congo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hilo, baadhi ya vijana waliokutwa wakizunguka madukani kuzikusanya, walisema wanazinunua na kuzisafirisha kwenda huko kwa ajili ya kuziuza kwa watumiaji. Walisema katika nchi hizo kuna soko kwa sababu zinakamata mawasiliano kama kawaida.

Gazeti hilo limemnukuu Lawrence Kyondo ambapo amesema wanazinunua kwa bei ya makubaliano na kwenda kuziuza katika soko la nje……….>>>’hatujaanza hii biashara leo, siku nyingi isipokuwa wenye maduka walikuwa bado wagumu kuziuza wakidhani hazitazimwa’

Monday, June 13, 2016

Aishi siku 555 bila moyo wake, akitumia moyo feki kwenye begi

Kwa wapita njia , kijana huyo mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa Michigan, alionekana ni mtu mzima akifurahia kuwapeleka watoto wake watatu katika park, akiwa na mdogo wake Dominique.
Kitu ambacho hakikuwa cha kawaida ni begi lake la kijivu alilolibeba mgongoni muda wote, ndilo lililokuwa likimuweka hai. Ndani ya begi hilo kulikuwa na mashine (power source) ya kusaidia kusukuma damu kwenye moyo huo feki kifuani kwake.
Moyo halisi wa Larkin ulitolewa kutoka mwilini mwake November 2014, na kuwekewa kifaa ambacho kilimuzesha kukaa nyumbani badala ya hospitali, wakati akisubiri kuwekewa moyo halisi wa binadamu.
Na hatimaye mwezi Mei mwaka huu, Larkin anaendelea vema baada ya kuwekewa moyo halisi wa binadamu katika kituo cha mishipa na moyo cha Frankel, katika chuo kiku cha Michigan, na kutarajiwa kurudi nyumbani kwake mapema ya wiki ijayo.
“Watu wengi wangeogopa kwenda muda mrefu na moyo feki, lakini nataka kuwaambia unatakiwa kwenda na woga, sikutaka kukubali upasuaji, ilinichukua wiki mbili kukubali, kwa sababu inasaidia, naenda nyumbani haraka baada ya upandikizaji, kwa sababu imenisaidia kuwa mwenye afya hata kabla ya upandikizaji”, alisema Larkin.
Kwa mujibu wa mtandao wa upandikizaji viungo (U.S. Organ Procurement and Transplantation Network), takwimu zinaonyesha kuna takriban wagonjwa 4,000 duniani, wanaosubiri kupandikizwa moyo wa binadamu.
Kijana huyo kutoka nchini Marekani alitoa wito kwa watu kujitolea viungo mbali mbali, ili kuweza kuokoa maisha ya watu wengine.
Imetafsiriwa kutoka CNN.
Mashine iliyokuwa ikimsaidia kusukuma moyo feki
Larkin akicheza mpira wa kikapu akiwa na begi lenye mashine inayomsaidia kusukuma moyo feki mgongoni mwake.

Saturday, June 4, 2016

Madhara ya Zoezi la Uzimaji Simu feki Sasa Dhahiri

Madhara ya zoezi la uzimaji wa simu bandia litakalofanywa na Mamlaka ya Mawasiliano TCRA ifikapo Juni 16 mwaka huu yameanza kuonekana kwa wafanyabiashara wa simu eneo la Kariakoo ambao baadhi yao wamefilisika na kuanza kufunga biashara zao. 
Wakizungumza na EATV iliyotembelea eneo hilo hii leo, wafanyabiashara hao wamesema kadri siku zinavyozidi kwenda wateja wamekuwa wakipungua kwa kasi huku wengi wakiacha kununua simu hadi lipite zoezi hilo wakiamini kwamba simu zitakazokwepo baada ya muda huo ndio zitakuwa simu halisi.
 
"Hili zoezi kwa kweli limesababisha baadhi yetu tufilisike kabisa...kama mimi hapa sina cha kuuza nimekula mtaji baada ya wateja kutofika dukani kwangu na sasa sina cha kuuza nimeamua kufunga duka nijaribu kufanya kitu kingine," amesema mmoja wa wafanyabiashara hao.
 
Wakiwa na nyuso zilizokata tamaa, wafanyabiashara hao wamesema kinachowaumiza sana ni mikopo waliyokopa kutoka taasisi za fedha ambayo wanatakiwa kuilipa kwa mujibu wa makubaliano waliyoingia na mabenki na taasisi husika za kifedha.
 
Aidha, katika kile walichokieleza kuwa ni madhara ya kisaikolojia; wafanyabiashara hao wameitaka TCRA kutobadilisha tarehe ya utekelezwaji wa zoezi hilo ili kurejesha imani kwa wateja kwani licha ya biashara ya simu, uchangamfu wa biashara katika eneo zima la Kariakoo hivi sasa umepungua.
 
"Kwa jinsi hali ilivyo sasa tunatamani hilo zoezi la kuzima simu bandia litekelezwe haraka sana kwani tumekuwa tukiathirika kisaikolojia kwani kwa upande mmoja unaambiwa simu unazouza ni feki wakati sio kweli lakini wakati huo huo hata hizo simu halisi unazouza wateja wanaogopa kununua...sasa ni bora mbivu na mbichi zijulikane mapema," amesema mfanyabiashara Andrew Mashauri.

Thursday, May 5, 2016

Mitandao yaharibu soko la magazeti, takwimu zaonyesha magazeti yanapitwa na wasomaji wa mitandao


Vyombo vya habari vya asilia hususani magazeti vinakufa. Hivi sasa vvyombo hivyo vinajikongoja kutokana na mauzo hafifu  na mdororo wa mapato kutoka matangazo na kupunguza wafanyakazi.

Ila wakati idadi ya wasomaji wa habari mtandaoni ikizidi kukua, wanaoperuzi mtandaoni  humo hawatumii muda mwingi kwenye magazeti tando, utafiti wa Pew Research Centre unaeleza. 

Katika utafiti wake wa hali ya vyombo vya habari 2015 (“State of the News Media 2015,”) imeonesha kwamba katika vyombo vya habari vya karatasi (print media), Digitali na TV, imeonesha Dhahiri kwamba magazeti yanaelekea kuzimu.

Utafiti huo umetolea mfano magazeti makubwa ambapo wasomaji wake wa mtandaoni wamewashinda kwa mbali kwa idadi ya wasomaji wa makaratasini, ambapo gazeti kubwa sana la New York Times la Marekani limetangaza kuwa nakala zake zipatazo 650,000 kwa wiki zimepitwa kwa mbali sana na wa mitandaoni
Hivi sasa kuna mjadala mitandaoni endapo kama Tanzania iko ama itafika huko. Mabishano ni makali ambapo wa makaratasini wanashikilia msimamo wao kuwa nchini hapa tasni ya habari mtandaoni bado ni change sana kuweza kutishia amani ya magazeti.

Upande wa digitali unajibu kwamba endapo kama kuna wahariri viburi wanaobeza kasi ya mitandao, basi wakae mkao wa kulala njaa muda si mrefu ujao, maana ni wachache wanaoendelea kupata habari kwa njia asili ya magazeti.

Upande wa digitali umeyasifia magazeti ya Global Publishers na la Mwananchi  anbayo ni dhahiri yana wahariri wanaokwenda na wakati na wanaojua nini wanachokifanya kwa kuanza na mapema kuogelea bahari ya maendeleo ya tasnia kwa vitendo kwa kuwa na vitengo vya mtandao vinavyopelekesha mbio magazeti yanayobeza technolojia hio kwa kubuni.

“Ni kweli kwamba Tanzania  bado sana kiteknolojia na miundombini kiasi cha habari za mtandaoni zikatishia uhai wa habari za makaratasini, lakini si uongo kwamba ukizingatia uharaka na gharama pamoja na kwenda na wakati muda si mrefu print media itakwenda na maji”,amesema blogger mmoja ambaye pia ni mwanahabari kwenye moja ya magazeti makubwa nchini.

Sunday, April 10, 2016

Hizi ni Simu zitakazokosa Huduma ya Whatsapp...

Huduma ya WhatsApp haitatumika tena katika simu zinazotumia mifumo kadha ya programu ikiwemo Blackberry 10, Nokia Symbian S60 na Windows Phone 7.1.

Kampuni ya Facebook inayomiliki huduma hiyo imesema inataka kuangazia kustawisha “huduma katika mifumo inayotumiwa na watu wengi.”

WhatsApp, itaacha kufanya kazi katika mifumo hiyo ya programu kufikia Desemba 2016. Licha ya kuacha kutumika katika simu nyingi za Blackberry, WhatsApp bado itaendelea kutumiwa katika simu za kisasa zaidi za Blackberry kwa sababu simu hizo hutumia mfumo wa Android.

Kampuni hiyo imejitetea na kusema kwamba haijawatupa wateja wake ambao wamechangia sana katika ufanisi wake lakini ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia.

“Simu hizi hazina uwezo wa kiteknolojia tunaohitaji kuendelea kuimarisha huduma yetu siku zijazo,” kampuni hiyo imesema.



Orodha kamili ya mifumo ya simu ambayo wateja hawataweza tena kutumia WhatsApp ni hii hapa:
Android 2.1 and Android 2.2

Blackberry OS 7 and earlier

Blackberry 10

Nokia S40

Nokia Symbian S60

Windows Phone 7.1

Kampuni hiyo imesema wakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp mwaka 2009, asilimia 70 ya simu wakati huo zilikuwa za BlackBerry na Nokia.”

Lakini sasa asilimia 99.5 ya simu zinatumia mifumo ya Google, Apple na Microsoft.

Source: BBC

Wednesday, April 6, 2016

Je, Umeinyaka Hii Huduma Mpya Kutoka Whatsapp?

mg_whatsapp_code_comp
BAADHI ya watumiaji wa Whatsapp wameingiwa na hofu leo baada ya kukuta ujumbe kwenye simu zao wenye maneno ya njano yakielezea huduma itakayokuwa ikitumika kulinda mawasiliano ya App hiyo baina ya mtumaji na mpokeaji wa ujumbe.
Huduma hiyo kwa kitaalam wanaita ‘end-to-end encryption’ ambapo voice calling, chating za group kwenye simu zote za iOS na Android zitakuwa na uwezo wa kutumia huduma hiyo.
UJUMBE WENYEWE HUU HAPA
messages
Hii inamaanisha serikali ama mtu yeyote itakuwa vigumu kusoma meseji zako labda umpatie simu yako na password. Kwa Ujumla hata WhatsApp wenyewe hawatakuwa na uwezo wa kuzisoma meseji za mtu. Ni mtumaji na mpokeaji wa meseji tu ndiyo watakuwa na uwezo wa kuona mejesi waliotumiana wala sio mtu mwingine katikakati.
WhatsApp wamesema, ‘Kuanzia sasa kama wewe na watumiaji wengine wa WhatsApp uliosevu namba zao watatumia toleo jipya la App hiyo (latest version), kila simu utakayopiga/pigiwa, meseji, chating za grupu, picha, video, faili na ujumbe wa sauti utakaotuma utakuwa umelindwa (secured) moja kwa moja kwa njia ya end-to-end encrypted.
‘Wazo ni jepesi tu hapa: ukituma ujumbe, mwenye uwezo ya kuona ujumbe huo ni yule uliyemtumia pekee, au grupu ambalo umetuma ujumbe wako. Hakuna mtu atauona ujumbe huo, sio wahalifu wa mitandao (cybercriminals), hackers wala serikali.

Ijue Mitandao 10 Maarufu Ya Kijamii Ya Kutafuta Wachumba

Tunatumia mtandao kila siku. Wengi wetu huchukua muda wao mwingi sana kuingia online na kuchat na marafiki, kupata habari, kudownload, kusoma udaku, kuangalia video nk. 
Well, wengine huingia online kutafuta mitandao ambayo ni spesheli ya kutangamana na kutafuta wachumba. Uzuri wa kutafuta wachumba kupitia mitandao ya kijamii ni kuwa una nafasi kubwa zaidi kuchagua mchumba ambaye anatabia ambayo unazipenda.
  

Leo kwa haraka nimeamua kuorodhesha mitandao bora zaidi ambayo ina umaarufu zaidi barani Afrika.

Mitandao ya kutafuta wachumba


1. Zoosk

Huu ni mtandao ambao wenyewe wanaupigia upato kuwa mtandao wa kutafuta wachumba unaoongoza kwa umaarufu bara la Afrika. Mtandao huu unaruhusu watumiaji kuweza kujamiiana na wenza katika mitaa unayoishi. Uzuri wa mtandao huu ni kuwa unatumia mashine inayoitwa Behavioral Matchmaking™ wenye uwezo wa kutambua mchumba atakaye kufaa zaidi kwa kutumia profile yako. Mtandao huu una watumiji zaidi ya milioni 25 duniani.



2. Tinder

Huu mi mtandao spesheli wa kutumia kitumizi. Mtandao huu ni rahisi kuutumia. Kile kinachohitajika hapa ni kusukuma upande wa kulia kupenda picha ya mtu ama kusukuma upande wa kushoto kutakaa picha ya mtu. Iwapo wewe na mwengine mumependezwa na picha zenu mtaorodheshwa kama wachumba wa kifani.



3. Lovoo

Huu ni mtandao ambao unauwezo wa kutafuta wachumba wanaoishi karibu na wewe. Watumiaji wa mtandao huu ni milioni 12, Mtandao huu hutumia teknolojia ya rada kuwatafuta wachumba walio karibu nawe.



4. Eskimi

Huu ni mtandao maarufu ambao una uwezo wa kuunganisha marafiki zako wa facebook ambao wako eskimi. Mtandao huu unakupa nafasi ya kuwaangalia na kutafuta wachumba kulingana na nchi, mikoa na miji tofauti tofauti.



5. SpeedDate

Huu ni mtandao unaokua kwa kasi zaidi. Ukiwa na watumiaji zaidi ya milioni 13, mtandao huu una uwezo wa kuwezesha kufanyika kwa deti kwa wakati uliopo na pia kuchat papo kwa hapo.



6. BeNaughty

Huu ni mtandao unaokuwezesha kutongoza, kujamiiana na kutangamana na wengine ambao wako single. Mtandao huu una uwezo wa kuwaorodhesha wanawake 100 wazuri zaidi hivyo kukupatia nafasi ya wewe kuchagua bila tatizo.



7. Tagged

Huu ni mtandao wenye watumiaji zaidi ya milioni 300. Mtandao huu unakupa nafasi ya kukutana na kipenzi chako kupitia kwa michezo ambayo inapatikana ndani yake.



8. Instadate

Mtandao huu ni maarufu zaidi nchini Liberia. Mtandao huu unakupa nafasi ya papo kwa hapo kuweza kuchat na watumiaji ambao wako single.



9. AYI – Are You Interested?

Huu ni mtandao wa watu wakubwa. Mtandao huu umeunganishwa na facebook ambapo unaweza kuangalia picha, kuapload picha, kulike na kujua nani yuko interested.



10. SayHi!

Huu mtandao unadai kuwa na uwezo wa kuwaunganisha wachumba wapweke kupata mapenzi, kuweza kutongoza, kuchat na pia kupata marafiki wapya. Jambo la kipekee kwa mtandao huu ni kuwa mtumiaji anaweza kutafuta mchumba kwa kuangalia ramani na pia kutafuta deti kwa sehemu za karibu unazoishi.

Saturday, April 2, 2016

EXCLUSIVE: Picha 5 Za Ujenzi Wa Kisasa Unaoendelea Uwanja Wa Ndege Dar, Jengo Jipya Litavyokuwa (Terminal 3 )

March 31 2016 millardayo.com ilipata kibali cha kupiga picha ujenzi unaoendelea wa kupanua uwanja na kujenga jengo jipya kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam, naambiwa huu uwanja unategemewa kukamilika December 2017 na sasa hivi ujenzi wa umekamilika kwa asilimia 60, uniachie na comment yako hapa chini baada ya kutazama hizi picha mtu wa nguvu
DSC_0232
Huu ni muonekano wake wa nje kwa sasa ujenzi ukiwa unaendelea
Dar es Salam exterior july 2013 0012
Ujenzi ukikamilika 2017 huu ndio utakuwa muonekano wake wa nje
DSC_0129
Muonekano wake kwa karibu sehemu watakapokuwa wanaingilia abiria wanaosafiri
Dar es Salam exterior july 2013 0013
Ujenzi ukikamilika 2017 huu ndio utakuwa muonekano wake wa nje
DSC_0136
Hii ni sehemu watakapokuwa wanakaa abiria, ujenzi unaendelea.
Dar es Salam interior july 2013 Concourse
Ujenzi ukikamilika patakuwa hivi sehemu wanapopumzikia abiria
Dar es Salam interior nov 20123 Checking Hall
Uwanja mpya pia utakuwa na ngazi za umeme na za kawaida ujenzi ukikamilika
Dar es Salam exterior july 2013 0014
Kutakuwa kuna madaraja ambapo ndege inaegeshwa halafu abiria wanashuka au kupanda moja kwa moja na sio kushuka kwenye ngazi zinazobebwa na magari kama zamani
DSC_0189
Hili ndio daraja ambapo ndege mbili zinaweza kupark ubavuni kwa mara moja kupandisha abiria au kushusha.
DSC_0170
Muonekano wa daraja hilo kwa ndani, abiria akiwa anasubiria kuelekea kwenye ndege.
Dar Es Salaam Ph2 high-rev
Ujenzi ukikamilika huu ndio utakuwa muonekano wa uwanja huo kwa juu
-millard ayo

Wednesday, March 30, 2016

Instagram Yafanya Mabadiliko Sasa Kuanza Kuonekana Hivi....Mastaa Wapatwa Na Wasiwasi

http://ichef-1.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2014/12/01/141201095350_instagram_logo_624x351_getty.jpg

Mabadiliko ya yaliomo katika mtandao wa instagram yamezua hisia kali miongoni mwa watumizi wake.

Mtandao huo una mpango wa kuweka ratiba ya mpangilio wa ujumbe hivyobasi kupanga machapisho kulingana na maslahi ya mtumiaji badala ya kuyapanga kulingana na mda.
Machapisho mengi ya watu maarufu ambao wana wasiwasi kwamba picha zao huenda zisionekane na watu wengi yamewataka wafuasi wao kufungua kitufe cha ujumbe.
Lakini Instagram imesema kuwa hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi.
''Tunasikiliza na tunawahakikishia kwamba hakuna mabadiliko yatakayofanyiwa machapisho yenu kwa sasa'',mtandao huo wa usambazaji picha ulisema katika ujumbe wake wa Twitter.
Hatua hiyo itauweka sawa mtandao huo na ule wa facebook ambao unamilikiwa na kampuni hiyo.
Kwa kufungua kitufe cha ujumbe,wafuasi wa watu hao maarufu watakuwa wakipata ujumbe kila wanapoweka machapisho yao.
Watu maarufu kama vile Kylie Jenner na mwanamitindo Cindy Crawford katika siku za hivi karibuni wamewataka mashabiki wao kufungua vitufe vyao vya ujumbe.

Monday, March 28, 2016

HIZI NDIZO SIMU ZITAKAZO ZIMWA NA TCRA


TCRA wametoa taarifa kwa umma miezi michache iliyopita juu ya kusudio la Mamlaka hiyo kusitisha matumizi ya simu bandia ifikapo mwezi Juni mwaka huu.

Ni hatua nzuri na ya kupongeza lakini kwa bahati mbaya,kwa mtazamo wangu,naona imetolewa tu kama "briefing" pasipo kuwa na msisitizo wa kutosha pengine kwasababu mwezi June bado ni mbali kitu ambacho si sahihi.

Ushauri:
Viongozi wa Mamlaka,ikiwa imebaki takribani miezi mitatu kutekeleza zoezi hili,nawashauri muongeze utoaji wa elimu na taarifa kwa umma juu ya zoezi hili na pia mtoe tahadhari kwa umma kuacha kuendelea kununua simu hizi bandia maana bila shaka bado ziko sokoni na huenda nyingine ziko kwenye meli zinakuja.

Cha kufanya:
Mamlaka kwa kushirikiana na makampuni ya simu,mnaweza mkaanda ujumbe mfupi wa maneno(sms) kuhusu zoezi hili ambao kila mtumiaji wa simu atalazimika kuupata ujumbe huo kwanza kabla hajaweza kuongeza salio kwenye simu yake au kabla ya kupata salio la simu yake pale mtumiaji atakapotaka kupata huduma hizo.

Pia,ujumbe huu ambao pia utamuelekeza mteja namna ya kugundua kama simu yake ni bandia au laa,unaweza pia kuja kama ujumbe wa awali pale mteja atakapotaka kutumia huduma za m-pesa,tigo pesa,airtel money,n.k.

Njia nyingine ni kuanzia sasa kutumia vyombo vya habari kueneza ujumbe huu na zaidi kutahadharisha umma kuacha kuendelea kununua simu hizi za bandia na pia ikibidi mshirikiane na Shirika la Viwango Nchini(TBS) kufanya ukaguzi wa kushitukiza katika maduka mbalimbali ya simu na kuchukua hatua kwa watakaokuwa wanaendelea kuuza simu hizi za bandia ila mjue nanyi hapa hamtakwepa lawama kwa kuacha simu hizi ziingizwe nchini.

Sababu za ushauri huu:
Muda uliobaki ni mchache na jambo hili linaonekana kutopewa uzito wa kutosha licha ya athari kubwa za kiuchumi na kijamii zitakazokuja kujitokeza hapo baadae endapo zoezi hili litatekelezwa kwa muda uliopangwa.

Ni wazi simu za bandia zilizoko katika matumizi ni nyingi kuliko simu original lakini ndio hizi hizi zinazotumika katika shughuli za kibiashara,kiuchumi na kijamii.

Kwa mfano,ukisitisha matumizi ya simu bandia,ni wazi utaathiri kwa kiasi kikubwa wale waliojiajiri kwa kufungua vibanda vya m-pesa,tigo pesa, n.k.

Hatari nyingine iwapo umma utakuwa kama umeshitukizwa katika utekelezaji wa zoezi hili,itakuwa ni kupanda kwa ghafla kwa bei za simu original due to sudden increase in demand baada ya simu bandia kuzuiwa.

Kwa mtazamo wangu,hapa patakuwa na athari ya ziada ambapo watu wengi kushindwa kumudu bei za simu original ambazo kwa kawaida huwa ziko juu ukiachilia mbali ongezeko la bei litakolotokana na ongezeka la mahitaji ya bidha hiyo(increase in demand).

Athari nyingine itakayotokana na kupanda kwa bei ni kuwafanya watu wengi washindwe kununua simu hizi kwa uharaka kufidia pengo litakalokuwa limejitokeza na hivyo kuchukua muda mrefu zaidi kwa hali kurejea katika hali ya kawaida.

Mbali na sababu hizo,TCRA kwa kuanza kutoa elimu hii mapema na kuhamasisha umma juu ya zoezi hili ,itakuwa imejivua lawama kwa kutimiza wajibu wake mapema kabisa maana watanzania wengi hungoja dakika za majeruhi kutekeleza wanayopaswa kuyafanya na hili kila mtu ni shahidi na tuna mifano mingi tu kama vile watu kujiandikisha dakika za mwisho kwenye daftari la mpiga kura,n.k.

Ni mtazamo na ni ushauri pia

Sunday, March 6, 2016

SAA ZINAZOWEZA KUTUMIWA KUIBA MITIHANI (CHABO).


Saa za kisasa ambazo zimetengenezwa mahususi kutumiwa kudanganya wakati wa mtihani zimekuwa zikiwakosesha usingizi walimu na wasimamizi wa mitihani.
 
Saa hizo zina uwezo wa kuweka akiba data na maelezo ambayo yanaweza kusomeka mtu anapofanya mtihani.
Aidha, zina kitufe cha dharura ambacho kinaweza kubadili uso wa saa hizo haraka sana na badala ya kuonesha habari ziwe zinaonesha uso wa kawaida wa saa.


Saa hizo zinatangazwa katika soko la kuuza bidhaa mtandaoni la Amazon.

Mojawapo ya aina ya saa hizo ina uwezo wa kuweka akiba data ya 4GB. Nyingine, ambayo itaanza kuuzwa baadaye mwaka huu, itakuwa na uwezo wa 8GB na inaweza kuhifadhi hata video.

Baadhi ya saa hizo, zina kifaa kidogo sana cha kusikizia ambacho hakitumii nyaya, jambo linalowezesha mtu kusikiliza kilichohifadhiwa kwenye saa hiyo bila kuonekana.

Tangazo moja katika mtandao wa Amazon linasema mtu anaweza kununua saa ya aina hiyo kwa $61 (£43).
Kuna pia matangazo ya saa hizo eBay.
Naibu mwalimu mkuu wa shule moja kutoka Bath, Uingereza anasema saa hizo zinaweza zikawashawishi wanafunzi kuhadaa katika mtihani.

Bw Joe Sidders wa shule ya Monkton Combe Senior School amesema ingawa saa hizo zinaweza kudhibitiwa kwa kutumia sheria zinazoharamisha simu na kompyuta kutoka vyumba vya mitihani, ni changamoto kubwa sana kwa watu wanaosimamia mitihani.

Amesema uuzaji wa saa hizo unafaa kudhibitiwa.
Kuna pia “kalamu za kuiba mtihani” ambazo zinaweza kuhifadhi habari na maelezo.


Ongezeko la matumizi ya saa kuiba yamefanya baadhi ya mashirika kupiga marufuku saa katika vyumba vya mitihani Uingereza.

Monday, February 15, 2016

Kabati la Nguo la Mmiliki wa Facebook Lashangaza Wengi.

Nilikuwa napita huku na huko katika mitandao,hatimaye nikakutana na maisha ya uvaaji wa nguo za mmiliki wa mtandao wa facebook MARK ZUCKEBERG.Huyu jamaa ametoa picha ya kabati la nguo zake,na kuelezea kuwa ndio kabati la nguo zake za kila siku azivaazo.

Mark anasema ili asipoteze akili nyingi kwa mkewe na kwake juu ya nini avae na ni nmana gani anatakiwa kuvaa,ameamua kuwa na nguo za aina moja katika kabati yake na kutoa "tender"(zabuni) kwa kampuni kumtengenezea aina hiyo ya nguo,pia ameamua kununua nyumba iliyo karibu kabisa na Makao Makuu ya Facebook ili asiwe anatumia usafiri wa aina yoyote zaidi ya kutembea toka nyumbani mpaka ofisini.


Ukifuatilia hata katika makongamano yake na mihadhara ya kitaaluma ktk vyuo na maeneo mbalimbali unaweza dhania kuwa Mark huwa habadilishi nguo,kumbe ana kabati lililojaa nguo za aina moja