Showing posts with label Bongomovie. Show all posts
Showing posts with label Bongomovie. Show all posts

Monday, June 13, 2016

Exclusive: Wastara Juma Anasa Ujauzito.......

Exclusive! Habari mpya ya motomoto ni kwamba, staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma amenasa ujauzito, Risasi Jumamosi linakuwa la kwanza kukupa mchapo huu!
Ujauzito huo ni wa aliyekuwa mumewe, Sadifa Juma, mbunge wa Jimbo la Donge, Visiwani Zanzibar ambapo kitendo cha mimba hiyo kuwa ya mbunge, kimemsumbua Wastara hadi kuamua kuondoka ili akapate muda mzuri wa kutafakari nchini Msumbiji.

Taarifa kutoka kwa vyanzo, zinaeleza kuwa Wastara alipoondoka nchini, aliwaaga baadhi ya mastaa wenzake kuwa anakwenda kufuata biashara zake za nguo nchini humo lakini Risasi Jumamosi lilichimba na kupata ubuyu ulionyooka kuwa aliondoka nchini kwa ajili ya kwenda kutafakari ujauzito huo.

NDUGU AVUJISHA UBUYU KAMILI
Ndugu wa karibu na Wastara ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazeti, amefunguka kuwa baada ya Wastara kuachika, aligundua ni mjamzito hivyo alichanganyikiwa na kuamua kwenda Msumbiji kwa ajili ya kutafakari zaidi ujauzito huo.
“Hakuwa na jinsi kwani akiangalia alishatoka kwa mwanaume, angewezaje kumwambia kuwa ana ujauzito wake? Akaamua kukimbilia huko kwa ajili ya kujipanga ingawa anavyoonekana anatamani amzalie mbunge huyo,” alisema ndugu huyo.

NDUGU AZIDI KUTIRIRIKA
Ndugu huyo alizidi kushusha ‘vesi’ kuwa mimba ya Wastara inasadikiwa kuwa na miezi miwili au mitatu kwani tangu aachane na mumewe huyo, alikuwa akiumwaumwa na wakati mwingine alikuwa akitapika hovyo ambapo mwanzo alificha lakini yalipomfika shingoni alifunguka.
“Alitufichaficha lakini baadaye akawa hana jinsi, akaona atueleze na sisi tumemshauri tu aende akapumzike na ajiandae kutuletea kiumbe kipya,” alisema ndugu huyo.
Baada ya habari hiyo kutua Risasi Jumamosi,  Wastara alitafutwa kwa njia ya simu ya mkononi, akafunguka:

“Dah! Sijui niseme nini, kiukweli watu wanaongea sana, nimeondoka nchini kwa shughuli zangu binafsi lakini maneno ni mengi, wewe si wa kwanza kunipigia simu. Sikutaka kuongea kabisa juu ya masuala yangu ya ndoa iliyopita wala maisha yangu kwa jumla.”

Risasi Jumamosi: Kwa nini unaongea hivyo wewe funguka swali nililokuuliza, una ujauzito au la?
Wastara: Ndiyo, kwani cha ajabu ni nini? Yule niliyekuwa nalala naye si shangazi yangu, kila mtu anajua niliolewa na aliyenioa (Sadifa) wala si mjomba wangu.

TUJIKUMBUSHE
Wastara aliachika Aprili, mwaka huu baada ya kufunga ndoa na Mbunge wa Jimbo la Donge, Sadifa Juma ambapo ndoa yao ilidumu kwa muda kwa miezi mitatu tu na kuvunjika.

GPL

Saturday, April 16, 2016

Rammy Achukia Kuitwa Kanumba Feki

gallll
Rammy Gallis
MAMBO vipi mpenzi msomaji wangu, kama ilivyo kawaida yetu ni kukupa wewe msomaji kitu roho inapenda kwa kuwa tunajua unapenda kujua maisha halisi ya mastaa wetu wa hapa Bongo.
Leo aliyetupendezeshea ukurasa wetu ni muigizaji anayefananishwa na marehemu Steven Kanumba, Rammy Gallis anayeishi maeneo ya Chang’ombe jijini Dar.
Ili kujua maisha yake halisi, twende pamoja chini:
Anapenda kufanya NINI akiamka asubuhi?
“Kitu cha kwanza kabisa napenda kufanya usafi wa mwili wangu na kukiweka kitanda nilicholalia katika hali ya usafi na kufanya mazoezi kwa ajili ya kuupa mwili nguvu na kuendelea na vitu vingine.”
Anapenda kufungua kinywa na nini? Mlo wa mchana je?
“Mara nyingi chai siyo mpenzi sana lakini kama nitakunywa napendelea iliyo na tangawizi ikiwa bila kitafunwa, mchana napenda kula chakula chochote kizuri kama wali nyama au ugali.”
Anapikiwa na nani?
“Mara nyingi napika mwenyewe ila nikitembelewa na ndugu zangu wa kike hunisaidia.”
Anapenda kufanya nini akiwa nyumbani?
“Napenda sana utulivu ambapo huwa najifungia ndani nikiangalia runinga na kusikiliza muziki.”
Vipi kuhusu kazi ndogondogo za nyumbani?
“Mimi sijivungi kila kazi nafanya mwenyewe kama kuosha vyombo na usafi wa nyumba kwa ujumla, sipendi kusubiria mtu aje anifanyie wakati uwezo ninao.”
Nini unachokichukia?
“Sipendi ukorofi na pia sipendezwi na mtu kuniudhi napenda sana kuwa na amani ya hali ya juu na sihitaji kumsonenesha mtu kwa njia yoyote ile.”
Anatarajia KUOA lini?
“(Kicheko) bado kidogo ila ninaye nimpendaye kwa dhati kabisa tuombe Mungu niweze kumuoa huyo.”
Anamzungumziaje Kanumba na kufanana kwao?
“Ni kweli tunafanana kidogo lakini namkumbuka kwa kazi zake nzuri ila kuna watu wananikorofisha kwa kuniita Kanumba feki, mimi na yeye tulikuwa tukifanana kidogo tu na inawezekana uwezo wa kazi zetu ni tofauti ila nitaendelea kumheshimu siku zote.”

Friday, April 8, 2016

Ujumbe Mzito Wakutwa Kaburini Kwa Kanumba!

IMG_3360Ujumbe uliokutwa kaburini kwa Kanumba.
Stori:  Mayasa Mariwata na Gladness mallya, Ijumaa
Wakati mama yake, Flora Mtegoa (pichani), baadhi ya wasanii na mashabiki wake wakikumbuka miaka minne ya kifo cha aliyekuwa staa mkubwa wa filamu za Kibongo, Steven Charles Kanumba ‘The Great’, kumezuka sintofahamu ya kukutwa ujumbe mzito wa kimapenzi kaburini kwa msanii huyo ambao unadaiwa kuwekwa na mrembo aliyefika mahali hapo mapema wiki hii.
TUJIUNGE MAKABURI YA KINONDONI
Kwa mujibu wa mtu aliyedai ni mmoja wa walinzi wa Makaburi ya Kinondoni, Dar, alikolazwa Kanumba kwenye nyumba yake ya milele, ishu hiyo ilijiri Jumanne wiki hii, majira ya jioni ambapo mwanadada huyo alionekana akishuka kwenye gari (halikutajwa ni aina gani) na kuelekea kaburini hapo.
IMG_3335Mrembo aliyekutwa kaburini.
Alisema kuwa, huku akiwa amejitanda mtandio na maua mkononi, baada ya kufika kaburini hapo alionekana akiangua kilio na kuangusha maombi mazito kabla ya kuacha ujumbe na kuondoka zake.
BOFYA HAPA KUKISIKIA CHANZO
“Haloo…naongea na Ijumaa? Njooni wenyewe mjionee kuna mtu yuko hapa kwenye Kaburi la Kanumba, lakini kajifunika sana hadi usoni.
“Mimi nimeshindwa kumbaini ni nani japokuwa kwa mtazamo wa haraka anaweza kuwa huyu Lulu (mwigizaji Elizabeth Michael) na hata wengi waliomuona wanadai huenda akawa ni yeye ila mimi sina uhakika kwa sababu sipo karibu na wasanii.
“Nimemuona akilia sana kisha akaweka kikaratasi na maua na kuondoka zake.
“Nimejaribu kumpiga picha kwa simu yangu labda ninyi mkija mnaweza kumtambua kwa hizi picha na kujionea wenyewe kilichoandikwa kwenye karatasi aliyoiacha maana kinashangaza,” alisema jamaa huyo na kuongeza:
“Unajua siyo yeye tu, mara kwa mara kuna watu huwa wanakuja sana kaburini kwa Kanumba. Ni utaratibu wa kawaida sana kwa watu kuja kuwatembelea wapendwa wao hapa lakini huyu alionekana kuwa tofauti kwa kujifichaficha na huo ujumbe aliouacha.
elizabethmichaelofficial_78Mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’.
IJUMAA MZIGONI
Baada ya kunyetishiwa tukio hilo, Ijumaa liliingia mzigoni ambapo bila kupoteza muda lilifika eneo la tukio ndani ya muda mfupi kwa kutumia bodaboda ziendazo kasi ili kukwepa foleni za jijini Dar ambapo lilipishana na mwanadada huyo kwenye gari akiondoka bila kumshtukia.
Hata hivyo, mapaparazi wetu waliambulia kuusoma ujumbe walioukuta kaburini hapo ambapo sehemu fupi ilisomeka:
UJUMBE WENYEWE
“Ni mwaka wa nne huu tangu umenitoka, upendo wako kwangu ulinifanya niwe wa kipekee hapa duniani, leo hii ungekuwa hai huenda tungekuwa mke na mume na tungekuwa na watoto lakini Mungu hakupenda hilo litokee. Nakukumbuka na nitakupenda daima. Pumzika kwa amani…”.
Baada ya kuuona ujumbe huo, Ijumaa lilimrudia mtoa habari huyo aliyeomba hifadhi ya jina ambaye alionesha picha hizo kwenye simu yake kabla ya kumrushia mmoja wa mapaparazi wetu.
NI LULU?
Hata hivyo, katika kuzitathmini picha hizo, mapaparazi wetu nao walishindwa kung’amua kama ni Lulu au ni staa gani mwingine aliyewahi kuwa mwandani wa Kanumba.
28Mama wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa.
Wengine waliowahi kudaiwa kutoka na Kanumba ambao huenda mmoja wao anahusika na ujumbe huo ni Wema Sepetu, Sylivia Shally, Aunt Ezekiel, Shamsa Ford, Agnes Gerald ‘Masogange’ na mastaa wengine wakiwemo pia wanawake wawili walioibuka na kudai wamezaa na staa huyo waliofahamika kwa majina ya Salma na Pascalia.
Ili kuweka sawa mzani wa habari hiyo, gazeti hili liliona ni vyema kumvutia waya Lulu ambaye anahisiwa kuwa ndiye aliyeweka ujumbe huo. Hata hivyo, simu yake ilionesha ipo ‘bize’ muda wote. Alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno (SMS) hakujibu.
HUYU HAPA MAMA KANUMBA
Kwa upande wake, mama Kanumba alipoulizwa kuhusu ishu hiyo alifunguka kuwa, licha ya kuwa imepita miaka minne tangu kifo cha mwanaye lakini hawezi kumsahau hadi naye atakapokutwa na umauti.
Kuhusu mwanamke aliyeonekana kaburini kwa Kanumba ikidhaniwa kuwa ni Lulu alikuwa na haya ya kusema:
“Kama wanasema ni Lulu inawezekana, nadhani labda aliamua kwenda siku hiyo kwa kuwa hakutaka kushiriki na mimi kwa sababu nashindwa kumhisi mtu mwingine kwa kuwa Kanumba alikuwa msiri sana. Mwanamke aliyewahi kunitambulisha ni staa mmoja tu na si Lulu.”
Steven-KanumbaMarehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake.
KUMBUKUMBU MUHIMU
Kanumba alifariki dunia Aprili 7, 2012 kwa kuanguka katika mazingira yaliyodaiwa kutokana na ugomvi kati yake na Lulu. Tukio hilo lilitokea nyumbani kwa Kanumba, Sinza ya Vatcan, Dar.
Baada ya kifo hicho, Lulu alikamatwa na kuwekwa Mahabusu ya Segerea jijini Dar na baadaye kuachiwa kwa dhamana ambapo kesi hiyo bado inasubiriwa kuanza kuunguruma.
Baada ya kutoka mahabusu, Lulu na mama yake, Lucresia Karugila walimfuata mama Kanumba na kuomba msamaha ambapo mama huyo aliupokea na kusema anamwona Lulu kama mtoto wake na yote ya nyuma yamepita.
Kuanzia hapo, Lulu na mama Kanumba wakawa na ukaribu wa kindugu huku kila mwaka wakifanya kumbukumbu ya Kanumba pamoja kabla ya mwaka jana kutibuana.

Monday, April 4, 2016

Irene Uwoya Adai Anapenda Kuigiza ‘Scene’ za Mahaba

Staa wa filamu Irene Uwoya amesema anapenda sana kuigiza ‘scene’ za mapenzi katika filamu kwa sababu ni kitu ambacho anaweza kukifanya kwa ukamilifu zaidi.

Muigizaji huyo ambaye alionyesha uwezo mkubwa katika filamu ya Fair Decision, Pretty Girl pamoja na Oprah, amekiambia kipindi cha Uhondo cha EFM kuwa filamu ya Oprah ndio filamu ambayo ilimpa mume.
Kiukweli scene za mapenzi (mahaba) nazipenda kwa kuwa nazifanya vizuri,” alisema Irene. “Kama filamu ya Oprah ndio filamu ambayo ilisababisha nikaolewa, mume wangu alinipigia simu akaniambia nimeona movie yako ya Oprah nataka nikuoe,” alifanunua zaidi.

Lakini ni movie ambayo ilinipa wakati mgumu sana kwa familia yangu, wakiona hii movie si wataniua?. Lakini bahati nzuri baada ya baba kuiona akanipa big up na akanipa ruhusa ya kufanya movie,” aliongeza Irene.

Irene Uwoya kwa sasa ni mama wa mtoto mmoja aitwaye Krish.

Sunday, February 21, 2016

Mama Yangu Hapendi Nihame Nyumbani Kwetu – Ray

Msanii wa filamu Vincent Kigosi ‘Ray’ baada ya kuchanwa kwenye wimbo wa Nay wa Mitego ‘Shika Adabu Yako’ kuwa bado anaishi kwao, amejibu tuhuma hizo kwa kudai anaishi kwao mpaka sasa ili kuwa karibu na Mama yake.
RAY543
Akizungumza katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM Ijumaa hii, Ray alisema yeye ni mtoto wa mwisho hivyo anahitaji kuwa karibu zaidi na Mama yake.
“Ni kweli naishi nyumbani na kuishi kwetu sio kama sina nyumba, na kuishi nyumbani sio dhambi. Uwezo wa kupanga ninao lakini mama yangu hapendi nihame nyumbani kwetu ,” alisema Ray.
“Kujitegemea ni maamuzi yako binafsi, mimi naishi nyumbani na mama yangu ni mtoto wa mwisho lakini huwa sipendi kujionyesha nina utajiri gani?, Sipendi kupost mali zangu, sinina nyumba, magari ni ishu zangu binafsi, kila msanii ana style yake ya maisha, mwingine anapenda kujionyesha kwenye mitandao ana mali gani,” aliongeza Ray.
Pia Ray alisema yeye na mpenzi wake Chuchu Hans kila mtu anaishi kwake.
“Mpenzi wangu anaishi kwake na mimi naishi nyumbani kwetu. Mama yangu alishaniambia hata nikihama atakuja kuishi na mimi nyumbani kwangu. Chuchu Hans anajua kuhusu hili hata nyumba anayoishi nimempangia mimi,” alisema Ray.

Saturday, February 13, 2016

Niva Amfungukia Nay Wa Mitego Baada Ya Kuchanwa Kwenye ‘Shika Adabu Yako’

Baada ya msanii Nay wa Mitego Kumchana Niva Kwenye ‘Shika Adabu Yako’ kupitia mtandao wa instagram Niva amefunguka haya; 
Alianza kuwa kuandika haya; 
“Jioni ya Leo ndio watu watajua. Kama natafuta Kiki kwako au wewe @naytrueboy umeamua kuipata Kiki kwangu coz ney watu wameanza kukujua 2013… mimi watu wameanza kunijua tangia elfu mbili na sita kupitia tamthili ya jumba la dhahabu kipindi hiko wewe upo manzese unatafuta kutoka.. mwenzio nikitajaga tamthili ya jumba la dhahabu uwa nawaumizaga watu wengi Sana coz uwa nawakumbusha kumbukumbu za maisha Yao ya kipindi icho wengine wenzao wamesha wazika walio kua wakiangalia nao. Sasa wewe @naytrueboy unakipi cha kuwakumbusha mashabiki zako.”
 
Kisha akaweka picha akweka picha hiyo hapo juu akiwa na Nay na kuandika; 
“Sasa mkitazama iyo picha mtangundua ni wiki ngapi zimepita na hapo mulizeni alikua wapi na kwanani na alifata nini Tena alikua anajipima mwili wake na wangu… niliwai kusema kuwa ni mdogo wangu kwaiyo kwangu yameisha nanimemsamee coz ni mdogo wangu ila kuusu kumuigiza na yeye kupo pale pale nimesha maliza kutoka moyoni” 

Exclusive:Kwa Mara Ya Kwanza Wema Sepetu Afunguka Kuhusu Mimba Yake Kutoka.... A To Z Mambo Yote Yapo Hapa

Mashabiki wa Wema Sepetu waliingiwa na hofu kali baada ya mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown kuandika post yenye utata.

“Pole Dada @wemasepetu mungu akupe nguvu ktk kipindi hiki kigumu, akupe moyo wa uvumilivu pia ili utoke hospitali ukiwa salama inshaallah, kazi Yake Mola haina makosa #INASEMEKANAETI,” aliandika Soudy kwenye Instagram.

Wengi walitafsiri post hiyo kuwa huenda ujauzito wa Wema ukawa umetoka. Wengine walienda mbali zaidi hadi kutengeneza chat za Whatsapp kukuza zaidi kama hiyo chini.


Hata hivyo inaonekana kuwa hakuna ukweli wowote. Wema amepost picha kwenye Instagram akiwa mwenye furaha na kuandika: It all began with a smile…”

Comments zote za mashabiki wake zinaonekana kujikita kwenye tetesi hizo.

“@wemasepetu my lv,pliiiiizzz stop kuonesha mimba yako in public for sometyms now wala mtu yoyote kushika tumbo lako,km siyo yo family members and baba k pliiiiiiizzzz,coz ushaona how people wish mimba yako iharibike au kitokee kitu kibaya kwenye mimba yako na kweli wamefurai as you see,pliz stop it kama unapenda kuitwa mama for real,yup waweza ukawa wawish for everyone to see yo preg as umesuffer alot kuipata,that is to prove pplo wrong kwamba hata wewe umeshika mimba and its de first tym,I know wat yu fil,ila tunaokupenda tuna wish ujifungue salama mdA ukifika..pliz pumzika mama for now mimba haiitaji stresses na hiyo ndo kitu naona maadui zako wanajaribu kufanya,to stress u,pliiiiiiizz @idrissultan take Care of the baby,kip wema out of negativity,#we in pressure now#minb,” ameandika shabiki mmoja.

Chanzo: Bongo5.com

Friday, February 12, 2016

Ester Kiama, Davina Watibuana kisa, Upatu

ester4
Ester Kiama
Mastaa wa filamu Bongo, Ester Kiama na Halima Yahya ‘Davina’ juzikati walitifuana kwa kutupiana maneno makali kupitia kundi lao la Mtandao wa WhatsApp kisa, kikiwa ni mchezo wa upatu.
Sosi ambaye ni memba wa kundi hilo alidai kuwa, wawili hao pamoja na mastaa wengine wana mchezo wao wa kupeana pesa ‘upatu’ lakini siku hiyo Ester akawa amechelewa kutoa, Davina akamtolea uvivu kwa kumchamba.
davina
Davina
“Walirushiana maneno makali sana hadi Ester akaamua kujitoa kwenye kundi hilo, yaani ilishangaza sana hadi watu wakahoji ni hizo pesa za upatu au kuna lingine,” kilidai chanzo hicho.
Davina hakupokea simu alipopigiwa lakini Ester alipotafutwa na kuulizwa juu ya habari hizo, alikuja juu akitaka atajiwe aliyevujisha, alipobanwa zaidi akakata simu.

Kwa Nini Soud Brown Kafanya Jambo La Ajabu Kuhusu Mimba Ya Wema Sepetu


Jana Mtangazaji wa Clouds alizua jambo Instagram kwa kuandika ujumbe tata kuhusu Wema Sepetu ..
Soudy brown kwenye instagram yake kapost picha ya wema kaandika :

 "Pole dada wema sepetu, mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu akupe moyo wa uvumilivu pia ili utoke hospitali ukiwa salama, inshallah kazi yake Mola haina makosa"

Kisha akaweka na hashtag #INASEMEKANAETI

Baada ya Ujumbe huo mashabiki wa Wema Sepetu walilipuka kutaka kujua ukweli wa jambo hilo huku wengine wakimrushia matusi Soudy Brown kwa kushusha ujumbe huo....

Mpaka sasa Wema Sepetu wala watu wake wa karibu hakuna aliyejitokeza na kutoa ufafanuzi kuhusu ujumbe huo wa Wema Sepetu kama ni Kweli ama la

Mrembo Na Mwigizaji Thea Adaiwa Kuhongwa Gari

STAA wa filamu Bongo, Salome Urassa ‘Thea’ sasa hivi anasukuma mkoko baada ya kutembea kwenye vumbi kwa muda mrefu lakini pia taarifa zilizo nyuma ya pazia zinadai eti kahongwa na mwanaume.

Inadaiwa baada ya Thea kumwagana na Michael Sangu, alijiweka kwa mwanaume mwenye nazo na ndiye aliyempa jeuri ya kumiliki gari hilo aina ya Toyota Passo.

“Thea sasa mambo safi, anatembelea makalio baada ya kuhongwa gari na yule bwana wake wa sasa,” kilidai chanzo hicho.

Baada ya kunyaka ‘ubuyu’ huo, Thea alitafutwa, alipopatikana alisema: “Hili gari sijahongwa na katika maisha yangu sitegemei kuhongwa na mtu yeyote, nimenunua kwa hela yangu ninayopata kwenye muvi.

Thursday, February 4, 2016

MWIGIZAJI BATULI AMJIBU RAY KIGOSI...AMTAKA APIGE PICHA MKATABA UNAOSEMA ALIPWE BAADA YA MWAKA MMOJA AUWEKE MTANDAONI


Bifu inayoendelea Kati ya Ray na Batuli yazidi Kupamba moto, Batuli amjibu Ray Kama Ifuatavyo;

Haki Ya Mtu Haizami
Swali: Movie Yako Nimecheza Mwaka Juzi Wiki Moja Kabla Ya Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani, Makubaliano Yetu Ya Kazi Kimkataba Ni Siku 10 Tu Lkn Ulienda Kinyume Na Matokeo Yake Nilifanya Kazi Yako Mwezi Mzima Wa Ramadhan Je Ulikuwa Sawa!?
Swali: Pamoja Na Usumbufu Wako Wote Nilifanya Kazi Sikufanya!? Kumbuka Nilikuwa Kwenye Swaumu

Swali: Toka Mwaka Juzi Mpaka Mwaka Jana Ni Mm Ndie Niliekuwa Nafuatilia Malipo Yng Ofisini Sio Chini Ya 20 Times Na Umekuwa Ukinikimbia Matokeo Yake Nikachoka Kuja, Simu Zng Umekuwa Ukizipokea Unapotaka Na Sms Unanijibu Unavyotaka Je Mkataba Wetu Ulisema Hivyo!?

Swali : Naimani Ww Una Mkataba Upo Ofisini Kwako Upige Picha Tuone Kama Upo Unavyodai, Binafsi Kila Mtu Anajua Nyumba Yng Iliteketea Moto Hivyo Sina Kitu Na Ndio Maana Umekuwa Ukinitendea Unyama Huu Je Kuna Anaeweza Kukaa Kimya Zaidi Ya Mwaka Mmoja Na Hatimae Unaona Kazi Inatoka Wakati Hujalipwa!?

Swali : Ni Movie Ngapi Nilizofanya Kwenye Kampuni Yako Chini Ya Johari!? Ni Zaidi Ya 3 Je Nililalamika!? Kwanini Hii Ambayo Johari Hakuwepo Nikaingia Mkataba Na Ww Iweje Nilalamike!?
Dhulma Itakufikisha Pabaya Sana, Tambua Nilifanya Kazi Yako Ktk Mazingira Magumu, Nilikuwa Kwenye Swaumu Baba Nilifuturu Mabarabarani Chipsi Na Vingine Visivyo Rasmi Yote Ni Ktk Kutimiza Kazi Yako,

Nionyeshe Mkataba Unaosema Nilipwe Baada Ya Mwaka 1 Na Kuendelea Hakika Umeonyesha Ulivyo Na Roho Ya Dhulma Sijawahi Kulalamika Popote Kuhusu Unachonifanyia Kwa Sbb Nilijua Ipo Siku Utanilipa Changu Matokeo Yake Umeona Ujivishe Ujemedari Lakini Haitokisaidia Chochote, Kama Haki Yng Basi Itanifuata Hata Nikiwa Kaburini....Be Blessed....Allah Bariq 

Monday, September 28, 2015

Barafu:Tunatatafuta Raisi wa Tanazania Sio wa Bongo Movies

Mi naona wenzetu wameamua kuchukua majina ya movie zao ndio waje kutuchanganya nao eti mama ongea na mwanao mala nimestuka eti kibajaji si majina ya movie hayo acheni utani tunatafuta raisi Wa Tanzania sio Wa bongo movie acheni maigizo yenu ila watanzania wameshaamua team mabadiliko 2015
Barafu Suleiman @barafusuleiman on instagram

Sunday, August 23, 2015

Haikuwa rahisi kumpata mshindi wa TMT na sasa imefikia mwisho NA HUYU NDO MSHINDI


Screen Shot 2015-08-23 at 2.59.29 AM
August 22 imetoa jibu kamili la Tanzania Movie Talent (TMT) na zawadi ya million hamsini kwa mshindi wake kituambacho kilikuwa ni kidendawili kikubwa kwa wafuatiliaji wa TMT na wapigakura kwa sababu ya idadi kubwa ya washiriki ni uwezo mkubwa katika mashindano
List ya watu kumi ndio walioingia kwenye fainal na hatimaye meza ya Majaji imetoa zawadi hiyo kwa mshindi wa TMT Denis Lwasai ambaye ni msanii aliyewahi kufanya kazi na marehemu Steve Kanumba kipindi cha uhai wake miaka kadhaa iliyopita…
Screen Shot 2015-08-23 at 2.59.36 AM
Screen Shot 2015-08-23 at 2.59.42 AM
Lulu na mbona ndio walikuwa waondozaji wa sherehe ya kumpata mshindi wa tmt
Screen Shot 2015-08-23 at 2.59.54 AM
Screen Shot 2015-08-23 at 3.00.01 AM
Washiriki wakionyesha uwezo wao mbele ya majaji
Screen Shot 2015-08-23 at 3.00.07 AM
Ray Kigosi kwa umakini akifuatilia mashindano ya TMT
Screen Shot 2015-08-23 at 3.00.12 AM
Screen Shot 2015-08-23 at 3.00.20 AM
Screen Shot 2015-08-23 at 3.00.26 AM
Screen Shot 2015-08-23 at 3.00.40 AM
Screen Shot 2015-08-23 at 3.00.46 AM
Screen Shot 2015-08-23 at 3.00.55 AM
Screen Shot 2015-08-23 at 3.01.24 AM
Screen Shot 2015-08-23 at 3.01.31 AM
Screen Shot 2015-08-23 at 3.01.37 AM
Screen Shot 2015-08-23 at 3.01.44 AM
Screen Shot 2015-08-23 at 3.01.55 AM
Screen Shot 2015-08-23 at 3.02.01 AM
Screen Shot 2015-08-23 at 3.02.11 AM
Haikuwa raisi kwa Ray kuvumilia kuzuia machozi yake baada ya Mshindi kutangazwa na kuhusishwa kuwa anafanana sana na marehem Steve Kanumba

Screen Shot 2015-08-23 at 3.02.21 AM
Screen Shot 2015-08-23 at 3.02.28 AM

Friday, August 21, 2015

Gabo:Sijaona Muigizaji wa Kushindana Naye Bongo Movies

Msanii wa filamu aliyejizolea umaarufu miaka ya
hivi karibuni, Salim Ahmed maarufu kwa jina la
Gabo amesema haoni msanii anayempa
changamato.
Akizungumza kwenye kipindi cha Take One cha
Clouds TV, Gabo alisema wengi wamekuwa
wakimwambia anaringa kutokana na kuwaambia
ukweli.
“Kwa hapa Tanzania sijui ndio maana wanasema
mimi naringa,” alisema Gabo alipoulizwa ni msanii
gani anayempa changamoto.
“Nyuma alikuwa Single Mtambalike, sasa hivi
sijaona wa kumtazama na kunipa changamoto
tuweze kushirikiana kupeana nguvu. Kwa single
sijui nisene vitu vinakwenda vinaisha! Lakini
simuoni tena yule, sasa hivi amekuwa akifanya kazi
anakuwa ni yule yule, hakuna mabadiliko. Lakini
nikimwangalia yule single wa filamu za nyuma
nasemaga yule jamaa, amebadilika kabisa na kuwa
wa kawaida,” aliongeza.
Gabo amesema kuwa pamoja na filamu za
Tanzania kuwa na changamoto, amefanikiwa
kupata mafanikio mengi.
“Mimi kama ningekuwa nchi nyingine ningekuwa
mtu mkubwa sana,” alisema.
“Ukiangalia uwezo wangu mimi na jinsi ninavyoishi
havilingani. Nimekuwa nikitembelea nchi kama
Afrika Kusini na Jumatatu kama Mungu akipenda
naenda Botswana, watu wanakuona huyooo kumbe
maandazi tu hamna chochote! Kitu kikubwa
ambacho nilikuwa nakihitaji kwa sasa ni kampuni
yangu ya Sarafu Media, nilitamani iwe strong mtu
akija anaogopa, lakini sasa ipo kampuni jina, mtu
akija anaona huyu naye anaanza.
Kingine mimi nimejenga nje ya sanaa, hata kwangu
pale nikilala najiona bado. Ndioa maana
nikapangisha kule nikaja kukaa Kinondoni ili
nitafute kwa jasho la filamu. Mimi ninachojivunia
kwa sasa kilichopatikana kutokana na filamu ni
gari (Passo), ndio maana sasa hivi naboresha zaidi
kazi zangu hata mtu akinihitaji kufanya filamu yake
aandae milioni 8,” alisisitiza

Monday, July 20, 2015

Shamsa amsapoti Nay Wa Mitego kui’push’ ngoma yake mpya ya ‘Sina Muda’.

Mwigizaji wa filamu za Kibongo,Shamsa Ford ambaye amekuwa akidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Staa wa Bongo Fleva,Nay Wa Mitego amemsapoti msanii huyo kwa kuongozana naye kwenye vituo mbalimbali vya redio na tv ikiwemo Clouds TV na kufanya mahojiano pamoja na kuipush ngoma yake mpya iitwayo Sina Muda.

Akizungumza na Clouds FM,Nay alisema kuwa wamekuwa wakiongozana na Shamsa kwenye vituo mbalimbali vya redio na TV ili kuipa nguvu zaidi na kuitangaza ngoma yake mpya kwa kuwa ni rafiki yake na amekuwa akimsapoti kwenye mambo mengi zaidi ya muziki wake.

‘’Shamsa ni rafiki yangu na amekuwa akinisapoti kwenye mambo mengi tu zaidi ya muziki wangu ndiyo maana nimekuwa nikiongozana naye kwenye vituo mbalimbali vya TV na redio kwa ajili ya mahojiano na kuitangaza zaidi ngoma yangu mpya ya Sina Muda,’’alisema Nay.

Hata hivyo Nay alisema kuwa ngoma yake hiyo mpya hakuitegemea kama itafanya vizuri kwa kuwa aliichukulia poa na hakuipa nguvu sana lakini ilivyopokewa vizuri na mashabiki ndiyo maana ameona aipe nguvu zaidi kwa kuitangaza kwenye vituo vya redio naTV.

‘’Unajua sikutegemea kama hii ngoma itapokelewa vizuri niichukulia poa tu lakini illivyopokelewa vizuri na mashabiki nimeona bora niipe haki yake nitumie nguvu zaidi kuitangaza nikiwa na binamu yangu Shamsa,’’alisema Nay.

Shamsa amsapoti Nay Wa Mitego kui’push’ ngoma yake mpya ya ‘Sina Muda’.

Mwigizaji wa filamu za Kibongo,Shamsa Ford ambaye amekuwa akidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Staa wa Bongo Fleva,Nay Wa Mitego amemsapoti msanii huyo kwa kuongozana naye kwenye vituo mbalimbali vya redio na tv ikiwemo Clouds TV na kufanya mahojiano pamoja na kuipush ngoma yake mpya iitwayo Sina Muda.

Akizungumza na Clouds FM,Nay alisema kuwa wamekuwa wakiongozana na Shamsa kwenye vituo mbalimbali vya redio na TV ili kuipa nguvu zaidi na kuitangaza ngoma yake mpya kwa kuwa ni rafiki yake na amekuwa akimsapoti kwenye mambo mengi zaidi ya muziki wake.

‘’Shamsa ni rafiki yangu na amekuwa akinisapoti kwenye mambo mengi tu zaidi ya muziki wangu ndiyo maana nimekuwa nikiongozana naye kwenye vituo mbalimbali vya TV na redio kwa ajili ya mahojiano na kuitangaza zaidi ngoma yangu mpya ya Sina Muda,’’alisema Nay.

Hata hivyo Nay alisema kuwa ngoma yake hiyo mpya hakuitegemea kama itafanya vizuri kwa kuwa aliichukulia poa na hakuipa nguvu sana lakini ilivyopokewa vizuri na mashabiki ndiyo maana ameona aipe nguvu zaidi kwa kuitangaza kwenye vituo vya redio naTV.

‘’Unajua sikutegemea kama hii ngoma itapokelewa vizuri niichukulia poa tu lakini illivyopokelewa vizuri na mashabiki nimeona bora niipe haki yake nitumie nguvu zaidi kuitangaza nikiwa na binamu yangu Shamsa,’’alisema Nay.

Saturday, July 18, 2015

JB AELEZA ALIVYOANZA UIGIZAJI KWA KULAZIMISHWA NA MAMA’KE

JABStaa wa filamu za Bongo, Jacob Steven ‘JB’.
WIKI iliyopita, tuliishia kwa kueleza jinsi alivyojitosa rasmi kwenye biashara ya kuuza nafaka za mahindi na mpunga akitoa katika mikoa ya Mbeya na Tanga. Tuliishia kwenye kipengele cha alipougua fangasi.
Je, nini kilifuata? Endelea sasa.
Kilikuwa ni kipindi kigumu mno maishani mwangu, sikuwahi kuwaza hata siku moja kama ningekuja kuugua ugonjwa kama huo,” anasema JB.
“Basi, maisha yakasonga kama kawaida huku biashara nayo ikizidi kuimarika kwa kuniletea mafanikio mengi, lakini nikiwa katika kilele hicho cha mafanikio, mara nikaanza kukutana na ushawishi wa jambo ambalo sikuwahi kuwaza hata siku moja kama ningeweza kulifanya, jambo lenyewe ni kufanya maigizo,” anasema JB.
JB anasema mtu aliyeanza kumshawishi ajiingize kwenye mambo ya uigizaji ni msanii mwenzake, Single Mtambalike ‘Richie’. Hata hivyo msanii huyu anaweka wazi kuwa haikuwa kazi rahisi sana kukubaliana na wazo la Richie, lakini kwa jitihada kubwa kutoka kwa Richie pamoja na watu wake wa karibu akiwemo mama yake mzazi, hatimaye alijikuta akikubali kujiunga na kundi la maigizo la Nyota Assemble.
“Kila nilipokuwa nikikataa, Richie alizidisha ushawishi, lakini pia hata ndugu zangu wa karibu akiwemo mama waliendelea kunisisitiza kuwa nafaa kabisa kuigiza na kwamba ndiyo karama na kipaji ambacho wanaamini Mungu alinizawadia kulingana na wao walivyokuwa wakiniona,” anasema.
JB anasema, licha ya kukubaliana na wazo la Richie, lakini hakujiunga moja kwa moja, akawa anawaahidi lakini siku ikifika, anaingiza visingizio vingi, hali iliyomlazimu mama yake mzazi kuingilia kati kwa kumuonya na udanganyifu aliokuwa akiwapa wenzake (akina Richie) kwa kuwaahidi jambo ambalo ilikuwa ni ngumu kulitekeleza.
“Mama ikabidi akomae na mimi bwana, kusema ukweli nilikuwa nimekubali kwa maana ya kuwaridhisha tu lakini sikuwa nimeafiki kwa kumaanisha kabisa, akili na mawazo yangu yote yalikuwa kwenye biashara tu na si kitu kingine,” anasema JB.
Wakati mazungumzo yanaendelea, ghafla ninamuona JB akinyamaza kimya kidogo huku shingo yake akiwa ameielekeza mahali kwa muda mrefu, nikalazimika kugeuka na kutazama mahali alipokuwa amegeukia.
Lilikuwa ni kundi la watoto wa mitaani wakipita huku na kule wakitafuta riziki, kufika hapo nikamuona JB akiinuka na kuwapungia mikono kwa ishara ya kuwaita, bila kuchelewa walikuja haraka sana hadi mahali tulipokuwa tumekaa na kumkumbatia JB bila uoga wowote huku naye akionekana kuwafurahia.
JB alitumia muda mwingi sana kuzungumza na watoto hao akiwatia moyo kuwa maisha ya tabu waliyokuwa wakiishi ni ya muda tu kwamba wasijisikie vibaya huku akiwataka waendelee kuwa na tabia njema kwa watu na kumheshimu kila mtu aliyeko mbele yao, ambapo kwa pamoja watoto hao waliitikia kwa furaha.
Hapohapo nikamuona JB akilala ubavu kidogo kisha kuchomoa waleti yake ya gharama na kuifungua na kutoa noti nyingi sana nyekundu, akawapa wale watoto waliokuwa zaidi ya 7, kila mmoja shilingi 10,000 na kuwataka watupishe kwa ajili ya mazungumzo yetu.
“Unajua ipo siri ambayo watu wengi sana hawaijui, ni siri ya kutoa na kusaidia wengine, ili Mungu akubariki, ni lazima uwe na moyo wa kutoa, kusaidia watu kwa kadiri unavyoweza, Mungu hawezi kukuacha kama ulivyo, amini maneno yangu mdogo wangu (mwandishi),” anasema JB huku akifungua chupa yake ya maji na kunywa taratibu.
“Basi bwana ngoja tuendelee, siku moja nikaona ngoja nikawatembelee kwenye ukumbi wao wa mazoezi, nilipofika nikaanza kwa kuchungulia kwanza kabla sijaingia ndani kabisa, nilichokishuhudia humo sikutaka hata kugeuka nyuma, haraka nikaondoka huku nikijiapiza kutorudia tena, na hata mpango wa kujiunga na uigizaji nikautoa kabisa akilini mwangu,” anasema JB.
Je, JB ameona nini? Usikose kufuatillia wiki ijayo.