Showing posts with label Bongofleva. Show all posts
Showing posts with label Bongofleva. Show all posts

Monday, June 13, 2016

PICHA:Msami kafanyiwa suprise na Meneja wake… kapewa gari

Ni mwimbaji na dancer kwenye muziki wa bongofleva anaitwa Msami Giovani leo June 11, 2016 bila kujua kitachotokea baada ya kufanya mazoezi asubuhi, meneja wake aitwae Rehema amemfanyia suprise ya kumzawadia gari aina ya Toyota Ipsum yenye thamani ya Tsh. milioni 15.
Hii ni baada ya single yake iitwayo Mabawa kufanya vizuri kwenye Radio, TV na hata kumpa mauzo ya shows nyingi zaidi majukwaani Tanzania, usisahau kwamba Msami ni bingwa wa kumiliki stage pia.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Mwigizaji Kajala ni miongoni mwa waliokuwepo kwenye suprise
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Meneja Rehema na uthibitisho wa kadi ya gari

Mneno haya RUBY Nna ASLAY yanayotambusha kuwa na mahusiano ya KIMAPENZI

Kama wewe ni mmoja wa watu wanaotumia mitandao ya kijamii hususani instagram, najua huenda ukawa umekutana na post za mastaa wa Bongofleva Ruby na Aslay ambazo zinatafsirika kama wapo kwenye mahusiano. Haijajulikana kwa mara moja kama ni kiki au ni serious ni wapenzi ila hii ndio ishu inayo trend kwa sasa.
rui
asa 2
Aslay baada ya kupata mtoto na majukumu yake mapya ya Umeneja.

PICHA :Hatimaye Msanii HARMONIZE Achora Tattoo Ya Sura Ya Diamond Platnumz

harmonize.JPG 4
Msanii wa bongo fleva Harmonize amechora tato ya Diamond Platnumz kwenye mkono wake, akijua jambo hili litashangaza wengi,haya ndio maelezo yake juu ya swala hili.

harmonize
“ Katika Maisha Yangu Sikuwahi Kuwaza Kuwa Itatokea Siku Nikajichora Tatoo But Diamond Nimtu Mwenye Mchango Mkubwa Sanaaaa Katika Maisha Yangu Leo Hii Mimi Ninathaminika Kutoka Kwenye Kunyanyasika Ninaheshimika Kutoka Kwenye Kudhalaulika Nimekuwa Maarufu Na Kupata Uthamani Mkubwa Kupitia Yeye Siotu Kwa Kipaji Nilicho Nacho Kwani Wangapi Wanavipaji…??? Naisaidia Familia Yangu Kwa Kile Nikipatacho Sihaba Akiwa Na Mchango Wake Mkubwa Sana…… Lakini Mwisho Wasiku Haya Ni Maisha Nahii Ni Dunia Inamambo Mengi Sanaa Hasa Sisi Vijana Ambao Niwepesi Wa Kujisahau Kinaweza Tokea Kitu Kidogo Sanaa Ukasahau Wema Na Fadhira Ulizotendewa, Lakini Pia Mungu Ndio Katukutanisha Na Karibia Watu Wengi Wanajua Tumekutanaje Kwamana Nimekuwa Nikiulizwa Katika Vyombo Vya Habari Tofauti Tofauti So Watu Wengi Wanajua Tulivyo Kutana But Hakuna Anaejua Tutaachana Vipi kwamana Sisi Ni Binadamu Kuna Kifo Leo Na kesho Huwezi Jua Yawanadamu Ni Mengi Siamini Kuwa Binadamu Wote Duniani Wanafurahia Mahusiano Na Ukaribu Wetu Na Huwezi Shindana Na Binadamu Ukijua Yambele Wenzio Wanajua Yanyuma Ndio Mana Yakujichora Hiii Picha Yake Amabayo Haitofutika Hadi Naingia Kaburini Hata ikitokea Hatupo Pamoja Nikiitazama Hii Picha Itabaki Kama Kumbu Kumbu Na Heshima Yangu Kwake Hadi Siku Yangu Ya Mwisho Haya Ni Maamuzi Yangu Binafsi

Saturday, June 4, 2016

Video: Party iliyofanyika Nyumbani Kwa Diamond Platnumz ya Kumkaribisha Rich Mavoko

June 2 2016 Ndio siku rasmi ambayo Lebel ya WCB ilimtambulisha Rich Mavoko kama msanii wa lebel hiyo, mtu wangu baada ya utambulisho huo uongozi wa WCB uliamua kufanya party ya Kumkaribisha Rich Mavoko pamoja na mke wa Meneja wa Harmonize (Ricardo Momo) kwenye familia hiyo, party ambayo ilifanyika nyumbani kwa Diamond Platnumz

Thursday, June 2, 2016

Hapa Nimekuwekea Video ya Mwanamuziki Diamond Akionyesha Meno yake ya Dhahabu Aliyonunua Kwa Bei Mbaya

Itakumbukwa kua wiki chache zilizopita video ya msanii Diamond ikionyesha akiwa katoboa pua ilisambaa na kusababisha watu wengi kumlalamikia kua kitendo hicho hakileti picha nzuri kwa jamii hasa ukizingatia kua yeye ni msanii mkubwa.

Ila sio wote waliochukizwa na jamba hilo, wapo waliomtetea wakisema yale ni maisha yake na ni ruksa kufanya jambo lolote lile analoamua. Sasa ikiwa ishu ya pua haijasahaulika sasa Diamond ameamua kuweka meno ya dhahabu akiwa nchini Marekani.

Diamond kupitia mtandao mmoja aliupload video kadhaa zikimwonyesha akiwa na meno hayo ya Dhahabu.

 Unaweza kumtazama Diamond akiwa na meno hayo hapa chini....

Thursday, April 28, 2016

VIDEO: Maneno ya Mr. Blue na MJ Records kuhusu tuhuma za Mr. II kuchukua beat ya Mr Blue

April 25 2016 Mr. Blue alianza kuhusishwa kwenye vichwa vya habari Tanzania baada ya kuonekana akilalamikia beat ya wimbo wake kutumiwa tena na Mr. II na kuifanyia video kabisa wakati ni beat ya wimbo wa Mr. Blue ambao alishauachia zaidi ya miezi sita iliyopita, kwenye hii video hapa chini kuna pande zote mbili za MJ Records na Mr. Blue.

NAY WA MITEGO Aingilia Beef la Sugu na Mr Blue..Amshauri Mr Blue Nae Afute Verse za Sugu Alafu Amshirikishe Yeye.

Ni siku chache zimepita tangu kutoka kwa video ya Freedom ya Sugu, video ambayo ameifanya na Director Hanscana, baada ya kutoka nyimbo hiyo kukatokea utata wa ngoma hiyo ambayo Mr blue akasema ngoma ni yake, sasa leo kupitia 255 ya Clouds FM Nay wa Mitego amefunguka kuhusiana na ngoma hiyo nakutaka kumpa idea Mr Blue.
"Blue angekuwa ni mshikaji wangu ningemshauri na yeye amtoe Sugu alafu kama inawezekana aniweke mimi kwenye chorus halafu tuharibu hali ya hewa tutajuana huko mbele ya safari, halafu kama ni hela ya kuifanyia Video ngoma hii mimi nitalipa hata kwa GodFather au Hanscana‘:-Nay wa Mitego"


Friday, April 15, 2016

Msanii Mpya wa Diamond Platnumz Anaitwa Raymond Ameachia Video ya Wimbo wake Itazame Hapa...

Video ya ngoma ya msanii wa WCB, Raymond ‘Kwetu.’ Imeongozwa na Godfather Productions.
Tazama Video Hapa Chini Alafu Utoe Maksi zako Kwenye Comment Box.... 


Saturday, April 9, 2016

KR Mullah Ajibu Tuhuma Na Sir Nature Kuhusu TID Na Matumizi Ya Madawa Ya Kulevya


Mwanamuziki KR Mullah amefunguka baada ya msanii mwenzake wa kundi la Wanaume Halisi Juma Nature, kusema kitendo cha KR kujiunga na Radar Entertainment, huenda kitamuharibu asipokuwa makini.

KR Mullah, amemtaka Juma Nature amuache kwa sasa afanye kazi, kwani kwa sasa anataka kubadilisha ladha ya muziki wake na huenda hajapendezwa na yeye kuingia Radar Entertainment na kuachana na Wanaume Halisi.
“Nilikuwepo ndani ya kundi la wanaume halisi, sasa labda anavyoona mimi nipo huku anaona kazi zake tena zitakuwa zinalegalega, pengine labda hakupendezewa mimi kwenda kufanya kazi na yule mtu na kwamba yeye alitegemea mi nifanye kazi naye,” alisema

Sambamba na hilo KR, amemuongelea TID ambaye Juma Nature alimtahadharisha kuwa makini nao wasije wakamuingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kuwa  hajawahi kumuona kutumia vitu hivyo.
“Kusema kweli zamani nilikuwa nasikia sikia hizi taarifa, lakini yeye mwenyewe alitangaza kuacha muda mrefu, lakini kwa sasa tangu nimeanza kukaa naye sijawahi kumuona akiitumia au akifanya hayo mambo, muda mwingi tunapiga stori za kikazi zaidi” alisema KR Mullah

Thursday, April 7, 2016

Uliiona Picha Ya Diamond Platnumz Kutoboa Pua?! Ukweli Ninao Hapa


Kwa saa kadhaa zimeenea taarifa za mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz kuonekana katoboa pua, hii habari imepewa nguvu kutokana na picha aliyoipost Diamond mwenyewe kwenye Instagram akionekana katoboa pua.
Ukweli ukoje? …ukweli ni kwamba Diamond hajatoboa pua kama wengi walivyodhani ambapo Meneja wake aitwae Sallam aliwajibu hivi mashabiki walioanza kuuliza >>> ‘Usiamini kila unachoona kwenye picha au unachoambiwa, mlikuwa mmelala sana amewaamsha kidogo’
SK
Maneno ya Meneja Sallam yanamaanisha kwamba sio kweli Diamond katoboa pua, ni mchezo tu na baada ya hiyo picha ya kutoboa pua Diamond aliweka picha nyingine inayoonekana hapa chini akiwa fresh kabisa watu wasiendelee kupanic.
Diamond 2

Mwanamuziki DIAMOND Atoboa "PUA" Na Haya Ndio Maneno Aliyosema

Supa Staa wa Bongo Fleva DIAMOND PLATNUMZ ametupia Picha Kwenye Akaunt yake ya Instagram akiwa ametobua Pua na kuweka kipini..

Hata hivyo Hali sio nzuri juu ya Mashabiki wake wengine wakimponda na wengine wakimpongeza..

Hivi ndivyo Alivyo andika kwenye Page yake ya FACEBOO...

Not everyone is going to like, want, accept or know how to receive your Energy...Make peace with that and keep Moving....👍
(Siku zote kumbuka: Sio kila mtu atapendezewa, Atafuraishwa ama kuridhika na ulifanyalo jifunze kulipokea Hilo na uendelee kupambana.... 👍) thank you @zarithebosslady for the Outfit💞 ‪#‎FromTandaleToTheWorldTour‬

Wednesday, April 6, 2016

Staa Nuh Mziwanda Atoboa Alichokuwa Akikifanya Kwa Shilole

nuh-mziwanda
Akizungumza katika kipindi cha Clouds E, Jamatatu hii, Nuh alisema hali hiyo ilimfanya apotee kimuziki na kukiki zaidi kimapenzi.

“Kwa Shilole nilikuwa nikifanya mapenzi sio muziki, ndio maana ukaona kwenye upande wa muziki sikuwa vizuri,” alisema Nuh. “Hata followers wetu walikuwa wanakuja kuangalia mapenzi na sio kwa ajili ya muziki. Ndio maana alikuwa anashindwa hata kunishauri kuhusu muziki wangu, kwa sababu kama angekuwa ni mtu sahihi angekuwa ananishauri kwenye masuala ya kujenga,” alifafanua Nuh.
Nuh amesema kwa sasa amejipanga yeye kama yeye kuachia kazi yake mpya ya kuimba pamoja na ya kurap.

Msanii Wa Bongo Baraka Da Prince Aweka Wazi Kuhusu Kolabo Yake Na Alikiba

 
Barack Da Prince amesema kuwa ana collabo na nyota wa Lupela Ally Kiba ambapo iko tayari, msanii huyo aliye wahi kuwika na ngoma Nina Imani Nawe na Siwezi.
Amesema nisamehe ni wimbo mpya ambao amemshirikisha Alikiba ambao utatoka hivi karibuni. 
"Alikiba ni kaka yangu ananishauri vitu vingi katika muziki nipo nae kwahiyo haikuwa kazi ngumu kumpata” hayo ameyasema kupitia kituokimoja na Television Nchini ambapo katika show hiyo aliambatana na mpenzi wake Najma (Naj).

Diamond: Target Yangu Kwa Mwaka Huu Ni Hii

diaaa

Pamoja na kuwa tumekuwa tukimshuhudia Diamond Platnumz akitangaza kolabo na wasanii wa kutoka Marekani lakini hakuna hata moja tuliyoona hata cover yake,mwaka jana rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete alimuunganisha Diamond na meneja wa Trey Song na ikasema kuwa kuna kolabo itafuta hiyo ni mbali na Swizz Beats,Alicia Keys,Alaine,Kanye West na wengine,na hivi karibuni tumeona picha ya Diamond akiwa na Awilo Longomba inawezekana kuna kolabo itafuata,sasa isue hua inaishia kwenye kupiga picha peke yake au inakuaje?

12093708_783599685109561_1894597186_n[1]

Diamond na familia yake wakiwa ‘Europe’ kwenye ‘tour’ ya kimuziki.
‘’Kuna kitu ‘sometimes’ tunasema wanamuziki wenzangu wa Tanzania tusikimbilie katika soko ikiwa kuna soko ambalo hatujalimaliza kwahiyo napiga hapa katikati kolabo nyingi za Waafrika ili niishike Afrika na nijizatiti zaidi usisahau kama mimi sijaanza ‘tour’ yangu rasmi Afrika bado kwasababu nishaona wanigeria wakipiga ‘tour’zao Gabon na sehemu zingine ,na ndio ‘target’ yangu kwa mwaka huu’’ Alisema Diamond.

‘’Na sio kwamba nilikuwa sipati ‘tour’ lakini nilikuwa sitaki kufanya shoo kiudogo ya watu elfu kumi kwenye ‘viklabu’ unaenda Ghana unapiga shoo klabu ni kujidharirisha watu wanakuona unaenda huko wanategemea upige uwanjani’’ Aliongeza Diamond.

Vanessa Mdee Analipwa Kila Muziki Wake Unapochezwa Kwenye Radio Na TV Yoyote South Africa

Kwenye dunia ya sasa Wasanii wa muziki pia wanayo nafasi ya kulipwa au kujiingizia pesa kutokana na vyanzo mbalimbali na hiyo yote ni kutokana na muziki wao ndio maana sio kitu kigeni tena kuona msanii analipwa pale nyimbo zake zinapochezwa redioni.

Kama ulikua hujui, mwimbaji staa wa Tanzania Vanessa Mdee huwa anapokea pesa zake mara kwa mara kutokana na nyimbo zake kuchezwa kwenye Radio na TV za Afrika Kusini ambapo hii imekua ni kanuni inayofatwa kwa baadhi ya nchi, Radio na TV kuwalipa wasanii kutokana na jinsi nyimbo zao zilivyochezwa.

Sio kila msanii anaweza kulipwa kama hivyo, kwa Wasanii wanaotoka nje ya nchi kuna vigezo vinatazamwa kukuwezesha kusajiliwa na mamlaka husika na baada ya hapo unakua kwenye mzunguko wa kulipwa kama Wasanii wengine wa nchi hiyo wanavyolipwa.

Vanessa anasema ‘Kwanini Tanzania tusiende juu zaidi? ni kitu kizuri sana hiki…… kuanzia nilipotoa wimbo wa no body but me niliofanya na rapper K.O wa South Africa ndio nimeanza kulipwa sababu nilikua sijajiandikisha kabla ya hapo, South Africa msanii yeyote mziki wake ukichezwa kwenye Radio, TV au migahawani na sehemu nyingine analipwa‘

Sijajua kwa Uganda lakini Kenya kumekua na hii sheria kwa muda sasa hivi na nilikwenda wakati flani nikaambiwa mpaka Taxi, Saluni, Baa na sehemu nyingine za public kama club za usiku na hotelini wamiliki wake hulazimika kulipia ada ya kila mwaka na kupewa stika maalum kuwaruhusu kucheza muziki wa Kenya ambapo Diamond Platnumz wa Tanzania hulipwa kila mwezi maana ni miongoni mwa wasanii wa nje ya Kenya waliojisajili kwenye mamlaka inayosimamia malipo hay

Monday, April 4, 2016

Diamond, Kiba Sasa Ni Vita Ya Kifamilia!

DSC_2781-001
Mkali wa Bongo fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’.

Dar es Salaam: Imevuja! Harakati za kusaka mafanikio na kufika mbali kimuziki zimeibua jipya kati ya wakali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ ambapo vita yao imehama kutoka kwa mtu na mtu na sasa imekuwa ya kifamilia.
Wachunguzi wa masuala ya burudani Bongo wanadai kwamba, kila mmoja anatumia familia yake kujifanyia matangazo (promo).Kwa mujibu wa sosi aliye karibu na Kiba, kwa sasa jamaa huyo anatembelea nyota au Waswahili wanasema viatu vya Diamond kwa kufuata staili ileile anayoitumia kujifanyia promo ambayo mpaka sasa imempa mafanikio makubwa.
KISIKIE CHANZO
“Hivi Wikienda mnajua kuwa kwa sasa Ali (Kiba) ameona afuate staili ya Diamond? Kwa sababu kama ninyi ni wafuatiliaji mtagundua kuwa zamani alikuwa hana mazoea ya kuanika familia yake kama ilivyo sasa.
AANISHA STAILI HIYO
“Kwa mfano ni hii staili yake mpya ya kutoka na mama, dada yake, Zabibu na sasa anatumia hata watoto kama Diamond anavyomtumia Tiffah (Latifah Nasibu).
IMG_8340-001Kiba akiwa na bimkubwa wake.
“Hii ni staili ambayo amekuwa akiitumia Diamond ambaye huwa anapenda kutoka na Esma (Platnumz) au Queen (Darleen) na mama yao, Sandra (Sanura Kassim) kisha anamuongezea Zari (Zarinah Hassan) na Tiffah.
UHUSIANO NAO WATAJWA
“Kiukweli kabla ya Diamond kuwa anafanya hivyo, zamani Kiba tulikuwa hatumuoni anaonesha uhusiano wake na mwanamke hadi ana watoto watatu kwa mama tofauti lakini hata siku moja, hakuwahi kuwaonesha mama zao kwa maana ya uhusiano alikuwa akifanya siri.
AANIKA UHUSIANO WAKE NA JOKATE
“Kuonesha kuwa anakanyaga viatu vya Dangote (Diamond), alivyoingia kwenye uhusiano na Kidoti (Jokate Mwegelo), akaanza kujiweka wazi kama Diamond huku habari zake zikitawala kwenye media (vyombo vya habari) mbalimbali ndipo akaanza kushaini,” kilisema chanzo hicho na kuweka pozi kidogo.
mond1Staa kunako Bongo fleva,  Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
MAMA ADAIWA KUTOA KIAPO
Chanzo hicho kiliendelea kunyetisha kuwa, Mama Kiba amekula kiapo cha kuhakikisha anamtoa mwanaye kama ilivyo Mama Diamond na kuahidi kuwa naye kwenye kila jambo atakalokuwa akilifanya kuhakikisha anampaisha mwanaye.
Kilitambaa na mistari kuwa, Mama Kiba anajua busara za mama humuongoza mtoto hivyo kwa sasa hataki kukaa mbali hivyo atafanya kila njia kuhakikisha mwanaye anakuwa juu.
KIBA AANGUSHA PATI YA MWANAYE AMAYA
‘Ubuyu’ ulizidi kumwagwa kwamba, katika kuonesha kuwa kwa sasa ameamua, hivi karibuni Kiba alimfanyia mwanaye, Amaya bonge la pati ya ‘bethidei’ akionekana akikata keki na kuruhusu mapichapicha tofauti na zamani ambapo alifanya mambo yake kwa usiri mkubwa.
DIAMOND MBELE KWA MBELE
Chanzo kingine cha upande wa Diamond kilieleza kuwa wakati Kiba akimfukuzia jamaa huyo kwa kufuata nyayo zake, msanii huyo naye ameongeza spidi ili kuzidi kufika mbali.
“Sasa hivi vita ni ya kifamilia zaidi, yaani Diamond ndiyo anazidi kuongeza familia ya Wasafi ili kila mmoja atumie fursa ya kumtangaza afike mbali zaidi,” kilisema chanzo hicho.
diamondplatnumzMondi akiwa na mamaake.
BOFYA HAPA KUMSIKIA KIBA
Baada ya kunyetishiwa habari hiyo, Wikienda lilimwendea hewani Kiba ili kupata ukweli wa kile kinachoelezwa ambapo mambo yalikuwa hivi;
Wikienda: Kiba mambo vipi? Nina maswali nataka kukuuliza maana kuna shabiki wako ametunyetishia ubuyu f’lani hivi.
Kiba: Hakuna shida ongea tu.
Wikienda: Kuna madai kuwa wewe kwa sasa unafuata staili ya Diamond kwa kuamua kumuanika mama yako kila kona, unalizunguziaje hili?
Kiba: Siyo kweli. Mama yangu aliniomba aje kwenye event yangu ndiyo maana nilimkubalia.
Wikienda: Mbona inadaiwa kuwa umeona ndiyo njia ya kukupaisha kwani zamani ulikuwa huna kawaida ya kuanika uhusiano wako wakati wa Jokate umemwanika kwa sababu ya kutafuta kiki?
Kiba: Ehee, endelea..
Wikienda: Samahani hivi wewe una baba?
Kiba: Ninaye ndiyo, yupo nyumbani Kariakoo (Dar). Kwani vipi?
Wikienda: Mbona hujawahi kumuanika kwa mashabiki wako?
Kiba: Siyo kweli, alishaonekana, kuna wakati waandishi walinifuata nyumbani nikapiga naye picha na naomba niseme tu mimi kuonekana na wazazi wangu siyo lazima, inategemea na ishu, kama ishu itakuwa ni lazima wazazi waonekane, wataonekana lakini kama haina ulazima hawataonekana.
d….Akiwa na Tiffah.
DIAMOND VIPI?
Alipotafutwa kuhusiana na ishu ya vita yao ya mafanikio kuwa sasa inahusisha familia, Diamond alifunguka:
“Kila mtu ana namna yake ya kutoboa ‘so’ siyo mbaya mtu ukitumia fursa zote zilizopo, mimi sasa hivi kuna vitu vipya kibao, hapa (Paris, Ufaransa) nimekutana na Fally (Ipupa) na Awilo (Longomba) na tayari mtoto wa Kimanyema nimeshafanya kweli,” alisema Diamond.
DIMOND NA KIBA
Diamond na Kiba wamekuwa kwenye vita kubwa ya kutafuta mafanikio ya kimuziki kwa muda mrefu ambapo wachambuzi wa burudani wanaitafsiri kuwa imechangia kuwasukuma mbele lakini imewagawa mashabiki wao.

Gardner Alazimishwa Kudansi Laivu Wimbo Wa Jide!

gardner (1)Mtangazaji anayetumikia Kituo cha Radio E-FM cha Dar, Gardner G Habash.
Noma sana! Mtangazaji anayetumikia Kituo cha Radio E-FM cha Dar, Gardner G Habash amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kulazimishwa kuserebuka wimbo mpya wa mtalaka wake, Judith Wambura ‘Jide’ unaoitwa Ndi Ndi Ndi.
Tukio hilo lilijiri juzikati ndani ya Ukumbi wa Maisha Basement uliopo Kijitonyama, Dar ambapo Gardner alikuwa MC wa shughuli ya bethidei za mastaa na watu wa kawaida waliozaliwa Machi.
Wakati shughuli ikiendelea huku watu wakikata keki na kufungua ‘shampeini’, ghafla DJ aliachia wimbo huo uliosababisha baadhi ya watu kupiga kelele wakitaka Gardner aucheze, jambo ambalo alilifanya kwa kunyong’onyea huku akirudi nyuma hadi msimamizi wa ukumbi huo alipomuomba DJ auondoe wimbo huo.
1458724449_0564_b (1)Judith Wambura ‘Jide’.
Hata hivyo, baada ya kubadilisha wimbo huo ambao inadaiwa Jide amemuimba Gardner, shughuli iliendelea kama kawa huku baadhi ya watu wakisema kuachana kwao si uadui kiasi cha kushindwa kucheza wimbo wake.
Wikienda lilipomtaka Gardner kuzungumzia ishu hiyo na kwamba wimbo huo ameimbwa yeye, hakuwa tayari. Kwa upande wake Jide alisema hajamuimba Gardner na kwa sasa hataki maswali yanayomhusu jamaa huyo ambaye walipeana talaka mapema mwaka huu baada ya kudumu kwenye ndoa kwa takriban miaka kumi.

Sunday, April 3, 2016

Msanii wa Bongo Fleva Afanya Uchafu Hadharani


Msanii Baraka Da Prince akiwa na mpenzi wake msanii wa kike Naj

Jide Azungumzia Msanii Wa Kiume Anaemfikiria Sasa

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Lady Jaydee ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa 'Ndi ndi ndi' amefunguka na kuweka wazi wazi msanii wa kiume ambaye kwa sasa anamfikiria katika kufanya nae kazi.

Kupitia Accout yake ya twitter ambapo alitoa nafasi ya maswali kutoka kwa mashabiki zake Lady Jaydee aliulizwa swali kama ataweza kufanya remix ya wimbo wake mpya na kama atafanya hivyo anadhani ni msanii gani wa kiume ambaye ataweza kufanya nae kazi hiyo. Ndipo hapo aliposema kwa sasa anamfikiri sana Mr Blue.

"Kiukweli mtu niliemfikiria hapo ni Mr Blue, naona ndio ata fit vizuri zaidi, Msanii wa Tanzania alieko akilini kwangu hivi sasa ni Mr Blue" alisisitiza Lady Jaydee.

Mbali na hilo msanii huyo aliweka wazi sababu za ukimya wake kwenye muziki kabla ya kuja na wimbo huo mpya na kusema kuwa huo ndio utaratibu wake toka amenza muziki na toka anatoka na Album ya kwanza mwaka 2001 yeye si mtu ambaye anatoka ngoma mara kwa mara bali huwa anajipa muda ya kujiandaa lakini hata hivyo nyimbo anazokuwa anatoa zinadumu muda mrefu ndiyo maana anakosa sababu ya kuharakisha kutoa kazi kila siku.

"Ndio utaratibu niliojiwekea miaka yote tangu Album ya kwanza 2001, mimi huwa sio msanii wa back to back lakini uzuri nyimbo zenyewe hudumu miaka mingi hivyo nakosa sababu ya kuharakisha kutoa kazi kila siku. Zitakapoisha nyimbo zilizomo kwenye album hii ya 7 itachukua muda tena kutoa zingine. Huwa najiandaa" alisema Lady Jaydee.

Baadhi ya mashabiki walitaka kufahamu msimamo wake juu ya wasanii kutumia vilevi na madawa ya kulevya na ndipo hapo Lady Jaydee aliposema kuwa ni sawa kutumia dawa za kulevya ila hyaina ubaya kwa msanii au mtu kutumia kilevi kidogo na kusema ili mradi usiwe kero kwa watu wengine.

"Si sawa kutumia dawa za kulevya ila haina ubaya kujichangamsha na Lager kiasi ilimradi usikere watu wengine. Vilevi vinatofautiana vipo visivyofaa vyenye madhara, si halali, situmii. Natumia halali Kama Wine na Beer". Lady Jaydee.


Mh.Temba – Fundi (Official Music Video)















PLAY VIDEO HAPA CHINI......ENJOY!