Showing posts with label FUMANIZI. Show all posts
Showing posts with label FUMANIZI. Show all posts

Friday, February 12, 2016

Askofu Amwomba Penzi Mtoto wa Mzee wa Kanisa

denti (1)-002
Askofu wa Kanisa la Jesus Deliverance Center (JDC) lililopo Tabata- Matumbi Dar, Derik Mathias

D AR ES SALAAM: Siku za mwisho?! Askofu wa Kanisa la Jesus Deliverance Center (JDC) linalotumia kauli mbiu ya Mlima wa Matengenezo ya Maombezi lililopo Tabata- Matumbi Dar, Derik Mathias amefikishwa kwenye dawati la Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers akidaiwa kutaka penzi la mtoto wa mzee wa kanisa lake (jina linahifadhiwa kwa sasa).
denti-(1)-001
Binti huyo
SIMU YAPIGWA OFM
Ilikuwa Februari 8, mwaka huu ambapo mtu mmoja aliyejitambulisha kuwa ni muumini wa kanisa hilo, alipiga simu chumba cha habari ya Magazeti Pendwa ya Global na kuomba kuongea na Kamanda wa OFM.
“Kamanda wa OFM, kuna askofu mmoja anaitwa Derik Mathias wa Kanisa la Jesus Deliverance Center, Tabata Matumbi ambaye amekuwa akimsumbua binti mmoja wa mzee wa kanisa lake mwenye miaka 15 akimtaka penzi licha ya binti huyo kumkatalia akimwambia yeye ‘bado mdogo’.”
denti (3)
Kanisa la Jesus Deliverance Center (JDC) lililopo Tabata- Matumbi Dar.
HABARI ZAFIKA KWA VIONGOZI
“Kufuatia tabia hiyo, baadhi ya viongozi wa kanisa walimuweka kikao cha siri askofu wao ili kumuonya lakini yeye alisema habari hizo si za kweli.
“Unajua kwa watu wa chini yake kumuweka kikao cha kuhusu mapenzi si sawa lakini walilazimika kwani tabia hiyo ilikithiri kiasi cha kuanza kuona kama kanisa linazama huku sisi tunaona,” alisema mtoa habari huyo.
ALICHUKUA NAMBA ZA SIMU KAMA ASKOFU
Mpashaji huyo aliendelea kusema: “Binti mwenyewe anasema alipoombwa namba ya simu aliitoa akijua ni baba askofu na kwa vile baba yake ni mzee wa kanisa na yeye pia ni muumini wa kanisa hilo, hakuona kama kuna kitu kibaya.”
OFM YAZUKA TABATA, YAONESHWA MESEJI, YACHOKA!
Baada ya taarifa hizo, makamanda wa OFM walisukuma pikipiki yao hadi Tabata na kuonana uso kwa uso na mtoa habari huyo.
MESEJI ZA ASKOFU MWAAA
Mnyetishaji wetu aliamua kuwaonesha OFM meseji za simu kutoka kwa askofu huyo kwenda kwenye simu ya mtoto wa mzee wa kanisa lake.
“Hebu oneni hizi meseji kwanza. Maana sisi tulimuuliza binti, unaposema askofu anakutongoza una maana gani? Isijekuwa anakutumia meseji akisema njoo unywe soda, ukadhani ndiyo kutongozwa,” alisema mpashaji huyo huku akiitoa simu kwa OFM.
MAJIBIZANO
Meseji za askofu huyo zilionesha kuwa, ameondokea kumpenda sana binti huyo hivyo kumtaka wakutane faragha.Binti huyo ambaye mtoa taarifa wetu alisisitiza kuwa ‘bado mdogo’, alimjibu askofu:
“Mimi siwezi kufanya mchezo huo kwa kuwa najua sitaweza. Mimi bado mdogo.”
ASKOFU ACHOMBEZEA
Licha ya majibu hayo, askofu huyo akiwa hajui yuko ‘mikononi mwa shetani’, alimjibu binti huyo kuwa, anaomba amkubalie japo kwa siku moja tu na asingeweza kumfanyia kitu kibaya kwani atakuwa makini.
ASKOFU AENDA MBELE ZAIDI
Katika hali iliyoonekana kuwa, askofu huyo alielemewa na majaribu, alimuita sehemu binti huyo akimtaka wakutane lakini binti akamwambia yuko peke yake nyumbani hivyo angeshindwa.
ASKOFU AITAKA BODABODA
Baada ya jibu hilo, askofu alimuuliza binti huyo kama anaweza kuchukua bodaboda ili amfuate nyumbani hapo lakini binti huyo alikataa akimwambia itakuwa noma.
OFM YATOA ONYO KALI
Baada ya kujiridhisha na ushahidi huo mkubwa wa meseji ikiwa ni sambamba na kuihakiki namba hiyo kuwa kweli ni ya Askofu Derik, OFM inampa siku 7 kuanzia leo (Ijumaa) kuacha mara moja kumsumbua binti huyo vinginevyo, OFM itaingia kazini na kumshughulikia mara moja!

Monday, January 11, 2016

Mke Afia 'Gesti' Akiwa na Mchepuko


Mwanamke mmoja (jina linahifadhiwa)  anayedaiwa ni mke wa mtu, amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni katika Manispaa ya Bukoba, akiwa na mwanaume mwingine anayesemekana ni hawara yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa, watu hao walienda katika nyumba hiyo ya kulala wageni iliyopo eneo la Hamugembe Januari 3, mwaka huu na kuchukua chumba namba nane.

Alisema siku iliyofuata saa 6:00 mchana, polisi walipokea taarifa kutoka kwa wahudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni kuwa katika chumba hicho kuna watu waliingia jana yake lakini hadi muda huo mlango wa chumba ulikuwa haujafunguliwa na kuna ukimya uliowatia hofu.

Alisema wahudumu hao waliambatana na polisi na walipofika eneo la nyumba hiyo walimkuta mmiliki wake ambaye alitoa funguo za akiba na kufungua chumba hicho.

“Polisi walipofungua chumba walikuta godoro liko chini lakini kitandani lilipopaswa kuwa kulikuwa na mwili wa mwanamke ukiwa umefunikwa shuka na kuuchukua kwenda kuuhifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera,” alisema.

Kamanda huyo wa polisi mkoa wa Kagera, alisema mtu aliyekuwa pamoja na mwanamke huyo (jina linahifadhiwa) ambaye ni dereva wa basi la abiria linalofanya safari zake kati ya Bukoba na Mwanza, hakukutwa katika chumba hicho na alifunga mlango kwa nje na kuondoka na funguo.

Hata hiyo, alisema chanzo cha kifo hicho hakijajulikana lakini kutokana na taarifa walizopata kutoka kwa msaidizi wa dereva huyo wamefanikiwa kumpata mtu aliyejitambulisha kuwa ni mume wa marehemu.

Kamanda Ollomi aliongeza kusema kuwa,  mume wa marehemu mkazi wa Butimba, jijini Mwanza, amepatikana na kukabidhiwa mwili wa mkewe, huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea na kwamba wafanyakazi wawili wa nyumba hiyo ya kulala wageni wanashikiliwa na polisi kwa upelelezi zaidi lakini pia kwa kitendo cha kuficha taarifa za wageni wanaolala katika nyumba hiyo

Saturday, December 26, 2015

Aibu ya Krismasi:AFUMWA AKINGONOKA NA MUME WA MTU

IMG-20151222-WA0016Issa Mnally
AIBU ya mwaka! Mwalimu aliyefahamika kwa jina la Henry wa shule moja maarufu iliyopo Kimara jijini Dar, amenaswa na mkewe aitwaye Sesy akiwa na mke wa mtu chumbani, Ijumaa linakupa mchapo kamili.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni nyumbani kwa mwalimu huyo aishie Kimara-Temboni, majira ya saa sita usiku baada ya mkewe kutonywa na majirani kuwa mumewe alizama chumbani na mchepuko huo ambao nao una mume.
IMG-20151222-WA0005Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio mke wa mwalimu huyo alikuwa Morogoro kusalimia wazazi wake kumbe mumewe alitumia mwanya huo kufanya yake katika chumba chao.
“Yaani mkewe ilikuwa kila akipiga simu kwa mumewe ili amtumie nauli arudi nyumbani mume huyo alikuwa akizungusha kumbe ndiyo alikuwa anataka uhuru zaidi kuendelea kufanya yake,” kilisema chanzo hicho.
IMG-20151222-WA0006Baada ya majirani kuusoma mchezo na kukerwa na tabia ya mwalimu huyo kufanya kitendo hicho na mwanamke huyo, siku ya tukio walimpigia simu mke wa mwalimu na kumueleza kuwa mumewe alimuingiza mwanamke huyo nyumbani kwake.
Kama hiyo haitoshi, majirani hao wakawapigia simu Makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) wa Global Publisher’s ambao walitinga eneo la tukio mara moja.
Mke baada ya kupata taarifa hizo, alikodi pikipiki lakini kabla ya kufika nyumbani kwake, Kimara-Temboni alianzia katika kituo cha polisi ili kuomba ulinzi na kutoa taarifa kwa kile kilichoendelea nyumbani kwake.
IMG-20151222-WA0002OFM walipofika katika eneo la tukio, walishuhudia mke wa mwalimu huyo akiangusha varangati baada ya kukuta mchepuko ukiwa umejaa tele ndani na mumewe wakiashiria kama walikuwa wanataka kufanya kitu.
Hata hivyo, polisi waliingilia kati na kumkamata mwalimu huyo na mchepuko wake kisha kuwapeleka kituoni kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya maelewano kwa kuwa hakukuwa na kesi ya msingi ya kuwabana kwa usaliti huo.

Saturday, October 17, 2015

AIBUUU:Afumaniwa, ajitosa baharini

Chande abdallah na issa mnally
AIBU! Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Zuhura maarufu kama Lolo Princessa ambaye ni mpenzi wa kijana anayejulikana kama Koko Byanco juzikati alijikuta akipata aibu kubwa baada ya kufumaniwa akiwa na mwanaume mwingine kiasi cha kusababisha mchepuko huo kujitosa baharini katika ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam kukwepa kipigo.
Tukio hilo lililotokea mchana kweupe na kuwastaajabisha watu, lilitokea jioni ya Oktoba 14 mwaka huu, wakati Watanzania wakiwa mapumzikoni kukumbuka siku ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kilichotokea miaka 16 iliyopita jijini London, Uingereza.
Mapema, dawati la Oparesheni Fichua Maovu (OFM) lilipata taarifa kutoka kwa Koko, akilalamika kuwa amenasa meseji kwenye simu ya mtu wake, ikionyesha mawasiliano na mwanaume mwingine, wakipeana ahadi ya kukutana ufukweni siku hiyo, ambazo zilikuwa na viashiria vyote vya kimahaba.
Koko alidai kwa muda mrefu, mwenzake huyo anayeishi naye Mabibo jijini Dar, alikuwa na tabia ya kuendekeza michepuko bila kujali kuwa wanatarajia kufunga ndoa Novemba mwaka huu na mara kwa mara amekuwa akiwalalamikia mashemeji zake lakini wamekuwa wakimuona muongo.
“Mpaka nimeamua kuja kwenu nataka mnisaidie jamani maisha yangu hayana amani kabisa, naomba mnisaidie nimnase mbaya wangu na hii tabia ikome kwa wote wenye mambo kama hayo. Mbaya zaidi kwao hawajui kama ananisumbua, hivi nataka mashemeji zangu wamuone ndugu yao anachonifanyia,” alisema Koko.
Koko aliwakusanya shemeji zake na OFM ikiongozana na wanausalama, waliondoka kuelekea Coco Beach ambako baada ya msako mkali miongoni mwa mamia ya watu waliokuwa ‘wakila bata’, walifanikiwa kuwaona wawili hao wakiwa wamekaa pembeni peke yao wakiendelea kujinafasi.
Baada ya kuwaona huku makamanda wa OFM wakianza kukusanya ushahidi kwa kupiga picha, mwanaume alishindwa kuvumilia na kuanzisha timbwili kali kwa mgoni wake, ambaye alipoona ‘jeshi’ kubwa likimsogelea, alilazimika kukimbilia ndani ya bahari huku akifukuzwa na mwenye mali.
Baada ya mchepuko kukimbia, Koko alirejea kwa Lolo na kuendeleza mashambulizi, ambayo hata hivyo yalidhibitiwa na mashemeji waliotaka suala hilo kumalizwa kwa mazungumzo. Katika utetezi wake, Lolo alidai aliamua kujifariji ufukweni kwa vile mara nyingi mpenziwe huyo hujifanya yuko bize, hoja ambayo haikukubaliwa kuwa kigezo cha kuchepuka

Saturday, October 3, 2015

FUMANIZI LA AINA YAKE SINZA, DAR...WAFUMWA LIVE CHUMBANI, KIDUME AKIMBILIA DARINI!SOMA ZAIDI

HILI ni fumanizi la aina yake! Achana na mafumanizi ya kawaida ambayo yamezoeleka, la safari hii ni la kipekee baada ya mgoni aitwaye Kibole Kalepe kukutwa chumbani na mke wa mtu, Asha Hemedi (pichani) kisha kukurupuka na kupanda darini haraka kukwepa kipigo, Ijumaa lina mkasa kamili. 

Mbaba Kibole Kalepe akiwa darini kuepusha kipigo baada ya fumanizi. Tukio hilo lililofunga umati wa watu wapenda ubuyu lilijiri Oktoba 28, mwaka huumaeneo ya Iteba-Sinza, jijini Dar baada ya mwenye mali, aitwaye Fikiri kurejea ghafla nyumbani na kumkuta mkewe akiwa chumbani na Kibole wakifanya yao.

Mke wa mtu, Asha Hemedi akihamaki baada ya fumanizi. SIKU YA TUKIO
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio Fikiri ambaye ni dereva wa masafa marefu aliaga kwamba anasafiri lakini akiwa hajafika mbali, gari liliharibika na kurudi nyumbani kuchukua vifaa na kabla hajagonga mlango, alisikia sauti ya mkewe na Kibole.

Mke wa mtu, Asha Hemedi akitaitiwa eneo la tukio. UVUMILIVU WAMSHINDA
Chanzo hicho kilizidi kushusha mistari kwamba, baada ya kusikia sauti hizo, Fikiri hakuweza kuvumilia aliamua kuwakatisha kwa kuwagongea mlango huku akitaja jina la mkewe ili amfungulie lakini hata hivyo ilichukua muda mrefu mlango kufunguliwa.
Makamanda wa Polisi wakimsindikiza Kibole Kalepe kwenye gari kuelekea kituo cha Polisi Magomeni. MLANGO WAFUNGULIWA
“Mume aliendelea kugonga mlango, baada ya muda mrefu kupita ukafunguliwa ambapo mke alikutwa akiwa ameloa jasho na kuhema kwa kasi kutokana na hofu, hata hivyo alikua amefunga khanga moja tu...

Mke wa mtu Bi. Asha Hemedi naye akichukuliwa na Polisi kuelekea kituoni.MGONI JUU YA DARI
“Mume alipoangalia kila kona kumtafuta mwanaume aliyekua naye hakumuona na alipochungulia darini alimuona mgoni wake amejificha, baadaye aliomba wapigiwe simu polisi waje kumuokoa,” kilisema chanzo.

Mtuhumiwa Kibole Kalepe na mke wa mtu wakiwa chini ya ulinzi wa Polisi. ACHIMBWA MKWARA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kwamba, wananchi wapenda mambo ya watu waliokuwa wamezingira nyumba hiyo walimwambia yeye ni mwizi hivyo watamshushia kipondo hevi, mgoni huyo alikataa na kudai kwamba hakuwa mwizi bali mgoni hivyo wasimuue.
“Jamani mimi siyo mwizi mimi ni mgoni, niitieni polisi,” alisikika Kibole.

Raia wakiwazodoa wagoni wakati wakipelekwa Kituo cha Polisi Magomeni. POLISI WAMTAITI
Wananchi walimuelewa wakaita polisi ambapo ndani ya muda mfupi walifika na kumshusha darini kisha kumkamata na mwananke wakawapeleka Kituo cha Polisi Magomeni.

Tuesday, July 14, 2015

AFUMANIWA GESTI AKIFANYA MAPENZI NA MUME WA DADA YAKE

Binti aliyetajwa kwa jina la Biena mkazi wa Kawe jijini Dar, hivi karibuni alipata aibu baada ya kufumaniwa ndani ya gesti (ipo maeneo hayohayo) akiwa na mume wa dada yake.
Biena akijificha baada ya fumanizi hilo.
Chanzo makini kilichokuwa eneo la tukio kilieleza kuwa, Biena na mume wa dada yake aitwaye Abasi wamekuwa na uhusiano kwa muda mrefu kabla ya juzikati kunaswa laivu wakiwa gesti.“Beina anaishi na dada yake aitwaye mama Saida, amekuwa akimzunguka kwa kutembea na shemeji yake hadi sisi majirani tukakereka.
“Sasa siku ya tukio mama Saida ambaye ni mjamzito alikuwa kalala, tukamuona  Abasi na Biena wakielekea gesti. Uzalendo ukatushinda, tukaona tumsaidie dada wa watu kuwafumania.“Tukaenda hadi kwenye ile gesti, tukawafumania wakiwa ndani, Abasi akaingia mitini mpaka leo hajulikani aliko, Beina akatoka na kukimbilia nyumbani kwa dada yake,” alisema mtoa habari huyo.
Akilia.
Mama mwenye nyumba aliyejitambulisha kwa jina la mama Farida alisema ni kweli binti huyo alikuwa akitembea na shemeji yake na majirani walichoshwa na hilo ndiyo wakaamua kumtolea uvivu. Biena alipobanwa alikiri kufumaniwa lakini akadai aliponzwa na tamaa ya chipsi kuku, akaomba msamaha kabla ya kurejeshwa kwao Tunduma. Mama Saida alipofuatwa na waandishi ili aongelee tukio hilo alishindwa kutokana na hali ya

Tuesday, June 23, 2015

MWENYE MKE ACHOMWA KISU NA MGONI!

Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
Riego Solo (28), mkazi wa Mbezi ya Tangi Bovu, Dar es Salaam anadaiwa kuchomwa kisu kwenye koromeo katika jaribio la kuchinjwa na mgoni wake aliyejulikana kwa jina moja la Jacob akiwa katika harakati za kumzengea mkewe.
Riego Solo (28), mkazi wa Mbezi ya Tangi Bovu akiuguza maumivu baada ya kuchomwa kisu na mgoni wake.
Tukio hilo la kinyume na kawaida ya wanaofumania kufanya uhalifu, lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita, Mbezi ya Tangi Bovu.
Taarifa zilizopatikana katika eneo la tukio zinadai kwamba, Solo alivamiwa na mgoni wake huyo hatua chache toka nyumbani kwake ambapo wananchi walimsaidia baada ya kupiga kelele na walipofika eneo la tukio walimkuta akitokwa na damu  huku akihangaika chini.
Akiuguzwa na mke wake aliyemsababishia kujeruhiwa na mgoni wake.
Uwazi baada ya kupata taarifa hizo, lilimfuata Solo nyumbani kwake akiwa ametoka Hospitali ya Mwananyamala, Dar alikolazwa.
Mwanaume huyo alikiri kufanyiwa jaribio la uchinjwaji shingoni na mgoni wake huyo. Alisema:
“Siku hiyo nilikuwa nimetoka kazini. Nilipofika nyumbani, sikukuta chakula, mke wangu alikuwa hajapika. Nikaamua kwenda kununua chakula mahali lakini karibu na hapa kwangu.
Akiwa amepumzika huku akiwa anasikilizia maumivu.
“Nikiwa njiani saa mbili usiku, nilivamiwa na mtu. Alinipiga kwanza kabla ya kuniwekea kisu shingoni, akanijeruhi. Lakini nilimwangalia vizuri nilimjua kuwa ni mgoni wangu, Jacob.
“Tulipambana naye, nikamzidi nguvu lakini tayari alishanijeruhi kwa kunichinja shingoni. Alikimbia huku akiniacha nikigaragara chini. Nilipiga kelele kuomba msaada. Naamini alikuwa na lengo la kuniua ili amrithi mke wangu lakini Mungu ni mkubwa bado nipo hai.
“Huyu Jacob, kuna wakati niliwahi kumuonya kuhusu mke wangu aachane naye, aliniambia amemuacha, hatarudia tena kutembea naye. Lakini cha kushangaza bado akawa anamnyemelea na amekuwa akijificha karibu na hapa kwangu. Watu ndiyo huwa wananiambia, sasa amenijeruhi.
“Kwa kweli Mungu mkubwa, aliyeniokoa wa kwanza ni dada mmoja anayenifahamu, alinikuta nikigaragara chini naye akapiga kelele. Watu walikuja na kunichukua hadi Kituo cha Polisi Kawe na kuchukua PF3 kwa ajili ya matibabu, nikapelekwa Hospitali ya Mwananyamala.
“Nilishonwa nyuzi kadhaa na kuwekewa ‘dripu’,  baadaye niliruhusiwa kurudi nyumbani lakini hali yangu ilibadilika ikabidi nirudishwe tena Hospitali ya TMS. Kwa sasa mke wangu aliyetaka kusababisha nipoteze uhai ndiye huyu anayeniuguza, bado nampenda, sitamwachia.”

Monday, June 22, 2015

AIBU KUBWA DAR! ANKO ANASWA GESTI NA MTOTO WA DADAKE WA MIAKA 14 TU WAKIFANYA YAO!

Binti anayesadikiwa kurubuniwa na anko yake. MCHAPO KAMILIGabriel Ng’osha
Tap! Jamaa mmoja, mkazi wa Gongo la Mboto-Mzambarauni jijini Dar ambaye jina lake halikufahamika amewekewa mtego wa nguvu kisha kunaswa akiwa katika harakati za kutaka kujivinjari na binti wa miaka 14, ambaye ni mtoto wa dada yake wa tumbo moja (jina linahifadhiwa).
Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lilijiri hivi karibuni ambapo ‘anko’ huyo ambaye ni dereva wa magari ya benki maarufu jijini Dar, alidaiwa kumsumbua binti huyo wa sekondari kwa muda mrefu.
Ilisemekana kwamba, kwa mujibu wa binti huyo, anko wake alikuwa akimnunulia soda baridi na kumuahidi kuendelea kumfanyia hivyo endapo atakubali ombi lake.

...Anko akiwa amewekwa chini ya ulinzi. Ilidaiwa kwamba, baada ya kuona usumbufu umezidi, binti huyo aliamua kukisanua kwa mzazi wake ndipo mtego bab’kubwa’ ukawekwa.

MAKUTANO GESTI
Baada ya mzazi kumpa mbinu zote za kuhakikisha hajirahisishi kwa mjomba wake, alitakiwa kumseti ili aumbuke ndipo binti akakubaliana na mjomba huyo wakutane gesti (jina kapuni) iliyopo maeneo hayo ya Mzambarauni.

KIBANO
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, mjomba mtu akiwa anajiandaa ‘kumtoa kafara’ mtoto wa dada yake ndipo dada mtu na shemeji yake wakaibukia gesti chumba namba 02 na kuzua timbwili la kukata na mundu kwa kumtia mtuhumiwa mikononi kwa msaada wa polisi.

Baada ya kutiwa mikononi na baba wa mtoto wa kike, aliamua kumpeleka hadi kwa askari mmoja anayelinda benki na kumpaki gari kwa lengo la kumpeleka mtuhumiwa kwenye kituo kidogo cha polisi kilichopo maeneo hayo ya Mzambarauni.
Hadi ‘shushushu’ wetu anaondoka kituoni hapo, jamaa huyo alikuwa akihojiwa huku akiomba suala hilo wakalimalize nyumbani.

Wednesday, June 17, 2015

Aibu Kubwa:Afumaniwa Gesti na Mume wa Dada Yake..

Binti aliyetajwa kwa jina la Biena mkazi wa Kawe jijini Dar, hivi karibuni alipata aibu baada ya kufumaniwa ndani ya gesti (ipo maeneo hayohayo) akiwa na mume wa dada yake.

Chanzo makini kilichokuwa eneo la tukio kilieleza kuwa, Biena na mume wa dada yake aitwaye Abasi wamekuwa na uhusiano kwa muda mrefu kabla ya juzikati kunaswa laivu wakiwa gesti.
  “Beina anaishi na dada yake aitwaye mama Saida, amekuwa akimzunguka kwa kutembea na shemeji yake hadi sisi majirani tukakereka.

“Sasa siku ya tukio mama Saida ambaye ni mjamzito alikuwa kalala, tukamuona  Abasi na Biena wakielekea gesti. Uzalendo ukatushinda, tukaona tumsaidie dada wa watu kuwafumania.

“Tukaenda hadi kwenye ile gesti, tukawafumania wakiwa ndani, Abasi akaingia mitini mpaka leo hajulikani aliko, Beina akatoka na kukimbilia nyumbani kwa dada yake,” alisema mtoa habari huyo.

Mama mwenye nyumba aliyejitambulisha kwa jina la mama Farida alisema ni kweli binti huyo alikuwa akitembea na shemeji yake na majirani walichoshwa na hilo ndiyo wakaamua kumtolea uvivu.

Biena alipobanwa alikiri kufumaniwa lakini akadai aliponzwa na tamaa ya chipsi kuku, akaomba msamaha kabla ya kurejeshwa kwao Tunduma. Mama Saida alipofuatwa na waandishi ili aongelee tukio hilo alishindwa kutokana na hali yake.

Sunday, June 14, 2015

MUME WA MTU APIGA PICHA ZA UTUPU NA MCHEPUKO!

mume wa mtu huyo akiwa na mchepuko.
 Dawa ambaye ni mume wa mtu, amedaiwa kujipiga picha za utupu akiwa na mchepuko wake uliofahamika kwa jina moja la Irene kisha kusambaa mitandaoni.Picha za wawili hao wenyeji wa Wilaya ya Lamadi, mkoani Simiyu zimedaiwa kuvuja mara baada ya rafiki wa Irene kuziiba kwenye ‘laptop’ ya Kaloli na kuzisambaza mtandaoni. 

Imedaiwa kuwa rafiki wa Irene ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alizivujisha picha hizo baada ya kugombana na Irene.Imeelezwa kuwa, vijana hao ni watoto wa wafanyabiashara wakubwa hivyo kitendo cha kusambaa picha hizo kimewasononesha.
Mwanahabari wetu aliwatafuta wahusika hao kwa njia ya simu. Irene simu yake haikuwa hewani lakini Kaloli alipatikana na kufunguka:Mwandishi: Habari? Unazungumza na mwandishi wa Global Publishers, nazungumza na Kaloli?
Kaloli: Ndiyo mimi.
Mwandishi: Tunazo picha zako hapo ukiwa uchi wewe na mpenzi wako Irene.
Kaloli: Mmezipataje hizo picha? Mwandishi: Picha zimetapakaa kwenye mitandao ya kijamii.
Kaloli: ‘Plizi’ naomba usitoe hiyo habari.
Mwanahabari wetu alikwenda mbali zaidi kwa kumtafuta mzazi wa Kaloli, Mzee Kaloli kumsikia anazungumziaje tukio hilo.“Ni kweli nimeziona hizo picha yaani ni aibu sana kwangu maana mimi ni mtu na heshima zangu na nimeshamkanya mara kadhaa mwanangu aachane na huyo Irene lakini hata hasikii.
“Asiyesikia la wazazi atafunzwa na ulimwengu nimeshaongea sana na Kaloli atulie na mkewe na hata huyo Irene mbona king’ang’anizi hivyo wakati mwanangu ana mke wake tena ana mtoto mdogo?  Wataniua kabla ya umri wangu nimechoka na tabia za Kaloli ananitia aibu,” alisema Mzee 

Wednesday, May 27, 2015

Mke amkodia Mchepuke wa Mumewe KIBAO KATA kumsuta akiwa Kazini...Matukio katika Picha

 
MWANAMKE mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja, mwishoni mwa wiki iliyopita alijikuta katika wakati mgumu baada ya kundi la wanawake kumvamia kazini kwake na kuanza kumsimanga kwa kitendo chake cha kuchepuka na mume wa mtu huku akipigiwa ngoma maarufu kama kibao kata. 
Wakimsimanga kwa staili ya kusasambua.
Tukio hilo lilitokea Mei 23 mwaka huu maeneo ya Kimara Mwisho, ambapo awali mke wa mume aliyechepuka, aliyejitambulisha kwa jina moja la Upendo, alidai mara kwa mara amekuwa akipokea taarifa kuwa mwanamke huyo anatembea na mumewe jambo lililomfanya amtafute, lakini alikataa katakata, akidai wao ni marafiki wa kawaida.
Akizungumza na waandishi wetu, mke huyo wa mtu alisema baada ya kuzungumza na mumewe mambo hayo yaliisha, lakini siku chache zilizopita aliiona simu ngeni ndani ya gari la mumewe, alipoipiga akagundua kuwa ni ya mwanamke huyo, jambo lililoibua upya mgogoro baina yao.
Ngoma ya kibao kata ikilindima wakati wa zoezi hilo.
“Nilimalizana na mume wangu lakini safari hii nikampigia simu yule mwanamke na kumpa tahadhari, lakini majibu aliyonipa nilipata hasira sana, eti alisema kama namchunga sana mume wangu basi nimjengee zizi nimfungie. Nikaona hizo ni dharau, nikaamua lazima nimsute,” alisema Upendo.
Kama  hiyo haitoshi mke huyo wa mtu alisema kuwa siku moja alipata taarifa kuwa mumewe amepigwa chupa na mchepuko huo, kisa kikiwa ni wivu wa kimapenzi ambapo katika sekeseke hilo gari yake ilivunjwa kioo jambo lililomzidisha hasira kiasi cha kumtafutia kibao kata.
Waandishi wetu waliokuwa katika kusaka matukio walilinasa tukio hilo ambapo walishuhudia umati wa kina mama wa mjini walioshushwa eneo hilo kutoka kwenye gari aina ya kirikuu, wakimvaa mwanamke huyo aliyekuwa saluni kwake bila habari kama ngoma hiyo imemfuata ili asutwe na mwenye mali.
Mke anayedai kuibiwa mumewe.
Katika hali ya kushangaza, ghafla aliwachoropoka na kutoka mbio kukimbilia chooni katika nyumba ya jirani na kujifungia ndani  huku juhudi za kumtoa zikishindikana.
Kama hiyo haitoshi ngoma ya kibao kata iliendelea kupigwa huku wakina mama wakimwaga radhi waziwazi, wakimchamba vilivyo huku mtaa ukiwa umefungwa kwa muda, kuhakikisha tabia ya mwanamke huyo inajulikana mtaa mzima hali iliyofanya umati wa watu kujaa wakitaka kushuhudia nini kinachotokea eneo hilo.

Friday, May 15, 2015

PADRI KATOLIKI ANASWA KICHAKANI AKINGONOKA

Waandishi wetu
KAMA mti mbichi unatenda haya, itakuwaje kwa mti mkavu?! Ndivyo inavyoweza kutafsiriwa kwa Katibu Mtendaji wa Idara ya Mawasiliano wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (Tanzania Episcopal Conference, TEC), Padri Anatoly Salawa kufuatia kunaswa kichakani akiwa na mrembo.
Padri Anatoly Salawa akitaharuki baada ya fumanizi hilo.
NI SAA 8: 02 USIKU
Kiongozi huyo wa dini alinaswa hivi karibuni majira ya saa 8: 02 usiku akiwa ndani ya gari aina ya Toyota RAV 4 lenye nambari ya usajili T 674 ADA kwenye kichaka kilichopo maeneo ya viwanda na gereji za magari makubwa, Kurasini jijini Dar.
Gari aina ya Toyota RAV 4 lenye nambari ya usajili T 674 ADA alilonaswa nalo Kiongozi huyo wa dini.
OFM WAPIGIWA SIMU
Huku mvua kubwa ikinyesha na baridi ikipuliza vilivyo achilia mbali baadhi ya maeneo ya jiji kutotulia kwa mafuriko na foleni, Makamanda wa Operesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers walipigiwa simu na mlinzi mmoja wa Kimasai wa kwenye gereji hizo na kunyetisha juu ya gari lililosimama karibu na eneo lao la lindo huku likinesanesa.
Mrembo aliyenaswa kichakani na Kiongozi wa dini.
Mlinzi huyo alieleza kuwa yeye na wenzake walilichunguza kwa makini gari hilo na kuona kuwa ndani yake kulikuwa na watu wawili wa jinsi tofauti lakini walishindwa kujua wazi kilichokuwa kikiendelea.
“Yero mpo wapi? Sisi ‘tumesa piga’ simu polisi wanakuja hapa fanyeni haraka, mnaweza kupata picha wakati hawa watu wanatimuliwa maana wapo vichakani hapa mita kama 20 kutoka barabarani. Tuna wasiwasi, huenda ni watu wabaya ‘wametufamia’,” alisema mlinzi huyo kwa lafudhi ya Kimasai.
Padri Anatoly Salawa akiwa pembeni ya gari.
WALINZI WAINGIWA SHAKA
Mlinzi huyo alisema kuwa mara kwa mara gari kama hilo  limekuwa likifika hapo majira ya usiku wa manane hivyo kuwafanya kuingiwa na shaka na kuamua kutafuta namba za simu za polisi na OFM.
“Hili gari huwa linakuja hapa mara kwa mara hivyo ikatulazimu kutafuta namba zenu OFM ili kama kuna maovu yanafanyika mje kuyafichua,” aliongeza mlinzi huyo. 
Toyota RAV 4 lenye nambari ya usajili T 674 ADA kwa ndani.
ENEO LA TUKIO
OFM, wakiwa na gari aina ya Toyota Cresta GX 100, walifika eneo la tukio ndani ya muda mfupi na kuwakuta polisi nao wakiwasili kisha kuchukua kwanza maelezo kwa walinzi hao bila kuwashtua wahusika kwenye gari.
Baada ya mahojiano na walinzi hao, walilifuata gari hilo na kulipekua ambapo hawakuamini macho yao baada ya kumkuta mtu mzima huyo katika gari hilo akiwa na mrembo aliyekuwa mtupu.
Mrembo huyo akifaa nguo baada ya kunaswa.
PADRI ADAI KUINGILIWA STAREHE ZAKE
Huku mvua ikiendelea kumwagika, padri huyo alionekana akiwa ametaharuki ndani ya gari asijue la kufanya.
Mara baada ya kuwanasa wawili hao, padri alijitetea kwa kusema kuwa, alikuwa ameingiliwa na wahuni katika starehe zake hivyo aliingia kwenye gari na kutimua na mrembo wake.
ATAFUTWA TENA
Kabla gazeti hili halijakwenda mitamboni, jana lilimtafuta tena padri huyo ili kama ana la ziada la kusema alitoe lakini simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa na baadaye ikazimwa kabisa.
SMS YA KWANZA YADUNDA
Baada ya muda simu hiyo iliwashwa tena na ndipo  alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (SMS) iliyosomeka; ‘mimi ni mhariri wa Gazeti la Ijumaa, naomba upokee simu, nina jambo muhimu sana la kuongea na wewe’. Hata hivyo, SMS hiyo haikujibiwa.
Padri Anatoly akijistili baada ya tukio hilo.
SMS YA PILI NAYO KIMYA!
Baada ya SMS hiyo, padri huyo aliendelea kupigiwa simu lakini bado iliita bila kupokelewa ndipo akatumiwa ujumbe mwingine uliosomeka hivi; ‘mkuu tumepata tukio lako ukiwa kichakani ndani ya gari usiku na mrembo akiwa mtupu. Wewe unalizungumziaje tukio hili? Kwa maana nyingine unajiteteaje? Tunaomba maelezo yako’.
Kama ilivyokuwa kwa ujumbe wa kwanza, nao huo haukujibiwa.
IJUMAA LATINGA KANISA LA MTAKATIFU JOSEPH
Ili kuendelea kumsaka padri huyo baada ya ukimya wa meseji, gazeti hili lilitinga kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph Jimbo Kuu la Dar es Salaam kwa lengo la kuomba msaada wa mawasiliano mengine kama yapo.
Hata hivyo, muumini mmoja aliyekutwa eneo hilo alisema mtu anayeweza kusaidia kupatikana kwa Padri Anatoly ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Tarcisiius Ngalalekumtwa.“Mimi sina namba yake, anayeweza kukusaidia ni (Tarcisiius) Ngalalekumtwa. Kwani ana nini huyo Padri Anatoly?”
Ijumaa: “Tukikutana na Ngalalekumtwa tutamwelezea. Lakini asante kwa ushirikiano wako.”
BOSI WAKE ASAKWA LAKINI.
Gazeti hili lilimtafuta bosi wa padri huyo Ngalalekumtwa ili kujua ana lipi la kusema juu ya tukio hilo lakini jitihada hizo ziligonga mwamba hivyo jitihada zinaendelea.
Mrembo akificha sura yake baada ya tukio hilo.
WALINZI WARUDIWA
Juzi mchana, Ijumaa liliwarudia walinzi hao wa Kimasai na kuwauliza kama wanamjua mtu aliyekuwa ndani ya gari hilo.
Mlinzi: “Sisi tulimuona kama mtu asiyefaa kwetu maana gari likija usiku tunakuwa na wasiwasi wa kuvamiwa. Kwa hiyo tunajiami kwa njia yoyote.”
Ijumaa: “Yule mrembo mnamjua kabla ya tukio la jana?”
Mlinzi: “Hapana. Hatujawahi kuonana na yeye.”
NGOMA BADO MBICHI
Ijumaa ndilo limeanzisha mwendo, magazeti mengine Pendwa ya Global Publishers yanafuatia. Endelea kusoma ili kujua kwa undani kuhusu tukio hilo. Mrembo ni nani na kwa nini walikuwa pale usiku huo?