Binti aliyetajwa kwa jina la Biena mkazi wa Kawe jijini Dar, hivi karibuni alipata aibu baada ya kufumaniwa ndani ya gesti (ipo maeneo hayohayo) akiwa na mume wa dada yake.
Chanzo makini kilichokuwa eneo la tukio kilieleza kuwa, Biena na mume wa dada yake aitwaye Abasi wamekuwa na uhusiano kwa muda mrefu kabla ya juzikati kunaswa laivu wakiwa gesti.
“Beina anaishi na dada yake aitwaye mama Saida, amekuwa akimzunguka kwa kutembea na shemeji yake hadi sisi majirani tukakereka.
“Sasa siku ya tukio mama Saida ambaye ni mjamzito alikuwa kalala, tukamuona Abasi na Biena wakielekea gesti. Uzalendo ukatushinda, tukaona tumsaidie dada wa watu kuwafumania.
“Tukaenda hadi kwenye ile gesti, tukawafumania wakiwa ndani, Abasi akaingia mitini mpaka leo hajulikani aliko, Beina akatoka na kukimbilia nyumbani kwa dada yake,” alisema mtoa habari huyo.
Mama mwenye nyumba aliyejitambulisha kwa jina la mama Farida alisema ni kweli binti huyo alikuwa akitembea na shemeji yake na majirani walichoshwa na hilo ndiyo wakaamua kumtolea uvivu.
Biena alipobanwa alikiri kufumaniwa lakini akadai aliponzwa na tamaa ya chipsi kuku, akaomba msamaha kabla ya kurejeshwa kwao Tunduma. Mama Saida alipofuatwa na waandishi ili aongelee tukio hilo alishindwa kutokana na hali yake.