Showing posts with label BONGO MOVIE. Show all posts
Showing posts with label BONGO MOVIE. Show all posts

Thursday, December 3, 2015

JB abainisha kinachoiua sanaa!

JBMkongwe wa filamu Bongo, Jacob Stephen ‘JB’.
MKONGWE wa filamu Bongo, Jacob Stephen ‘JB’ ameweka wazi kinachochangia sanaa ya filamu ionekane kama imepwaya na kukosa thamani katika soko kuwa ni wasanii kuishiwa ubunifu na mipango mikakati ya kuendana na mabadiliko ya teknolojia.
Akichonga na kona ya Bongo Movies, JB alisema kuwa sanaa kama sanaa ipo na kamwe haiwezi kufa, isipokuwa vizazi ndani ya sanaa ndiyo hubadilika kulingana na nyakati, lakini mtu yeyote anaweza kuja na kitu kipya kinachogusa maisha ya kawaida na kuwika, kuliko hata waigizaji wakongwe.
“Kwani muziki wa Kongo si ulionekana kama umekufa, lakini baada ya Koffi Olomide kuachia Ngoma ya Selfie, muziki wao haujarejesha heshima yake? Kwa hiyo sanaa huwa haifi ila watu ndiyo huishiwa.

Sunday, January 4, 2015

MADHARA YA USAFIRI NA MISONGAMANO YA WATU VICHOCHEO VYA MAGONJWA

Ni wazi kuwa wengi wanatumia usafiri wa
umma kwa sababu ya uwezo, lakini unayo
madhara yake mengi kwa afya zao
Asubuhi inapofika, aghalabu asilimia 80 ya
Watanzania huongoza njia kutafuta usafiri


wa umma kwa ajili ya kuelekea katika
shughuli zao mbalimbali ambazo ni pamoja
na kujitafutia riziki.
Usafiri unaotumiwa zaidi ni wa mabasi ya
abiria, maarufu kwa majina mbalimbali hasa
daladala.
Hata hivyo, ndani ya daladala kuna kero
kubwa ya msongamano wa watu, ambao
haumpi abiria hata nafasi ya kupumua,
kupata hewa safi, kupiga chafya kwa
ustaarabu, kupenga au hata kukohoa.
Si hivyo tu kwani maeneo mengi nchini ni
yenye msongamano wa watu na ni makazi
yasiyopimwa. Hiki ndicho chanzo cha
kuenea kwa maradhi mengi kwa
Watanzania walio wengi.

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya Kifua
Kikuu Duniani, yaani Machi 24, imebainika
kuwa msongamano wa watu hasa kwenye
vyombo vya usafiri huenda kukawa ndicho
chanzo cha kuenea kwa maradhi hayo.
Hivi karibuni, Shirika la Afya Duniani (WHO)
lilitangaza kuwa watu milioni saba duniani
hufa kila mwaka kutokana na uchafuzi wa
hewa na nusu ya watu hao hufa kwa
sababu ya kuvuta hewa chafu kwenye
maeneo ya ndani yenye msongamano wa
watu.

"Ni lazima tupumue, na ndiyo maana ni
vigumu kuzuia maambukizi ya uchafuzi
huu," anasema mkurugenzi wa utafiti wa
mazingira wa Chuo cha Mazingira cha Kings,
Uingereza
WHO inaeleza kuwa, hewa chafu inayovutwa
kwenye mazingira husababisha vipande
vidogo vidogo kuingia kwenye mapafu na
kusababisha muwasho, na kudhurika moyo
jambo linalosababisha maradhi sugu ya
moyo au shinikizo la damu.

Kwa mwaka 2012, kulikuwa na vifo milioni
43 vilivyosababishwa na uchafuzi wa
mazingira wa ndani kwa ndani kama vile
msongamano wa watu, kupikia ndani kwa
kutumia kuni au mkaa.
Shirika hilo lilishauri kuwa ni vyema watu
wakaepuka kusafiri wakati wa
msongamano mkubwa, au kuepuka maeneo
yenye viwanda na kuacha tabia za kupika
ndani ya nyumba kwa mkaa au kuni.
Kwa mfano, msongamano unachangia
maradhi ya saratani wakati wa kuzaliwa,
kiharusi na maradhi ya moyo.

Utafiti uliofanywa na Robert Msigwa wa
Chuo Kikuu cha Dalian, China, kitengo cha
Sayansi ya Hesabu kuhusu madhara ya
usafiri wa umma Tanzania, ulibaini kuwa,
kwa kipindi cha miaka 12 (2000 hadi 2012)
Tanzania imezalisha tani 86,000 za hewa
chafu na kutokana na usafiri, msongamano
wa watu na magari yanayozalisha hewa
chafu. Uchafuzi huu husababisha maradhi
ya macho na mfumo wa hewa.
Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani ya
mwili na ya Mfumo wa Hewa, Meshack
Shimwela anatolea mfano wa usafiri wa
daladala na kusema kuwa maradhi ya Kifua
Kikuu wakati mwingine husambaa kwa
sababu ya msongamano kwenye daladala.

"Iwapo madirisha yamefungwa ndani ya
basi la abiria, watu wamesongamana na
ndani kuna mgonjwa wa Kifua Kikuu
anayekohoa, hapo maambukizi huweza
kutokea," anasema.
Anasema hata hivyo iwapo mgonjwa wa TB
hajakohoa na madirisha ya gari yapo wazi,
hewa inaingia, basi hakuna maambukizi
yoyote yanayoweza kutokea.

Anaongeza kuwa, maradhi ya ngozi pia
huweza kusambazwa iwapo watu waliopo
kwenye msongamano wa basi la abiria
watakuwa wamegusana kwa kipindi fulani
na mtu asiye na maradhi kama hatanawa
kwa maji na sabuni baada ya muda mfupi.
Msongamano wa watu na magari
unasababisha maradhi ya ngozi, ajali,
zinaweza kutokea, msongamano watu
husababisha pia watu hao hutupa taka
hovyo jambo linalochochea kuenea kwa
maradhi.

Mtaalamu wa Mazingira kutoka Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam, Dk Frederick Mwanuzi
yeye analigusia suala hili katika pande mbili,
kwanza anasema msongamano wa watu
hasa ndani ya vyombo vya usafiri
husababisha kutokea kwa ajali
zinazosababisha vifo.

Pia, anaeleza kuwa, watu
wanaposongamana eneo moja ni rahisi
zaidi kuchafua mazingira kwa kutupa taka
hovyo ambazo nazo kwa upande mwingine
zinasababisha kuenea kwa maradhi.
"Lakini pia, maradhi ya mfumo wa hewa ni
rahisi kuambukizwa katika eneo lenye
msongamano wa watu, maradhi kama TB
husambaa kwa urahisi maeneo haya"
anasema Dk Mwanuzi.

Ripoti nyingi zinaeleza kuwa ongezeko la
idadi ya watu sambamba na lile la magari
yanayotumia mafuta kama ya dizeli na petrol
husababisha maradhi. Inaelezwa kuwa
kufuka kwa moshi wa magari, treni na
pikipiki zinazotumia mafuta hayo huchangia
uchafuzi wa mazingira ambao kwa kiasi
kikubwa husababisha maradhi ya mfumo
wa hewa kama pumu na mafua.

Wakati huo huo, Dk Innocent Godman,
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akili na
Ushauri Nasaha kwa watumiaji wa dawa za
kulevya, yeye anaona athari kubwa zaidi
kwenye msongamano wa magari ambao
huwaathiri wanaadamu moja kwa moja.

Dk. Godman anasema msongamano wa
magari, husababisha uchafuzi wa mazingira
kwa kiasi kikubwa lakini pia husababisha
msongo wa mawazo kwa madereva na
abiria.
"Watu wanapokaa kwenye foleni kwa muda
mrefu, hupata msongo wa mawazo, ambao
husababisha hasira za kupoteza kipato na
kuchelewa kule wanakokwenda, hivyo
huweza kupata magonjwa ya akili,"anasema
Dk. Godman

Anasema, ndiyo maana si ajabu
kuwaona madereva na
makondakta wa usafiri wa umma
au hata magari ya watu binafsi,
wakitoleana lugha chafu hasa
kipindi cha msongamano mkubwa
wa magari.

"Maradhi yanayoingia moja kwa
moja mwilini mwa binadamu kwa
sababu ya msongamano wa watu
na magari ni maradhi ya mfumo
wa hewa, moshi wa kwenye
magari, msongamano ndani ya gari
husababisha watu kushindwa
kupata hewa safi na kuvuta hewa
yenye kemikali hatari," anasema.

Tuesday, December 30, 2014

JIMBO LA KOROGWE; MTO UMEPITA JIMBONI, MAJI NI SHIDA

Mbunge wa Korogwe Nasir akichangia hoja ya mafuta bungeni.
Makala:Mwandishi Wetu,
BAADA ya wiki iliyopita safu hii kutembelea Jimbo la Temeke, wiki hii tupo Jimbo la Korogwe Mjini linaloongozwa na mbunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuph
Abdallah Nassir.
Baadhi ya wapiga kura waliozungumza na safu hii walisema matatizo mengi ya Jimbo la Korogwe yanatokana na usimamizi mbovu wa viongozi wa ngazi za juu.
Wapiga kura wa Kitongoji cha Kilole, wao walizungumzia shida ya maji kwamba ni tatizo sugu kwao ambapo wakati wa kampeni ya ubunge mwaka 2010, mheshimiwa Nassir aliahidi kutatua shida hiyo.
“Sisi hapa Kilole kama unavyoona, Mto Pangani unapita hapa lakini maji ni shida! Tuliamini mbunge wa sasa angetatua tatizo hilo lakini imekuwa sivyo na muda wa uchaguzi mwingine huo unakuja 2015,” alisema Kilaviani, mkazi wa Kilole-Misufini.
Mbunge anajibu: “Kusema ukweli suala la maji kwa Kitongoni cha Kilole limekwisha kwa sehemu kubwa, si kama ilivyokuwa wakati naingia madarakani. Sehemu ambazo bado, naamini mpaka mwakani katikati litakwisha kabisa.”
Wapiga kura wa Kitongoji cha Manundu (Makao Makuu ya Wilaya ya Korogwe) wao walilia na miundo mbinu, hasa barabara kama kutoka maeneo ya maungano ya  Barabara Kuu ya Korogwe Moshi na kwenda Hospitali ya Wilaya Magunga.
“Sisi tunaomba barabara zitengenezwe, hasa zile za kuingia mitaani, kama ile ya kutoka barabara kuu ya kwenda Moshi na kwenda Hospitali ya Magunga.“Lakini pia uwanja wa mpira Korogwe hakuna. Uliopo hauleti moyo wa kuinua michezo hapa Korogwe,” alisema Jumanne, mkazi wa Manundu.
Mbunge anajibu: “Barabara nyingine zimetengenezwa katika kipindi changu. Unajua si rahisi sana kukamilisha barabara zote za jimbo lakini ni mkakati ambao unaendelea mpaka barabara zote zitakapokuwa sawa.”
UCHAKAVU WA MJI
Baadhi ya wapiga kura walizungumzia namna Manispaa ya Korogwe ilivyochakaa na kutoa taswira mbaya kwa mji huo ambao ndiyo katikati ya Mkoa wa Tanga.
“Korogwe ya sasa inaonekana kuchakaa sana. Ni wilaya ipo katikati na zamani kulikuwa na minong’ono kwamba Korogwe ingekuwa mkoa lakini kwa mwendo wa sasa sidhani kama inawezekana.
“Mji unaonekana kuchakaa sana, umekuwa mwekundu kwa sababu barabara ni vumbi tupu. Hii inaonesha hata uchumi wa wilaya upo chini kwa sasa kuliko zamani.
“Kuna ujenzi wa stendi mpya kule Mbugani, umesimama hadi sasa hakuna kinachoendelea. Mimi nadhani ili kusukuma gurudumu la maendeleo kwenye jimbo hili ni lazima kumpata mbunge mwenye nia ya dhati,” alisema Mwailengo, mkazi wa Manundu ambaye alisema yeye na Chadema ni damudamu.
Mbunge anajibu: “Wananchi wengine wanaamini hata ujenzi au ukarabati wa nyumba zao ni jukumu la mbunge. Nyumba anazosema zimechakaa ni za wananchi. Uchumi wa mtu mmojammoja unategemea namna familia ilivyo.
“Manundu ambayo ni makao makuu ya wilaya, nyumba nyingi ni za zamani, lakini watu kwa sasa wanajenga sana nje ya mji kama vile Majengo, Vetenari ambako viwanja vinapatikana kwa urahisi na wengi wamenunua kule.“Kuhusu stendi ni mkakati ambao unaendelea  na upo kwenye mpango wa mji, hakuna ubadhirifu au ufisadi kwenye ujenzi wa stendi hiyo.”
VITABU MASHULENI
Pia ni tatizo lililolalamikiwa sana na wapiga kura kwamba wanafunzi wanasoma katika uhaba wa vifaa vya kusomea.
“Mimi kama mpiga kura nadhani ninachoweza kukilalamikia ni vitabu mashuleni. Ni kilio cha muda mrefu sana,” alisema mama Musa, mkazi wa Majengo.Mbunge anajibu: “Wakati naingia madarakani suala la uhaba wa vifaa vya kufundishia lilikuwa sugu lakini kusema kweli nimepigania sana ambapo kama utatembea shule nyingi za jimbo langu watasema namna nilivyopambana.”
HUDUMA MBAYA HOSPITALI YA WILAYA
Wapiga kura wa Jimbo la Korogwe hawakuacha kuizungumzia Hospitali ya Wilaya ya Korogwe, Magunga ambapo walisema:
“Hii hospitali yetu ya wilaya tatizo kubwa ni wauguzi. Unaweza kufika pale na mgonjwa wako ukakaa naye mapokezi kwa muda mrefu hata kama ana hali mbaya. Hii inawauma sana wananchi wa Korogwe.
“Mimi iliwahi kunitokea siku moja, tumempeleka mgonjwa pale matokeo yake akakaa mapokezi kwa muda mrefu, baadaye tukaoneshwa baiskeli ya kumpakia mgonjwa wetu hadi chumba cha matibabu tena kwa kumsukuma sisi wenyewe, ni haki kweli?” alihoji Dan Joseph, mkazi wa Kitongoji cha Kitonga.
Mbunge anajibu: “Hilo linawezekana kwani kila muuguzi anakuwa na wito tofauti na wengine. Nitalifuatilia hilo. Lakini kusema kweli mimi na viongozi wengine tumekuwa tukipigania sana kuhakikisha huduma kwenye hospitali tena kama ile ya wilaya inakuwa ya kujituma kwa wauguzi.”
NENO LA MWISHO
Mwisho, Mbunge Nassir alisema kuwa, ni vyema kama kuna ahadi hajaitekeleza wapiga kura wakamfuata yeye lakini ni mbaya sana watu kuendesha kampeni za chini kwa chini na kusema maneno ya kumpaka matope hali inayomshangaza.
“Kuna ahadi nimetekeleza zipo ambazo bado, nawaomba wapiga kura wangu tushirikiane jamani. Tabia ya watu kuanza kampeni za chini kwa chini si nzuri,” alisema.

Saturday, December 27, 2014

Naibu Waziri Mhe. January Makamba azindua Kundi la Kaone Sanaa Group Dar Live

Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia .Mhe. January Makamba amezindua Kundi la Kaone Sanaa Group Dar Live usiku huu, hapa akiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo.
Wasanii wa Kaole wakiwa stejini
...akiongea na wanahabari mara baada ya kuwasili Dar Live
...akiwa katika picha ya pamoja na Kaone
...akiongozwa na Meneja Mkuu wa Dar Live, Abdallah Mrisho kwenda meza kuu
...akiwa meza kuu na viongozi wa Kaone
....msanii Msaga Sumu akifanya vitu vyake jukwaani

Friday, December 26, 2014

PATCHO MWAMBA AKANUSHA KUFUMANIWA, KUPIGWA

Patcho Mwamba akiwa katika ofisi za Global Publishers Ltd leo.
Patcho akipozi na mwandishi Nyemo Chilongani wa Global.
Picha ya Patcho iliyozua utata mitandaoni.
MWIGIZAJI na mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia, Patcho Mwamba hivi punde ameibuka katika ofisi za mtandao huu na kukanusha vikali taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa amefumaniwa akiwa na mke wa mtu na kupokea kipigo.
Akiongea na mtandao huu, Patcho amesema picha iiliyozagaa mitandaoni aliipost mwenyewe juzi baada ya kupata aleji ya macho ambapo baadaye ilisambaa mitandaoni ikidaiwa kuwa kapigwa baada ya fumanizi.
"Unajua nina aleji na pombe pamoja na vumbi, nikitumia tu pombe lazima macho yangu yavimbe
juzi nilikunywa Windhoek mbili na usiku hali yangu ikabadilika na macho kuvimba, baada ya tukio hilo niliamua kujipiga picha na kuipost katika mtandao wa Instagram na hapo ndipo balaa likazuka" Alisema Patcho akiwa katika ofisi za mtandao huu zilizopo Mwenge-Bamaga, Dar.

MAMA KANUMBA: KRISMASI KWANGU NI MBAYA...MWANANGU ANGEKUWEPO NINGEKUWA NA AMANI


Flora Mtegoa ambaye ni mama wa marehemu Steven Kanumba.
FLORA Mtegoa ambaye ni mama wa marehemu Steven Kanumba, amesema kuwa Sikukuu ya Krismasi kwake imekuwa mbaya kutokana na kifo cha mama yake mzazi kilichotokea mwaka huu tarehe na mwezi aliyofia Kanumba.
Akizungumza na Amani, mama Kanumba alisema kuwa anashindwa kuelewa ni kwa nini matatizo kwake yanakuja siku ambayo mwanaye Kanumba alifariki kitu ambacho kinampa wakati mgumu hadi akili yake inashindwa kufanya kazi.
“Siwezi kusema nina furaha wakati mama yangu hayupo na hiyo ndiyo inayonipa wakati mgumu wa kutokuwa na furaha kwenye maisha yangu, nina majonzi ya muda mrefu pengine Kanumba angekuwepo basi ningeweza kula kwa amani,” alisema

PICHAZ: MTUMZIMA SUPER STAR SINGER PATCHO MWAMBA ALA KIPIGO CHA MBWA MWIZI KWA KUBAMBWA NA MKE WA MTU!!

instagram.com/selfielife


Picha kwa hisani ya @selfielife instagram Inasemekana kuwa mwigizaji  na mwanamuziki wa Dansi Patcho Mwamba, amepewa kipigo cha nguvu hadi kumvimbisha uso kama unavyomuona hapo juu, baada ya kufumaniwa na mke wa mtu.

Habari hizi zinaenea kwa kasi zaidi mtandaoni kama moto wa vifuu…hakuna taarifa rasmi japokuwa hadi sasa Patcho au watu wake wakaribu hadi sasa hawajajitokeza  kukanusha taarifa hizi.