Showing posts with label Habari Za Mitaani. Show all posts
Showing posts with label Habari Za Mitaani. Show all posts

Sunday, June 19, 2016

Utameza Mate Kama Fisi! See What This Naughty Swahili LADY was Doing in Private (VIDEO)

Forget about Wadada wa Mjini and their fake dancing styles, Swahili ladies are the real deal.
They have mastered the skills of teasing men with seductive dance moves that leave little to one’s imagination.

See what this hot Swahili lady was doing in her house. 

Aliyelawiti Watoto Wawili Akijifanya Polisi Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 60 Jela

MAHAKAMA ya Wilaya ya Bunda, mkoani Mara imemhukumu, Ally Mpemba au Ustadhi (32), Mkazi wa Mtaa wa Bunda Stoo mjini Bunda kifungo cha miaka 60 jela baada ya kupatikana na hatia ya kubaka watoto wawili kwa zamu akijifanya polisi.

Adhabu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Bunda, Said Kasonso, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo pasipo kuacha shaka yoyote.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Hamuza Mdogwa, kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Januari 17 mwaka huu, majira ya saa 8:30 mchana, katika kijiji cha Kitaramanka wilayani hapa.

Alisema kuwa mshtakiwa huyo aliwakuta watoto hao wakiwa katika eneo hilo na akawatisha kuwakamata akidai kuwa yeye ni askari Polisi na kwamba wamefanya kosa hivyo atawachukua maelezo yao na baadaye awapeleke kituoni.

Aliongeza kuwa mshtakiwa huyo alitoa Sh 200 na kumpatia mtoto mmoja aende akanunue daftari la kuandikia maelezo yao, na baada ya mtoto huyo kwenda ndipo alipombaka aliyebaki na kisha kumwambia adhabu yake imekwisha sasa aende nyumbani.

Alisema kuwa baada ya yule aliyetumwa daftari kurudi, Mpemba alimbaka pia na kumuamuru arudi nyumbani adhabu yake imekwisha na kwamba watoto hao baada ya kufanyiwa unyama huo walikwenda kutoa taarifa nyumbani kwa wazazi wao.

Aidha alisema kuwa Ofisa Mtendaji wa kata hiyo kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji hicho walimkamata mshtakiwa huyo na kumfikisha Polisi.

Kabla ya adhabu kutolewa mshtakiwa huyo alipewa fursa ya kujitetea na akaiomba Mahakama hiyo impunguzie adhabu.

Hata hivyo mwendesha mashitaka huyo aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa huyo kwa sababu makosa aliyofanya ni ya kinyama na ya udhalilishaji mkubwa kwa watoto hao wenye umri wa miaka 16 kila mmoja.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Kasonso, alisema kuwa ameridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na kwamba kwa kosa la kwanza la kubaka mtoto wa kwanza ataenda jela miaka miaka 30 na la pili pia atatumikia kifungo cha miaka 30 jela na adhabu zote zinakwenda kwa pamoja hivyo atatumikia kifungo cha miaka 30 jela ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine wenye nia na tabia kama hiyo.

Monday, June 13, 2016

VIDEO: Jionee wizi mpya wa mpesa na tigo pesa, jamaa kaibiwa 720,000


http://mobilemarketingmagazine.com/wp-content/uploads/2015/08/M-Pesa-Mobile-Money-User-Tanzania-Africa.jpgUtapeli umekua mwingi sana hapa mjini, watu wengi wanatapeliwa kila siku. Kutapeliwa ni kutapeliwa tu haijalishi ujanja utakaotumika ni wa sasa au wa zamani. Ila siku za karibuni kumetokea aina mpya ya utapeli ambao wahathirika wakubwa ni watu wanaotoa huduma za Mpesa na Tigo Pesa.

Kama utakavyoona katika video hii ni ngumu sana kugundua kama umeshatapeliwa mpaka baada ya mdaya mda upite. Kwa mfano huyu jamaa aliyetapeliwa hapa kaibiwa 723,000 na matapeli hao. Hebu tazama video hii na wewe usije ukaibiwa kama huyu.


Tuesday, May 31, 2016

Fundi Mabasi Ajinyonga kwa Kuchoka Kuuguaugua!

Mwili wa marehemu Charles ldd Ngozoma ukiingizwa kwenye gari la polisi.
Hali tete! Mtu aliyetajwa kuwa ni Fundi Mkuu wa Kampuni ya Mabasi ya Al- Jabil ya mkoani hapa, Charles ldd Ngozoma mwishoni mwa wiki iliyopita alitoka nyumbani kwake, Msamvu na kwenda kujinyonga nyumbani kwa mdogo wake, Mwembesongo jirani na Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Usharika wa Bethel Revival Temple, Uwazi lilishuhudia mwili.
Mwili wa marehemu ukitolewa ndani ya chumba alichojinyongea huku wananchi wakishuhudia tukio hilo.
Tukio hilo lililojaza umati kutokana na umaarufu wa marehemu, saa 7 mchana wa Mei 26, mwaka huu nyumbani kwa Rajab ldd Ngozoma  ambaye ni mdogo wake huku kisa kikidaiwa ni marehemu huyo kuchoka kuugua mara kwa mara.
Akizungumza na Uwazi kuhusu madai ya kaka yake kujinyonga nyumbani kwake, Rajab alisema:
“Kaka alikuwa akiumwa mara kwa mara na leo kaja kwangu akaniambia kichwa kinamuuma, hivyo nikamnunulie dawa dukani.
“Cha ajabu, niliporeja na dawa, nimemkuta kaka akining’inia, amejinyonga chumbani kwangu.
“Awali alipofika alikuwa ameshika kitu mkononi, inaonekana alishika kamba ambayo ameitumia kujinyongea. Kule kunituma dukani ilikuwa ni njia ya kuniondoa ili apate uwanja mpana wa kujinyonga.”
Kwa upande wake, Mwinyimvua Rajab Ngozoma ambaye ni baba mdogo wa marehemu, alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, alisema:
“Marehemu ni mtoto wa marehemu kaka yangu, alipofariki dunia baba yake alimuacha mdogo, nikamlea mimi na kumbadilisha dini, kutoka dini ya mama yake ya Kikristo na kuwa Muislam dini ya baba yake. Tulimpa  jina la Ahmed lakini kwa kuwa alisilimu akiwa mtu mzima, jina la Charles ndilo lililozoeleka.
Alipotakiwa kueleza mazingira ya marehemu huyo kujinyonga, alisema:
“Siku za karibuni marehemu alikuwa mgonjwamgonjwa, akachanganyikiwa akili. Ikumbukwe mwanangu alikuwa fundi mkuu wa gereji ya mabasi hivyo baada ya kupata matatizo ya kiafya alipumzika kazi.
“Lakini kwa mshangao jana katoka kwake kaenda kujinyongea kwa mdogo wake.”
Marehemu alizikwa juzi Jumamosi kwenye Makaburi ya Mwembesogo, Morogoro.

Mgonjwa: Nateseka Na Mfupa Wa Fuvu La Kichwa Tumboni

Yassin Khalid Salum.

MWANAUME anayefahamika kwa jina la Yassin Khalid Salum, 34, mkazi wa Mtoni Mtongani jijini Dar anapitia kipindi kigumu cha mateso kutokana na tatizo linalomkabili la kutolewa mfupa kwenye fuvu lake na kuwekwa tumboni ili kuoteshwa sehemu zilizopata hitilafu, ambapo kidonda cha tumboni katika sehemu ulipowekwa mfupa huo kinamsumbua ikiwa ni pamoja na kutoa usaha mara kwa mara.
Akizungumza na gazeti hili kwa majonzi, Yassin anayejishu-ghulisha na ufundi redio na televisheni anasema alipata ajali usiku wa kuamkia Mwaka Mpya wa 2013 wakati akirejea nyumbani kwake baada ya kumaliza shughuli zake za ufundi.
Akisimulia mkasa huo, Yassin alikuwa na haya ya kusema: “Nilikuwa katika baiskeli yangu Mtongani Dar,  Mtaa wa Namba Tano napandisha kilima ghafla lilitokea nyuma yangu gari lililokuwa limekatika breki na kuigonga baiskeli yangu, mimi nilikwenda kupigiza kichwa kwenye mtaro na baada ya hapo nikapoteza fahamu.
“Nilipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, baada ya kupigwa x-ray madaktari walibaini kuwa nilipata tatizo kwenye fuvu langu, ikabidi watoe sehemu ya mfupa penye tatizo wakaiweka tumboni ili kuiotesha lakini kiukweli katika sehemu hiyo ambayo wameiweka inasumbua sana.
“Mimi ni baba wa watoto watatu na kutokana na matatizo yanayonikabili, sina msaada wowote ule kwa watoto hawa malaika wa Mungu.
“Sina baba, mama yangu ni mzee hajiwezi kwa lolote lile, napata tabu maana hata kaka yangu aliyekuwa ananisaidia siku hizi hafanyi hivyo tena, naombeni msaada Watanzania wenzangu.
“Nimefuatilia kliniki kuanzia mwaka 2013 na wiki iliyopita nimeambiwa natakiwa kulazwa ili mfupa uliowekwa tumboni utolewe na kurudishwa kichwani. Huduma hiyo nimeambiwa inagharimu shilingi 200, 000 pesa ambazo nimeshindwa kuzipata hivyo naomba msaada Watanzania wenzangu,” alisema Yassin kwa huzuni.
Yeyote aliyeguswa na tatizo la mgonjwa huyo na ana nia ya kumuokoa kutoka katika mateso anayopata, awasiliane naye kwa namba ya simu 0714 972370- Mhariri.

Saturday, April 16, 2016

Ombaomba Wabuni Mbinu Mpya!

IMG_20160328_163339
Watoto wakiwa kwenye harakati za kuomba.
Stori:  Hamida Hassan na Mayasa Mariwata
Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutangaza kuanza kwa oparesheni ya kuwaondoa ombaomba mtaani, hali imezidi kuwa mbaya na sasa ombaomba hao wamebuni mbinu mpya kujipatia pesa huku wakimpiga chenga ya mwili kiongozi huyo.
Katika maelezo ya Makonda, ombaomba hao wanatakiwa kurudi makwao kwa kutumia gharama zao kama walivyotumia pesa zao kuja jijini ambapo alisisitiza kuwa, itakapofika Jumatatu (keshokutwa) zoezi la kuwaondoa kwa nguvu litaanza.
IMG_20160328_163357…..Zoezi hilo likiendelea.
Kufuatia agizo hilo, gazeti hili juzi lilifanya zoezi la kuzunguka kwenye maeneo yenye ombaombao wengi hasa sehemu za makutano ya barabara kama vile Magomeni Mataa, Fire na Moroco na kubaini kuwa, watu hao wamebadili staili ya kuomba.
Mmoja wa vijana wanaofanya biashara ya kuuza maji katika maeneo ya Fire-Kariakoo jijini Dar alisema:
“Sasa hivi wale wamama na wababa hawaonekani kabisa huku barabarani, wanampiga chenga Makonda. Wanajificha na kuwatuma watoto wao kuja kuomba, halafu mtoto akija kuomba anasema kabisa ametumwa na mama yake ili wapate nauli ya kurudi kwao.
“Ndiyo maana huwezi kuwaona wazazi wa watoto wao kule pembeni mwa barabara kama ilivyokuwa awali. Wanakuambia kabisa naomba hela nipate nauli ya kurudi kwetu! Sasa kama una huruma utashindwa kutoa pesa?” alihoji kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Rashidi Omari.
IMG_20160328_163433Kwa nini watoto ndiyo wanaonekana?
Inaelezwa kuwa, sababu ya wazazi wa watoto ombaomba kujificha ni kukwepa kukamatwa kwani watoto wao hata wakikamatwa bila wazazi wao ni kazi bure.
“Unajua lengo la serikali ni kuwarudisha ombaomba wote kwao, sasa wakiwakamata watoto tu bila wazazi wao, zoezi haliwezi kufanikiwa, ndiyo maana unatakiwa kupatikana ushirikiano wa kutosha kuwabaini wazazi wa watoto hao wanaowatuma kuomba ili mpango wa kuwarudisha makwao ufanikiwe,” alisema Salim Jumbe, dereva wa daladala inayofanya safari zake kati ya Posta na Makumbusho na kuongeza:
“Halafu hawa watoto hata hawaogopi magari, wanatembea katikati ya barabara bila kohofia pikipiki na magari, ndiyo maana unasikia kila siku wanagongwa lakini hawasikii, waondolewe kwa nguvu tu.”
Ni tatizo kubwa
MakondaMkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa ombaomba hao ni tatizo kubwa jijini Dar kwani wamekuwa wakisababisha usumbufu mkubwa kwa wasafiri na hata watembea kwa miguu.
“Yaani kazi hii imeonekana kama ni halali sasa, kila kukicha wanazidi kuongezeka na wengine usipowapa pesa wanakutukana, kukukwangulia gari yako na hata kukutemea mate. Mbaya zaidi ukitoa pesa yako kwa kumuonea huruma, kesho lazima aje tena barabarani, matokeo yake wananogewa.
“Mimi nadhani hili aliloanzisha Makonda liungwe mkono na watu wote, kweli wana hali mbaya lakini naamini kuna maisha mengine wanaweza kuishi kuliko haya ya kuja kuombaomba,” anaeleza mama Janeth wa Kinondoni.

Jiji la Dar es Salaam Kufumuliwa na Kupangwa Upya


Waziri wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema Jiji la Dar es Salaam litafumuliwa na kupangwa upya baada ya Ramani ya Mipango Miji (Master Plan) mpya kukamilika.

Pia, amesema Serikali ipo kwenye mkakati wa kuhakikisha ndani ya miaka 10 ijayo, ardhi yote nchini itakuwa imekamilika kupimwa na kupangwa kwa matumizi mbalimbali. 

Akizungumza na wadau wa Sekta ya Uendelezaji Ujenzi Dar es Salaam jana, Waziri Lukuvi alisema Jiji la Dar es Salaam linaongoza kwa ubovu wa upangaji miji. 

Alisema kwa sababu hiyo, ameagiza kuandaliwa kwa Mpango Mji Mpya ambao utakamilika Julai, baada ya ule wa awali kuoneakana mbovu. 

“Mwanzo hatukufanya vizuri. Tuliajiri Consultant (mshauri) wa Master Plan (Mipango Miji) kutoka Italia sitaki kumtaja na yule Mswahili na wengine walioshirikiana nao, lakini kwa ufupi walifanya vibaya. Fedha imekwisha lakini kazi siyo nzuri,” alisema. 

Sunday, April 10, 2016

Msanii Mwigine wa Bongo Anayeteketea Kwa Madawa ya Kulevya Huyu Hapa....

Wauza unga kuweni na huruma kwa watanzania wenzetu,yule Dogo Mfaume wa enzi zile za "kazi yangu ya dukani" ndo basi tena sasa hivi kashakua teja....daah vipaji vya ukweli vinazidi kupotea kwa ngada.

Mlaaniwe wote mnaouza unga kuanzia nyie wenyewe na vizazi vyenu vyote.

..."kazi yangu ya dukanii aaahahh yaniweka matataniii wanao nirudisha nyuma wengi wao majiraniii"

MAKONDA: Marufuku kwa wanaotoa Pesa kwa Omba omba kando ya barabara

Mkuu wa mkoa wa Dsm Paul Makonda amepiga marufuku wananchi wanaotoa Pesa kwa Omba omba kando ya barabara kwa kuwa wanachangia uwapo wa watu hao huku baadhi ya watu wakiwatumia watoto hao kujipatia kipato kinyume cha sheria.

Akizungumza jijini dsm Bw.Makonda amesema kumekuwa na Ongezeko kubwa la watoto katika barabara kadhaa za jiji la dsm wakijihusisha na Kuomba pesa huku wanaowatuma wakiwa wamekaa pembeni jambo ambalo ni kinyume na sheria lakini pia linahatarisha Usalama wa watoto hao.

Aidha amesema mkakati uliokuwapo kwa kushirikiana na Ustawi wa jamii, Tamisemi pamoja na manispaa kuhakikisha kuwa watoto hao wanakusanywa na kuwekwa katika vituo maalum huku wanaohusika na kuwatumia kufanya kazi hiyo wakichukuliwa hatua.

Thursday, April 7, 2016

Watu Watano Wafariki Dunia Jijini Dar Kwa Kuangukiwa Na Kifusi.


Watu watano wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa, baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuangukiwa na kifusi na mti wakiwa wamelala, ajali hiyo ilisababishwa na kupasuka kwa karo la majitaka la nyumba ya jirani iliyo juu ya mlima.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Christopher Fuime alisema chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa karo hilo na kwamba maji yaliyotoka kwa kasi yaling’oa mti, kifusi na kisha kuifunika nyumba ya jirani iliyojengwa bondeni na kusababisha vifo hivyo.

Alisema tukio hilo lilitokea jana alfajiri katika Mtaa wa Ukwamani Kata ya Kawe jijini Dar es Salaam, na waliokufa ni Ephraim Manguli (47), watoto wake Daniel Ephraim (5) na Frederick Ephraim (1). Wengine ni mjukuu wa mwenye nyumba hiyo, Greyson Clarence (3) pamoja na msichana wa kazi za ndani aliyetambulika kwa jina moja la Maria.

“Majeruhi ni pamoja na Emilia Nakiete (19) aliyejeruhiwa mkono wa kulia na kidevu na Fadhili Fariji (8) aliyejeruhiwa mguu wa kulia. Wengine watatu walitibiwa katika Hospitali ya Mwananyamala na kuruhusiwa. Majeruhi wawili bado wamelazwa na miili ya marehemu imehifadhiwa hospitalini hapo,” alisema Kamanda Fuime.

Baada ya kutafutwa, mmiliki wa nyumba hiyo Blandina Clarence Akilizao (49), alisema nyumba yake ilikuwa na wapangaji sita wenye familia, huku familia yake ikiwa na watu saba.

“Ndani ya nyumba nilikuwa na watoto wawili, wadogo zangu wawili na wajukuu wawili, pia kulikuwa na familia tano zilizokuwa na watu 17 jumla,” alisema mama huyo kwa uchungu.

Blandina alisema nyumba hiyo aliachiwa na mumewe aliyefariki dunia mwaka 2000 na kwamba hivi sasa hana msaada wowote, kwani akiba ya fedha aliyokuwa nayo kiasi cha Sh200,000 imefukiwa na kifusi na hajui namna ya kuipata.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye ni mpangaji, Msafiri Nyamolelo alisema ajali hiyo ilitokea ghafla na kabla ya ukuta kuanguka, ulisikika mlipuko na baadaye kelele za maji, kisha kishindo kikubwa juu ya paa.

“Karo lilipasuka na kwa kuwa ardhi hiyo hapo juu kwa muda mrefu ni dampo lenye mifuko mingi, ardhi ilikuwa imeoza, hivyo miti mikubwa ambayo iliota huko iling’oka baada ya karo kupasuka na kutua juu ya paa la nyumba sambamba na udongo kutoka juu nao ukafunika,”alisimulia Nyamolelo.

Akizungumzia tukio hilo, Katibu Mtendaji wa Mtaa wa Ukwamani, Kata ya Kawe Kassim Mbezi alisema chanzo cha ajali ni kupasuka kwa karo la choo na maji yaliyomwagika ambayo yaliuzoa mti huo na kifusi kilisombwa na kuifunika nyumba hiyo.

“Tulipofika eneo la tukio tuliwakimbiza majeruhi wote Mwananyamala, lakini kwa bahati mbaya walifariki baada ya kufika mapokezi wote walitoka wakiwa bado wanahema, lakini ilipofika saa tatu asubuhi tukaambiwa kwamba kulikuwa na ‘house girl’ hivyo baada ya kufukuafukua tukaupata mkono na baadaye kuufikia mwili mzima, huyu tulimtoa akiwa tayari amefariki,” alisema Mbezi.

Mbezi alitoa wito kwa wakazi wa bonde hilo kuhama kwa kuwa gema bado linaonekana na ni hatari na changamoto kubwa ni namna ya kukabiliana na maafa kabla ya kutokea. 

Wednesday, April 6, 2016

Aunty Lulu Agida Bia Asubuhi Asubuhi

IMG_3291Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ akipiga mtungi huku akijilipua na fegi.

 Mwanadada asiyeishiwa matukio mjini, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ hivi karibuni alinaswa akigida bia na kuvuta sigara asubuhi na mapema, akionekana kukaidi agizo la Rais John Joseph Magufuli la kuwataka watu kuachana na tabia ya kunywa pombe saa za kazi.
Paparazi wetu alimnasa Aunty Lulu ndani ya baa ya Mango Garden, Kinondoni jijini Dar ambapo alikuwa anakunywa bila wasiwasi huku akishushia na kuvuta sigara hali iliyosababisha watu kumkodolea macho huku wengine wakijadili amekuwaje siku hizi kulewa asubuhi tena muda wa kazi.
“Jamani Aunty Lulu amebadilishwa na nini maana siyo mara ya kwanza kumuona anakunywa muda wa kazi huku akivuta sigara kwa wingi, hilo pakti la sigara analotembea nalo atamaliza kuvuta sasa hivi,” alisema mtu mmoja aliyekuwa akinywa supu katika baa hiyo, wakati msanii huyo akipuliza moshi bila woga.
IMG_3288Baada ya paparazi wetu kumpiga picha za kutosha, alimfuata Aunty Lulu na kumuuliza kulikoni kunywa pombe muda wa kazi na kukiuka maagizo ya rais ambapo alisema;
“Unajua siku hizi nafanya kazi ya biashara ya kusafiri mikoani hivyo siku ambayo napumzika kama hivi nakunywa kuanzia asubuhi ili kutuliza mawazo, hizi sigara navuta ili kupunguza mwili maana niliambiwa na watu kwamba zinapunguza unene, nataka kurudi kuwa miss kama zamani.
“Agizo la rais sijalisikia bado lakini najua hapa sijavunja sheria maana si unajua kila mtu ana siku yake ya mapumziko na mimi leo niko mapumziko ndiyo maana nakunywa saa hizi.”

Tuesday, April 5, 2016

Sakata La Kijana Aliyefufuka Baada Ya Kufa Lachukua Sura Mpya

Hatimaye Sakata la Uvumi na madai ya kijana,Nyabongo Manosa,ambaye inadaiwa alikufa kwa Malaria mwaka 2013 na kuzikwa na baadaye kudaiwa kuonekana hai katika kijiji cha Iroganzala,Wilayani Mbogwe Mkoani Geita mwaka 2015 limechukua sura mpya.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga Mponjoli Rotson,
Kwa Mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Rotson amesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya Polisi kwa kushirikiana na mamlaka zingine ikiwemo ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serkali kuazisha na uchunguzi wa kisayansi ili kubaini ukweli juu ya marehemu anaedaiwa kuzikwa na kufufuka.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga Mponjoli Rotson, amesema Uchunguzi huo unafanyika kupitia jalada la uchuguzi Namba MB/IR/867/2015 liliofunguliwa kuchunguza tuhuma za vitendo vya ushirikina ambapo Uchunguzi utahusisha pia Vinasaba vya DNA.

Aidha katika kesi hiyo Polisi inamtafuta Bw. Emanuel Mutabo[ 42]anayehusishwa na tukio hilo anatafutwa baada ya kutoweka kusikojulikana toka Septemba 14 mwaka 2015 toka nyumba yake iliyolindwa na Polisi kutovunjwa na wananchi.

Kamanda Rodson amesema Nyabongo Manosa [19]alionekana 14 Septemba 2015 katika hali inayohusishwa na mazingira ya kishirikina maarufu kama MSUKULE ikiwa na maana ya mtu anayedaiwa kufariki na kisha kufufuliwa kwa ajili yakutumikishwa katika kazi za shambani na nyumbani.

Kamanda Rotson amesema Baada ya tukio hilo mtu mmoja aliejulikana kwa jina la Manosa Benjamini, mkazi wa kijiji cha Shinyanga A katika kata ya Nyakafuru wilayani Mbogwe alijitokeza akiwa na mkewe na kudai kuwa marehemu aliedaiwa kufufuka alikuwa mtoto wao aliyefariki kwa Maralia june 7 na kuzikwa june 8, 2013 katika kijiji cha Mpunze wilayani Meatu.
Mkuu huyo wa polisi amesema kuwa Bw. Manosa Benjamin, alikabidhiwa kijana huyo kupitia Ofisi ya Ustawi wa jamii wilaya ya Mbogwe, ili kuishi naye wakati uchunguzi wa kina ukiendelea kwani hapakuwepo na uthibitisho wowote wa kisayansi uliofanyika hatua ambayo imeendelea kuibua Uvumi na hofu ndani ya jamii.

Kukamilika kwa uchunguzi huo unaotarajiwa kukamilika ndani ya wiki mbili kutoka sasa kutahitimisha hofu na Uvumi wa tukio hilo ambalo kila kunapokucha limekuwa likiibua hisia tofauti ndani ya jamii bila kupata majibu ya kiuhalisia.

Majambazi Sugu Yakuiba Magari Aina ya Noah Yadakwa DAR...Kama Ulishawahi Ibiwa Gari Soma Hapa

Wezi wa Magari wamedakwa waligeuza nyumba yao maeneo ya Boko/Bunju Yard ya Magari ya Wizi , Kama kuna ndugu jamaa au Rafiki aliibiwa Noah mpe Taarifa afike Oysterbay police ‪#‎UlinziShirikishi‬..

Monday, April 4, 2016

Mke Anasa Picha Chafu Za Hawara...Bofya Hapa Kuziona!

IMG-20141109-WA0005
IMG-20141122-WA0006Hawara huyo akiwa amepozi.

Dar es Salaam: Aibu ya mwaka! Mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Flora, mkazi wa Kimara-Bonyokwa, Dar anadai kunasa picha chafu za hawara wa mumewe, Wikienda lina ubuyu kamili.
Akizungumza na gazeti hili huku akiangua kilio, Flora ambaye ni mke wa mtu aliyezaa naye mtoto mmoja, alidai kwa muda mrefu mumewe amekuwa akimbadilikia kitabia na chanzo cha kuzinasa picha hizo chafu ni baada ya kukabidhiwa simu na mumewe huyo.
“Mume wangu anafanya kazi ya kukatisha tiketi Ubungo (Dar). Wiki chache zilizopita alirudi nyumbani akiwa na simu mpya (smart phone), nikamuuliza alipoipata, akanijibu kuna abiria alikwenda ofisini kwao akitaka kusafiri na hakuwa na nauli kamili hivyo akampatia hiyo simu kama sehemu ya nauli,” alisema mwanamke huyo.
Flora alisimulia kuwa baada ya mumewe huyo kukaa na simu kwa siku kadhaa, alimuomba aitumie kwa kuwa alikuwa akitumia simu ndogo.
“Akanipa ile simu, nikaweka memori kadi yangu niliyokuwa naitumia kipindi cha nyuma. Sikuwa na wazo kama angeweza kuweka picha chafu kwenye simu. Lakini siku moja katika kupekuapekua picha zangu katika simu hiyo ndipo nikakutana na picha chafu za mwanamke mwingine ambaye nilishahisi ni hawara yake,” alisema Flora.
IMG-20141122-WA0007…..Akiwa magetoni kwake.
Baada ya kuzinasa picha hizo, Flora alimuonesha mumewe ambapo aliruka kiunzi kuwa hamjui huyo mtu bali zilikuwepo kwenye simu na alipozidi kumbana alisema kuwa ni marafiki tu.
“Sikuridhishwa na majibu. Niliamua kufunga safari hadi kazini kwake lakini kabla sijafika nikakutana na marafiki zake nikawaonesha yule mwanamke kwenye simu, wakaniambia wanamfahamu anaitwa Kashinde lakini nisifanye vurugu niwakutanishe wote kwa utulivu. Nikafanya hivyo, nikamuuliza mume wangu yule ni nani akaniambia rafiki, nikamgeukia na yule mwanamke akaniambia kuwa ni mpenzi wake halafu akaondoka kwa madai kuwa ana kazi nyingi za kufanya.
“Nilirudi nyumbani nikiwa na hasira ukiangalia mume wangu ni halali alishapeleka hadi mahari nyumbani, wazazi wangu na wakwe wanajuana na hapa nilipo naishi kwenye nyumba ya wakwe zangu,” alifunguka Flora akianika picha hizo ambazo gazeti hili lina nakala zake.
Baada ya Wikienda kumwagiwa madai hayo, lilimsaka hawara huyo kujua ukweli ambapo alipojua ni ofisi za magazeti pendwa alishtuka:
“Ni kweli nazifahamu hizo picha ni za kwangu, huyo mtu namfahamu lakini tulikuwa wapenzi na sasa hivi tumeachana. Kwa hiyo sasa kaka utanisaidiaje kwa hilo tafadhalini naomba nije ofisini kwenu tuongee.”
Ili kuweka mzani sawa, wakati mwanamke huyo akiendelea kubembeleza asamehewe, Wikienda lilimgeukia mwanaume huyo ambaye alicharuka:
“Huyo aliyekupa maelezo picha ni kweli, lakini amesema ni mke wangu naishi naye au nimemuoa? Kuna huyu dada ambaye sasa hivi nimezaa naye, niliamua kukaa naye japo tulisumbuana naye akarudi tena. Sasa kama yeye ameleta picha huko hajanidhalilisha mimi au atakuwa hajamdhalilishe yule.
zzzzzzzzzzzzzzzzxMke anayedaiwa kunasa picha hizo.
“Hata ushahidi mmoja kusema nimemuoa hamna, ndoa za sasa hivi watu wanakaa na mtu wanazaa naye wanaona mtu yupoje, ukiona anakuletea chenga unaachana naye kwanza kwa kifupi siyo mke wangu ni hawara wangu tu na ajue hilo. Mimi nina mke wangu wa ndoa, alikuwa Nairobi (Kenya) sasa hivi yupo Egypt (Misri).”

Mwanafunzi wa Darasa la Tano Ajinyonga Kwa Kutumia Khanga ya Mama Yake..

ccccccccccccccc-zDada wa marehemu akilia baada ya mdogo wake kujinyonga.

Morogoro: Mshtuko! Mwanafunzi wa wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Mchikichini ‘B’ ya mjini hapa, Anosisye Gidion (12), ameacha viulizo kibao baada ya kujinyonga kwa kutumia kitenge cha mama yake, Judith Kilalu ‘Mama Kapipi’.
Tukio hilo la kuhuzunisha lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita, majira ya saa 1:00 asubuhi nyumbani kwao maeneo ya Mji Mpya mjini hapa.
DSC_5576Kitenge cha mama yake alichotumia kujinyongea.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Ashura na rafiki wa marehemu, Hussein walisema kuwa chanzo cha denti huyo kujinyonga kilidaiwa kuwa ni kitendo cha mama yake kumchapa na kumtishia kumpeleka polisi baada ya kuchukizwa na kitendo chake cha kurudi nyumbani saa 6:00 usiku huku akidaiwa kuonekana akiwa na kundi haramu la vibaka la Kizazi Jeuri.
DSC_5584Mama mzazi akilia kwa uchungu.
“Anosisye alichelewa kurudi nyumbani, ilipofika saa 4:00 usiku, mama yake aliamua kumtafuta akaambiwa alionekana akiwa na lile kundi lililokupora wewe (mwandishi wetu) maeneo ya Stendi ya Daladala ya Mji Mpya,” alisema mmoja wa mashuhuda hao huku akirekodiwa.
DSC_5579Mashuhuda wakifuatilia tukio hilo.
Kwa upande wake, mama mzazi wa denti huyo aliyeangushiwa zigo la lawama juu ya kifo cha mwanaye alisema: “Mwanangu alichelewa kurudi nyumbani usiku. Nilizunguka kumtafuta, nikaambiwa alionekana akiwa na Kizazi Jeuri hivyo nilimchapa sana na kumtisha kukicha nitampeleka polisi.
“Kulipokucha aliandaa nguo za shule, cha ajabu nimemkuta amejinyonga. Inauma sana jamani.”
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa  wa Makaburi B, Amiri Kombo aliyekuwepo eneo la tukio alithibitisha kutokea kwa tukio hilo katika mtaa wake.
DSC_5591Polisi wakichukua mwili wa marehemu kwaajili ya uchunguzi.

Sunday, April 3, 2016

GARI Lateketea Kwa Moto Pamoja Na Dereva Akiwa Ndani.. Share Habari Hii Imfikie Mwenye Gari

KUNA GARI IMEPATA AJALI MAENEO YA MBEZI BEACH AFRICANA GARI NO T598BEL TOYOTA LANDCRUISER DEREVA KAUNGUA HAJAFAHAMIKA HATA KWA SURA,SAMBAZA UJUMBE HUU GROUP TOFAUTI ILI WENYE NDUGU WAMFAHAMU,GARI LIPO POLISI KAWE.

Saturday, April 2, 2016

Makonda Awageukia Bodaboda, Awaahidi Pikipiki Kwa Sh 3,500 Kwa Siku, Kuingia Mpaka Mjini

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekutana na waendesha pikipiki za kubeba abiria maarufu kama Bodaboda mkoani humo na kuwapa ahadi nono za kuwainua kimaisha kupitia biashara hiyo.
Pamoja na mambo mengine, Makonda ameahidi kuwapa pikipiki bodaboda hao kwa marejesho ya shilingi 25,000 kwa wiki (sawa na shilingi 3,500) kwa siku na baadae kuwaachia wazimiliki wao.
Mwendesha bodaboda akiwa amepakia abiria watatu kwenye chombo hicho cha usafiri, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao, kama walivyokutwa eneo la Mwembeyanga, jijini Dar es Salaam juzi.  Picha na  Joseph Zablon
Mwendesha bodaboda akiwa amepakia abiria watatu kwenye chombo hicho cha usafiri, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao, kama walivyokutwa eneo la Mwembeyanga, jijini Dar es Salaam juzi. Picha na Joseph Zablon (Maktaba)
Katika hatua nyingine, Makonda ameahidi kuwatengenezea mpango mzuri wa utakaowawezesha bodaboda hao kuingia katikati ya Jiji, tofauti na ilivyo sasa.
Ahadi ya Makonda kuwaruhusu Bodaboda kuingia Jijini ni ukamilifu wa ahadi ya Rais John Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana.
Juzi, Meya mpya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (Chadema) pia aliahidi kuhakikisha Bodaboda wanaweza kuingia mjini kwa utaratibu maalum.

Friday, April 1, 2016

Mkazi wa Mwananyamala Apandishwa Mahakamani Kwa Kutishia Kumuua Rais Magufuli Kwa Kujitoa Mhanga


Kondakta wa daladala, Hamim Seif (42) mkazi wa Mwananyamala Ujiji, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kutishia kumuua Rais John Magufuli kwa maneno.

Seif alipandishwa kizimbani mahakamani hapo jana mchana na kusomewa shtaka hilo na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kenneth Sekwao.

Mshtakiwa huyo alikana shtaka hilo na Hakimu Mkazi, Hellen Liwa alisema kuwa dhamana ya mshtakiwa huyo iko wazi na alitakiwa kuwa na wadhamini wawili, kutoka taasisi ya Serikali inayotambulika, ambaye atasaini hati ya dhamana ya Sh2 milioni.

Licha ya dhamana yake hiyo kuwa wazi, mshtakiwa huyo alishindwa kukamilisha masharti hayo kwani baada ya kusomewa mashtaka alipoulizwa kama alikuwa na wadhamini alishindwa kuwapata.

Akimsomea shtaka linalomkabili, Wakili Sekwao alisema kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Machi 10 mwaka huu katika baa ya Soweto, Makumbusho wilayani Kinondoni kinyume cha kifungu cha 89 (2) (a) na kifungu cha 35 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu.

Wakili Sekwao alisema akiwa katika baa hiyo, mshtakiwa alitishia kumuua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli kwa maneno kwa njia ya kujitoa mhanga.

Kwa haya mambo anayoyafanya Rais Magufuli, mimi nimo tayari kujilipua kwa kujitoa mhanga ili kumuangamiza,” alisema Wakili Sekwao akimnukuu mshtakiwa huyo.



Hata hivyo, Wakili Sekwao alisema upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na akaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa.

Thursday, March 31, 2016

Maiti Ya Gomewa Mochwari Katika Hospitali Ya Temeke Kisa RUSHWA..

‘Maiti’ ya mmoja wa wana kikosi cha Operesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers, hivi karibuni iligomewa kupokelewa na wahudumu wa Mochwari ya Hospitali ya Wilaya ya Temeke jijini Dar baada ya wahusika hao kukataa rushwa, Amani lina stori kamili.
Hivi karibuni, OFM ilipokea malalamiko kutoka kwa raia wema kuwa, wahudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini hapo wamekuwa wakipokea rushwa ili kulaza maiti kwa siri na pesa hizo huingia mifukoni mwao bila uongozi kujua.
“Nyie watu wa OFM, hamna habari tu, pale mochwari ya Temeke kumekuwa na utaratibu wa ‘nyuma ya mlango’ yaani ukiwa na maiti yako kuingiza inawezekana tu. Unachotakiwa ni kuwa na pesa kidogo unawapoza kisha unawapa maiti wanakuhifadhia kwa siku utakazoamua mwenyewe.
“Mara nyingi wanalaza maiti kwa shilingi elfu hamsini mpaka laki moja kutegemea na siku ambazo maiti italala. Wengine wanaofanya hivi ni wale wanaotoa maiti mfano Lindi kupeleka Arusha, wanalaza pale, asubuhi yake wanaanza safari,” alisema raia huyo.
 Baada ya kupata madai hayo, OFM ilijipanga na kuingia kazini kwa kutengeneza ‘maiti’ wao ambaye ni mmoja wa wana kikosi hicho, lengo likiwa kuona kama kuna ukweli wa madai hayo.
Baada ya kumtengeneza marehemu huyo, OFM walifunga safari hadi hospitalini hapo na kufika kwenye ofisi za watoa huduma wa mochwari na kumtoa mmoja wao pembeni ili kupanga  naye dili la rushwa kabla ya kwenda kuleta ‘maiti’.
“Jamani, tunaomba msaada wenu, tumetokea Kibaha, Pwani, hapo kwenye gari tuna maiti ya ndugu yetu ambayo inatakiwa kulazwa katika mochwari yenu kwa siku mbili kabla ya kusafirishwa kwenda Mtwara, tafadhalini tunaomba msaada wenu na hapa tuna kiasi hichi cha pesa (OFM ikatoa shilingi elfu hamsini ili kumkabidhi).”
Hata hivyo, mhusika huyo alikataa katakata kupokea kiasi hicho cha pesa na kusema kuwa katika kitengo hicho hawajawahi kupokea mrungula kwa kulaza maiti hata kwa siku moja.

“Kwanza kabisa hatujawahi kupokea kiasi chochote cha fedha ili kulaza maiti kwa njia za mkato. Hapa kuna utaratibu wake ambapo maiti ikija inatakiwa iwe na uthibitisho wote kutoka kwa daktari sambamba na malipo halali kisha ndiyo tunalaza,” alisema mhudumu huyo huku akiwataka OFM kwenda kwenye ofisi yao ili kufuata taratibu.
Baada ya kukataliwa hapo, OFM iliondoka eneo la tukio na kujiridhisha kuwa, hakuna mrungula wowote unaotolewa kwa kulaza maiti kwenye mochwari hiyo.

OFM inawapongeza wafanyakazi hao wa mochwari kwa kufanya kazi kwa maadili kwani wakati wanafanyiwa jaribio la kupewa pesa, kamera ya OFM inayopiga picha kwa masafa marefu ilikuwa tayari kwa tukio hilo.
Huo ndiyo uadilifu unaotakiwa kwa watumishi wa umma na wa taasisi nyingine hasa katika utawala huu wa serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ ambaye kauli mbiu yake ni Hapa Kazi Tu!

-Gpl