Showing posts with label HIP HOP. Show all posts
Showing posts with label HIP HOP. Show all posts

Sunday, May 29, 2016

Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye Akerwa na Ving'ang'anizi wa Madaraka

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye amezitaka nchi za Afrika kuhakikisha zinakubali kubadilishana madaraka pale chama kimoja kinaposhindwa kuongoza ili kuepusha nchi kuingia kwenye machafuko.

Aidha, Sumaye alisema ni vyema wataalam wakaongoza nchi kwa kubuni mbinu mbalimbali za kujikwamua kiuchumi.

Sumaye aliyasema hayo jana Jijini hapa wakati akizungumza kwenye kongamano la Nafasi ya Wasomi na Wafanyabiashara Katika Kujenga na Kukuza Uchumi wa Nchi, lililoshorikisha viongozi wa vyama, wafanyabiashara na wasomi wa kada mbalimbali wa Arusha.

Sumaye alisema uongozi ni kubadilishana nafasi na katika nchi za Ulaya kwa mfano, chama kikishindwa kutawala kinakubali lakini kwa nchi za Afrika kuna uroho wa madaraka au ubinafsi.

"Tunataka kuwajengea uwezo wasomi wetu kwa kujiamini na kujipatia fursa za kujikwamua kiuchumi," alisema Sumaye ambaye alikuwa Waziri Mkuu kwa miaka 10 mfululizo kati ya 1995-2005, kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi.

"Ubinafsi tuache, tukishindwa uchaguzi achia ngazi.Mimi niliyasema haya nikiwa CCM na leo hii nipo Chadema nasema unapoang'angania madaraka, aidha unaogopa ukiachia utasababisha machafuko au ubinafsi."

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Dk. Vincent Mashinji akifungua kongamano hilo, alisema chama chake kinataka kutengeneza mabepari wa kitanzania ambao watajiongeza wenyewe katika kujiinua kiuchumi.

Alisema Arusha ni mji wa kitalii hivyo ni vyema wafanyabiashara wakatumia fursa zilizopo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi, na inawezekana Jiji hilo kuwa na fursa nyingine za kibiashara badala ya kutegemea madini ya Tanzanite pekee.

Monday, April 11, 2016

Bunge Labana Matumizi na Kuokoa Bilioni 6.....Rais Magufuli Aagiza Fedha Hizo Zikabidhiwe Kwa Magereza Na JKT Ili Kutengeneza Madawati 120.000


Rais Magufuli ameipongeza ofisi ya Bunge kwa kubana matumizi na kufanikiwa kuokoa shilingi Bilioni 6, ambazo zitatumika kutengeneza madawati ya wanafunzi wa shule na amezitaka ofisi na taasisi nyingine za serikali kuiga mfano huo.

Ameagiza fedha hizo zipelekwe Idara ya Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili vyombo hivyo vifanye kazi ya kutengeneza madawati yanayotarajiwa kuwa zaidi ya 120,000 ambayo yatasambazwa katika shule ili kukabiliana na tatizo la wanafunzi wanaokaa chini kwa kukosa madawati.

Hundi Kifani ya fedha hizo imekabidhiwa kwa Mheshimiwa Rais na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Akson, ambaye amesema Ofisi ya Bunge imetekeleza wito wa serikali wa kubana matumizi ambapo kiasi hicho cha shilingi Bilioni 6 kimepatikana kwa kipindi kifupi cha takribani nusu mwaka.

Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilila ametaja maeneo ambayo Bunge limebana matumizi kuwa ni Safari za nje ya nchi, Mafunzo nje ya nchi, Machapisho na ununuzi wa majarida, Shajala, Chakula na Viburudisho, Mtandao, Malazi hotelini, Matibabu ya wabunge na familia zao nje ya nchi, Umeme, Maji, Simu na Uendeshaji wa Mitambo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pia ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga  Bi. Anne Kilango Malecela na Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Abdul Rashid Dachi, kufuatia mkoa huo kutoa taarifa zisizo sahihi kuwa hauna watumishi hewa.

Rais Magufuli ametangaza kutengua uteuzi wa Viongozi hao wa Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 11 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, mara baada ya kupokea Taarifa ya Mwaka 2014/2015 ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), na kupokea hundi kifani ya shilingi Bilioni 6 kutoka Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizotokana na kubana matumizi.

Dkt. Magufuli ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa kuwa Mkoa wa Shinyanga hauna watumishi hewa, aliamua kutuma timu ya ukaguzi iliyokwenda kufanya uchunguzi ambapo hadi kufikia jana tarehe 10 Aprili, 2016 imebaini kuwepo watumishi hewa 45 huku zoezi likiwa linaendelea katika wilaya mbili za Ushetu na Shinyanga Vijijini.

“Na wale wote wa Shinyanga ambao walisemekana ni zero, hakuna mtumishi hewa, walikuwa tayari wameshalipwa shilingi milioni 339.9, nimejiuliza sana, na nikajiuliza sana na kwa kweli nimejiuliza sana na kwa masikitiko makubwa, kwa nini Mkuu wa Mkoa alisema hakuna mtumishi hewa?” Amesisitiza Rais Magufuli

Rais Magufuli amesema baada ya kutengua uteuzi wake, Anne Kilango Malecela atapangiwa kazi nyingine.

Pamoja na hatua hiyo, Dkt. Magufuli ametaka wakuu wa mikoa yote wawafichue watumishi hewa wote ili waondolewe mara moja, na ameagiza timu iliyofanya uchunguzi Mkoani Shinyanga itumike kufanya uchunguzi katika mikoa mingine kwa lengo la kukomesha upotevu mkubwa wa fedha za umma.

Katikati ya Mwezi Machi, 2016 Rais Magufuli aliwaagiza wakuu wa mikoa yote nchini kusimamia zoezi la kuwaondoa watumishi hewa wote katika orodha ya malipo ya mshahara, ambapo mpaka tarehe 31 Machi, 2016 Jumla watumishi hewa 5,507 walibanika.

Kati ya shilingi Bilioni 583 ambazo serikali imekuwa ikitumia kila mwezi kwa ajili kulipa mishahara, kati ya shilingi Bilioni 53 na 54 zimekuwa zikipotea kutokana na kulipa mishahara ya watumishi hewa.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam-11 Aprili, 2016

Sunday, April 3, 2016

IMANI:Video Ya Afande Sele Aelezea Kwanini Akifa Anataka Mwili Wake Uchomwe Moto..

‘Hii ni imani ambayo nimeifikiria muda mrefu na nikajua lazima niifate, kila mtu ana kitu ambacho anakiamini na kwangu naamini moto ndio kila kitu kwenye maisha, kama maandiko yanavyosema Mungu ni moto ulao… naamini moto ndio mfumo ambao hata Mungu anatokana na moto wenyewe‘ – Afande Sele
Kwenye sentensi ya pili Afande amesema ‘wakisema Mungu hajulikani au Mungu hujui ni kitu gani hapo kwangu siwezi kuamini kitu ambacho hakionekani kwa hiyo mimi naamini Mungu ni lile jua linalowaka sababu ndio moto mkuu kuliko mioto yote, sasa kama Mungu ni moto ulao basi mimi napaswa niliwe na moto ule‘
‘Naamini nikichomwa moto nitakua majivu, unaposema Mungu ni moto ulao inamaana mimi moja kwa moja nitakua nimeliwa nimeingia ndani ya Mungu mwenyewe, hata kesho nikifariki nikachomwa moto nikawa majivu, sipendi kufufuliwa kwenye mazingira ya ubinaadamu tena sababu nimegundua ubinaadamu sio kitu kizuri cha kujivunia‘
‘Japo binadamu wanaweza kujivunia sababu ndio wanatengeneza Ndege, Magari na vitu vingine…. binadamu ndio kiume mbaya na muovu, msaliti, mnafiki, batili kuliko kiumbe chochote katika ulimwengu, hata dunia yenyewe itamalizwa na binadamu na sio kiumbe mwingine kwahiyo ili kuukana huu ubinadamu sipaswi kuzikwa kwenye udongo, nikizikwa kwenye udongo manake nitafufuliwa kama binadamu tena kitu ambacho sikitaki‘ – Hayo ni maneno ya Afande Sele msanii wa siku nyingi kwenye muziki wa bongofleva
Kwa kumalizia, Afande amesema ‘Mungu ninaemwamini mimi ni moto na moto mkuu kuliko yote ni jua hata samaki anayeishi chini ya bahari kabisa jua likiwaka asubuhi anatoa mgongo juu inamaana anatoa heshima yake kwa Mungu, hiyo ndio imani yangu na wala simlazimishi mtu mwingine yeyote aamini ninavyoamini mimi, hata familia yangu na watoto wanajua baba akifa anatakiwa kuchomwa moto’
Ukitaka kufahamu zaidi aliyoyasema Afande Sele tazama hii video hapa chini…

Friday, April 1, 2016

FID Q Ajibu Tuhuma Za Kutaka Kumuoa Salama Jabir Wa Mkasi TV


Kwa kipindi cha miaka kadhaa iliyopita kulikuwapo na tetesi kuwa msanii wa Hip Hop, Fid Q yupo katika mahusiano ya kimapenzi na mtangazaji wa kipindi cha Mkasi, Salama Jabir na wana mipango ya kufunga ndoa.

Fid Q amejibu swali kama ni kweli aliwahi kutaka kumuoa Salama kwa miaka kadhaa iiiyopita wakati alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha Ala za Roho kinachoruka kupitia Clouds Fm na kukanusha taarifa hizo kuwa siyo sahihi.

“Sio kweli … hizo stori niza uongo,” Fid Q alimjibu mtangazaji wa kipindi hicho, Diva na baada ya hapo aliingiza mada nyingine na Diva kuachana na swali hilo.

Thursday, March 31, 2016

Afande Sele Akiri Kutumia Bangi…Aomba Serikali Iruhusu BANGI

Afande sele
Msani mkongwe wa Hip Hop ambaye alitupa karata yake kwenye siasa na kufeli Afande Sele, ameitaka serikali kuruhusu biashara na matumizi ya bangi, ili kuongeza pato la taifa kwa kuilipia kodi biashara hiyo.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Afande Sele amesema iwapo zao hilo la biashara likiruhusiwa rasmi nchini na kuwekewa mfumo maalum wa matumizi itasaidia kukuza uchumi.
“Hatuna barabara, hatuna madawa hospitalini, hatupati fedha kwa sababu hatupati fedha nyingi kwenye kodi zetu, lakini tungeingiza bangi kwenye mfumo wenye kuruhusiwa na tukaweza kuiwekea mazingira rasmi ya matumizi yake tukauza ndani na nje ya nchi tungeweza kukusanya kodi kwa kiasi kikubwa sana, tungejenga nchi yetu”, alisema Afande Sele.
Pamoja na hayo Afande Sele ameonyesha kushangazwa na kitendo cha serikali kukataza bidhaa hiyo ambayo inajumuishwa kwenye madawa ya kulevya, na kuingiza rizla ambazo hutumika kusokotea bangi.
“Taifa tupige hatua lazima tuachane na vitu flan vyenye unafiki, Tanzania wengi wanasema sivuti bhangi lakini upande wa pili wanavuta, au serikali inasema ina sheria za kuzuia bangi lakini bangi zinalimwa vijijini huko bangi zinauzwa na serikali hii hii ambayo ndio inaingiza rizla bandarini zinalipiwa kodi, lakini zile rizla hazina kazi yoyote katika taifa kama sio kunyongea bangi kwa hiyo serikali inafahamu na viongozi wanafahamu lakini bahati mbaya kuna unafiki”, alisema Afande Sele.

Sunday, February 21, 2016

Ben Pol Aitaja Hii Sababu Kuwa Ndio Maana Hatofuga Rasta, Kuvaa Hereni Au Kujichora Tattoo

Benard Paul ‘Ben Pol’ amesema  hapendi na hatauchora ‘tattoo’ mwili wake kama baadhi ya wasanii na watu maarufu wafanyavyo kwa kuwa anauheshimu sana.

Ben Paul alisema imekuwa ni kawaida kwa idadi kubwa ya wasanii kujichora ‘tattoo’ na kuwa na mwonekano wa tofauti na watu wengine, lakini kwake jambo hilo halina nafasi.

“Japo ni msanii lakini sipendi kuwa na mwonekano wa tofauti kama kufuga rasta, kuvaa hereni au kujichora mwilini kwa sababu nauheshimu mwili wangu, ndiyo maana nipo kawaida kila wakati,” alifafanua.

Msanii huyo aliongozana na msanii mwenzake, Juma Musa ‘Jux’ walipotembelea ofisi za Kampuni ya New Habari (2006) Ltd kwa lengo la kutangaza wimbo wao mpya wa ‘Nakuchana’

Tuesday, February 16, 2016

Young Killer:Nilikuwa Nikimtazama Nature Kwenye Video

young kila
Erick Msodoki ‘Young Killer

MSANII wa Hip Hop anayefanya vizuri na wimbo wake wa Popote Kambi aliomshirikisha Juma Nature, Erick Msodoki ‘Young Killer’ amefungukia furaha yake kufanya kazi na mkongwe Juma Nature kwa kuwa amekuwa akimtazama kupitia televisheni tangu akiwa mdogo.
Akipiga stori na paparazi wetu, Young Killer alisema kuwa furaha yake ilitimia pale alipofanya naye ngoma ambayo kwa sasa mapokezi yake ni makubwa tofauti na mwanzoni.JUMA n
Juma Nature
“Unajua mtu kama Nature nimekua mtaani nikimuona tu kwenye video. Nimeandika sana mistari yake kwenye madaftari yangu, hivyo kumshirikisha mtu kama yeye kwangu ni furaha sana,” alisema Young Killer.

Monday, February 15, 2016

Nay Wa Mitego: Nitauawa Muda Wowote

Nyota wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.

 Hali ni tete! Siku chache baada ya nyota wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kuwasiliba wasanii wenzake kwenye wimbo wake mpya wa Shika Adabu Yako, ameibuka akidaiwa kujisalimisha polisi kufuatia kutishiwa kuuawa na watu asiowafahamu.
CHANZO CHAWEKA WAZI
Kwa mujibu wa chanzo chetu, baada ya kuachia wimbo huo, jioni yake tu, Nay alipigiwa simu na watu asiowafahamu wakimtaka aupotezee wimbo huo kabla haujamgharimu maisha kwa njia yoyote ile.
APUUZA, ATUMIWA MESEJI
Chanzo kilidai kuwa, Nay alipuuzia simu hizo lakini alishangaa ilipofika asubuhi siku iliyofuata, alikuta ujumbe wa maneno (SMS) kwenye simu yake ukiwa na maneno makali na ya kuendelea kumtishia kifo.
NAY2Picha iliyotengenezwa kumdhalilisha Ney wa Mitego.
INSTAGRAM NI ZAIDI
Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa, Nay, akiwa anafikiria namna ya kukabiliana na vitisho hivyo, aliingia kwenye akaunti yake ya Instagram ‘direct’ (moja kwa moja) na ‘hamadi’ akakutana na ujumbe ukiwa na vitisho vya kumuua.
“Jamaa hana raha hata kidogo, amekutana na meseji na simu alizopigiwa. Ameamua kuzima simu zake zote. kilisema chanzo hicho.“Kwa sasa anajiandaa kwenda mkoani Lindi kuna shoo hivyo tunapata hadi wasiwasi kama jamaa ataweza kweli kufanya kazi inavyotakiwa,” Chanzo.
KWENDA POLISI
Imezidi kudaiwa kwamba, baadhi ya watu wake wa karibu na mama yake mzazi, walimshauri aende akaripoti Kituo cha Polisi Kimara (jirani na nyumbani kwake) kwa vile anaweza kupata matatizo makubwa.
MAMA YAKE ANALIA TU
“Mbaya zaidi, mama yake naye, amepaniki kiasi kwamba analia tu. Inabidi sisi ndiyo tumpe moyo maana anafikiria hatima ya mwanaye kwani kila anapokwenda akikutana na watu wanamlalamikia juu ya wimbo huo,” kilisema chanzo hicho.
sirroKamanda Simon Sirro.
WIKIENDA LAMSAKA
Baada ya kupenyezewa ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Nay kutaka kujiridhisha kuhusu madai hayo lakini hakuwa hewani. Ilibidi kumtafuta mtu wa karibu yake na ndipo alipopatikana.
Naye alikiri kutishiwa kuuawa. Alisema hatua ya awali alichukua uamuzi wa kwenda Kituo cha Polisi Kimara, Dar lakini hakufunguliwa faili la kesi kwa maelezo kuwa, usiku huo askari wasingeweza kufanya hivyo badala yake walimtaka arudi kesho yake.
HUYU HAPA NAY
“Hapa nilipo nimechanganyikiwa. Kwa hali ilivyo nimeona bora niende polisi maana najua nitauawa wakati wowote. Nilikwenda Polisi Kimara lakini sikufanikiwa, sasa najiongeza, nitakwenda Kituo cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (kwa Kamanda Simon Sirro).
Wikienda: “Nimesikia unakwenda Lindi kwenye shoo, sasa huko Polisi Kanda Maalum umeshakwenda au utakwenda ukirudi?”
bskjNay: “Kwanza nilikwenda polisi pale Kimara, wakashindwa kufungua faili. Waliniambia niende asubuhi lakini nimeshindwa kwa kuwa nimeondoka Dar na hapa nipo Lindi.
“Ila kuna ujumbe nimeukuta Insta (Instagram) ni mbaya sana. Nimepanga nikirudi nienda Kanda Maalum, lakini kuna wenzangu niliokuja nao hapa Lindi wamenishauri niende Kituo cha Polisi Kikuu cha hapahapa nikaripoti.”
TIMU WEMA WAMFANYA VIBAYA
Wakati huohuo, wadau wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu (Team Wema), wanadaiwa kuchukua picha ya mrembo huyo akiwa kwenye gari na kuipachika sura ya Nay ili aonekane ni demu.
Kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, picha hiyo imeenea huku wengi wakikitafsiri kitendo hicho kuwa ni cha kutaka kumdhalilisha Mbongo Fleva huyo aonekane ni shoga.
Katika wimbo huo ulioleta figisufigisu, kuna kipengele Nay alisema Wema hana mimba bali anatafuta kiki ya msimu hali iliyotibua hasira za Team Wema.

Monday, February 8, 2016

Kichanga atelekezwa nje ya kanisa!

IMG-20160204-WA0005Kichanga kinachodaiwa kutelekezwa kanisani.
Stori: Chande Abdallah, Wikienda
Mbeya: Dunia haina huruma! Kichanga kinachokadiriwa kuwa na umri usiozidi miezi miwili, kimeokotwa jirani na Kanisa Katoliki Parokia ya Uyole kwenye Kijiji cha Hasanga, Mbeya baada ya kutelekezwa na mtu anayesadikiwa kuwa ni mama yake mzazi aliyetajwa kwa jina la Asha Shafii.
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri Februari 4, mwaka huu baada ya wakazi wa kijiji hicho kupita jirani na eneo hilo wakiendelea na shughuli zao na kukiona kichanga hicho kikiwa kimevishwa nguo vizuri na kuhifadhiwa kwenye kichochoro cha kuelekea kanisani.
IMG-20160204-WA0003Wananchi wakiwa na kichanga hicho.
Kwa mujibu wa wakazi wa Hasanga, mtoto huyo atakuwa ametelekezwa na mama yake baada ya kutokea kwa mgogoro kwenye familia yake kwa kuwa haonekani kutokea familia ya kimaskini.
“Huyu mama aliyemtupa atakuwa na mgogoro wa kifamilia maana mtoto mwenyewe amevalishwa vizuri, ana afya yake tena ni mzima kabisa, huyu atakuwa ametokea familia inayojiweza tu,” alisema mmoja wa wapita njia aliyejitambulisha kwa jina la Emmanuel Joseph.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, mwenyekiti wa mtaa huo, Remy Mgaya alisema kuwa alipata taarifa za mtoto huyo kisha kwenda kumshuhudia.Alisema kwa sasa mtoto huyo amemkabidhi kwenye Dawati la Jinsia la Kituo cha Polisi Cha Uyole ambao wanaendelea na upelelezi ili kumpata mzazi wa mtoto huyo.
IMG-20160204-WA0001Mgaya aliongeza kuwa pembeni mwa mtoto huyo kulikutwa mkoba mdogo ambao ndani yake kulikuwa na nguo za mtoto na kadi ya kliniki iliyoonesha jina la mzazi kuwa ni Asha Shafii.
“Inasikitisha kwa kweli, ni mtoto mzuri wa kiume, mimi mwenyewe nilipomuona anacheka tu vizuri nilitamani awe wa kwangu, hili suala lipo mikononi mwa polisi na huyu mzazi atapatikana tu,” alisema mwenyekiti huyo.

Saturday, February 6, 2016

Mbowe Amtosa Zitto Kabwe Baraza La Mawaziri


Kambi rasmi ya upinzani bungeni, imetangaza baraza lake la mawaziri kivuli ambalo Chama cha ACT Wazalendo, chenye mbunge mmoja, Kabwe Zitto, ndicho hakikuingizwa kwenye baraza hilo. Kiongozi wa kambi hiyo, Freeman Mbowe alitangaza jana bungeni baraza hilo.

Chadema chenye wabunge wengi katika kambi hiyo, kina mawaziri vivuli wengi ikilinganishwa na vyama vingine na wakati huo huo, kina wizara nyingi ambazo kinaongoza peke yake kwa maana ya kuwa na mawaziri na naibu mawaziri vivuli.

Mbowe alisema idadi ya wizara alizotangaza inafanana na ya wizara za Serikali ya Awamu ya Tano ambazo zipo 19.


Mbali na kutangazwa kwa majina hayo ,Bunge lilifanya uchaguzi wa wajumbe wa kuliwakilisha kwenye taasisi mbalimbali za kibunge.

Wajumbe hao ni wa Tume ya Utumishi wa Bunge, Bunge la Afrika (PAP), Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-PF), Kamati ya Utendaji wa Bunge la Jumuiya ya Madola (CPA) na Umoja wa Wabunge Duniani (IPU).

 Akitangaza wabunge walioshinda katika uchaguzi huo, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema idadi ya wajumbe waliorudisha fomu za kuwania nafasi hizo ilikuwa inalingana na idadi ya nafasi zilizokuwa zikiwaniwa, hivyo kuwafanya wote kupita bila kupigiwa kura.

1.Tume ya Utumishi wa Bunge Kangi Lugola, Fakharia Shomar Khamis, Mary Chatanda, Mussa Azzan Zungu, Salim Hassan Turky, Magdalena Sakaya na Peter Msigwa.

2.Bunge la Afrika Mboni Mhita, Asha Abdullah Juma, Dk Faustine Ndugulile, Stephen Masele na David Silinde.

3.Jukwaa la Wabunge wa SADC Jamal Kassim Ali, Esther Mmasi, Selemani Zedi na Ally Abdallah Saleh.

4.Kamati ya Utendaji ya Bunge la Jumuiya ya Madola Amina Mollel, Maria Kangoye, Zainab Vullu, Khamis Mtumwa Ali, Salum Rehani, Japhet Hasunga, Josephat Kandege, Dk Raphael Chegeni, Jitu Soni, Immaculate Semesi, Juma Hamad Omar na Tundu Lissu.

5.Umoja wa Mabunge Duniani Dk Pudenciana Kikwembe, Juma Othman Hija, Mohamed Mchengwerwa, Peter Serukamba na Susan Lyimo. 

Wednesday, February 3, 2016

NEY WA MITEGO: MRISHO MPOTO AKIAMUA KUINGIA KWENYE HIP HOP, HAKUNA WA KUMSHINDA BONGO.

Nay wa mitego
Raper Ney wa Mitego amesema, kwa uwezo wa kutunga mashairi alionao Msanii wa nyimbo za asili Mrisho Mpoto, basi akiamua kuingia na kuanza kufanya muziki wa Hip hop asingekuwa na mpinzani Tanzania.
Ney ameuambia mtandao wa Bongo 5 kuwa, labda Fid q ndio msanii pekee anayeweza kushindana na Mpoto.
“Huyu jamaa nafikiria anaumiza kichwa kiasi gani kuandaa kazi zaye, anatumia akili nyingi sana ndio maana nasema akiingia kwenye muziki wa Hip hop atakuwa hana mpinzani” alisema.
Baba Curtis amewataka pia mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwani ataachia kazi mpya hivi karibuni.

Thursday, January 28, 2016

Kwa hali hii Nchi inaliwa JAMANI

IMG_1436Mahekalu wanayomiliki.
Makongoro oging’, AMANI
DAR ES SALAAM: Da! Wakati Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ akiendelea kutumbua majipu kwa vigogo mbalimbali serikalini, hasa wanaotuhumiwa kwa ufisadi, Amani limenasa vigogo wengine wanne wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao wamejenga mahekalu ya mabilioni ya shilingi huku wakiishi maisha ya juu kama ‘miungu watu’, kweli nchi inaliwa! Awali, mahekalu mengine yaliyosemekana kuwa ni ya vigogo wa mamlaka hiyo, yalinaswa na kutolewa kwenye gazeti hili.
CHANZO CHAZUNGUMZA NA AMANI
Mapema wiki hii, chanzo chetu cha habari kilifika kwenye ofisi za gazeti hili na kuonana na wahariri wa Global Publishers kulalamikia maisha ya baadhi ya vigogo wa TRA kwamba ni ya anasa sana wakiwa wanaishi kwenye mahekalu (majumba) ya kifahari huku Watanzania walio wengi wanaishi kwa mlo mmoja tena kulala kwa kubanana.
IMG_1411Moja ya hekalu lililoko maeneo ya Mbezi.
MSIKIE MWENYEWE
“Jamani ndugu zangu, lengo la mimi kuja hapa ni kutaka kuwaambia kwamba, kuna vigogo wa TRA wanaishi Mbezi Beach. Wamejenga majumba ya kifahari. Wanamiliki magari ya kisasa, lakini najua pesa zao ni za ufisadi.
“Nimekuwa nikifuatilia kwenye vyombo vya habari ili kuona kama kuna siku watawekwa hadharani lakini wapi! Naamini serikali haijawajua. Wale wakifuatiliwa, watabainika namna walivyoitafuna hii nchi na ndiyo maana wanaishi kwa kuabudiwa hata na viongozi wa serikali ya mtaa.”
KWENYE VIKAO WANATUMA WAWAKILISHI
“Sisi wenye vijumba vya kujenga miaka saba havijaisha tunajisikia vibaya sana. Ni majirani zetu lakini hatuonani. Wakitoka nje ya mageti yao wamo ndani ya magari yenye tinted. Wananuka pesa hata familia zao. Wanaogopwa mtaani.
“Siku kukiwa na kikao cha serikali ya mtaa kuzungumzia mambo ya maendeleo wanatuma wadogo zao, shemeji zao, wengine wanatuma hata mahausigeli. Hivi ni haki kweli jamani?!”
IMG_1414KUONEKANA KWAO
“Mimi nimewahi kuwaona wawili tu kwa nyakati tofauti, walikuwa wana shida kwenye ofisi za serikali ya mtaa. Kusema ule ukweli nchi hii inaliwa sana. Kama kila mmoja angefanya mambo kulingana na kipato chake halali, taifa lingekuwa mbali sana. Lakini watu wanaiibia serikali kwa ajili ya kujitajirisha na familia zao,” alisema mtoa habari huyo.
KUNA DOGO WA MIAKA 27 NAYE
Wakati mtoa habari wetu akihitimisha hivyo, vyanzo vingine vya habari vimesema kuwa, kijana wa miaka 27 (jina linahifadhiwa kwa sasa), mfanyakazi wa kawaida (kama ‘mfagizi’) wa TRA anamiliki jumba la kifahari lenye vyumba vya kulala 10, sebule 2, vyoo vya umma vitatu, sehemu ya kulia chakula 2 huku msingi wa nyumba ukiwa na urefu wa nyumba nyingine.
“Huyu dogo ana miaka kama 27 tu, lakini anamiliki jengo la kifahari huko Goba. Maisha yake kwa ujumla ni ya kutumbua raha. Kumbe hawa jamaa wa TRA wana pesa sana. Mimi sikuwahi kufikiria. Sasa kwa nini walimu na polisi wanahangaika namna hii?” alihoji mtoa habari wetu.
IMG_1417AMANI LASAKA UKWELI
Baada ya kunyetishiwa ubuyu huo, mapaparazi wetu walizama mtaani ili kujiridhisha. Ilibidi mapaparazi wetu wamtafute Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbezi Beach, Pantaleo Mushi ambaye alikiri kuwa, baadhi ya nyumba katika eneo hilo ni za wafanyakazi wa TRA.
“Ni kweli baadhi ya nyumba za mtaa wangu ni za watu wa TRA, lakini hayo mengine siyafahamu kabisa. Ila kama mnataka kujua zaidi, nendeni wenyewe. Maisha ya watu ni utaratibu wao wenyewe, wanavyoishi ni vile watakavyo,” alisema.
Amani: “Vipi lakini, kukiwa na vikao vya serikali za mtaa wanajitokeza?”
Mwenyekiti: “Wanafika…wanafika.”
Amani: “Mbona tunasikia wanatuma wawakilishi?”
Mwenyekiti: “Labda wanapokuwa na udhuru.”
land-rover-range-rov-8_1600x0wMfano wa mikoko wanayomiliki.
KIJANA NA AMANI
Baada ya kuzungumza na mwenyekiti huyo, juzi, saa 5:28 asubuhi, gazeti hili lilimpigia simu kijana huyo ambapo baada ya mwandishi kujitambulisha jina na chombo cha habari, alikata simu.
ILIVYOKUWA IKIJULIKANA
Baadhi ya watu waliozungumza na Amani kuhusu vigogo wa TRA kujenga majumba ya kifahari maeneo ya Mbezi Beach walisema kuwa, awali waliamini kwamba, nyumba za maeneo hayo nyingi ni za wafanyabiashara na Wazungu waliweka makazi yao nchini.
“Jamani mimi nilipokuja kugundua kwamba, waliojenga Beach wengi ni jamaa wa TRA, TRL (Shirika la Reli Tanzania) na TPA (Mamlaka ya Bandari Tanzania), nilishangaa sana, zamani nilijuwa ni wafanyabiashara wakubwa na Wazungu wanaoishi nchini,” alisema Hamud Hassan Lukwu, mkazi wa Mbezi.
Akizungumza na wakazi wa Ngarenaro jijini Arusha hivi karibuni akiwa njiani kuelekea kwenye Kambi ya Jeshi Monduli, JPM alisema kuwa, mpango wake wa kutumbua majipu viongozi wa serikali ambao wanatumia pesa za umma kwa manufaa binafsi utaendelea mpaka watakapokwisha wote.
mercedes-benz-cls-class-01TAKUKURU WATOA NENO
Akizungumza na wanahabari jijini Dar juzi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), Valentino Mlowola alitoa onyo kwa taasisi nyeti nchini, zikiwemo zinazohusika na matumizi ya fedha za umma kufuata sheria, taratibu na kanuni.
Mlowola alisema kumekuwepo na malalamiko mengi kwa wananchi kuwajulisha matendo ya rushwa na ufisadi yanayoendelea hapa nchini.
Alisema kutokana na hali ya wananchi kuona nia ya serikali ya awamu ya tano katika kushughulikia matatizo ya rushwa na ufisadi ametoa onyo kwa maofisa wa umma wanaofanya rushwa na ufisadi kuwa sehemu yao ya kazi na miradi ya kuwaingizia kipato kuacha mara moja.