Nay wa mitego
Raper
Ney wa Mitego amesema, kwa uwezo wa kutunga mashairi alionao Msanii wa nyimbo
za asili Mrisho Mpoto, basi akiamua kuingia na kuanza kufanya muziki wa Hip hop
asingekuwa na mpinzani Tanzania.
Ney
ameuambia mtandao wa Bongo 5 kuwa, labda Fid q ndio msanii pekee anayeweza
kushindana na Mpoto.
“Huyu
jamaa nafikiria anaumiza kichwa kiasi gani kuandaa kazi zaye, anatumia akili
nyingi sana ndio maana nasema akiingia kwenye muziki wa Hip hop atakuwa hana
mpinzani” alisema.
Baba
Curtis amewataka pia mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwani ataachia kazi mpya
hivi karibuni.