Wednesday, February 3, 2016

SHILOLE: KUTENGANA NA NUH HAKUZUII ‘NYANG’ANYANG’A’

Msanii wa muziki nchini Tanzania, Zuwena Mohamed ‘Shilole’

Mrembo mwenye vituko nchini Tanzania, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, amedai kuwa kutengana kwake na mpenzi wake Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, hakuwezi kuzuia project ya wimbo wake mpya.
Amedai kuwa ni kweli wimbo huo wa ‘Nyang’anyang’a’ ulikuwa mahususi kwa ajili ya mpenzi wake Nuh, lakini kutengana kwao hakuwezi kusababisha project hiyo kuvunjika kwani hajamtaja kwa jina hivyo promo lazima iendelee.
Wanamuziki nchini Tanzania, Nuh Mziwanda na mpenzi wake Zuwena Mohamed 'Shilole'
Wanamuziki nchini Tanzania, Nuh Mziwanda na mpenzi wake Zuwena Mohamed ‘Shilole’
“Wimbo huu haunipi ugumu wowote kwasababu wimbo nimeimba bila kumtaja jina la mtu, ila nimesema nilimuimbia aliyekuwa mpenzi wangu Nuh Mziwanda,”alisema Shilole
Amesema “Hakuna kitu ambacho kitanifanya nishindwe kuendelea ‘kupromote’ wimbo wangu kwa kuwa hainipi ugumu wowote kabisa kwa kuwa tumeshatengana,”.
Wapenzi hao wametengana hivi karibuni na kila mtu kuficha ukweli wa kitu gani hasa kimesababisha kutengana kwani wamekuwa na kawaida ya kupigana, kugombana na kurudiana baada ya kutengana, lakini sasa hawajaweka bayana chanzo.