BAADA ya kuandamwa sana katika mitandao ya kijamii kuhusu kutofunga vizuri vifungo vya suti yake,
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Stephen Wasira ameamua kumuona mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi ili aanze kumtengenezea suti zake.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Stephen Wasira ameamua kumuona mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi ili aanze kumtengenezea suti zake.
Waziri Wasira akijaribu kurekebisha suti yake iliyokosewa kufungwa vifungo na kuzua mjadala mitandaoni.
Mhe. Wasira ameamua kukutana na mbunifu huyo aliyeanza mara moja kumchukua vipimo vyake ili amtengenezee mavazi yake ambayo atakuwa akiyatumia katika shughuli zake mbalimbali za kiserikali.
Picha za Waziri Wasira zilienea mitandaoni alipopiga picha ya pamoja akiwa na Viongozi wa Kanisa la Kisabato kwenye Uwanja wa Taifa, Dar huku koti la suti yake likiwa limekosewa kufungwa vifungo.
Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii walirusha picha mbalimbali zikimuonesha Mhe. Wasira huku mmoja wa watangazaji akisema kuwa iwapo akikubaliwa, atajitolea kuwa wabunifu wa suti zake za mitoko ili jambo hilo lisijitokeze tena.
Mhe. Wasiara akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kanisa la Kisabato kwenye Uwanja wa Taifa, Dar huku koti la suti yake likiwa limekosewa kufungwa vifungo.
Kwa kuamua kumuona Sheria Ngowi, Mhe. Wasira atakuwa amepata mti shamba wa tatizo hilo lililotawala mitandao ya kijamii hivi karibuni.