Showing posts with label Madawa ya kulevya. Show all posts
Showing posts with label Madawa ya kulevya. Show all posts

Sunday, June 19, 2016

Ray C apelekwa sober house Bagamoyo, uongozi wa sober wazungumzia


Muimbaji mkongwe wa muziki nchini, Rehema Chalamila ‘Ray C’ Ijumaa hii amepelekwa Life and Hope & Rehabilitation Centre (Sober House) iliyopo Bagamoyo kwa ajili ya kusaidiwa kuanacha na matumizi ya Madawa ya kulevya, uongozi wa sober hiyo umethibitisha.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku moja toka aonekane katika video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikionyesha jinsi anavyosaidiwa na jeshi la polisi baada ya kudaiwa kutaka kijichoma kisu.

Mmoja kati ya wasimamizi wa kituo cha Life and Hope & Rehabilitation Centre (Sober House) ambacho pia kilimsaidia Chidi Benz kuachana na matuzi ya Madawa ya kulevya, Karim Banji, amesema kuwa ni siku moja toka Ray C apelekwe katika kituo hicho.

“Kweli jana tumempokea Ray C, na kusema kweli kwa sasa siwezi zungumzia maendeleo yake kwa sababu ni siku ya kwanza, lakini leo mchana amekula vizuri na nimemuacha amepumzika,” alisema Karim.

Pia alisema bado hajajua Ray C atakaa kwa muda gani ndani ya sober house.

“Kusema kweli mgonjwa akiletwa hapa, atapimwa afya na baada ya hapo anawekwa katika chumba maalum kwa siku tatu ili aweze kukabiliana na hali ngumu, na baada ya hapo ataendelea na matibabu ya kawaida, kwa hiyo kikubwa ni kuombea tu,” alisema Karim.

Thursday, June 2, 2016

Babu Tale Alimtelekeza Chidi Benz Sobber House - Mkuu wa Kituo

Akizungumza na E news ya East Africa Tv mkuu wa Bagamoyo sobber house amesema chanzo cha Chidi Benz kuondoka kwenye kituo chao ni kutelekezwa na waliompeleka.

Anasema tangia Chidi apelekwe pale hakukuwa na huduma zozote zinazotumwa kama walivyokubaliana na kila walipokuwa wanamtafuta Babu Tale hakuwa tayari kupokea simu wala kutoa ushirikiano.

Anasema pia kukosekana kwa vitu muhimu ndio vilifanya Chidi aondoke na wala hakutoroka.

Japo Sijajua ni vitu gani walikubaliana awe anapeleka.


My take, kama ni kweli hii ishu basi Tale amekosea sana hakufanya uungwana. Ni kama kamtumia Chidi kupata kick

Mwimbaji Country Boy ajitokeza na Kumtetea Young Dee Kuhusu Madawa ya Kulevya




Rappa Country Boy amesema hajawahi kushuhudia rafiki yake wa zamani Young Dee akitumia Madawa ya kulevya.

Young Dee amekuwa akikanusha mara kadhaa taarifa ya kutumia Madawa ya kulevya lakini bado amekuwa akiandamwa na maswali mengi kuhusu matumizi ya Madawa ya kulevya.

Akiongea na Bongo5 Jumapili hii, County Boy ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa Young Dee, amesema hajawahi kushuhudia rafiki yake huyo akitumia Madawa ya kulevya lakini kama anatumia basi atakuwa amuheshimu sana ndio maana hajawahi muonyesha dalili yoyote.

“Young Dee nimekaa naye kwa muda mrefu kiukweli, kusema kweli kabisa sijawahi muona akitumia,” alisema Country Boy. “Maneno yapo na kila kitu kinatokea na kila kitu kinasikika, kama ni kweli anatumia basi nahisi alikuwa ananiheshimu sana, kwa sababu ni mwanangu nimekaa naye pamoja kwa muda mrefu sijawahi kuona kitu chochote kibaya zaidi tu ya ulevi wa kawaida, pombe tu,”

Aliongeza, “Lakini hiki kitu sio vizuri kwa mtu yeyote yule, kwa sababu hakina faida yoyote zaidi ya kukupoteza,”

Country Boy na Young Dee kwa sasa sio washikaji kama zamani, kwa wawili hao walipisha lugha baada ya Young Dee kujiondoa katika Kundi la ‘Mtu Chee’ ambalo lilikuwa linaundwa na Young Dee, Stamina pamoja na country boy

Sunday, May 1, 2016

Madawa ya KULEVYA yamponza Ferooz


Baada ya ukimya wa muda mrefu sana wa wakongwe wa muziki wa Bongo Flava story zilizopo mtaani ni kuwa Ferooz ni miongoni mwa wasanii wanaotumia madawa ya kulevya na ndiyo sababu iliyompoteza kwenye reli ya muziki.
Kupitia Enewz Ferooz alikanusha tuhuma hizo na kudai kuwa misongo ya mawazo ndo huwa inawapelekea wasanii kuingia katika matumizi hayo ya madawa ya kulevya na kuwataka wengine wasifanye hivyo.
Ferooz amesema kuwa “Ni mara kumi upate UKIMWI kuliko uwe unatumia madawa ya kulevya” lakini pia akaongezea kwakusema “Nawashauri watu wengine pamoja na wasanii wenzangu wasije wakajaribu kufanya hivyo”.

Tuesday, April 26, 2016

Watu Watatu Wakamatwa na Madawa ya Kulevya Aina ya Mirungi Mkoani Kilimanjaro


Watu watatu akiwemo raia wa Kenya wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya Mirungi na Bangi kilo 54 na misokoto ya Bangi 4,500 ikisafirishwa kutoka nchini
Kenya kwenda mkoani Arusha.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Bw.Wilbrod Mutafungwa amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika maeneo ya njia panda Himo wilaya ya Moshi na Sanya juu wilaya ya Siha wakiwa wameficha madawa hayo ya kulevya kwenye miili yao kuanzia maeneo ya tumboni hadi miguuni.

Amewataja waliokamatwa ni Vitalis Victor mfanyabiashara mkoani Arusha, Naftal Mvoyi mkazi wa Voi nchini Kenya, Maulid Maulis mkazi wa Arusha ambao walikuwa wakisafirisha Mirungi kilo 44 kwa kutumia magazeti na gundi ya karatasi na kisha kuifunika kwenye nguo walizokuwa wamevaa wakitokea nchini Kenya kuelekea jiji la Arusha.

Ripota wetu amefanikiwa kuzungumza na baadhi ya vijana wanaojihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya katika manispaa ya Moshi na kueleza kwamba changamoto kubwa inayowabaili ni ukosefu wa ajira hali inayowasababisha baadhi yao kujihusisha na matukio ya uhalifu.

Matumizi ya madawa ya kulevya yameathiri vijana wengi kiafya kutokana na baadhi yao kushindwa kufanya shughuli za maendeleo na hivyo kulazimika kujihusisha na matukio ya wizi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Sunday, April 10, 2016

Mange Amshukia RAY C Sakata la Matumizi ya Madawa ya Kulevya..Atoboa Siri ya Ray C Kuondolewa Kwenye Progarm ya Methadone

Katika Jitihada za kumsaidia Ray C , Mange Kimambi Amefunguka Haya Hapa Chini:

"Confirmed news, Ray C ametolewa kwenye program ya kunywa dawa ya Methadone Mwananyamala Hospital. Alikuwa kila akipimwa mkojo anakutwa bado anatumia. Pale wanatoa dawa kwa masharti.Ray C anaweza kukaa wiki hajaenda kunywa dawa, ile dawa hakuna mgonjwa anaweza kukaa siku hata 1 hajanywa, Arosto yake ni hatareeeeee unaambiwa bora Arosto ya heroine kuliko Arosto ya methodone, so ukiona mgonjwa kapitisha hata siku moja hajafika kunywa dawa ujue tu anatumia Tena hata bila kumpima mkojo. Sasa Ray C alikuwa anakata wiki hajafika kwenye dawa . Ndo wakaona wamkatie mbali. Ambao bado mnamtetea Ray as if nyie ndo mnampenda sana nenda pale wanapopokea dawa kila siku Kama utamuona Ray C. Huyo boyfriend wake wa Sasa anaitwa Frank alikuwa rafiki wa Lord Eyes,ni muuzaji na mtumiaji, Kwahiyo hapo ni parefuuuu....

Anyways point sio kumwanika Au kumwandama huwa nawapinga mno global Kwa kuandika habari za uongo Kila siku Ila Kwa hili la kumwandama Ray C acha wamwandame wanamsaidia . Maana Ray C anafanya juu chini kuaminisha watu uongo ili aendelee kujimaliza.

hata Mimi sijui anasaidiwaje , Kama rehab keshapelekwa, Kama methadone keshakunywa sijui kilichobaki. Tusichukulie hii issue kijuu juu huyu msichana akiachwa Sasa hivi atawajoin kina Whitney Houston kiutani utani Hivi Hivi.... Embu tushauriane jinsi ya kumsaidia Maana Mimi sina idea aiseeee.... Alafu akifa tutajisikia vibaya mnoooo kuwa tulikaa pembeni tunaangalia. Sitaki kujua mama yake ana hali gani 🏽. Watoto wanajua kutesa wazazi jamani, I can't imagine mtoto wangu mmoja aje kuwa hivi jamani naweza kufa kwa kuumwa roho !

Challenge kubwa ya kuwasaidia addicts inabidi wawe tayari kubadilika. Inabidi wao wenyewe ndo waamue na sio mtu umforce. Yani Ray C inabidi aamue she wants to live" 

Source:Mangekimambi Insta

Saturday, April 9, 2016

KR Mullah Ajibu Tuhuma Na Sir Nature Kuhusu TID Na Matumizi Ya Madawa Ya Kulevya


Mwanamuziki KR Mullah amefunguka baada ya msanii mwenzake wa kundi la Wanaume Halisi Juma Nature, kusema kitendo cha KR kujiunga na Radar Entertainment, huenda kitamuharibu asipokuwa makini.

KR Mullah, amemtaka Juma Nature amuache kwa sasa afanye kazi, kwani kwa sasa anataka kubadilisha ladha ya muziki wake na huenda hajapendezwa na yeye kuingia Radar Entertainment na kuachana na Wanaume Halisi.
“Nilikuwepo ndani ya kundi la wanaume halisi, sasa labda anavyoona mimi nipo huku anaona kazi zake tena zitakuwa zinalegalega, pengine labda hakupendezewa mimi kwenda kufanya kazi na yule mtu na kwamba yeye alitegemea mi nifanye kazi naye,” alisema

Sambamba na hilo KR, amemuongelea TID ambaye Juma Nature alimtahadharisha kuwa makini nao wasije wakamuingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kuwa  hajawahi kumuona kutumia vitu hivyo.
“Kusema kweli zamani nilikuwa nasikia sikia hizi taarifa, lakini yeye mwenyewe alitangaza kuacha muda mrefu, lakini kwa sasa tangu nimeanza kukaa naye sijawahi kumuona akiitumia au akifanya hayo mambo, muda mwingi tunapiga stori za kikazi zaidi” alisema KR Mullah

Friday, April 8, 2016

Mastaa Bongo Waanza Kuchunguzwa Msako wa Wauza Unga...Zari wa Diamond Naye Pia Achunguzwa

Imefahamika kuwa ule msako wa Wauza unga sasa umenoga hadi kufikia kuchunguzwa kwa mastaa mbali mbali wa bongo hasa wale wanaosafiri mara kwa mara nchi za nje...Habari zinasema uchunguzi huo sasa unamgusa mpaka mpenzi wa Diamond Platnumz ajulikanaye kama Zari Hassan ambae Safari za Bongo kwenda South Afrika na kurudi hazimuishi....

Wednesday, April 6, 2016

Mwanamuziki Ray C Afunguka Siku Atakayo Maliza Kutumia Dawa Za Methadone..


Ameandika Haya Kupitia Ukurasa wake wa Instagram...


rayc1982 Mungu ni mwema siku zote ni takriban miaka mitatu sasa nameza dawa ambapo mwezi June mwaka huu namaliza dose,sambamba na hilo namshukuru mungu mpka Jana nimeambiwa vijana wote 80 nilio washawishi na ninaoendelea kuwashawishi kuachana na madawa wanaendelea na matibabu hapa Dar es Salaam ukiacha wale mikoa niliotembelea. Kwa mantiki hiyo nashukru taasisi ya ray c foundation Kwa mchango huo..Nimekaa na familia yangu,ndugu na jamaa pamoja na mashabiki wangu wamenishauli kuachana na binadamu wasio penda mafanikio yangu.Wanao Fanya juhudi za kuhakikisha wananiandama kwenye MEDIA bila kuangalia upande wa pili kwamba kachangia nini.Hasahasa Kwa manufaa yao binafsi Mimi kama Ray c namwachia mungu atawaliapa

Thursday, March 31, 2016

Afande Sele Akiri Kutumia Bangi…Aomba Serikali Iruhusu BANGI

Afande sele
Msani mkongwe wa Hip Hop ambaye alitupa karata yake kwenye siasa na kufeli Afande Sele, ameitaka serikali kuruhusu biashara na matumizi ya bangi, ili kuongeza pato la taifa kwa kuilipia kodi biashara hiyo.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Afande Sele amesema iwapo zao hilo la biashara likiruhusiwa rasmi nchini na kuwekewa mfumo maalum wa matumizi itasaidia kukuza uchumi.
“Hatuna barabara, hatuna madawa hospitalini, hatupati fedha kwa sababu hatupati fedha nyingi kwenye kodi zetu, lakini tungeingiza bangi kwenye mfumo wenye kuruhusiwa na tukaweza kuiwekea mazingira rasmi ya matumizi yake tukauza ndani na nje ya nchi tungeweza kukusanya kodi kwa kiasi kikubwa sana, tungejenga nchi yetu”, alisema Afande Sele.
Pamoja na hayo Afande Sele ameonyesha kushangazwa na kitendo cha serikali kukataza bidhaa hiyo ambayo inajumuishwa kwenye madawa ya kulevya, na kuingiza rizla ambazo hutumika kusokotea bangi.
“Taifa tupige hatua lazima tuachane na vitu flan vyenye unafiki, Tanzania wengi wanasema sivuti bhangi lakini upande wa pili wanavuta, au serikali inasema ina sheria za kuzuia bangi lakini bangi zinalimwa vijijini huko bangi zinauzwa na serikali hii hii ambayo ndio inaingiza rizla bandarini zinalipiwa kodi, lakini zile rizla hazina kazi yoyote katika taifa kama sio kunyongea bangi kwa hiyo serikali inafahamu na viongozi wanafahamu lakini bahati mbaya kuna unafiki”, alisema Afande Sele.

Wednesday, March 30, 2016

Anayemmaliza Ray C Huyu Hapa

 Mwanaume anayeonekana pichani ukurasa wa kwanza anaitwa Frank. Katika habari hii tunamtaja kwa jina moja tu, Risasi Mchanganyiko linakwambia yeye ni nani!
SASA FRANK NI NANI?
Frank anatajwa kuwa, ndiye aliyechangia kwa sehemu kubwa kumrudisha msanii wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ katika utumiaji wa madawa ya kulevya ’unga’.
Katika Gazeti la Ijumaa Wikienda ambalo ni ndugu wa damu na hili la juzi Jumatatu, ukurasa wa mbele kulikuwa na habari yenye kichwa kisemacho; RAY C ANASWA KAZIMIKA!
MSINGI WA HABARI
Habari hiyo ililenga kuonesha ni namna gani msanii huyo amerejea katika matumizi ya unga baada ya kumwathiri miaka mitatu iliyopita na kupata matibabu kwenye kitengo cha waathirika wa unga Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu wa Kinondoni, Mwananyamala jijini Dar.
ALITOKEA ARUSHA
Simulizi inasema kuwa, Frank ni mwenyeji wa jijini Arusha ambako wazazi wake wanaishi huko lakini kiasili ni mtu wa kutoka Mkoa wa Mbeya.
ALIKUJAJE DAR?
Kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka Hospitali ya Mwananyamala, Frank aliwasili jijini Dar mwanzoni mwa mwaka huu kwa lengo la kupata tiba ya dawa za Methadone ambazo hutumiwa na waathirika wa unga.
“Akiwa anatumia dozi hiyo, inaonekana pia alikuwa akiendelea na unga. Ndiyo tatizo la waathirika wengi wa madawa ya kulevya. Haitakiwi kuchanganya jamani. Wanapochanganya, wanashindwa kupona.
“Sasa sijui ilikuaje, ghafla akakutana na Ray C na kuanza kushikamana kama marafiki wakubwa. Ray C naye, kipindi hicho alikuwa anatumia Methadone, lakini naye hakuacha unga. Nasikia pia wakawa wapenzi,” kilisema chanzo hicho kikiomba hifadhi ya jina lake kwa vile si msemaji wa hospitali hiyo.

TUKIO LA KARIBUNI
Chanzo kinaendelea: “Sasa juzikati tu hapa, Frank yakamkuta mazito. Akiwa maeneo ya Mwananyamala, tena peke yake, alizidiwa na unga na kujikuta akizimika.
“Baadhi ya watu walipomwona, waliamini jamaa ameugua ghafla na yuko na hali mahututi, wakambeba na kumkimbiza Hospitali ya Mwananyamala ili kuokoa maisha yake.
“Bahati mbaya ni kwamba, alifikishwa pale madaktari wakiwa wameshaondoka. Lakini kutokana na hali yake kuwa mbaya, muuguzi mmoja alimpigia simu daktari na kumjulisha. Akaambiwa kama atachelewa, anaweza asimkute jamaa. Ikabidi arudi na kumpatia matibabu.”
WANAOMJUA FRANK
Baadhi ya watu wanaomjua kijana huyo wameliambia gazeti hili kuwa, mwonekano, Frank anafanana sana na Mbongo Fleva, Waziri Makuto ‘Lord Eyez’ ambaye ndiye mwanaume wa kwanza kutajwa kumfundisha Ray C kubwia unga.

MAMA RAY C ATAFUTWA
Juzi, tulimpigia  simu mama yake Ray C, Margaret Mtweve ili kujua Ray C anaendeleaje na afya yake baada ya hivi karibuni kunaswa akiwa amezima, lakini simu ya mama huyo iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
KINACHOWAMALIZA CHAJULIKANA
Kwa mujibu mwa muuza unga mmoja ambaye jina lake linafichwa, aliliambia gazeti hili kuwa wavutaji wengi wa Bongo wanatumia cocaine kutoka Pakistan na Afghanistan, inayojulikana zaidi kama Musharaf, ambayo ni hafifu na yenye kuuzwa bei rahisi.
“G moja (G ni ujazo wa gramu moja) ya Musharaf inauzwa kwa shilingi kati ya 23,000 hadi 25,000 ambayo inaweza kutoa ‘pinch’ (kipimo cha chini kabisa kinachouzwa kwa watumiaji wa aina ya akina Ray C) kati ya 20-40. Cocaine kutoka Brazil, ambayo ndiyo bora, inayoitwa na watu wa unga kama Mchezaji au Pele, inauzwa kwa shilingi kati ya 50,000 hadi 60,000 kwa G moja.”

“Matajiri wengi wa Kihindi, Waarabu na Waswahili kama f’lani (anatajwa mfanyabiashara mkubwa) wanatumia cocaine ya Pele ambayo haitaki kabisa uchafu, ndiyo maana unawaona wako fresh kabisa.
“Ile Musharaf inakuwa mbaya zaidi kwa sababu wauzaji wa hapa wanachanganya na Baking Powder (Hamira) ili iwe nyingi na hivyo kutoa pinch nyingi zaidi.”
00301047-b58ba41202d313a9834230ea50e40135-arc614x376-w1200HUYU HAPA MKEMIA
“Baking poda iliyochanganywa kwenye madawa ya kulevya kama cocaine ina madhara makubwa kwenye mwili wa binadamu iwapo itatumiwa kwa muda mrefu au kwa kiwango kikubwa. Baada ya kuingia kwenye mwili wa binadamu, baking poda huvunjwavunjwa na kutengenezwa madini chumvi ya sodiamu na carbonate ambayo huchukuliwa moja kwa moja kwenye mzunguko wa damu.
“Hii husababisha kuongezeka kwa kiwango cha madini chumvi ya sodiamu (ambayo yamo ndani ya baking poda) tofauti na kiwango kinachotakiwa kwenye mwili.
“Madhara makubwa ya matumizi ya baking poda kwenye mwili wa binadamu ni mishipa ya damu kushindwa kufanya kazi, ugonjwa wa moyo, kuongezeka kwa kiwango cha sukari mwilini (hyperosmolar), maji kuzidi kwenye damu kuliko kiwango cha kawaida (hypervolemic), kuongezeka kwa sodiamu na kupungua kwa maji mwilini kuliko kawaida (hypernatremia),” alisema mkemia huyo aliyejitambulisha kwa jina la Lindege.

Tuesday, March 29, 2016

Uongozi Wa Bagamoyo Sober House Wazungumzia Maendeleo Ya Chidi Benz

Ikiwa ni wiki moja toka Chidi Benz achukuliwe na meneja wa Diamond, Babutale pamoja Kalapina na kupelekwa Life and Hope Rehabilitation Organization iliyopo Bagamoyo kwa ajili ya kusaidiwa kuacha matumizi ya Madawa ya kulevya, uongozi wa Sober hiyo umeeleza maendeleo ya rapa huyo.

Akizungumza katika kipindi 360 cha Clouds TV Jumanne hii, Mkurugenzi wa Life and Hope Rehabilitation Organization, Bwana Al-Karim Banji amesema Chidi Benz amekuwa msikivu na afya yake imeanza kurudi.

“Chidi Benz anaendelea vizuri sana, tena nimeshangaa amepata hamu ya kula kitu ambacho ni tofauti kwa waathirika wengine,” alisema Bwana Banji.

“Mimi mwenyewe nilikaa na Chidi Benz nikaongea nae na alinisikiliza sana, nilimwambia maneno mengi ya busara, alinisikiliza na akaniambia mimi niko tayari kubadilika. Kwa hiyo Chidi Benz anaendelea vizuri na ana kula vizuri yaani yupo very positive,” aliongeza.

Banji alisema ndani ya miezi miwili mpaka mitatu Chidi Benz anaweza kukaa sawa kabisa kwa kuwa anapitia semina mbalimbali za kumjenga kiakili.

Pia Banji amewataka watanzania kuacha kumsema vibaya kwa ile ni hatua ya maisha ambayo binadamu yeyote anaweza kuipitia.

Ray C Akana Kurudia Madawa ya Kulevya


Msanii Ray C amevijia juu vyombo vya habari vinavyoandika taarifa za uongo juu yake, kuwa amerudia kutumia madawa ya kulevya, na kuahidi safari hii atavifikisha mahakamani.

Katika ukurasa wake wa instagrama Ray C ameandika ujumbe mrefu kuhusu vyombo vya habari vinavyomchafua, na kwamba wana mpango wa kukwamisha harakati zake za kupambana na madawa ya kulevya.

“Hujuma hizi najua mnazifanya ili niishie njiani katika harakati za kupambana na dawa za kulevya nchini, Mimi na taasis yangu nitaendelea kusonga mbele na hakika sitakwamishwa na nyumbu kama hawa kwanza mwonekano wa picha uko wazi mimi sina nywele fupi kiasi hicho Ray C wa sasa si yule wa kipindi na enzi hizo now I'm not catalysts of drugs, hata hivyo tayari nimewasiliana na mwanasheria wangu ili niweze kuwawajibisha hawa nyumbu” aliandika Ray C.

Pia Ray c amesema kwa sasa yuko kwenye maandalizi ya mwisho kuandaa nyimbo yake, japokuwa bado yuko kwenye dozi ya methadone, inayotibu uathirika wa madawa ya kulevya.

“Mimi Niko katika maandalizi yangu ya mwisho ya kuaanda nyimbo yangu japo bado niko katika dose ya methadone”, aliandika Ray c.

Monday, March 28, 2016

Ray c anaswa kazimika

IMG-20160325-WA0002
Ray C akiwa hoi na kinachodaiwa kuwa ni utumiaji wa madawa ya kulevya.

DAR ES SALAAM: LICHA ya kutumia nguvu nyingi kukanusha habari zinazochapishwa na Magazeti Pendwa ya Global Publishers kuwa, amerejea kwenye matumizi ya madawa ya kulevya ‘unga’, hatimaye staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amenaswa ‘laivu’ akiwa ‘ameangusha gari’ kando ya barabara, habari ndiyo hiyo!
Ray C ambaye kila anapoandikwa na Magazeti ya Global kuhusu kurejea kwenye unga, amekuwa akimtupia shutuma Mkurugenzi wa Global, Eric Shigongo kwamba anamchafua, alinaswa na mapaparazi wetu hivi karibuni maeneo ya Mwananyamala Magengeni, Dar akiwa amezima yeye na mwanaume aliyekuwa naye hali iliyompa urahisi paparazi wetu kuwafotoa picha za kutosha.
IMG-20160325-WA0000…..Wakiwa kwenye stimu kali.
ISHU ILIANZA JANUARI
Januari mwaka huu, gazeti hili liliripoti habari iliyokuwa na kichwa; CHIMBO LA UNGA LA RAY C LAGUNDULIKA.
Baada ya habari hiyo kutoka, Ray C aliikanusha kupitia ukurasa wake wa Instagram akisema:
“Seriously kwa kweli huwa naumia sanasana kuona binadamu mwenzangu anadiriki kuniharibia jina langu ili yeye apate kula! Hamjui mnaniathiri kiasi gani na hizi habari zenu! Hiyo habari yaani ni ujingaujinga tu umeunganishwa na picha yangu bila hata uoga mmeichukua kutoka kwenye page yangu ya Insta. Mnazitumia kunichafulia jina langu tena wakati ndiyo kwanza nahangaika kurudi kwenye kazi yangu.”
IMG-20160325-WA0001
TV ANDAGRAUNDI IKAMSAPOTI
Kama hiyo haitoshi, kituo kimoja cha runinga cha muda mrefu nchini lakini bado kiko ‘andagraundi’ kilimpa nafasi Ray C akanushe habari ya Ijumaa Wikienda pasipo kujua gazeti hili lilijiridhisha kabla ya kuandika habari hiyo.
SHIGONGO ATAKA UKWELI
Baada ya Ray C kuyaponda Magazeti ya Global kwenye runinga kwa kudai yanamchafua, Shigongo alimuagiza Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa, Oscar Ndauka kupanga makachero kutokea kwenye kikosi maalum cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ili kufuatilia nyendo za msanii huyo kama kweli anaonewa au la na kutaka matokeo yaliyo kamili!
IMG-20160325-WA0004OFM KAZINI
Timu ya OFM ilipangwa kwa zamu kumfuatilia Ray C kwa saa ishirini na nne ili kujiridhisha juu ya malalamiko yake, hasa kwamba Global inaungaunga picha za zamani ili kupata habari kama alivyosema kwenye Instagram yake.
Tangu Januari hiyo, timu ya OFM ilianza kuwa sambamba na Ray C huku makachero wengine wakiwasaka watu wake wa karibu ili kusikia chochote kutoka kwao.
FRONTIJUMAAGazeti la Ijumaa, toleo namba 799 la Novemba 2-8, 2012
MSIKIE HUYU
“Mimi ni miongoni mwa watumiaji wa madawa ya kulevya ambaye nilishawishiwa na Ray C kuacha na kunileta hapa kwenye Kituo cha Mwanayamala (hospitali) kwa ajili ya kuanza kumeza Methadone (dawa za kuponya waathirika wa madawa ya kulevya) ili niweze kurudia hali yangu ya kawaida. Hali yangu sasa niko safi na najitambua.AMSIKITIKIA
RAY-C-akimishukur-Rais-KikweteRais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipomsaidia Ray C, Ikulu Jijini Dar.
RAY C
“Kinachoniuma ni Ray C ambaye aliniunganisha hospitali kwa mbwembwe, yeye ameshindwa kuendelea na kapata bwana ambaye amemsaidia kurudia tena matumizi ya unga kushinda zamani. Huwezi amini kwa sasa mwenzetu gari limewaka upya, anawasumbua hata madaktari wetu, wakati mwingine wamekuwa wakishindwa kumhudumia.
RAY-na-Mamama-na-Dada-yake-ikulu
FULL VURUGU
“Akija hapa kituoni kuchukua dawa muda wote ni kuwasimanga hawa wauguzi wetu jambo ambalo linatukera sana kwani anatuharibia hata sisi ambao alituleta. Aliyemponza ni Frank. Frank alikuja hapa kituoni kama mwathirika na kuanza kutumia dawa.
“Baada ya kukutana na Ray C na kuwa marafiki, wameshindwa kuendelea kutumia dawa. Badala yake wamekuwa wakivuta unga kiasi cha kuzima na kuleta fujo tu. Huyu Frank anaishi Mwananyamala karibu na hapa hospitali,” alisema mwathirika mmoja akiomba kufichiwa jina lake.
MADAKTARI WALIMSUSA
Akaendelea: “Unajua  madaktari wa hapa  walifikia hatua ya kujivua kumhudumia na kumrejesha kwao kipindi kile alipofanya fujo Posta. Ninasema haya kwa uchungu maana hata sisi tunaokunywa naye dawa hakuna hata mmoja anayeweza kummudu zaidi ya huyo Frank ambaye naye gari limeshachanganya, anampoteza kabisa Ray C,” kilisema chanzo hicho.”
JK ANYOOSHA MIKONO, AMUACHIA MAGUFULI
Chanzo kingine kilichopo kwenye hospitali hiyo kililiambia Ijumaa Wikienda kuwa, kutokana na JK kumsaidia alipokuwa madarakani na mrembo huyo kurejea tena kwenye unga, amenyoosha mikono, jukumu hilo litabaki kwa rais wa sasa, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’.
“JK ameshanyoosha mikono. Hawezi tena kumuelewa huyu dada, amemuachia Magufuli naye labda ajaribu kwani ndiye aliyeko madarakani,” kilisema chanzo hicho.
RAY C MWENYEWE HUYU HAPA
Alipotafutwa Ray C juzi na kusomewa madai hayo na kuelezwa juu ya kupigwa picha zinazomuonesha akiwa amezima, alifunguka:
“Kweli kuna picha nimesikia watu walinipiga nikiwa nimezimika lakini siyo kwamba nilivuta unga kiasi hicho, picha hizo nilipigwa kweli nikiwa nimezima baada ya kunywa dawa hapo hospitali maana dawa ninazokunywa huwa ni kali sana, saa nyingine huwa nashindwa kujizuia na kujikuta nimezima.
“Kwanza unatakiwa ujue kwamba hizi dawa siku zote ukinywa hata kama ungekuwa na nguvu kiasi gani lazima kuna muda unafikia hatua ya kushindwa kabisa kujimudu na saa nyingine huwa tunalala hata na wenzangu kwani hata hizo picha wamenipiga chini ya mti hapahapa jirani na eneo la hospitali, siku hiyo nilikuwa nimezidiwa sana.”
AMTAJA FRANK KAMA ‘BEBI’ WAKE
“Ninachokijua nilala chini ya mti na Frank lakini hata ukiangalia nyuma yetu pia
kuna watu kibao ambao nao walikuwa wamelala baada ya kunywa dawa na kuzidiwa, sasa sijui wewe hizo zangu na huyo mpenzi wangu umezitoa wapi,” alisema Ray C.
DAKTARI WA WAATHIRIKA AZUNGUMZA
Baada ya utetezi huo wa Ray C, gazeti hili lilimwendea hewani daktari wa tiba kwa waathirika na unga kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (jina lipo) na kumuuliza kama matumizi ya dawa za Methadone yanaweza kumzimisha mtumiaji ambapo alisema:
“Kama anayetumia Methadone baada ya kuathirika hatatumia madawa ya kulevya hawezi kuzima kwa namna yoyote ile. Ukimwona mtu anazima ujue anachanganya, yaani anameza Methadone pia anaendelea kubwia unga.”
TUMEFIKAJE HAPA?
Ray C aliyewahi kutamba na nyimbo nyingi kali, ikiwemo Na Wewe Milele, alijikuta ametopea kwenye madawa ya kulevya baada ya kutumbukia kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa staa wa Hip Hop Bongo, Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez’ ambaye naye anadaiwa kutumia.
Baadaye wawili hao walimwagana huku Ray C akichanja mbuga katika eneo hilo hali iliyomlazimisha ‘kustaafu’ muziki kutokana na mwili kukosa mawasiliano katika kupanga mikakati.
Gazeti damu moja na hili, Ijumaa, toleo Namba 799 la Novemba 2-8, 2012 lilitoa picha za Ray C akiwa amezimika na habari yenye kichwa; DAH!
RAY C. Tukio hilo lilijiri maeneo ya Magomeni, Dar.
JK ASOMA, APATA UCHUNGU
Wiki moja baada ya gazeti hilo kuingia mtaani likielezea hali ya Ray C, JK alimwita Ikulu ya Dar es Salaam yeye, mama yake mzazi, Margaret Mtweve na ndugu mwingine hali iliyoonesha kuwa, aliisoma habari hiyo kwenye Gazeti la Ijumaa.
Lengo la kumwita lilikuwa kumsaidia mwanamuziki huyo kwa tiba na uangalizi wa kina jambo ambalo lilifanyika na akarudia kwenye hali yake ya kawaida.
Mwaka 2015, baada ya minong’ono mingi kwamba msanii huyo amerejea katika matumizi ya unga, magazeti ya Global yaliandika habari hiyo na Ray C akawa anakanusha mara kwa mara mpaka majuzi aliponaswa akiwa amezima.
JK ALIVYOMSAIDIA RAY C

Babu Tale: Niko Tayari Kumsaidia Msanii yeyote Anayetaka Kuacha Madawa ya Kulevya

Meneja wa Diamond Babu Tale katamka kuwa yuko Tayari kumsaidia msanii yeyote yule ambaye yuko tayari kuacha madawa ya kulevya, kasema milango iko wazi kama ambavyo kamsaidia Chid Benzi ambaye kapelekwa sober House Bagamoyo.

Pamoja na hayo kadai haikuwa kazi rahisi kwa Chid Benzi maana pamoja na kumpeleka sober bado alikua "akistua" njiani, njia nzima alikua akivuta hii midude.

Mungu ambariki sana huyu jamaa

Sunday, March 27, 2016

Tetesi ya kwamba Ray C amerudi kwenye matumizi ya Madawa ya kulevya isipuuzwe..

Matumizi ya Madawa ya kulevya hapa nchini yanaongezeka kwa kasi sana. Huku ikionekana wasanii ni moja kati ya waathirika wa kubwa wa janga hili. Tumeona hivi karibuni rapa mkongwe Chidi Benz jinsi alivyothorofika kutokana na matumizi ya Madawa ya kulevya.Ray C
Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na tetesi kwamba Ray C amerudi katika matumizi ya madawa ya kulevya ingawa mara kadhaa amekuwa akikanusha taarifa hizo.
Waswahili wana msemo mashuhuri usemao ‘Lisemwalo lipo’ kwa nini asitajwe msanii wengine, na mara nyingi wasanii wote ambao hutumia Madawa ya kulevya, uanza kwa kukataa hadi pale akapozidiwa ndipo anaweka wazi. Tumeshuhudia kwa Chidi Benz, Ray C, Q Chief na wengine.
Februari mwaka huu, Ray C alikanusha vikali taarifa ya kwamba amerudi kwenye matumizi ya madawa ya kulevya , “Hata siju moja sikawahi pata msaada wowote kutoka kwenu japo kunichangia nauli tu ya kuja kwenye dawa kila siku hakuna hata anaenisaidia huu mwaka wa tatu bado naendelea kunywa dawa na ni kila siku ya mungu siku saba kwa wiki hakuna sikukuu wala msiba na ukikosa mwili unauma vibaya sana yani it’s not easy but am a fucking hard working woman na ni mwanamke jasiri napambana na siogopi kujaribu, napambana na haya madawa na nayapinga na kamwe sintorudi nyuma na hizi nuksi mzipeleke kwenye familia zenu,” aliandika Ray C katika instagram yake.
Lakini kauli hiyo bado haiendani na maisha yake halisi ya sasa, kwani Ray C bado anadaiwa kuoneka katika mitaa ya Mwananyala akiwa katika hali mbaya licha ya kuwa huu ni mwaka (3) akitumia dosi ya Methadone. 
Rais mstaafu Jakaya Kikwete tayari alishafanya kazi kubwa ya kumsaidia Ray C na kumfikisha hapa alipo sasa. Huu ni wakati wa wasanii wenzake kupokea kijiti na kumsaidia, Vita ya kupambana na Madawa ya kulevya ni ya wote, kila mmoja amwongoze aliyepotea njia na sio kuiachia serikali.

Thursday, March 24, 2016

Madee Amedai Angekuwa Ameathirika na Matumizi ya Madawa ya Kulevya, Angewataja Wanaomuuzia


Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection Madee Ali amesema kama angekuwa anatumia Madawa ya kulevya na tayari ameshaathirika basi angewataja wale wanaomuuzia ili kuisaidia serikali kutokomeza matumizi ya madawa ya kulevya.
Madee2

Akizungumza katika kipindi cha Enewz cha East Africa Television, Madee amesema serikali inaweza kutokomeza biashara ya Madawa ya kulevya kama ikiwatumia wale walioathirika.

“Ningekuwa mimi natumia Madawa ya kulevya na tayari yameshaanza kuniathiri si utaulizwa imekuwaje kuwaje, nani amekufundisha hizi mambo, umeanza wapi umenunua kwa nani, ina maana nitaanza kumtaja yule ambaye ameniuzia, na ambaye ameniuzia mimi kikete, yeye atamtaja bosi wake, bosi wake atamtaja yule bosi wake mkubwa kwa hiyo ile cheni yote itakuja mpaka itamfikia yule kigogo anayeingiza kutoka nje”, alisema Madee

Pia Madee alisema ingawa wasanii wana nafasi yao katika kupambana na biashara ya Madawa ya kulevya, lakini serikali ndio chombo ambacho kinaweza kupambana na biashara hiyo na inatokomeza kabisa.

Wednesday, March 23, 2016

MABASI YAENDAYO KASI KUANZA NDANI YA WIKI HII


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mabasi yaendayo kasi (DART) yataanza kufanyiwa majaribio ndani wiki moja kuanzia sasa ili madereva waanze kuzoea njia na taa za kuongozea magari.

“Wataanza na mabasi kati ya 30 – 50 ambayo yatapita kwenye njia zote za mradi huo. Zoezi hilo litafanyika ili watumiaji wengine wakiwemo waendesha daladala, bodaboda na watembea kwa miguu waweze kutambua kuwa njia ya mabasi yaendayo kasi si ya kwao, hivyo waanze kuzoea,”alisema.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Machi 22, 2016) wakati alipofanya ziara ya ghafla katika Soko la Kimataifa la Samaki la Feri iliyokuwa na lengo la kuangalia mfumo wa majiko ya gesi sokoni hapo na kukagua ujenzi wa ukuta unaotenganisha soko hilo na mabasi yaendayo kasi.

Waziri Mkuu ambaye ametembelea soko hilo kuanzia saa 5:10 hadi saa 5:54, alitoa jibu hilo wakati akijibu maombi ya mfanyabiashara mmoja, Bw. Sharifu Ramadhani ambaye alisema wanatumia fedha nyingi kwa ajili ya usafiri kwa vile mabasi mengi yanaishia Mnazi Mmoja. 
“Mabasi yanaishia Mnazi Mmoja na huku ni mbali kwa hiyo tunalazimika kutembea kwa miguu kwa sababu kukodi taxi ni gharama kubwa,” alisema.

Akifafanua kuhusu hatua iliyofikiwa kwenye utekelezaji wa mradi huo, Waziri Mkuu alisema: 
“Hivi sasa wanakamilisha ufungaji wa mitambo ya kukatia tiketi ambapo abiria atakuwa na kadi kama za benki ambayo anaijaza fedha halafu anapita kwenye mashine, kiasi cha nauli kinakatwa halafu anaingia kwenye basi, hakutakuwa na muda wa kukata tiketi.”

Alisema tatizo la usafiri kwa wafanyabiasha wa feri litakwisha hivi karibuni baada ya mabasi hayo kuanza.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMANNE, MACHI 22, 2016.