Brighton Masalu
STAA mkongwe wa sinema za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ ametoa ushuhuda mzito (confession) baada ya kukiri kuishi maisha ya starehe ikiwemo unywaji pombe na kukosea mwanaume sahihi wa maisha kwa kuingia kwenye uhusiano tofauti jambo aliloliita ni ‘kumtumikia shetani kwa pombe na ngono’.

Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu hivi karibuni katika mahojiano maalum, Mainda ambaye kwa sasa ni mlokole wa ‘tuimbe na kusifu’ aliweka wazi kuwa kipindi cha nyuma, shetani alimzidi nguvu kwa kujichanganya maeneo ya baa na kunywa pombe jambo ambalo kwa sasa kila akikumbuka huishia kusikitika.
Alisema, kwa sasa hana mpenzi na kwamba hatafuti lakini anamngojea yule ambaye anaamini atatoka kwa Mungu kwa wakati muafaka.Mainda aliweka wazi kuwa anamshukuru Mungu kwa kumuongoza katika njia nyoofu huku akiainisha kuwa maisha bila ya kuwa na Mungu ni ya ajabu sana.
“Kwa kweli maisha ya zamani yalikuwa ya ajabu, ulevi wa pombe, kutoka na wanaume tofauti nikidhani ndiye mwanaume sahihi, zilikuwa ni nguvu za shetani, namshukuru Mungu kwa kunibadilisha kwa kiwango hiki kwani nilimtumikia sana ibilisi kwa mambo machafu, viongozi wangu wa dini wananipa mwanga mkubwa mno juu ya Neno la Mungu na kila nikikumbuka maisha ya nyuma, huwa siyatamani kabisa,” alisema Mainda.