Showing posts with label ELIMU. Show all posts
Showing posts with label ELIMU. Show all posts

Tuesday, June 7, 2016

Mikopo ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St Joseph (SJUIT) Yafutwa......Waliokuwa chini ya Programu ya Miaka Mitano ya Ualimu Watakiwa Kurudi Diploma

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha St Joseph (SJUIT) Kampasi ya Arusha (kilichofutiwa usajili), waliokuwa chini ya programu ya shahada ya miaka mitano ya ualimu wa sayansi, wametakiwa kusoma ngazi ya cheti au stashahada. 

Kama watataka kusoma ngazi ya juu, watapaswa kuomba upya udahili.

Aidha, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imesema wanafunzi waliokuwa wakipata mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), mikopo yao pia imesimamishwa.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Simon Msanjila alitoa agizo hilo jana kupitia taaarifa kwa vyombo vya habari. 

Profesa Msanjila alisema hatua hiyo, inatokana na kubainika kwamba wanafunzi hao hawastahili kusoma shahada na pia hawakustahili kupewa mkopo.

“Tunawafahamisha wanafunzi wa SJUIT waliokuwa kwenye programu ya miaka mitano kwamba watatakiwa kuishia daraja la cheti na stashahada... Kama wanafunzi hao watataka kuendelea na masomo ya juu, watatakiwa kuomba upya,” ilisema taarifa hiyo.

Februari 25, mwaka huu, Wizara kupitia Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) baada ya kujiridhisha kuwa Kampasi ya Arusha ya Chuo Kikuu cha Mt. Joseph Tanzania imepoteza sifa na vigezo vya kuendelea kutoa elimu ya chuo kikuu, ilifuta kibali cha kuanzishwa kwake.

Iliidhinisha uhamisho wa wanafunzi wote, waliokuwa wanasoma katika Kampasi hiyo ya Arusha kwa gharama za Chuo Kikuu cha SJUIT. 

Aidha, ilifuta udahili wa wanafunzi wapya katika programu ya shahada ya miaka mitano ya ualimu wa sayansi.

Ilielekeza wanafunzi waliokuwa wakiendelea na masomo katika programu hiyo, wahamishiwe katika Kampasi ya Luguruni, Dar es Salaam. 

TCU ilielekeza kwamba wanafunzi watalazimika kwanza kuhitimu katika ngazi ya Stashada, kama ilivyokuwa imeidhinishwa na Tume hapo awali. 

Wanafunzi waliohamishiwa kwenye vyuo mbalimbali, waendelee na masomo.

Taarifa hiyo ilisema wakati wa mchakato wa uhamisho, wanafunzi wote walihakikiwa kubaini kama wanakidhi vigezo vya kusoma kwenye ngazi hiyo. 

Wanafunzi wote waliokuwa wakisoma programu hiyo ya miaka mitano, walihamishiwa kwenye Kampasi ya Luguruni, jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo kutokana na mchakato wa uhakiki, baadhi ya wanafunzi walikutwa hawana sifa za kujiunga na mafunzo hayo ya ualimu. 

Wale waliobainika kuwa na sifa, walitaarifiwa kuendelea na masomo kwenye kampasi hiyo ya Luguruni.Wanafunzi katika kundi hili waliobainika kuwa na vigezo, walitaarifiwa kuendelea na masomo katika Kampasi ya Luguruni. 

"Maana ya kuwa na vigezo vya ufaulu tunavyovizungumzia hapa ni kwamba wanafunzi husika wamefaulu katika masomo lengwa yanayowawezesha kusoma Cheti cha Ualimu Daraja “A” ambacho ni kigezo cha kwanza kwa mujibu wa mtaala wa programu hiyo."

Friday, June 3, 2016

Video ya Rais Magufuli Akipigilia Msumari Sakata la Wanafunzi 'Vilaza' Waliofukuzwa UDOM

Video  ya  Rais  Magufuli  Akipigilia  Msumari  Sakata la Wanafunzi 'Vilaza'   Waliofukuzwa UDOM

Thursday, June 2, 2016

Walioandaa Mgomo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Kuadhibiwa

Wakati Rais John Magufuli akitarajia kuwasili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo, wanafunzi walioandamana wakishinikiza malipo yao ya fedha za kujikimu juzi, huenda wakakumbwa na hatua za kinidhamu.

Wanafunzi hao huenda wakaadhibiwa kwa kosa la kukikuka sheria ndogo ya chuo kwa kuandaa mkusanyiko pasipo kibali cha menejimenti.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma), Florens Luoga alisema jana kuwa, mamlaka za nidhamu chuoni hapo zinaendelea na uchunguzi kubaini nani aliyehusika katika tukio hilo.

“Taratibu na sheria ndogo za chuo haziruhusu mtu kuandaa mkusanyiko ambao haujaidhinishwa na menejimenti. Taratibu hizo lazima ziheshimiwe ili ziendelee kuwa imara. Hivyo tunasubiri ripoti ya waliohusika,” alisema Luoga.

Juzi, wakati wa maandamano ya wanafunzi hao walikuwa wakipaza sauti iliyotolewa na Rais Magufuli wakati wa kampeni za kuwania wadhifa huo akisema:

“Serikali yangu haitarajii kuona mwanafunzi akifukuzwa chuo kwa kosa la kugoma kisa mkopo, bali ikitokea mgomo, watawajibisha maofisa wa Bodi ya Mikopo kwa kuchelewesha fedha.”

Taarifa zilizopatikana jana zilieleza kuwa fedha za wanafunzi hao zimeshawekwa kwenye akaunti zao, juzi jioni.

Rais wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo, Erasmi Leon alisema licha ya wanafunzi hao kukiuka utaratibu, haoni sababu za kuwachukulia hatua kwani hawakusababisha madhara wala uharibifu wowote.

“Endapo kamati ya nidhamu itaamua kufanya hivyo ni vyema wakafanya suala hilo kimantiki na kibinadamu na endapo usimamizi wa sheria ukifuata zaidi unaweza ukasababisha kuibuka kwa mambo mengine tofauti,” alisema Leon.

Alisema wanaendelea kuwasihi wanafunzi kuhakikisha suala hilo halijitokezi tena kwani linaitia doa Serikali yake, uongozi wa chuo na Taifa kwa jumla.

Wanafunzi hao waligoma kuanzia Jumatatu usiku na mgomo wao kuisha juzi, baada ya kupewa fedha zao ambazo zilichelewa kwa madai ya uhakiki wanafunzi hewa unaondelea.

Tuesday, May 31, 2016

Wanafunzi wa chuo kikuu cha cha Dar es salaam Wagoma

Wanafunzi wa chuo kikuu cha cha Dar es salaam mpaka sasa wamegoma wakiishinikiza bodi ya mikopo kutoa fedha kwa ajili ya kujikimu.
 
Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi, Shamila Mshengema amesema mgomo huo ni matokeo ya taarifa zisizoeleweka zilizo kuwa zikitolewa na bodi juu ya lini fedha hizo zitatolewa.
 
Kwa kawaida pesa ya chakula huingiziwa kila baada ya siku 60 na mpaka sasa yapata wiki mbili pesa hiyo haijaingizwa
 
Mgomo huo unakuja zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya Rais Magufuli Kuzulu chuo hicho kwa ajili ya uzinduzi wa jengo la Maktaba.

Kauli ya Serikali kuhusu wanafunzi 7802 wa UDOM waliorudishwa nyumbani

Hii ndo Kauli ya Serikali kuhusu wanafunzi 7802 wa UDOM waliorudishwa nyumbani

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) Profesa Tunus Mgaya Aliyesimamishwa Kazi na Waziri wa Elimu Afunguka Mambo Mazito

ALIYEKUWA Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Profesa Tunus Mgaya amesema amesikitishwa na taarifa zilizoandikwa katika vyombo vya habari za kukosoa maamuzi ya serikali ya kuwasimamisha kazi kuwa hayakuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa.

Mgaya ambaye hakuwa tayari kueleza kama taratibu za kusimamishwa kwao zilifuata utaratibu au la, amewataka waandishi wa habari kuwa na vyanzo vya uhakika katika habari zao.

“Mimi nikiwa miongoni mwa watendaji waliopumzishwa kazi, napenda kueleza kuwa sihusiki na taarifa hizo, suala hili limeshapita na kutolewa uamuzi na serikali na tuiache Tume iendelee kufanya kazi,” alisema Profesa Mgaya alipozungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kukabidhi ofisi.

Aidha, Profesa Mgaya aliweka wazi kuwa, anaunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika kuhakikisha kuwa watanzania wengi zaidi wanapata elimu ya msingi bure na kutolewa kwa elimu inayokidhi viwango stahiki kitaifa na kimataifa na kusema jambo hilo ni jema na linapaswa kuungwa mkono kwa nguvu zote.

Katika hatua nyingine, alimtaka Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi , Profesa Joyce Ndalichako kuendeleza jitihada za kuinua ubora wa elimu katika ngazi zote ili kuwa na taifa lenye watu walioelimika vizuri na lenye mchango mkubwa katika kuendeleza taifa.

Saturday, April 9, 2016

Thursday, April 7, 2016

Taarifa Za Uzushi Kuhusu Walimu Kushonewa Sare Inayosambazwa Katika Mitandao Ya Kijamii


WIZARA YA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI
TAARIFA KWA UMMA

YAH: TAARIFA ZA UZUSHI KUHUSU WALIMU KUSHONEWA SARE INAYOSAMBAZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi inakanusha taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari “NDALICHAKO NA WALIMU TZ”.

Taarifa hiyo inadai kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa walimu wanaandaliwa sare watakazo vaa wakati wa kazi.

Tunapenda kuufahamisha umma kuwa Taarifa hizi si za kweli. Aidha, Wizara inawataka watu wanaoeneza taarifa za kizushi za aina hii waache kufanya hivyo ili kuepusha usumbufu unaojitokeza.

Hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika kuanzisha na kueneza uzushi huu.

IMETOLEWA NA

KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
07/04/2016

Tuesday, April 5, 2016

Walimu Walazwa UCHI na Kuchapwa Viboko


Ofisi ya Elimu wilayani Kisarawe, Mkoa wa Pwani imelazimika kuwapa likizo walimu saba wa Shule ya Msingi Mingwata ili kuwajenga kisaikolojia baada ya kukithiri kwa matukio ya kishirikina yanayowakumba katika shule hiyo.

Walimu hao wanakumbana na matukio ya ajabu ikiwamo kujikuta uchi, kupigwa fimbo na mtu asiyeonekana na kulazwa nje ya nyumba zao.

Mmoja wa walimu walioathirika na matukio hayo, Emmanuel Shaaban alisema yeye na familia yake hawana raha kutokana na matukio hayo kwa kuwa usiku huvuliwa nguo na kujikuta wamelazwa sehemu nyingine, huku wakiwa wamechanjwa kwa wembe mwili mzima.

“Tarehe 26 mwezi wa pili, siku ya Alhamisi sitaisahau kabisa. Ndiyo siku ambayo nilikatwa viwembe mwili mzima na hali yangu ilikuwa mbaya, niliishiwa nguvu na mwili ukawa na ganzi na nilipokwenda hospitali niliambiwa sina ugonjwa,” alisema Shaaban.

Alisema alipotoka hospitali alikwenda kijijini kwao mkoani Mwanza na huko aliendelea kuwa na hali mbaya kutokana na kuzimia mara kwa mara kwa sababu ya maumivu ya kichwa hadi alipotibiwa kienyeji.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Mikidadi Mbelwa alisema awali alikuwa akiona vituko usiku na mchana, lakini alivumilia huku akitunza siri bila kuwaeleza wenzake ili asiwakatishe tamaa.

Mbelwa alisema baadhi ya matukio aliyokutana nayo ni kuvuliwa nguo usiku, kulazwa eneo jingine, kuchapwa viboko, kumwagiwa damu kwenye korido ya nyumba, kuchanjwa kwa wembe, kuzungukwa na nyoka mwilini, kuona mtu na kisha anapotea na kutupwa kwenye mashimo.

Mzazi wa watoto wanaosoma katika shule hiyo, Asha Kondo alikiri kuwapo kwa matukio ya watoto kuugua na kuanguka hadi uongozi wa kijiji ulipopeleka mganga wa kienyeji kutoa kinachodaiwa ni uchawi.

Mratibu wa Elimu wa Kata ya Marui, Damaru Charles alisema amekuwa akipokea malalamiko hayo na kuyawasilisha ngazi za juu.

Ofisa Elimu Msingi wilayani hapa, Aurelia Rwenza alisema tatizo hilo linawapa shida walimu na kurudisha nyuma maendeleo ya elimu katika sehemu hiyo.

“Kwa kweli walimu wameathirika, hivi sasa tunatakiwa kuwajenga kisaikolojia,” alisema.

Monday, April 4, 2016

Mabenki sasa kupata Taarifa za wadaiwa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) mwishoni mwa wiki imesaini mkataba na Kampuni ya CreditInfo Tanzania Ltd utakaowezesha taarifa za wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu kufikishwa katika Kitengo Uratibu za Taarifa za Mikopo (Credit Reference Bureau) kilichopo katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kampuni ya CreditInfo Ltd ina leseni iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.

Hivyo basi, mnufaika wa mikopo ya elimu ya juu ambaye ataomba mkopo kutoka kwenye taasisi yoyote ya kifedha hapa nchini, taasisi hiyo itakuwa na uwezo wa kuhakiki kama mwombaji huyo ni munufaika wa mkopo wa elimu ya juu na ikiwa ana nidhamu ya kurejesha mikopo.

Kwa mujibu wa mkataba huo, HESLB itawasilisha orodha ya wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu kwa kampuni ya CreditInfo ambayo itahakikisha taarifa za wakopaji zinapatikana kwa taasisi zote za kifedha, yakiwemo mabenki, ili taasisi hizo zijiridhishe kabla ya kutoa mikopo mipya kwa wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu.

“HESLB ina furaha kufanya kazi na CreditInfo kama mdau mpya. Tunawasihi wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu waanze kulipa madeni yao ili wawe na hadhi ya kukopesheka na taasisi za kifedha,”alisema kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Jerry Sabi wakati wa hafla fupi ya kutia saini mkataba huo katika ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa CreditInfo Tanzania Ltd Bw. Davith Kahwa amesema lengo la kampuni yake ni kuhakikisha fursa za ukopaji zinazongezeka na wakopaji wanakuwa na nidhamu kwa mikopo waliyopata.

“Wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu ambao wamekuwa wakilipa watapata fursa ya kipekee ya kujadiliana na taasisi za kifedha kuhusu viwango vya riba kwa sababu ya nidhamu wanayoionyesha kwa mikopo yao,” alisema Bw. Kahwa katika hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Meneja wa CreditInfo Tanzania Bw. Van Reynders.

”Tumedhamiria kuiunga mkono HESLB katika kutekeleza majukumu yake hususan yale ya ukusanyaji mikopo iliyoiva,” aliongeza Mtendaji Mkuu huyo wa CreditInfo Tanzania Ltd.

HESLB ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi Julai 2005 ili kutoa mikopo kwa watanzania wahitaji na pia kukusanya mikopo iliyoiva ambayo imekuwa ikitolewa na Serikali tangu mwaka 1994.

Hadi sasa, zaidi ya Tshs 2.1 trilioni zimetolewa kwa watanzania na, kati ya hizo, Tshs 258 bilioni zimeiva na hivyo kutakiwa kukusanywa kutoka kwa wanufaika.

Kiasi kilichobaki kinajumuisha fedha walizopewa wanafunzi ambao bado wanaendelea na masomo na ambao muda wa kuanza kuwadai (miezi 12 baada ya kumaliza masomo) haujafika.

CreditInfo Tanzania Ltd ni sehemu ya Kampuni ya Kimataifa inayofanya kazi kwenye nchi zaidi ya 20 duniai na inayojishughulisha na usimamizi wa taarifa za mikopo. Ilisajiliwa na Benki Kuu ya Tanzania mwaka 2013.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Jerry Sabi (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya CreditInfo Tanzania Ltd Bw. Davith Kahwa wakisaini mkataba ambao utaiziwezesha taasisi za kifedha zinazotoa mikopo nchini kuhakiki taarifa za waombaji mikopo, ambao ni wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu, kabla ya kuwapa mikopo mipya. Wengine ni Bw. Frimat Tarimo, Mwanasheria wa HESLB na Bw. Van Reynders, Meneja wa CreditInfo Tanzania. (Picha: HESLB).

Saturday, March 12, 2016

Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako 'Atibua' Dili la Bilioni 4........Fedha Hizi Zilipangwa Kutafunwa Ndani ya Siku Nne


Waziri wa Elimu, Mafunzo ya Ufundi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amezuia Ulaji wa Sh bilioni 4 zilizokuwa zitumike kwa ajili ya semina ya siku nne.

Akizungumza wakati akifunga mkutano mkuu wa tatu wa maofisa elimu mkoa na wilaya nchini, Profesa Ndalichako alisema amezuia mafunzo yaliyokuwa yagharimu Sh4 bilioni ambayo mtu mmoja alitengewa Sh4 milioni kwa ajili ya semina ya siku nne.

“Ina maana kila mtu alikuwa alipwe shilingi milioni moja kwa siku. Kweli hatuoni aibu kutumia fedha hizo kwa mafunzo. Watu walewale wanaokwenda kwa mafunzo yaleyale,” alisema. 

Alisema wakati hayo yote yakitendeka, wanafunzi wananyeshewa mvua kwa kukosa madarasa na wanakaa chini kwa kukosa madawati.

Profesa Ndalichako, pia alisema amegundua ufisadi katika Sh66 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya mafunzo, ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule nchini.

Alisema Novemba mwaka jana, Serikali ilitoa Sh63 bilioni katika mikoa yote nchini, kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu.

Profesa Ndalichako alisema baadhi ya fedha hizo zilitolewa bila kufuata utaratibu sahihi, hivyo kufanya wengine kutofahamu kama kuna fedha kama hizo zilitolewa.

“Kuanzia Jumatatu nitapeleka orodha na kiasi cha fedha kilichopelekwa kwa Ma-RC (wakuu wa mikoa) na Ma-DC (wakuu Wilaya) nchini ili mzione. Fedha zitawatokea puani…cha mtu sumu, kama ulikula fedha hizo uhakikishe unazirejesha.”

Bila kumtaja jina, Profesa Ndalichako alisema kuna mtu alitumia Sh60 milioni kukarabati darasa moja la shule ya msingi.

“Hiyo ni ukarabati wa darasa tu la shule za msingi. Wale waliokula fedha hizo nawaambia zitawatokea puani, hatuwezi kuwavumilia,” alisema.

Akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Maofisa Elimu wa Wilaya na Mikoa (Redeoa), Juma Kaponda alishauri walimu wa shule za msingi waimarishwe kwa maarifa na lugha ya Kingereza.

Hata hivyo, alisema ni vyema stashahada ya elimu ya msingi ifundishwe kwa Kingereza .

Sunday, March 6, 2016

SAA ZINAZOWEZA KUTUMIWA KUIBA MITIHANI (CHABO).


Saa za kisasa ambazo zimetengenezwa mahususi kutumiwa kudanganya wakati wa mtihani zimekuwa zikiwakosesha usingizi walimu na wasimamizi wa mitihani.
 
Saa hizo zina uwezo wa kuweka akiba data na maelezo ambayo yanaweza kusomeka mtu anapofanya mtihani.
Aidha, zina kitufe cha dharura ambacho kinaweza kubadili uso wa saa hizo haraka sana na badala ya kuonesha habari ziwe zinaonesha uso wa kawaida wa saa.


Saa hizo zinatangazwa katika soko la kuuza bidhaa mtandaoni la Amazon.

Mojawapo ya aina ya saa hizo ina uwezo wa kuweka akiba data ya 4GB. Nyingine, ambayo itaanza kuuzwa baadaye mwaka huu, itakuwa na uwezo wa 8GB na inaweza kuhifadhi hata video.

Baadhi ya saa hizo, zina kifaa kidogo sana cha kusikizia ambacho hakitumii nyaya, jambo linalowezesha mtu kusikiliza kilichohifadhiwa kwenye saa hiyo bila kuonekana.

Tangazo moja katika mtandao wa Amazon linasema mtu anaweza kununua saa ya aina hiyo kwa $61 (£43).
Kuna pia matangazo ya saa hizo eBay.
Naibu mwalimu mkuu wa shule moja kutoka Bath, Uingereza anasema saa hizo zinaweza zikawashawishi wanafunzi kuhadaa katika mtihani.

Bw Joe Sidders wa shule ya Monkton Combe Senior School amesema ingawa saa hizo zinaweza kudhibitiwa kwa kutumia sheria zinazoharamisha simu na kompyuta kutoka vyumba vya mitihani, ni changamoto kubwa sana kwa watu wanaosimamia mitihani.

Amesema uuzaji wa saa hizo unafaa kudhibitiwa.
Kuna pia “kalamu za kuiba mtihani” ambazo zinaweza kuhifadhi habari na maelezo.


Ongezeko la matumizi ya saa kuiba yamefanya baadhi ya mashirika kupiga marufuku saa katika vyumba vya mitihani Uingereza.

Thursday, February 25, 2016

Usithubutu kwenda kwenye Usaili wa kazi bila kufahamu mambo haya manne

Interview
Usaili wa kazi ni hatua muhimu kwa kila mwenye ndoto ya kuajiriwa na kupata kazi ya ndoto yake. Lakini ni hatua yenye vikwazo vidogo vinavyogeuka kuwa mlima wa kikwazo pale ambapo msailiwa ataruka hatua hizi nne muhimu katika maandalizi yake.
Kutofahamu mambo haya muhimu kabla ya kuingia kwenye usaili, huwafanya wasailiwa wengi kujikuta wakijuta kuingia kwenye usaili husika au kufikiri kuwa hawana bahati ya kupata kazi wanayoitamani kwa kuwa wamejibu vizuri maswali mengi waliyoulizwa.
Lakini maswali unapaswa kufahamu kuwa mambo haya manne yatakupa asilimia zaidi ya 80 ya ushindi kwenye maswali yoyote utakayoulizwa na wasaili. Hata kama maswali utakayoulizwa unayafahamu vilivyo, lakini kushindwa kuyaunganisha na mambo haya kutakuangusha vibaya na huenda ukambilia kudhani ulinyimwa kazi kwa makusudi.
Fahamu vizuri Kampuni/shirika husika
Hii ni hatua ya kwanza na muhimu sana katika ushindi wa usaili husika. Karibu kila swali utakaloulizwa litakuwa na uhusiano na hili.
Hivyo, unapaswa kufahamu vizuri kazi na huduma au bidhaa zinazotolewa na shirika husika,  dhima na dira na lengo kuu la kampuni/shirika hilo. Unapaswa pia kuhakikisha unafahamu washindani wa kampuni husika hususan kama inafanya biashara yoyote.

Tambua Udhaifu, Uimara, Fursa na Hatari/vitisho ambavyo kampuni husika inakutana navyo. Ni rahisi kufahamu mambo hayo endapo utatumia muda wako kufanya utafiti wenye mantiki kuhusu kampuni husika. Taarifa hizi zote unaweza kuzipata kwa kusoma tovuti ya kampuni husika pamoja na machapisho yao mbalimbali.
Hii itakuongezea hali ya kujiamini kwa kuwa unamfahamu vizuri mwajiri wako.
Fahamu kiundani majukumu yote ya nafasi unayowania
Hapa simaanishi tu kukariri majukumu uliyoandikiwa kwenye tangazo la nafasi ya kazi, bali kufahamu kwa kina kinachotegemewa kutoka kwako.
Muajiri wako anatarajia mtu atakayemuajiri awe anajitambua vizuri na amejiandaa kuyakabiri majukumu yake. Anatarajia kuona nia na uwezo wa mtu anayemhitaji kwenye usaili husika.
Ukiyafahamu vizuri majukumu yako na mipaka yake, utakuwa na uwanja mpana wa kujibu maswali yako kwa kumshawishi muajiri kuwa majumu husika unaweza kuyakabili kwa ufanisi zaidi. Kila swali litakaloelekezwa kwako, lijibu ukiwa na picha ya majukumu yako pamoja na kampuni yako.
Kwanini unahitaji kazi hiyo na kwanini unadhani wewe ndiye mhusika 
Mwajiri anahitaji sana mtu anayejielewa kama nilivyosema awali, ‘self determined and focused’. Unapaswa kujiuliza vizuri kwanini unahitaji kazi husika, huku ukilizingatia pia swali kuwa unadhani kwanini wewe ndiye mtu unayefaa zaidi kuliko wote.
Kama hufahamu kwanini unahitaji nafasi hiyo, sio kwa sababu unahitaji pesa, hilo linajulikana na ni vyema usiligusie kabisa. Zungumzia upande wa pili wa ‘Career’ yako hasa na unavyotaka kuleta mabadiliko kwenye kazi husika. Ni muda mzuri wa kujinadi.
Ifahamu vizuri, imeze CV yako
Curriculum Vitae (CV), ni maandishi yanayokueleza wewe ulivyo na uhusiano wako na kazi husika. Isome vizuri CV yako baada ya kuandika mambo muhimu unayopaswa kuyaandika. Tutaelezea siku moja kipi hakipaswi kuwekwa lakini huwekwa na wengi.
Usiiache nukta iliyo kwenye CV yako ikupite bila kuielewa vizuri. Isome tena na tena na uelewe kwanini umeandika yote uliyoandika na namna ya kuyaelezea.
Kumbuka katika usaili, CV yako inaweza kuzaa maswali mengi na ikakuinua au kukuangusha. Kumbuka ku-update CV yako kila unapotaka kazi fulani, usiitupe tu kwa kazi yoyote, mengine yanaweza kuwa yanakuinua kwenye kazi A, lakini  yakawa chanzo cha kukukoseha kazi B.

Friday, February 19, 2016

Huyu Ndo Binti Aliyeongoza Kitaifa Katika Matokeo ya Mtihani wa Kidato Cha Nne

Huyu ndiye Mwanafunzi aliyeshika nafasi ya kwanza  Kitaifa katika Mtihani wa Kidato cha Nne  toka  shule  ya  Canossa Girls.Anaitwa Butogwa Charles Shija, akiwa mwenye furaha, nyumbani kwa wazazi wake Kipunguni Jijini la Dar es Salaam jana. 
 

Huyu anaitwa Congcong Wang,ameshika Nafasi ya pili Kitaifa.Amemaliza kidato cha nne Feza Girls.Ni  Mtanzania mwenye asili ya China

Thursday, February 18, 2016

Breaking News: Matokeo Ya Mtihani Kidato Cha Nne -2015 Yametoka....Yatazame Hapa


Baraza la mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2015 yanayoonesha kiwango cha ufaulu kushuka kwa asilimia 0.80.
 
Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles Msonde amesema kuwa jumla watahiniwa 272,947 sawa na 67.53% ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2015 wamefaulu tofauti na mwaka 2014 ambapo ufaulu ulikuwa 68.33%.
 
Msonde amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, waliofaulu ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 11,125 (64.84) na wavulana wakiwa 124,871 (71.09).
 
Amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, ufaulu umeshuka kwaasilimia 1.85 ikilinganishwa na mwaka 2014.
 
Aidha kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, Dkt Msonde amesema watahiniwa 31,951 sawa na asilimia 64.80 wamefaulu ikilinganishwa na watahiniwa 29,162 (61.12) waliofaulu mwaka 2014.
 
Kwa upade wa ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule, Msonde amesema waliopata daraja la kwanza ni 9,816 sawa na asilimia 2.77, daraja la pili ni 31,986 sawa na asilimia 9.01, daraja la tatu ni 48,127 sawa na asilimia 13.56.
 
Aidha waliopata daraja la nne ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 na waliopata daraja la sifuri (waliofeli) ni 113,489 sawa na asilimia 32.09.
 
Watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa kati ya daraja la kwanza hadi la tatu ni 94,941 sawa na asilimia 24.73 wavulana wakiwa 56,603 sawa na 29.99 na wasichana 38,338 sawa na asilimia 19.63.
 
Amesema kwa upande wa ufaulu wa masomo kwa watahiniwa wa shule, ufaulu wa juu kabisa ni wa somo la Kiswahili ambapo asilimia 77.63 wamefaulu huku ufaulu wa chini kabisa ukiwa ni wa somo la Basic Mathematics ambapo asilimia 16.76 wamefaulu.
 
Matokeo hayo yamepangwa katika mfumo wa madaraja (Division) badala ya ule wa wasatani wa alama (GPA) kama ambavyo iliagizwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi hivi karibuni.


Wednesday, February 17, 2016

Taarifa Muhimu Kuhusu Matokeo Ya Kidato Cha Nne 2015 (CSEE) 2015


Baraza la Mitihani la Tanzania limekuwa likipigiwa simu na watu mbalimbali wakiomba ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imetangaza kuwa matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2015 yamezuiwa kwa muda hadi tarehe 08/03/2016.

Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwajulisha watahiniwa na umma kwa ujumla kuwa taarifa hizo ni za UONGO na zinalenga kupotosha umma na kuleta taharuki.

Hivyo, Baraza linaomba umma kuzipuuza taarifa hizo kwa kuwa Wizara haijasitisha utoaji wa matokeo hayo. Matokeo yatatangazwa mara tu mchakato utakapokamilika.

Imetolewa na,
AFISA HABARI NA UHUSIANO

Monday, February 8, 2016

Mwalimu Mkuu Ashushwa Cheo na Kukamatwa na Takukuru Kwa Rushwa ya KUKU


Mkuu wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Amani Mwenegoha amemvua wadhifa wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sinamila, Mashaka Lusotola na kumrudisha kuwa mwalimu wa kawaida.

Hatua hiyo ilikuja baada Mwenegoha kubaini kuwa walimu wa shule hiyo wamekuwa na tabia ya kuwaagiza kuku, wazazi wanaowaandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza.

Mwenegoha alichukua maamuzi hayo, baada ya kuthibitisha kuwa mwalimu huyo mkuu, ameshindwa kudhiti tabia hiyo ya walimu walio chini yake.

Akizungumzia kusimamishwa kwake, Mwalimu Lusotola alisema amefurahi na kufananisha adhabu hiyo na kumpiga teke chura.

Tayari mwalimu huyo amekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupamaba na Rushwa (Takukuru), leo anatarajia kwenda kuandikisha maelezo, huku akisisitiza kuwa hajaomba kitu chochote kwa wazazi.

Thursday, February 4, 2016

BINTI WA KITANZANIA AMAYESOMA INDIA ADHALILISHWA KWA KUPIGWA NA KUVULIWA NGUO

Mtanzania anayesoma India amepigwa, kuvuliwa nguo na kisha kulazimishwa kutembea akiwa uchi na kundi la watu nchini humo.

Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 21 (jina linahifadhiwa) anayesoma shahada ya biashara, mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Acharya, Bangalore, alifanyiwa ukatili huo akiwa na Watanzania wengine wanne.

Gazeti la Deccan Chronical la Bangalore, liliripoti kuwa tukio hilo lilitokea Januari 31, baada ya mwanafunzi raia wa Sudan, Ismail Mohammed kugonga gari la raia mmoja wa India, mkazi wa Hesaraghatta aliyekuwa na mkewe na kusababisha kifo cha mama huyo.

Nusu saa baadaye, Watanzania watano akiwamo aliyevuliwa nguo, walifika katika eneo hilo wakiwa kwenye gari ndipo kundi la watu hao lilipoanza kumshambulia binti huyo, kisha kumvua nguo na kumlazimisha atembee uchi.

Baada ya kuchoma gari lililosababisha ajali hiyo, kundi hilo pia liliteketeza gari alilokuwamo Mtanzania huyo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Mindi Kasiga alisema Balozi wa Tanzania nchini humo, John Kijazi ameshakutana na wanafunzi hao na ameshazungumza na Serikali ya India kuhusu tukio hilo.

Gazeti la Deccan Chronical liliripoti kuwa licha ya polisi waliokuwapo eneo hilo hawakuchukua hatua yoyote hata pale msamaria mwema aliyejitokeza kumsitiri msichana huyo kwa fulana yake ambaye pia alipigwa huku fulana hiyo ikichanwa.

Mshauri wa masuala ya sheria kwa wanafunzi kutoka Afrika wanaosoma Bangalore, Bosco Kaweesi alinukuliwa na gazeti la The Chronical akisema hata dereva wa gari alilokuwa  Mtanzania huyo, Micah Pundugu alipigwa na kujeruhiwa vibaya.

 Alisema hata pale msichana huyo alipojaribu kupanda basi ili kujinusuru na zahama hiyo, abiria walimshusha.