Showing posts with label FIESTA. Show all posts
Showing posts with label FIESTA. Show all posts

Friday, December 26, 2014

TAMASHA LA WAFALME: MZEE YUSUF AFANYA KWELI, NYOMI YAPAGAWA DAR LIVE

Mfalme wa Taarab, Mzee Yusuf akilishambulia jukwaaa la Dar Live na kuwaacha hoi mashabiki waliofurika vilivyo.
Mzee Yusuf akifanya yake stejini.
Mzee Yusuf na madansa wake wakionyesha umahiri wao juu ya steji ya kupanda na kushuka ya Dar Live.

Wednesday, November 5, 2014

JE WAJUA DAVIDO ALILIPWA MILIONI 65 KWA SHOW ALIYOFANYA FIESTA??? HIKI NDO ALICHOKISEMA MWANA FA KUHUSIANA NA MKWANJA HUO..

Davido picha
Kwa mujibu wa MwanaFa akiwa kwenye kipindi Choice fm ni kuwa Davido alilipwa Dolla 40,000 kupiga show Fiesta.
Fa alihoji kwa nini waandaaji wasiwalipe dolla 10,000 wasanii wanne wa Bongo wapige show kali kuliko kuzipoteza kwa show mbovu ya Davido?
Je wadau wa Fiesta ni kweli kuwa show ya Davido haikuwa na thamani hiyo au ni kujikweza tu kwa Fa na wenzake?

Sunday, October 26, 2014

UPENDO ULIVYOSAMBAZWA KWENYE FIESTA KIGOMA OCTOBER 25 2014

7Ilikua ni zamu ya Kigoma ( 89.3 CloudsFM) kusambaziwa upendo wa tamasha la Fiesta ambalo mwaka huu wa 2014 limefanyika kwenye miji 18 ambapo Kigoma na Mtwara ndio imekua miji ya mwisho kulishuhudia likiongozwa na Linah, Madee, T.I.D, Stamina, Rachel, Ali Kiba, Linex, Baba Levo, Mr. Blue, Chege na Makomando.
6
2
5
8
9
10
1
11
13
14
3
4
15
16
17
19
18
20
21
22
23
24
25
26
27

Friday, October 24, 2014

T.I AMEHOJIWA TENA MAREKANI NA KUZUNGUMZIA MENGINE MAPYA KUHUSU TANZANIA

T.IClifford Joseph Harris, Jr. a.k.a T.I mkali kutoka Marekani aliyeangusha show ya nguvu katika jukwaa la Fiesta 2014 siku ya Jumamosi Oktoba 18 2014 katika viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam, bado ameendelea kuyasimulia mazuri na makubwa ya kuvutia aliyokutana nayo Tanzania.
Katika mahojiano aliyofanya New York Marekani na kituo maarufu cha redio Power 105.1kwenye show ya Breakfast Club, T.I amesema tangu aanze kufanya muziki hajawahi kufanya show kwenye jukwaa lolote mbele ya mashabiki zaidi ya 50,000.
T.I amelinganisha idadi hiyo kubwa aliyokutana nayo Tanzania kuwa ni sawa na kufanya show katika uwanja wa mpira wa miguu na kuujaza kwa show moja, kitu ambacho anakiona kabisa sio rahisi na ndio maana hii ya Leaders imekua kubwa kwake.
Swali la kuhusu Ebola bado liliulizwa kwa T.I kama alichukua tahadhari kwa kufanya utafiti kabla ya kwenda Afrika na kusema hakuwa na hofu yoyote alipokuja Tanzania, zaidi alikuwa akifikiria tu kuhusu mpenzi wake, hata hivyo hakukutana na Ebola wala kuona hata dalili za uwepo wake na kusisitiza kwamba mara nyingi Ebola imekua ikiwapata Wanaowahudumia wagonjwa’
Kwenye sentensi nyingine rapper huyu mwenye umri wa miaka 34 alisifia jinsi alivyopokelewa vizuri na kusema Tanzania ni watu wazuri hivyo akamwambia Dj Envy kwamba ataenjoy sana kwenye safari yake ya Afrika December mwaka huu.
Video ya T.I akiwa katika mahojiano hayo nimeshare na wewe mtu wangu wa nguvu, unaweza kuitazama hapa.

Wednesday, October 22, 2014

EXCLUSIVE!!!:- SENTENSI 4 ZA MENEJA WA SUPER MEGA STAR DIAMOND PLATZNUMZ KUHUSU YALIYOJIRI JUMAMOSI LEADERS CLUB AT FIESTA!!

 
 
Hizi ni sentensi 4 alizozisema.
 
1.Sisi tumechukulia sehemu ya mashindano,uzuri sisi tuliambiwa na uongozi wa Clouds kabla ya Diamond hajapanda ilikua saa 3 kamili tukaitwa tukaambiwa kuna watu wamejiandaa kumzomea Diamond.
 
2.Kama uongozi tulikaa na msanii wetu na kumjenga kisaikolojia na kumwambia kuna hivi vinatokea wao walitaka aanze Davido kisha afate Diamond kupunguza watu watakaozomea tukasema hapana pangeni show yenu kama ilivyokuwa ni sehemu ya mashabiki kufurahi.
 
3.Hatujaathirika kwamba msanii wetu ameshuka tunapoona watu wanapiga kelele kwa ajili yako au huna sifa ile unatakiwa uangalie umekosea wapi unaenda wapi,hatuna makosa kwa mashabiki wetu.
 

4.Kikubwa Diamond anafanya vizuri tunatakiwa kuhamisha macho yetu tumpigie kura Diamond kwenye tuzo za Channel O Music Awards, kwa sababu mwisho wa siku chema chajiuza kibaya chajitembeza

Tuesday, October 21, 2014

T.I AWATUKANA WAMAREKANI WANAOMWAMBIA TOUR YAKE TANZANIA ( AFRICA) ITAPELEKA EBOLA MAREKANI. TAZAMA ALIVYOMTUKANA HUYU.

Mfalme wa Kusini, T.I. amemind. Tangia weekend iliyoishia alipokuwa akipost picha za ujio wake nchini Tanzania, baadhi ya followers wake wajinga wa Marekani wamekuwa wakimkejeli kuwa anaweza kurudi Marekani akiwa ameambukizwa ugonjwa wa Ebola.

T.I
T.I. akitumbuiza kwenye Fiesta, Dar es Salaam
Katika kuthibitisha kuwa amekuwa akisoma comments zao, T.I. ameonekana kutofurahishwa na kauli hizo za kipuuzi na ameamua kumtolea uvivu mmoja wao aliyemtelea habari hizo za Ebola.
B0VimJYIEAAzAn3

Monday, October 20, 2014

FIESTA 2014: KAMA NOMA NA IWE NOMA!

Kama noma na iwe noma! Tamasha la Serengeti Fiesta 2014, wikiendi iliyopita lilifunga mitaa ya Jiji la Dar na viunga vyake ambapo burudani ya kufa mtu ilidondoshwa kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar na kugubikwa na matukio kibao nyuma ya pazia, likiwemo la msanii kutoka Nigeria, Davido ‘kupafomu’ pamoja na serikali kumkataza, Ijumaa Wikienda lina ripoti kamili.
Nyomi ya watu ikiwa imefurika Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar kumshuhudia T.I katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2014
SHUGHULI YAANZA
Shughuli ilianza kwa madansa ‘kusheki’ ambapo Kundi la Makomando ndilo lililoanzisha makamuzi na kupokea shangwe kubwa.
Baada ya Makomando, Wanaume TMK wakiongozwa na Chegge na Temba ndiyo waliofuatia, wakapiga shoo hevi na kupokea shangwe kubwa.
Msanii kutoka Nigeria, David Adedeji Adeleke 'Davido' akitoa burudani kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 ndani ya Ledears Club.
Madee na Dogo Janja walipafomu pamoja baada ya kitambo kirefu tangu walipogombana,
Vanessa Mdee akafuatia na kunogesha na madansa wake kwa zogoazogoa, akaja Ommy Dimpoz ambaye naye alikamua kisawasawa bonge la shoo.
Msanii wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz akitumbuiza kwa staili yake kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2014 Dar Leaders.
SAPRAIZI YA DIMPOZ
Kwa mara ya kwanza, Ommy Dimpoz alitambulisha remix ya wimbo wake wa Tupogo kwa mahadhi ya mnanda au mchiriku ambapo yeye na madansa wake waliserebuka kinoma wakishirikiana na Msaga Sumu.
Msanii wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee akifana yake na Ommy Dimpoz.
YOUNG KILLER, BANANA ZORRO NAO JUKWAANI
Baada ya hapo, mtu mzima Banana Zorro alivamia jukwaa akiwa na Young Killer na Umebadilika ambapo nao walipokelewa vizuri na nyomi iliyokuwa imefunga uwanjani kabla ya Young Killer kubaki mwenyewe na kukisanua ileile.
Msanii Waje kutoka Nigeria akitoa shoo.
MSANII KUTOKA DUBAI MH!
Msanii wa kwanza mgeni kupanda stejini alikuwa Ash Hamman kutoka Dubai ambaye ngoma zake hazikuwa zikijulikana kiivyo.
ZAMU YA WAJE KUTOKA NIGERIA
Msanii wa pili mgeni alikuwa ni Waje kutoka Nigeria ambaye alianza kwa kufundishwa kutamka maneno ya Kiswahili yakiwemo ‘nipeleke nyumbani’ ambaye kimavazi aliacha maswali kwa kuvaa kisweta cha aina.
Msanii huyo alimpagawisha Madam Rita na kujikuta akishindwa kujizuia, akaserebuka na kinywaji chake mkononi.
Msanii kutoka, Kenya Victoria Kimani akipagawisha mashabiki jukwaani.
VICTORIA KIMANI
Msanii wa tatu kutoka nje alikuwa ni Victoria Kimani wa Kenya ambaye aligonga ngoma zake mbili lakini kilichoonekana ni kwamba zilikuwa hazijulikani na wengi pamoja na kwamba alipata shangwe kimtindo.
Mwingine wa kimataifa alikuwa ni Bob Man wa Nigeria ambaye alipagawisha kwa reggae baada ya kupiga akapela ya Wimbo wa One Love wa Bob Marley huku akichombeza na maneno ya Kiswahili kama ‘mambo vipi’ na ‘nakupenda’. Alipojaribu kuwasifia warembo wa Kibongo, masela wakamaindi kidizaini fulani.
Bob Man aliendelea kufanya yake akisaidiwa na Victoria Kimani, wakakamua Prokoto ambapo Dimpoz aliungana nao, shangwe zikazidi kupamba moto.
Burudani ilizidi kukolea, akapanda mtangazaji na msanii wa Bongo Fleva, Adam Mchomvu ambaye alikamua kwa sana.
Msanii zao la THT, Rachel akikamua stejini na mashabiki zake
RACHEL, WACHEZA SHOO WAKE WAVAMIA JUKWAA
Msanii zao la THT, Rachel naye alipanda jukwaani na mashabiki wake sita waliokuwa wamevalia nguo zinazofanana, wakakamua ngoma yake ya Nashukuru Umerudi, na nyingine kibao lakini mashabiki walipooza kimtindo kwani nyimbo zake zilikuwa na mzuka wa chini, ikafuatia ngoma nyingine ya Umependeza, mashabiki kwa mbali wakaanza kuamka.
Recho akitumbuiza katika Tamasha la Fiesta.
BARNABA NA SHAA NAO WAPANDA JUKWAANI
Msanii mwingine, Barnaba Elias ‘Barnaba Boy’ naye alifuatia na ngoma yake mpya ya Wahalade, nyomi ikaamka na shangwe zikaanza kuonekana kutoka kila upande, akafuatia Shaa ambaye alitoa kali baada ya kutaka aitwe Mrs MJ (Master Jay).
Msanii Shaa akiendelea na makamuzi ndani ya Viwanja vya Leaders Kinondoni.
Ikafuatia burudani ya nguvu kutoka kwake ambapo alikamua Wimbo wa Lover Lover, ukaamsha popo, ukafuatia Promise, mashabiki wakazidi kuchangamka huku wacheza shoo wa msanii huyo nao wakizikonga nyoyo za mashabiki.Akaendeleza makamuzi, akafanya Remix ya Hoi iliyowakumbusha watu mbali, akamalizia na Sugua Gaga iliyobamba vibaya.
Msanii wa Bongo Fleva, Linah Sanga akilishambulia jukwaa.
NYANDU TOZ, BLU NOMA SANA
Msanii Nyandu Toz naye alifuatia jukwaani akipigwa tafu na Blu na memba wengine wa Micharazo, wakapata shangwe ya kufa mtu. Blu akabaki peke yake jukwaani, akakamua kinoma. Baada yake, walipanda jukwaani Yamoto Band, watu wakachangamkia makamuzi yao ile mbaya.
Msanii wa kitambo Mwana FA akikamua ngoma zake kali stejini.
MWANA FA ADHIHIRISHA UKONGWE WAKE
Mwana FA naye alipanda kwa staili ya kipekee, ngoma zake mpya na za kitambo zikawabamba mashabiki ile mbaya.
Mtangazaji Godwin Gondwe aliushtua umati uliokuwepo uwanjani hapo ambapo alisikika akitangaza taarifa ya habari ya dharura (breaking news), watu wakakaa mkao wa kusikia kilichojiri, kumbe anampandisha Stamina, akakamua kinoma na kupishana na Nay.
Staa wa Bongo Fleva, Emanuel Elibariki 'Nay wa Mitego' akitumbuiza katika Tamasha la Fiesta.
DIAMOND, ALI KIBA KAMA SIMBA NA YANGA
Muda uliwadia ambapo watangazaji mayanki wa Clouds FM, Hamis Mandi ‘B12’ na Dj Fetty walipanda jukwaani na kuanza kuwauliza mashabiki nani mkali kati ya Diamond na Ali Kiba, watu wote wakajibu: Kibaa! Kibaa!
Mkali wa ngoma ya Mwana, Ali Kiba na Mdogo wake Abdu Kiba wakikonga nyoyo za mashabiki stejini.
Wakauliza tena nani mkali kati ya Simba na Yanga, kila mmoja akatoa jibu lake.
ALI KIBA KWA STEJI
Mkali wa ngoma ya Mwana, Ali Kiba alipanda jukwaani, akapokelewa na shangwe la kufa mtu ambapo kwa upande wa mastaa, Rose Ndauka, Dida, Jack Pentzel na mumewe walimshangilia Ali Kiba kinoma, Halima Kimwana na Aunt Ezekiel wao walikuwa tofauti kabisa na Ali Kiba, walikuwa wakimsubiri Diamond.
Ali Kiba alifanya makubwa jukwaani, katikati kiliingia kibwagizo ambapo kiti cha kifalme kilifutwa vumbi, Ali Kiba akakikalia na kuvalishwa taji la ufalme, maneno ya The Return of The King yakakisindikiza kibwagizo hicho, ikafuatia ngoma ya Mwana iliyomaliza ubishi, mpaka anashuka jukwaani, bado mashabiki walionekana kuwa na kiu kubwa.
Kundi la weusi likiwakilisha.
LINAH, WEUSI NI SHEEDAH!
Baada ya hapo, msanii zao la nyumba ya vipaji Tanzania, Esterlina Sanga ‘Linah’ aliyekuwa ametinga kivazi ‘chenye hoja’ alipanda jukwaani, akafunika mbaya na ngoma zake kali ikiwemo Ole Themba, wacheza shoo wake kibao wakakamua ile mbaya kitamaduni na kuchangamsha shoo nzima. Walifuatia Weusi waliopanda na sapraizi ya kupanda jukwaani kwa msanii Lord Eyez, makamuzi ya kigumu yakaendelea ambapo wakali kibao wakiongozwa na Joh Makini walifanya yao, uwanja wote ukalipuka kwa shangwe ya nguvu kwa muda mrefu.
Diamond Platinumz na Davido wakionyesha umahiri jukwaani.
DIAMOND AAAH WAPI!
Ilifuatia zamu ya mkali wa ngoma ya Mdogomdogo, Diamond Platinumz ambapo mashabiki wake walitangulia, akafuatia Diamond ambapo aliimba Remix ya Uswazi Take Away na Chegge, kombati zikazagaa jukwaani hata alipopanda Nay wa Mitego kumsindikiza kwenye ngoma ya Muziki Gani. Hata hivyo, shangwe hazikuwa kiivyo kama kwa Ali Kiba, akaendelea kukamua ngoma kibao lakini cha ajabu wakati akiendelea na shoo, zilianza kusikika kelele za kumtaja Ali Kiba, mpaka mchizi anamaliza, zomeazomea zilikuwa zikisikika chini kwa chini.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma 'Diamond' akikamua jukwaani.
DAVIDO KAMA NONA NA IWE NOMA!
Licha ya mahakama kumzuia Davido kufanya shoo kutokana na matatizo ya kimkataba, waandaaji wa shoo hiyo, Clouds Media Group walimpandisha kuashiria kama noma na iwe noma na kuifanya serikali iduwae, harufu ya vita kati ya waandaaji na serikali ikaanza kunukia. Jina la Davido lilipotangazwa, tofauti na wasanii wengine, ilimchukua zaidi ya dakika nne kupanda jukwaani, akaibuka na kuanza makamuzi.
Hata hivyo, bado hakupata shangwe za nguvu kama ilivyotegemewa, akaimba nyimbo ambazo hazijulikani na wengi.
Mkali T.I, rapa kutoka nchini Marekani akifunga Shoo kwa makamuzi makali hadi naiti kali.
'Hata alipopanda Diamond kukamua naye Number One Remix, mambo yalikuwa ni yaleyale, hakukuwa na shangwe kama ilivyotegemewa. Kwa mbali watu walionekana kuamka alipokamua Skelewu na kumalizia na Aye.
Rapa kutoka nchini Marekani, Clifford Harris,'T.I' akitoa burudani kwenye tamasha la Fiesta Leaders Club jijini Dar .
T.I JUKWAANI
Mkali T.I, rapa kutoka nchini Marekani aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu, alidondoka jukwaani na kukamua ngoma zake kibao pamoja na zile alizoshirikishwa, amshaamsha zikatawala mwanzo mwisho na kuhitimisha msimu wa burudani wa Serengeti Fiesta 2014. Ilikuwa ni sheeeda!