Showing posts with label VITUKO. Show all posts
Showing posts with label VITUKO. Show all posts

Tuesday, April 5, 2016

Huyu Ndo Mkuu Wa Wilaya Anaye Ongoza Kupiga Picha Za Vituko...Zitazame Hapa

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesera, amesema zamani kabla maisha yake kuwa mazuri alishawahi kubeba mizigo (kuli) Bandarini.
Richard amewashangaa watu wanaodhania yeye anaigiza baadhi ya vitu anavyofanya, wakati ni vitu ambavyo amevipitia katika maisha yake na ni kawaida.
“Wanasema anapenda kubeba watoto, ndio kwa sababu napenda watoto, wanasema anapenda kubebe mizigo, jamani mimi hapo kabla mambo hayajawa mazuri nilikuwa kuli wa mizigo Bandarini” alisema Kasesera
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhZG-yn0-Db-ZB4ZDUV1SCFb8cj1OY_e_GR0MpVam1yi0rD-ysqagpNM1BnCBbGeINSW4zajECTqbWCemQ_9eSGgwhHPyCkC4aNaMABGJw6f-JY069bCAUT0ERM_BSlWDXDjXgaqHQJLh4/s640/12735588_1225317000829026_1997684427_n.jpghttp://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2015/12/S3.jpghttps://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh6XL6-T3BVjlKuH_Widp_1DGdHk1FaVgLFZpAocwRy3iEBeVWQXp8XDk7etmbr6RB56V0UxPBog7eif1eP3Weo7jf-sw-Ung_iLW0jl0xahkyShmaJsvs7_vfF4LuA4-bCk2Dtt2uC6WM/s1600/12714299_1225322964161763_558045385_n.jpghttps://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh-H1mnWvFZarimsyZGnBG3UBfTQ2qwUO0GMe1CtJ6M-qDwjBOUcEE4HBKz7dtF6A-FWgI1dYV0TGMi2O_Q090CA4mILd7d3rVBDRPS4dHbMrNUNlE9O-5trbU9asUjBzXSDUq6-1vL8827/s1600/IMG_6079.JPGhttp://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2015/12/S51.jpghttps://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiuMHtVDzH9F_d-SmUTFyVBitrVk3Po2DdwLgJU7cPOvplJgzuvyEdSpcU8CitJpw0T8Wi_8NeNzRsJqW4VkrPv1EYClbBqpzvKNfqzfKQ9Kj9Zf_t4krNWuORNEdTS6JT4dEFHtbJBJnmm/s640/IMG_4991.JPGhttps://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjIjItPc-gkAb-HOXV6W3pzQPsGMXbSGz12M7aqwiRWhluWEsfevsxD7qZ90SGrSvb8gBV5MjbHnHpxVRLpspQPOny_Ld1RpxTRgABIDEbOPw0s37bgWINuR_48q_3T3_vHPex6dYEjziQ8/s1600/IMG_5051.JPGhttps://njiakwelinauzima.files.wordpress.com/2015/04/dscn0961.jpghttps://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhLgXVe-nA7WWnZjORyBBFI85wwIwOq98UEn5qtcbhS4wWV0XGA66XTZwENdoNE24i2CzO2wU4hg1by7RpUwlr6KyKXOAQS42zKaASzWo9X8EO9eYbLjPgX-6IirytMQWNoIJ1Tq3qn9YoM/s640/blogger-image-1432879812.jpg

Saturday, April 2, 2016

Picha Za Mkuu Wa Wilaya Ya Iringa Mijini DC Richard Kasesela Zilivyozua Gumzo Mitandaoni


Kwa siku kadhaa sasa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini mkoani Iringa, Richard Kasesela amezua gumzo katika mitandao mbalimbali ya jamii huku wanaomjadili wakiwa na mitizamo tofauti.
Mjadala huo unatokana na picha mbalimbali za kiongozi huyo, zilizotupiwa mtandaoni zikimuonyesha akiwa katika matukio mbalimbali.
Kasesela ni kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM)na amewahi kuwania kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya ubunge mkoani Mbeya, lakini aliishia ngazi ya kura ya maoni huku kumbukumbu zikionyesha alishiriki hatua hiyo mwaka 2010 na 2015
Baadhi ya picha hizo, zinamuonyesha Kasesela akiwa katika kazi mbalimbali za jamii, michezo, maisha ya kawaida na mambo yanayohusisha silaha.
Baadhi ya watu wanahoji iwapo matendo hayo ni wito au kumfurahisha mteuzi wake? Kasesela aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya Oktoba 2015, uteuzi uliofanywa na Rais wa wakati huo, Jakaya Kikwete.

Friday, April 1, 2016

Hizi Katuni Zimetikisa Sanaa!!Kwa Katuni Zaidi Bofya Hapa




Video Ya Wabunge Saba Wakitolewa Nje Ya Bunge La Kenya Baada Ya Kupiga Filimbi Rais Uhuru Akihutubia

Nchini Kenya ni Wabunge wa Upinzani kupiga filimbi sekunde chache tu baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuanza kulihutubia bunge la nchi hiyo ambapo KTN wamesema hizo filimbi zilisababisha hotuba ya rais ichelewe kusomwa kwa zaidi ya dakika 30.

kitendo cha Wabunge wa upinzani kukosa nidhamu hii kulimfanya spika wa bunge la Kenya Justin Muturi kuamuru kutolewa nje ya bunge kwa Wabunge saba ambao walitolewa na askari wa bunge kwa mabavu.. 

Tazama hizi video..

Saturday, December 26, 2015

TRA watikisa utajiri wa Dk.Fadhili

DOKTA-FADHILI-AMZAWADIA-ZARI-BAISKELI.jpgDk. Fadhili Emily.
Mwandishi wetu
KASI ya Rais Dk. John Pombe Magufuli inatikisa kila kona. Baada ya mtabibu Dk. Juma Mwaka ‘JJ Mwaka’ kuibukiwa hospitalini kwake na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hamis Kigwangalla wiki iliyopita na kuagizwa uchunguzi wa uhalali wa huduma zake, hali imekuwa tete kwa mtatibu mwingine, Dk. Fadhili Emily anayemiki kliniki ijulikanayo kama The Fadhaget Sanitarium iliyopo Afrikana Mbezi Beach jijini Dar.
dk fadhili (9)Imeelezwa kuwa, Dk. Fadhili ametikiswa na kasi hiyo kutokana na utajiri wake hali ambayo imesababisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutilia shaka uhalali wa utajiri alionao kwa kulinganisha na kipato chake.
dk fadhili (8)CHANZO CHAANIKA MAMBO
Chanzo makini kimeweka wazi kuwa Dk. Fadhili amepata taarifa kuwa tumbuatumbua ya Magufuli itamfikia, kwani tayari TRA wameshamweka kwenye ‘tageti’ zao na muda wowote watamkagua ili kujiridhisha kama mali alizonazo anamiliki kihalali na kama analipa kodi stahiki.
“Dokta ameshapewa hizo taarifa. Lazima atakuwa tumbo joto, maana si unajua kila mtu anatilia shaka ule utajiri wake, haufanani hata kidogo na umri wake.
dk fadhili (3)MALI ANAZOMILIKI
“Daah! Jamaa ni noma. Ana nyumba za ghorofa zaidi ya tatu Mbezi Beach halafu zote za gharama. Ana magari ya kutembelea matatu yote ya gharama; Toyota MRS, Toyota Land Cruiser V8 na Toyota Celca.
“Katika hiyo mijengo mitatu, moja anaishi yeye, lingine amepanga kuweka TV yake maana anataka kufungua kituo cha runinga na nyingine wanakaa wafanyakazi wake na tena ana vitu vingi tu ambavyo anavifanya siri,” kilisema chanzo hicho.
dk fadhili (5)TRA WAMEMFIKIA?
Jitihada za kumpata Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata ziligonga mwamba lakini hata hivyo alipatikana mmoja wa maofisa wa mamlaka hiyo ambaye aliomba jina lake lisichorwe gazetini, kwa kuwa si msemaji ambapo alisema wao kama mamlaka, wamedhamiria kukusanya kodi kadiri iwezekanavyo hivyo kama Dk. Fadhili naye amekwepa, watamfikia.
“Tumedhamiria kwa dhati kwenda na kasi ya Dk. John Pombe Magufuli rais wetu. Hakuna atakayekwepa kodi halafu tusimfikie. Niwasihi wote ambao wamekuwa wakikwepa kodi, walipe mapema kabla hatujawafikia,” alisema afisa huyo.
dk fadhili (2)DK ASAKWA
Gazeti hili lilimtafuta Dk. Fadhili kwa njia ya simu, alipopatikana na kusomewa madai hayo ya utajiri wake kutiliwa shaka, alisema hata yeye amesikia kuwa TRA pamoja na mamlaka nyingine zinamchunguza ili ikibainika amefanya ubabaishaji sehemu wamtumbue.
“Ninazo hizo taarifa lakini labda tu nikwambie, mimi sina kitu hata kimoja cha magumashi. Nimeanza kutoa huduma ya kitabibu kwa miaka mingi iliyopita kuliko hata hao madokta maarufu mnaowasikia wakijitangaza.
dk-fadhili-(1)“Nimejenga nyumba zangu nyingi tu Mbezi tangu miaka hiyo. Nalipa kodi kadiri inavyohitajika. Nawasubiri hao TRA. Magari yangu yote nalipa kodi kama kawaida. Mimi siyo mbabaishaji. Hii kazi nimeisomea, nina vyeti.
“Mimi simkimbii mtu katika hospitali kama wao. Nipo muda wote, nikitoka labda liwe ni suala la kazi maana nina matawi mengi mikoani huwa naenda pia kutoa huduma,” alisema Dk. Fadhili.

Thursday, November 26, 2015

Monday, September 28, 2015