Saturday, April 2, 2016

Picha Za Mkuu Wa Wilaya Ya Iringa Mijini DC Richard Kasesela Zilivyozua Gumzo Mitandaoni


Kwa siku kadhaa sasa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini mkoani Iringa, Richard Kasesela amezua gumzo katika mitandao mbalimbali ya jamii huku wanaomjadili wakiwa na mitizamo tofauti.
Mjadala huo unatokana na picha mbalimbali za kiongozi huyo, zilizotupiwa mtandaoni zikimuonyesha akiwa katika matukio mbalimbali.
Kasesela ni kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM)na amewahi kuwania kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya ubunge mkoani Mbeya, lakini aliishia ngazi ya kura ya maoni huku kumbukumbu zikionyesha alishiriki hatua hiyo mwaka 2010 na 2015
Baadhi ya picha hizo, zinamuonyesha Kasesela akiwa katika kazi mbalimbali za jamii, michezo, maisha ya kawaida na mambo yanayohusisha silaha.
Baadhi ya watu wanahoji iwapo matendo hayo ni wito au kumfurahisha mteuzi wake? Kasesela aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya Oktoba 2015, uteuzi uliofanywa na Rais wa wakati huo, Jakaya Kikwete.