Saturday, December 26, 2015

TRA watikisa utajiri wa Dk.Fadhili

DOKTA-FADHILI-AMZAWADIA-ZARI-BAISKELI.jpgDk. Fadhili Emily.
Mwandishi wetu
KASI ya Rais Dk. John Pombe Magufuli inatikisa kila kona. Baada ya mtabibu Dk. Juma Mwaka ‘JJ Mwaka’ kuibukiwa hospitalini kwake na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hamis Kigwangalla wiki iliyopita na kuagizwa uchunguzi wa uhalali wa huduma zake, hali imekuwa tete kwa mtatibu mwingine, Dk. Fadhili Emily anayemiki kliniki ijulikanayo kama The Fadhaget Sanitarium iliyopo Afrikana Mbezi Beach jijini Dar.
dk fadhili (9)Imeelezwa kuwa, Dk. Fadhili ametikiswa na kasi hiyo kutokana na utajiri wake hali ambayo imesababisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutilia shaka uhalali wa utajiri alionao kwa kulinganisha na kipato chake.
dk fadhili (8)CHANZO CHAANIKA MAMBO
Chanzo makini kimeweka wazi kuwa Dk. Fadhili amepata taarifa kuwa tumbuatumbua ya Magufuli itamfikia, kwani tayari TRA wameshamweka kwenye ‘tageti’ zao na muda wowote watamkagua ili kujiridhisha kama mali alizonazo anamiliki kihalali na kama analipa kodi stahiki.
“Dokta ameshapewa hizo taarifa. Lazima atakuwa tumbo joto, maana si unajua kila mtu anatilia shaka ule utajiri wake, haufanani hata kidogo na umri wake.
dk fadhili (3)MALI ANAZOMILIKI
“Daah! Jamaa ni noma. Ana nyumba za ghorofa zaidi ya tatu Mbezi Beach halafu zote za gharama. Ana magari ya kutembelea matatu yote ya gharama; Toyota MRS, Toyota Land Cruiser V8 na Toyota Celca.
“Katika hiyo mijengo mitatu, moja anaishi yeye, lingine amepanga kuweka TV yake maana anataka kufungua kituo cha runinga na nyingine wanakaa wafanyakazi wake na tena ana vitu vingi tu ambavyo anavifanya siri,” kilisema chanzo hicho.
dk fadhili (5)TRA WAMEMFIKIA?
Jitihada za kumpata Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata ziligonga mwamba lakini hata hivyo alipatikana mmoja wa maofisa wa mamlaka hiyo ambaye aliomba jina lake lisichorwe gazetini, kwa kuwa si msemaji ambapo alisema wao kama mamlaka, wamedhamiria kukusanya kodi kadiri iwezekanavyo hivyo kama Dk. Fadhili naye amekwepa, watamfikia.
“Tumedhamiria kwa dhati kwenda na kasi ya Dk. John Pombe Magufuli rais wetu. Hakuna atakayekwepa kodi halafu tusimfikie. Niwasihi wote ambao wamekuwa wakikwepa kodi, walipe mapema kabla hatujawafikia,” alisema afisa huyo.
dk fadhili (2)DK ASAKWA
Gazeti hili lilimtafuta Dk. Fadhili kwa njia ya simu, alipopatikana na kusomewa madai hayo ya utajiri wake kutiliwa shaka, alisema hata yeye amesikia kuwa TRA pamoja na mamlaka nyingine zinamchunguza ili ikibainika amefanya ubabaishaji sehemu wamtumbue.
“Ninazo hizo taarifa lakini labda tu nikwambie, mimi sina kitu hata kimoja cha magumashi. Nimeanza kutoa huduma ya kitabibu kwa miaka mingi iliyopita kuliko hata hao madokta maarufu mnaowasikia wakijitangaza.
dk-fadhili-(1)“Nimejenga nyumba zangu nyingi tu Mbezi tangu miaka hiyo. Nalipa kodi kadiri inavyohitajika. Nawasubiri hao TRA. Magari yangu yote nalipa kodi kama kawaida. Mimi siyo mbabaishaji. Hii kazi nimeisomea, nina vyeti.
“Mimi simkimbii mtu katika hospitali kama wao. Nipo muda wote, nikitoka labda liwe ni suala la kazi maana nina matawi mengi mikoani huwa naenda pia kutoa huduma,” alisema Dk. Fadhili.