Saturday, December 26, 2015

Mbunge ampa Wema ujauzito

wema3Mwigizaji Wema Sepetu ‘Madam’.
Mwandishi wetu
MJINI bwana! Habari nyingi huanzia kwenye mikeka, siku hizi wenyewe wamezimebatiza jina la ‘Ubuyu’ ambapo kwa sasa ishu kubwa inayozagaa mitaani ni mwigizaji Wema Sepetu ‘Madam’ kupachikwa mimba na mbunge maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Bunge la 11 (jina kapuni kwa sasa), vyanzo vinasema.
Pitapita ya sikio la Gazeti la Ijumaa katika Jiji la Dar es Salaam, hivi karibuni ilikutana na Ubuyu huo kuwa mwigizaji huyo amenasa ujauzito wa mwanasiasa huyo ambaye ni kijana mwenye utajiri mkubwa anayetajwa kwa sasa kumiliki vilivyo penzi la Madam.
10954224_1534823986770647_1165745805_nKUMBUKUMBU KABLA YA HABARI
Kwa muda mrefu, Wema amekuwa akihaha kusaka mtoto baada ya kupitia kwenye uhusiano na wanaume tofauti akiwemo Yusuph Jumbe, Steven Kanumba (marehemu), Nasibu Abdul ‘Diamond’ na CK (yule kigogo).
Akiwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanaume hao kwa hesabu yake na nyakati tofauti, mara kadhaa msanii huyo maarufu amekuwa akikebehemiwa na mahasimu wake kuwa ni mgumba jambo ambalo limekuwa likimhuzunisha.
HABARI KAMILI
Ijumaa baada ya kuzinasa habari za ujauzito wa msanii huyo, lilijongea kwenye vyanzo vyake na kukutana na ushuhuda huu kutoka kwa rafiki wa karibu wa Wema ukisema: “Suala la mimba sijui lakini Wema na mheshimiwa wana uhusiano.
“Ukaribu wao ulianza wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu (Wema alikuwa akimnadi mgombea urais wa CCM, John Magufuli), mpaka leo wanaendelea.”
MIMBA KABAAH!
Baada ya chanzo cha karibu na Wema kutoboa mfereji wa uhusiano na kuliacha suala la ujauzito kwenye sintofahamu, wachapakazi wa Ijumaa waligeuza masikio yao upande wa mheshimiwa mbunge ili kupata ubuyu mwingine ambapo suala la mimba lilitajwa waziwazi.
“Sitaki kunukuliwa ila mimi nimemsikia mheshimiwa akidokeza kuwa Wema ni mjamzito, kwangu mimi kama rafiki yake naona ni jambo jema, hiyo ndiyo kazi ya mwanaume kaka…hahahahaha!” Mmoja kati ya marafiki wa mbunge huyo alisema na kumalizia kwa kicheko.
WEMA NA MBUNGE FULL KICHEKO
Inaelezwa na vyanzo vyetu kuwa baada Wema na mbunge huyo kuwa wazazi watarajiwa wote kwa pamoja wamekuwa na furaha ya aina yake huku kila mmoja akimsisitiza mwenzake kuwa makini ili upepo mbaya usipite kati yao.
Aidha, katika hali inayoashiria kuwepo kwa kitu cha tofauti kwa msanii huyo aliyepata kuwa Miss Tanzania 2006, hivi karibuni aliandika kwenye akaunti ya Instagram kuwa anayo sapraizi ya nguvu kwa mashabiki wake.
Baadhi ya wadau wa masuala ya burudani wamehusisha sapraizi aliyoitangaza Wema na habari za ujauzito wake unaotarajiwa kumaliza kejeli juu yake kuwa yeye ni sawa na mti usiozaa kwamba hauna thamani.
MBUNGE NI TAJIRI MKUBWA
Mbali na umaarufu wa mbunge huyo timu ya Ijumaa ilijiridhisha kuwa mwanasiasa huyo ni tajiri anayemiliki migodi ya madini na kufanya biashara mbalimbali zikiwemo za usafirishaji mizigo na abiria anazofanya kupitia magari yake.
Kutokana na utajiri huo, habari zinadai kuwa mbunge huyo ndiye anayempa jeuri ya fedha Wema ambayo inamfanya aishi maisha ya ‘nyodo’ kama wasemavyo watoto wa mjini.
WEMA, MBUNGE WATAFUTWA
Katika kukamilisha weledi wa habari, gazeti hili lilimtafuta mbunge huyo kwa njia ya simu ili azungumzie ishu hiyo lakini hakuweza kupatikana hewani jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa jina lake kuhifadhiwa.
Kwa upande wa Wema naye hakuweza kupatikana kwa namba zake za simu sambamba na ile ambayo chanzo chetu kilisema ni mpya jambo linaloifanya habari hii kuwa na mwendelezo baada ya kujiridhisha kwa kupata kauli za pande zote mbili.
AUNT ANENA
Kama haitoshi gazeti hili lilimtafuta shosti wake wa karibu na Wema, Aunt Ezekiel ili naye afunguke kidogo juu ya madai ya ujazito wa rafiki yake ambapo mahojiano yalikuwa hivi:
Ijumaa: Mambo anti’ake?
Aunt: Safi cha umbea wangu, nipe mpya.
Ijumaa: Naona shosti yako Wema karudi ili umpe mafunzo ya kulea mimba, mpe hongera zake, kushika mimba ya mbunge si jambo dogo.
Aunt: Kwani kakuambia yeye mwenyewe? Kwanza niko naye hapa, anasema simu zako amekuwa anaziona lakini hataki kupokea.
Baada ya mazungumzo hayo ilisikika sauti ya Wema ikisema: “Tena mwambie ni ya miezi 6, tatizo nini?”