Issa Mnally
AIBU ya mwaka! Mwalimu aliyefahamika kwa jina la Henry wa shule moja maarufu iliyopo Kimara jijini Dar, amenaswa na mkewe aitwaye Sesy akiwa na mke wa mtu chumbani, Ijumaa linakupa mchapo kamili.
AIBU ya mwaka! Mwalimu aliyefahamika kwa jina la Henry wa shule moja maarufu iliyopo Kimara jijini Dar, amenaswa na mkewe aitwaye Sesy akiwa na mke wa mtu chumbani, Ijumaa linakupa mchapo kamili.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni nyumbani kwa mwalimu huyo aishie Kimara-Temboni, majira ya saa sita usiku baada ya mkewe kutonywa na majirani kuwa mumewe alizama chumbani na mchepuko huo ambao nao una mume.
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio mke wa mwalimu huyo alikuwa Morogoro kusalimia wazazi wake kumbe mumewe alitumia mwanya huo kufanya yake katika chumba chao.
“Yaani mkewe ilikuwa kila akipiga simu kwa mumewe ili amtumie nauli arudi nyumbani mume huyo alikuwa akizungusha kumbe ndiyo alikuwa anataka uhuru zaidi kuendelea kufanya yake,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya majirani kuusoma mchezo na kukerwa na tabia ya mwalimu huyo kufanya kitendo hicho na mwanamke huyo, siku ya tukio walimpigia simu mke wa mwalimu na kumueleza kuwa mumewe alimuingiza mwanamke huyo nyumbani kwake.

Kama hiyo haitoshi, majirani hao wakawapigia simu Makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) wa Global Publisher’s ambao walitinga eneo la tukio mara moja.
Mke baada ya kupata taarifa hizo, alikodi pikipiki lakini kabla ya kufika nyumbani kwake, Kimara-Temboni alianzia katika kituo cha polisi ili kuomba ulinzi na kutoa taarifa kwa kile kilichoendelea nyumbani kwake.

OFM walipofika katika eneo la tukio, walishuhudia mke wa mwalimu huyo akiangusha varangati baada ya kukuta mchepuko ukiwa umejaa tele ndani na mumewe wakiashiria kama walikuwa wanataka kufanya kitu.
Hata hivyo, polisi waliingilia kati na kumkamata mwalimu huyo na mchepuko wake kisha kuwapeleka kituoni kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya maelewano kwa kuwa hakukuwa na kesi ya msingi ya kuwabana kwa usaliti huo.