Hayo ni maelezo aliyoyatoa Mr. Hasheem Lundenga mbele ya Waandishi wa habari Dar es salaam October 21 2014 kuhusu ishu ya Miss Tanzania ambae aliandikwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mrembo huyu kudanganya umri, elimu na mambo mengine.
‘Walidai kwamba Miss Tanzania ana mtoto baada ya kutoka picha moja akiwa na mtoto, nasema katika utafiti wetu sisi Miss Tanzania hana mtoto na mwenye vithibitisho halali kwamba ana mtoto atuletee, kama kuna uthibitisho wa cheti cha kuzaliwa cha mtoto….. leta hicho cheti’ – Lundenga
‘Hili la sisi kuchukua rushwa kutoka kwa baba wa Sitti, Abbas Mtemvu…. jamani hii ni stori ya kijingajinga, ni mambo ya kipumbavu sana kuandika haya mambo, hamjui taratibu zetu tunavyowapata majaji na wanavyofanya kazi…Majaji huwa wanatafutwa siku nne za mwisho na huwa hakuna mtu anajua atakua Jaji na huwa tupeleka majina 15 BASATA na wao ndio wanaturudishia majina tisa ya Majaji waliopitishwa’ – Lundenga
‘Kuhusu swala la yeye kuzungumza kifaransa, mtu anajua lugha ya kimataifa mbona kwenye mashindano ya dunia wanazungumza Kifaransa na lugha nyingine? lakini mbona hata kwenye fainali alijibu kwa Kiingereza pia? Kifaransa zilikua ni mbwembwe kuwashawishi Majaji, na kweli walishawishika na ndio maana akashinda’ – Lundenga
‘Wote walioshiriki Miss Tanzania 2014 akiwemo Sitti walituletea vyeti vyao Original vya kuzaliwa tarehe 13 na kisha tukatoa nakala kupitia hivyo vyeti vyao Original’ – Lundenga
‘Sisi kazi yetu sio kupeleleza sana, tukipata information chache zinatutosha… kama mtu anatatizo na hiki cheti cha Sitti cha kuzaliwa akafanye utafiti, ukipata ukweli tuletee sisi lakini kazi ya uchunguzi sio ya kwetu’ – Lundenga
Waandishi wa habari walipotaka awaambie na uthibitisho kama aliripoti Polisi kuhusu kupotea kwa cheti chake, Sitti alisema ‘sikutegemea haya maswali leo kwahiyo sikuja nimejiandaa kihivyo, kama mtakua mnahitaji kunihoji mnaweza kupanga siku yenu na mkanihoji’ – Sitti
Kuhusu ukweli kama hati ya kusafiria pamoja na leseni ya gari vilivyosambazwa mitandaoni ni kweli vikionyesha kwamba amezaliwa mwaka 1989, Sitti amesema ‘Sitogusia hilo swala sababu nilivyokua nakuja kuomba Miss Tanzania niliomba cheti cha kuzaliwa, hivyo vitu vingine ni maisha binafsi…. kwahiyo sidhani kama na nyie mngependa kuona mtu anachukua leseni ya gari au Passport iwe ya kweli ama feki na kuiweka kwenye mtandao’
Hayo ndio maelezo yaliyotolewa leo kwenye mkutano na Waandishi wa habari…. kama una comment yoyote iandike hapa chini na itatufikia.