Friday, September 19, 2014

ODAMA: NAANZAANZAJE KUMFICHA BWANA’NGU?


Mwanadada anayeuza nyago kwenye filamu za Kibongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amekanusha tuhuma ya kumficha mwandani wake na kufunguka kuwa, marafiki na familia yake wanamjua hivyo haoni sababu ya kumfanya kila mtu amjue.
Mwanadada anayeuza nyago kwenye filamu za Kibongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’
Odama alikuwa akizungumzia madai ya kumficha mwanaume aliyezaa naye huku baadhi wakisema, hataki mtu yeyote amjue kwani ni mume wa mtu.
“Hivi naanzaanzaje kumficha mwandani wangu? Halafu nimfiche ili iweje? Ndugu na marafiki zangu wanamjua, wasiomjua wawe na subira, kila jambo lina wakati wake,” alisema Odama ambaye juzikati alinaswa akiwa ‘very close’ ukumbini na mwanaume aliyefahamika kwa jina la Daudi ambaye ni mume wa mtu.