MVUA iliyoanza kunyesha usiku wa kuamkia leo imesababisha foleni ndefu katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam hasa katika eneo la Bamaga-Mwenge.
Mtandao huu umefanikiwa kunasa picha zinazoonyesha magari yakiwa katika foleni ndefu katika makutano ya barabara za Shekilango na Ali Hassan Mwinyi eneo la Bamaga.