Friday, June 26, 2015

LINAH Ajiweka kimaaba kwa kaka yake ZARI

Linah1
Staa wa Muziki wa kizazi kipya, Estelinah Sanga ‘Linah’ akiwa ameketi na William Bugeme ‘Boss Mtoto’ ambaye ni kaka wa Zarina Hassan ‘Zari’ kiukoo.

MREMBO anayefanya poa kunako Bongo Fleva, Estelinah Sanga ‘Linah’, anadaiwa ‘kujiegesha’ kimahaba kwa shemeji yake Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aitwaye William Bugeme ‘Boss Mtoto’ ambaye ni kaka wa Zarina Hassan ‘Zari’ kiukoo.IMG-20150602-WA0025Ndani ya Ukumbi wa Triple 7 uliyopo Kawe jijini Dar hivi karibuni, paparazi wetu aliwaona wakiingia sambamba na kukaa beneti kama mtu na mpenzi wake jambo lililozua maswali kibao kutoka kwa wateja waliokuwepo ukumbini hapo.
Linah1Linah na Boss Mtoto katika pozi la kimahaba.Mbali na kunaswa siku hiyo, pia paparazi wetu amekuwa akiwashuhudia mara kadhaa wawili hao wakiwa pamoja katika kumbi mbalimbali za starehe jijini Dar.
nnjMara ya mwisho, Linah na Boss Mtoto walikuwa pamoja kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo za Kili Music zilizofanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, mapema mwezi huu.
Ndani ya Triple 7, paparazi wetu aliamua kumfuata Linah ili ajiridhishe uwepo wake na mwanaume huyo ambapo msanii huyo alijing’atang’ata na kusema:
“Huyu ni mtu wangu huwa natoka naye. Sijui umenielewa? Natoka naye sehemu mbalimbali.Ila kukutoa wasiwasi tambua kwa sasa sina mpenzi na nina haki ya kuwa naye, sina mpaka wa kujiachia na Boss Mtoto,” alisema.