Thursday, January 1, 2015

UJAUZITO ALIONAO MBONI APATE NEEMA KWA KUHAMISHA KIPINDI KUTOKA EATV HADI TBC

Mkurugenzi wa The Mboni  Show, Mboni Masimba.
UJAUZITO alionao Mkurugenzi wa The Mboni  Show, Mboni Masimba umeonekana kumpa neema kwani amepata bahati ya kupata udhamini mkubwa wa kipindi chake kutoka kwa mfuko wa hifadhi ya jamii (PSPF) pamoja na kuhamishia kipindi chake TBC 1 ambacho kitarushwa rasmi kuanzia tarehe 2 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Habari Maelezo,  Mboni alitupiwa maswali na waandishi wa habari sababu ya yeye kuonekana amevimba, ambapo alibabaika kujibu moja kwa moja.
“Jamani hali niliyonayo ni ya kawaida ambayo mwanamke yeyote anaweza kuipata”, alisema Mboni
Hata hivyo wapo waliosema kuwa Mboni amepata neema baada ya kupata ujauzito.