Thursday, September 25, 2014

Picha: Filamu ya ‘Mbwa Mwitu’ ya Kajala yazinduliwa Mlimani City..!! FANYA KUONA TRELA HAPA NA PICHA ..!!!

Msanii wa filamu nchini, Kajala Masanja jana amefanikiwa kuzindua filamu yake mpya ‘Mbwa Mwitu’ ndani ya ukumbi wa sinema wa Mlimani City jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali wa filamu pamoja na wanamuziki.

Kajala akizungumza na waandishi wa habari
Kajala akizungumza na waandishi wa habari

Akizungumza na Bongo5 kwenye uzinduzi huo, Kajala amesema filamu hiyo ni maalum kwaajili ya kuelimisha jamii hasa hasa vijana kuacha kujiingiza katika makundi ya uhalifu.
“Serikali imefanya kazi kubwa sana kupambana na makundi mbalimbali ya uhalifu,” amesema Kajala. “Kuna makundi mengi ulikuwa unayasikia, sijui Dogo Dogo, Mbwa Mwitu na mengine mengi. Nikaona kumbe ninaweza kufanya kitu ili kuelimisha vijana kuhusu madhara ya kujihusisha na matukio ya uhalifu, ndo wazo la kufanya filamu ya Mbwa Mwitu.”
“Kwahiyo ni filamu fupi sana ambayo imetengenezwa na Kajala Entertainment kwaajili ya kuelimisha jamii. Ndani ndani ya filamu kuna matukio mbalimbali ya kinyama, kuna scene ambayo ilinipa shida sana kuifanya, inauma sana! Yaani mtoto wangu alikuwa anajihusisha na mAtukio kama hayo sasa ghafla akakamatwa na kuchomwa moto mbele yangu iliniuma sana,” aliongeza Kajala.

Kajala, Babu Tabe na Mkubwa Fela
Kajala, Babu Tabe na Mkubwa Fela

Pia Kajala alisema ili kuifanya filamu hiyo iwe nzuri aliwatafuta vijana ambao walihusika kwenye matukio mbalimbali ya uhalifu na kuzungumza nao. “Pia niliwatafuta vijana mbalimbali ambao niliambiwa walihusika na matukio mbalimbali ya uhalifu na kungumza nao. Wengi wanasema kutokana na walivyoponea chupuchupu kuuawa inabidi waachane na hiyo tabia kabisa. Mimi kama mimi nilijaribu kuwaelimisha na kuwaambia madhara mbambali yanayotokana na kuwa wahalifu.”
Hizi ni picha za uzinduzi huo.

Kajala akiwa kwenye ndinga yake
Kajala akiwa kwenye ndinga yake


Country Boy akiwa na Mubenga
Country Boy akiwa na Mubenga


H.Baba akiwa na mke wake Frora Mvungi
H.Baba akiwa na mke wake Flora Mvungi

Irene Paul kwa mbele kabisa akiwa na wadau mbalimbali wakifuatilia filamu
Irene Paul kwa mbele kabisa akiwa na wadau mbalimbali wakifuatilia filamu hiyo

Kajala akiwa na  Martin Kadinda, mwanae Paula pamoja na mtu wao wa karibu
Kajala akiwa na Martin Kadinda, mwanae Paula pamoja na mtu wao wa karibu

Kajala
Kajala


Keisha akiwa na Lamata
Keisha akiwa na Lamata


Msanii wa filamu Tausi (katikati) akiwa akiwa na wasanii wenzake
Msanii wa filamu Tausi (katikati) akiwa akiwa na wasanii wenzake

Wadau mbambali wakiangalia filamu mpya ya Kajala
Wadau mbambali wakiangalia filamu mpya ya Kajala


Baby Madaha
Baby Madaha


IMG_5728
Kajala akiwa na Odama


IMG_5724
Quick Rocka


Mtangazaji wa kipindi cha Take One ndani ya Clouds TV, Zamaradi Mtetemwa
Mtangazaji wa kipindi cha Take One ndani ya Clouds TV, Zamaradi Mketema



IMG_5705

IMG_5737
IMG_5738

IMG_5756