Halima mdee
Mbunge
wa Kawe jijini Dar es Salaam, Halima James Mdee, jana amezua mjadala bungeni
baada ya kuweka wazi kuwa anakerwa na kitendo kinachotajwa na baadhi ya Wabunge
kwamba Rais hatajwi wala haguswi na hoja.
Akichangia
Bungeni jana, Mdee alidai wakati Rais Magufuli alipokuwa waziri wa Ujenzi
walipanga kukarabati barabara ya kilometa 5004 lakini zikakarabatiwa 2700
pekee.
Wabunge
wa CCM walicharuka wakimtaka Halima, kutotumia wala kumtaja Rais kwa Dhihaka
kwa kuwa kanuni za Bunge haziruhusu.
“Kwa
mujibu wa kanuni ya 64 fasili ya kwanza, Mbunge hatotumia kwa dhihaka jina la
Rais katika mjadala, Mbunge anayeendelea anatumia jina la Rais kwa Dhihaka
naomba aendelee bila kumtaja” Alisikika Mbunge mmoja wa chama cha Mapinduzi.
Mbunge
huyo kijana wa CHADEMA, alijibu hoja hiyo kwa kusema jukumu la Bunge ni
kuirekebisha Serikali hivyo yuko sawa kumtaja.
“Nasema
hivi hii biashara ya kufanya rais ni mtu ambae hashikiki wala hatajwi wala
haguswi iachwe, kwa sababu jukumu la Bunge ni kuirekebisha na kushauri
Serikali” Alisema.