Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shehe Issa Ponda akizungumza na wanahabari.
KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
Tanzania, Shehe Issa Ponda amemkumbusha Rais Dk. John Pombe Magufuli
kusuluhisha mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar.
Ametoa kauli hiyo leo katika
Msikiti wa Kichangani jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari juu
ya namna Dk.Magufuli anavyoweza kutatua mgogoro huo ili kuzuia machafuko kwani
kuna viashiria vya machafuko kipindi hiki.
Ponda alisema Rais Magufuli anao
wajibu wa kutekeleza ahadi aliyoitoa wakati akihutubia Bunge kuwa ndio
suluhisho la mgogoro huo wa kisiasa pasipo kusababisha Zanzibar kuingia katika
dhiki na uhasama uliopitiliza.
Aidha, alisema msajili wa vyama
vya siasa nchini pia anaweza kuingilia kati mgogoro huo kwani anayo mamlaka ya
kuwakutanisha viongozi wa kisiasa wa pande mbili za CCM na Cuf kwa kukaa na
kutafuta suluhu ya mzozo huo.