Ni staa wa Bongo Fleva anayebamba na Ngoma ya Make Me Sing. Diamond
anashikilia usukani kati ya mastaa wa Bongo wenye mashabiki wengi ambao
ni zaidi ya milioni mbili (2,046,428).
Ni staa wa filamu Bongo. Wema Sepetu anashikilia nafasi ya pili akiwa na wafuasi zaidi ya milioni moja na nusu (1,594,606).
Ni mtangazaji maarufu nchini akimiliki pia studio yake binafsi ya kurushia matangazo. Millard ambaye amejizolea umaarufu kwenye mitandao na redio ana mashabiki zaidi ya milioni moja na nusu (1,577,345).
Mwanamitindo na Muigizaji, Jokate Mwegelo anasimama katika nafasiya nne akiwa na mashabiki
zaidi ya milioni moja na laki nne (1,497,197). Jokate
kwa sasa anamiliki lebo yake ya Kidoti inayojishusisha
na bidhaa za urembo.
Unaweza kumuita Wolper Gambe. Mwanadada huyu ambaye ni mkali katika
tasnia ya uigizaji Bongo, ana mashabiki zaidi ya milioni moja na laki nne
(1,476,933).
Vee Money kama anavyojulikana katika tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva, naye ni miongoni
mwa mastaa wenye mashabiki wengi akiwa na mashabiki zaidi ya milioni moja na laki nne (1,401,187).
Ni staa wa Muziki wa Bongo Fleva pamoja na filamu. Shilole ama
Shishi amejizolea umaarufu kwenye nyimbo kama Malele na Namchukua, ana
mashabiki wengi kwenye mitandao ambao ni zaidi ya milioni moja na laki tatu. (1,377,428)