Jengo likiporomoka
Tainan, Taiwan
TETEMEKO kubwa la ardhi limeikumba nchi ya Taiwan, na kuporomosha majengo kadhaa likiwemo jengo la ghorofa 17 ambapo hadi sasa watu watano akiwemo mtoto wa miaka 10, wamethibitishwa kufariki dunia.
Mtoto wa miaka mitano akiokolewa
Tetemeko hilo la kipimo cha Ritcher 6.4 limetokea usiku wa mananee karibu na mji wa Tainan, Kusini mwa nchi hiyo.
Watu zaidi ya 370 wamejeruhiwa kutokana na tetemeko hilo ambapo kikosi cha Uokojai chini humo kimefanya jitihada na kufanikiwa kuwaokoa zaidi ya watu 200 kutoka kwenye jengo hilo, huku ingawa waokoaji wangali wanajaribu kuwafikia watu wengine ambao inadhaniwa wangali wamekwama katika mabaki ya jengo hilo.
Waokoaji wakifanya jitihada za kuokoa walionasa kwenye jengo hilo.
Kumetokea matetemeko mengine madogo matano mda mfupi baada ya tetemeko hilo kuu.
Idara ya kusimamia maswala ya chini ya radhi inasema kuwa tetemeko hilo lilitokea sehemu ya juu pekee, hali ambayo husababisha madhara makubwa zaidi.
Taarifa zaidi tutaendelea ku-update
Ramani inayoonesha eneo la tukio huko Taiwani.Hali ilivyokuwa
Uokojai ukiendeleaMajengo yakiporomoka.
Uokojai ukiendeleaMajengo yakiporomoka.
PICHA NA DAILY MAIL