Tuesday, February 3, 2015

HATIMAYE JOTI WA ORIGINAL COMEDY AMVISHA PETE MCHUMBA WAAKE WA SIKU NYINGI

 
Kwa mujibu wa mtandao wa JF, Mwigizaji wa vichekesho Lucas Mhuvile, almaarufu kama Joti, anayepiga kazi kwenye kampuni ya Orijino Komedi, amemvisha pete mpenzi wake wa siku nyingi, ikiwa ni ishara na dalili njema kwamba safari ya kuelekea kwenye taasisi muhimu zaidi duniani ya NDOA imewadia.Akiwa na swahiba wake wa siku nyingi, Mr. Mjuni Sylvatory a.k.a Mpoki, Joti alionekana mwenye furaha muda wote kwa kutimiza tendo hilo huku akiwa amealika watu wachache sana kuhudhuria tukio hilo.

Paparazi bado haijazithibitisha taarifa hizi.
 Kama ni kweli, tunampongeza sana na kumtakia kila la kheri yeye pamoja na mwenza wake.