MBWA mwenye umri wa miaka saba anayeitwa Scooby ni miongoni mwa mbwa 35 maarufu wanaotumiwa na Jeshi la Ulinzi la Uingereza amenunuliwa vifaa malum vya kumkinga hasa awapo kazini.
Scoobyamenunuliwa miwani maalum ambayo itamsaidia kuzia vumbi kuingia machoni, viatu maalum kuzui miba na vitu vingine vinavoweza kumletea madhara awapo kazini pamoja headphone maalum kwa ajiri ya kunasa sauti mbalimbali zikiwemo za wahalifu na waongozaji wake.
Scooby ni miongoni mwa mbwa wakongwe kwenye kambi ya Jeshi ya Jeshi kikosi maalum cha mbwa (105 Military Working Dog Squadron). Amefanya kazi kwa miaka mitano tangu 2012 kwenye mapigano ya Afghanistan. Kazi yake kubwa ni ukaguzi wa mizigo, vyombo vya moto na kunusa ili kutambua kama kwenye kuna madawa ya kulevya.
Vifaa hivyo vitamsaidia wakati wa mafunzo maalum ya miezi mitatu nchini humo. “Mbwa huyo hang’ati hovyo. Amefundishwa vizuri na amezoea mazingira hasa ya kazi.” Alisema Steve Hood ambaye ni mkufunzi wa mbwa huyo.