Benard Paul ‘Ben Pol’ amesema hapendi na hatauchora ‘tattoo’ mwili wake kama baadhi ya wasanii na watu maarufu wafanyavyo kwa kuwa anauheshimu sana.
Ben Paul alisema imekuwa ni kawaida kwa idadi kubwa ya wasanii kujichora ‘tattoo’ na kuwa na mwonekano wa tofauti na watu wengine, lakini kwake jambo hilo halina nafasi.
“Japo ni msanii lakini sipendi kuwa na mwonekano wa tofauti kama kufuga rasta, kuvaa hereni au kujichora mwilini kwa sababu nauheshimu mwili wangu, ndiyo maana nipo kawaida kila wakati,” alifafanua.
Msanii huyo aliongozana na msanii mwenzake, Juma Musa ‘Jux’ walipotembelea ofisi za Kampuni ya New Habari (2006) Ltd kwa lengo la kutangaza wimbo wao mpya wa ‘Nakuchana’