Sunday, December 21, 2014

STEPS YASHUSHA BEI ZA FILAMU ZA KIBONGO SASA ZITAUZWA KWA 1500



Wasanii wa filamu pamoja na kampuni ya usambazaji wa filamu nchini ‘Steps Entertainment’ wameamua kushusha bei ya filamu hadi kufikia shilingi 1,500 kwa nakala moja ili kujaribu kupambana na waharamia wa kazi za wasanii.



Muigizaji Salma Jabu aka Nisha ambaye hufanya kazi na kampuni hiyo ameiambia Bongo5 kuwa imewabidi wafanye hivyo ili kuwawezesha watanzania wote kuwa na uwezo wa kupata kopi halisi za kuacha kununua feki.

“Kweli tumekaa na Steps, tunaona njia pekee ya kupambana na waharamia wa kazi zetu ni kupunguza bei ya filamu zetu,” amesema Nisha. “Kuanzia mwezi February 2015, filamu zitaanza kuuzwa kwa bei ya shilingi 1,500 za kitanzania badala ya 3,000 kama bei ya rejereja. Kwahiyo kama utakuwa unahitaji mbili ina maana utatoa shilingi 3,000. Tumeshuka ili kumshawishi mtanzania kuacha kununuA filamu za mitaani kwa bei ya 1,000, ni bora tupunguze hii filamu yetu orijino iliyokuwa inauzwa 3,000 tupunguze mpaka 1,500 ili aweze kuinunua,” ameongeza.

“Kwahiyo kama alikuwa anahitaji mbili, anatoa shilingi 3,000 badala ya 6,000 ambayo ilikuwa bei ya mwanzo. Kwahiyo sisi kama wasanii tumeona bora tuuze kwa bei hiyo tukiwa tuna imani tutauza filamu nyingi na tutakuwa tunapata faida.”



Pia Nisha amewataka watanzania kumuunga mkono kwa kununua filamu yake mpya, ‘Hakuna Matata’ inayotarajiwa kutoka December 22 mwaka huu.