WATU kadhaa wamejeruhiwa katika ajali iliyolihusisha Basi la Shalom Express lililokuwa likitokea Sumbawanga - Mbeya lililogonga Coaster iliyokuwa inatokea Mbeya- Tunduma eneo la Sogea, Tunduma jioni hii. Coster lilikuwa likijaribu ku-overtake lori ndipo lilipogongwa na basi hilo. Idadi kamili ya majeruhi wa ajali hiyo bado haijafahamika.