Imedaiwa kuwa rafiki wa Irene ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alizivujisha picha hizo baada ya kugombana na Irene.Imeelezwa kuwa, vijana hao ni watoto wa wafanyabiashara wakubwa hivyo kitendo cha kusambaa picha hizo kimewasononesha.
Mwanahabari wetu aliwatafuta wahusika hao kwa njia ya simu. Irene simu yake haikuwa hewani lakini Kaloli alipatikana na kufunguka:Mwandishi: Habari? Unazungumza na mwandishi wa Global Publishers, nazungumza na Kaloli?
Kaloli: Ndiyo mimi.
Kaloli: Mmezipataje hizo picha? Mwandishi: Picha zimetapakaa kwenye mitandao ya kijamii.
Kaloli: ‘Plizi’ naomba usitoe hiyo habari.
Mwanahabari wetu alikwenda mbali zaidi kwa kumtafuta mzazi wa Kaloli, Mzee Kaloli kumsikia anazungumziaje tukio hilo.“Ni kweli nimeziona hizo picha yaani ni aibu sana kwangu maana mimi ni mtu na heshima zangu na nimeshamkanya mara kadhaa mwanangu aachane na huyo Irene lakini hata hasikii.