TANZANIA, Taifa Stars imeanza vibaya mechi za Kundi G kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika baada ya kufungwa mabao 3-0 na Misri usiku huu mjini Alexandria.
Mabao yote ya Misri yalipatikana kipindi cha pili, wafungaji Rabia dakika ya 61, Morsi dakika ya 65 na Mohamed Salah dakika ya 70.