Msanii wa filamu aliyejizolea umaarufu miaka ya
hivi karibuni, Salim Ahmed maarufu kwa jina la
Gabo amesema haoni msanii anayempa
changamato.
Akizungumza kwenye kipindi cha Take One cha
Clouds TV, Gabo alisema wengi wamekuwa
wakimwambia anaringa kutokana na kuwaambia
ukweli.
“Kwa hapa Tanzania sijui ndio maana wanasema
mimi naringa,” alisema Gabo alipoulizwa ni msanii
gani anayempa changamoto.
“Nyuma alikuwa Single Mtambalike, sasa hivi
sijaona wa kumtazama na kunipa changamoto
tuweze kushirikiana kupeana nguvu. Kwa single
sijui nisene vitu vinakwenda vinaisha! Lakini
simuoni tena yule, sasa hivi amekuwa akifanya kazi
anakuwa ni yule yule, hakuna mabadiliko. Lakini
nikimwangalia yule single wa filamu za nyuma
nasemaga yule jamaa, amebadilika kabisa na kuwa
wa kawaida,” aliongeza.
Gabo amesema kuwa pamoja na filamu za
Tanzania kuwa na changamoto, amefanikiwa
kupata mafanikio mengi.
“Mimi kama ningekuwa nchi nyingine ningekuwa
mtu mkubwa sana,” alisema.
“Ukiangalia uwezo wangu mimi na jinsi ninavyoishi
havilingani. Nimekuwa nikitembelea nchi kama
Afrika Kusini na Jumatatu kama Mungu akipenda
naenda Botswana, watu wanakuona huyooo kumbe
maandazi tu hamna chochote! Kitu kikubwa
ambacho nilikuwa nakihitaji kwa sasa ni kampuni
yangu ya Sarafu Media, nilitamani iwe strong mtu
akija anaogopa, lakini sasa ipo kampuni jina, mtu
akija anaona huyu naye anaanza.
Kingine mimi nimejenga nje ya sanaa, hata kwangu
pale nikilala najiona bado. Ndioa maana
nikapangisha kule nikaja kukaa Kinondoni ili
nitafute kwa jasho la filamu. Mimi ninachojivunia
kwa sasa kilichopatikana kutokana na filamu ni
gari (Passo), ndio maana sasa hivi naboresha zaidi
kazi zangu hata mtu akinihitaji kufanya filamu yake
aandae milioni 8,” alisisitiza