Thursday, February 4, 2016

MWIGIZAJI BATULI AMJIBU RAY KIGOSI...AMTAKA APIGE PICHA MKATABA UNAOSEMA ALIPWE BAADA YA MWAKA MMOJA AUWEKE MTANDAONI


Bifu inayoendelea Kati ya Ray na Batuli yazidi Kupamba moto, Batuli amjibu Ray Kama Ifuatavyo;

Haki Ya Mtu Haizami
Swali: Movie Yako Nimecheza Mwaka Juzi Wiki Moja Kabla Ya Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani, Makubaliano Yetu Ya Kazi Kimkataba Ni Siku 10 Tu Lkn Ulienda Kinyume Na Matokeo Yake Nilifanya Kazi Yako Mwezi Mzima Wa Ramadhan Je Ulikuwa Sawa!?
Swali: Pamoja Na Usumbufu Wako Wote Nilifanya Kazi Sikufanya!? Kumbuka Nilikuwa Kwenye Swaumu

Swali: Toka Mwaka Juzi Mpaka Mwaka Jana Ni Mm Ndie Niliekuwa Nafuatilia Malipo Yng Ofisini Sio Chini Ya 20 Times Na Umekuwa Ukinikimbia Matokeo Yake Nikachoka Kuja, Simu Zng Umekuwa Ukizipokea Unapotaka Na Sms Unanijibu Unavyotaka Je Mkataba Wetu Ulisema Hivyo!?

Swali : Naimani Ww Una Mkataba Upo Ofisini Kwako Upige Picha Tuone Kama Upo Unavyodai, Binafsi Kila Mtu Anajua Nyumba Yng Iliteketea Moto Hivyo Sina Kitu Na Ndio Maana Umekuwa Ukinitendea Unyama Huu Je Kuna Anaeweza Kukaa Kimya Zaidi Ya Mwaka Mmoja Na Hatimae Unaona Kazi Inatoka Wakati Hujalipwa!?

Swali : Ni Movie Ngapi Nilizofanya Kwenye Kampuni Yako Chini Ya Johari!? Ni Zaidi Ya 3 Je Nililalamika!? Kwanini Hii Ambayo Johari Hakuwepo Nikaingia Mkataba Na Ww Iweje Nilalamike!?
Dhulma Itakufikisha Pabaya Sana, Tambua Nilifanya Kazi Yako Ktk Mazingira Magumu, Nilikuwa Kwenye Swaumu Baba Nilifuturu Mabarabarani Chipsi Na Vingine Visivyo Rasmi Yote Ni Ktk Kutimiza Kazi Yako,

Nionyeshe Mkataba Unaosema Nilipwe Baada Ya Mwaka 1 Na Kuendelea Hakika Umeonyesha Ulivyo Na Roho Ya Dhulma Sijawahi Kulalamika Popote Kuhusu Unachonifanyia Kwa Sbb Nilijua Ipo Siku Utanilipa Changu Matokeo Yake Umeona Ujivishe Ujemedari Lakini Haitokisaidia Chochote, Kama Haki Yng Basi Itanifuata Hata Nikiwa Kaburini....Be Blessed....Allah Bariq