Thursday, February 4, 2016

HESABU YA MATUKIO YA UJAMBAZI TANZANIA KUANZIA MWAKA 2013 MPAKA 2015 IMEFANYWA, DAR IMEONGOZA



Jana Febr 03 2016 Bunge la 11 liliendelea mjini Dodoma na moja ya ripoti zilizonifikia ni hii ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya NchiHamad Yusuf Masauni alivyowasilisha ripoti ya matukio ya Ujambazi na yale ya Watu kujichukulia sheria mikononi.
Waziri Masauni anasema “Matukio ya ujambazi yanayohusisha uporaji wa fedha yalikuwa kama ifuatavyo, mwaka 2013 matukio 1266, 2014 matukio 1127, 2015 matukio 913,  jumla ni matukio 3306 ambayo yalisababisha vifo 91 na majeruhi 189
Majambazi 2
 “Mikoa iliyoongoza ilikuwa ni Dar es salaam ilikuwa na matukio 733,  ukifuatiwa na Mara matukio 375 na takwimu za matukio ya kujichukuliasheria mkononi zinasema ni jumla ya matukio 2100 yaliyoripotiwa katika vituo mbalimbali vya polisi nchini
Hapa nimekusogezea sauti ya Naibu Waziri Masauni, unaweza kuisikiliza yote.

BOFYA HAPA KUONA WAKIRUSHIANA RISASI NA POLISI