Kwa wapita njia , kijana huyo mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa Michigan, alionekana ni mtu mzima akifurahia kuwapeleka watoto wake watatu katika park, akiwa na mdogo wake Dominique.
Kitu ambacho hakikuwa cha kawaida ni begi lake la kijivu alilolibeba mgongoni muda wote, ndilo lililokuwa likimuweka hai. Ndani ya begi hilo kulikuwa na mashine (power source) ya kusaidia kusukuma damu kwenye moyo huo feki kifuani kwake.
Moyo halisi wa Larkin ulitolewa kutoka mwilini mwake November 2014, na kuwekewa kifaa ambacho kilimuzesha kukaa nyumbani badala ya hospitali, wakati akisubiri kuwekewa moyo halisi wa binadamu.
Na hatimaye mwezi Mei mwaka huu, Larkin anaendelea vema baada ya kuwekewa moyo halisi wa binadamu katika kituo cha mishipa na moyo cha Frankel, katika chuo kiku cha Michigan, na kutarajiwa kurudi nyumbani kwake mapema ya wiki ijayo.
“Watu wengi wangeogopa kwenda muda mrefu na moyo feki, lakini nataka kuwaambia unatakiwa kwenda na woga, sikutaka kukubali upasuaji, ilinichukua wiki mbili kukubali, kwa sababu inasaidia, naenda nyumbani haraka baada ya upandikizaji, kwa sababu imenisaidia kuwa mwenye afya hata kabla ya upandikizaji”, alisema Larkin.
Kwa mujibu wa mtandao wa upandikizaji viungo (U.S. Organ Procurement and Transplantation Network), takwimu zinaonyesha kuna takriban wagonjwa 4,000 duniani, wanaosubiri kupandikizwa moyo wa binadamu.
Kijana huyo kutoka nchini Marekani alitoa wito kwa watu kujitolea viungo mbali mbali, ili kuweza kuokoa maisha ya watu wengine.
Imetafsiriwa kutoka CNN.
Mashine iliyokuwa ikimsaidia kusukuma moyo feki
Larkin akicheza mpira wa kikapu akiwa na begi lenye mashine inayomsaidia kusukuma moyo feki mgongoni mwake.