Rais Sisi na mfalme Salma wa Saudia
Mfalme wa saudia ametangaza kwamba daraja linalounganisha taifa hilo na Misri litajengwa juu ya bahari ya shamu.
Mfalme Salman alisema katika taarifa kwamba daraja hilo litaimarisha biashara kati ya mataifa hayo mawili.
Alitoa tanagazo hilo wakati wa siku ya pili ya ziara yake katika mji mkuu wa Cairo.Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi alisema kuwa daraja hilo litatajwa baada ya mfalme huyo wa saudia.
Rais Sisi ni mshirika wa karibu wa serikali ya Saudia.
''Tulikubaliana na ndugu yangu rais Abdul-Fattah al-Sisi tujenge daraja linalounganisha mataifa yetu mawili'',alisema mfalme huyo.
''Hii ni hatua ya kihistoria ya kuunganisha mabara ya Africa na Asia na itaimarisha biashara kati ya mabara haya mawili'',aliongezea.