Friday, April 8, 2016

Nyani Apandikizwa Moyo Wa Nguruwe

160406115349_k_h_fungscience_photo_library_512x288_khfungsciencephotolibrary_nocreditMoyo wa Nguruwe.
Maryland, Marekani
WANASAYANSI kutoka Taasisi ya Kitaifa ya Moyo, Mapafu na Damu huko Maryland nchiniMarekani wanasema kuwa wamefanikiwa kuweka moyo wa nguruwe katika nyani kwa zaidi ya miaka miwili.
Matokeo yake yanaweza kupiga hatua katika tiba ya upandikizaji wa viungo vya wanyama katika binaadamu huku kukiwa kuna upungufu wa binadamu wanaotoa viungo vyao.
mbegu-bora-kabisa-ya-land-race-ukifanya-mchezo-jamaa-kitunzwa-vizuri-anaweza-kufikisha-hata-kilo-250Nguruwe.
Upandikazi wa viumbe tofauti husababisha mmenyuko wa kinga na kusababisha kukataliwa kwa kiungo hicho na mwili unaofanyiwa upasuaji huo.
Lakini wanasayansi kutoka Marekani na Ujerumani walitumia muundo wa jeni pamoja na dawa zinazopunguza kinga. Kazi yao imeelezea katika jarida la mawasiliano ya kiasilia.
1Nyani.
Ni muhimu kwa sababu inaleta uwezekano wa kutumia viungo hivyo kwa binaadamu, kulingana na mwandishi mwenza Muhammad Mohiuddin kutoka Maryland, alikiambia chombo cha habari cha AFP.
Upandikizaji wa kutumia viumbe tofauti unaweza kuokoa maisha ya wengi kila mwaka ambayo hupotezwa kutokana na ukosefu wa viungo vya binaadamu kwa upandikizaji.
CHANZO NA BBC SWAHILI