Mara ya kwanza mwanamke huyu alipatwa na tukio kama hili miaka kumi iliyopita, alipoenda kuripoti tukio hilo Polisi mtuhumiwa wa kosa la kumuingilia kwa nguvu mwanamke huyu ilishindikana kukamatwa kutokana na kukosekana kwa ushahidi.
Safari hii mwanamke huyo Adele Barber ameamua kumng’ata ulimi mwanaume ambaye alitaka kumbaka ili kupata ushahidi wa kupeleka Polisi na kisha upimwe DNA utakaowezesha mtuhumiwa kukamatwa.
Akisimulia tukio hilo amesema alikuwa anapita kwenye uchochoro huko Dunstable, England akasikia mtu anakuja nyuma yake lakini hakuhisi chochote, jamaa huyo alimkimbilia kwa nyuma na kumsukuma kwenye uzio, wakati anataka kumbaka alimng’ata ulimi na kuukata na kubaki na kipisi mdomoni na kwenda nacho nyumbani, mume wake akawaita Polisi na kuwapa ushahidi huo ambao ulisaidia mtuhumiwa kukamatwa.