Monday, December 8, 2014

BAD NEWS: MTU MWENYE UNENE MKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI AFARIKI DUNIA...ALIKUWA NA KILO 444!

Rekodi mbalimbali zimekuwa zikivunjwa kila siku Duniani, siku chache zilizopita tuliisikia ile ya watu wawili waliovunja rekodi mbili kubwa ile ya mtu mfupi kuliko wote na mtu mrefu kuliko wote Duniani kukutana kwa mara ya kwanza.
Leo kuna taarifa kuhusu mtu aliyekuwa akishikilia rekodi ya mtu mnene kuliko wote duniani kwa kuwa na uzito wa Kilo 444, Keith Martin ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 44.
Wakati wa uhai wake aliwahi kufanywa upasuaji na  robo tatu ya nyama za kwenye tumbo lake ilikuwa imeondolewa na kufanikiwa kumpunguza nusu ya uzito wa mwili wake, ambapo kifo chake kimetokea miezi nane toka afanyiwe upasuaji huo kwa kuugua ugonjwa wa Pneumonia.
Kabla ya upasuaji Martin alikuwa anakula Calories 20,000 kiasi ambacho ni mara kumi ya kiasi ambacho kinapendekezwa kuliwa na mtu mzima.
Moja ya vitu alivyopendelea kula wakati wa kifungua kinywa ni Pizza na Mayai na kutokana na tatizo la uzito mkubwa Martin aliwahi kukaa ndani ya nyumba yake huko Uingereza kwa miaka 10 bila kutoka nje kutokana na kuelemewa na uzito mkubwa.
Moja ya dada zake amesema wana majonzi kumpoteza ndugu yao na bado wanaendelea kuomboleza msiba huo.
fattest-man-2-600x395
fattest-man-3-600x325
Fattest-Man-in-World-600x376