Wednesday, July 2, 2014

JACK WOLPER ALIA NA ULAWITI DHIDI YA WATOTO

Wakati  sheria  ikizidi  kuwatia  hatiani  wale  nguli  wa  kulawiti  watoto, staa  wa  bongo  movie, Jackline  Wolper  amesema  kuwa  hata  kwa  upande  wake  huwa  anasikitishwa  na  vitendo  hivyo  kwani   kufanya  hivyo  ni  kuwatia  doa  katika  maisha  yao……
 
Staa  huyo  alisema  kuwa  kitendo  cha  kulawiti  mtoto  ni  cha  kinyama  na  kwamba  haoni  sababu  ya kucheka  na  watuhumiwa  bali  wanatakiwa  kufikishwa  mahakamani  ili  sheria  ichukue  mkondo  wake…
 
Jackline Wolper
Jackline Wolper
“Kuna  watoto  wanalawitiwa  na  kubakwa  huko  vijijini  na  hata  hapa  mjini, lakini  unakuta  wazazi  wanazungumza  nyumbani  na  kuyamaliza  bila  kujua  yule  mtoto  ameathirika  kiasi  gani, inauma  sana, ni  lazima  wafikishwe  mahakamani  ili  sheria  ichukue  mkondo  wake”,alisema  Wolper